Read Microsoft Word - Onion Brochure in Swahili.doc text version

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI

UTANGULIZI Vitunguu maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya ubaridi wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Nchini Tanzania, vitunguu maji hulimwa kwenye mikoa ya Iringa wilaya ya Kilolo mpakani mwa mkoa wa Morogoro na kwenye maeneo ya mto Ruaha, mkoani Arusha sehemu za Mang'ora na Babati, Kilimanjaro, na Morogoro wilayani Kilosa sehemu za Lumuma na Malolo na baadhi ya sehemu za Mkoa wa Singida.

Kipato kikubwa na hivyo huinua uchumi

Hali ya Udongo

Vitunguu maji huhitaji udongo wenye rutuba, usiopasuka, usiotuamisha maji na wenye mboji ya kutosha. Hali ya udongo katika kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Unaweza kuuza mara moja au kuhifadhi

Hali ya hewa

Hali ya hewa ifaayo ni ile ya ubaridi wastani. Joto linalohitajika ni kati ya nyuzi joto 13 hadi 24°C ingawa kwa miche iliyoko kwenye kitalu joto zuri ni la nyuzi 20 hadi 25°C. Joto la juu hufanikisha utengenezaji wa kitunguu na ukaukaji.

Uoteshaji miche na Upandaji

Vitunguu maji huoteshwa zaidi kwa kutumia mbegu kwenye kitalu na kisha kupandikizwa shambani. Kiasi cha kilo 3.5 cha mbegu hutoa miche ya kutosha kupandikiza eneo la hekta moja ya shamba.

Aina ya Vitunguu maji

Kuna aina nyingi ya vitunguu maji. Aina hizi zinaweza kutofautishwa kulingana na: (i) rangi ya ganda la nje la kitunguu kilichoishavunwa; (ii) radha (utamu au ukali) wa kitunguu chenyewe; (iii)mahitaji ya mwanga katika uzaaji: kuna aina yenye kuhitaji siku fupi (mwanga wa saa 10 hadi 12 kwa siku) na aina ihitajio siku ndefu (saa 13 hadi 14 za mwanga kwa siku) ili kuweza kuweka kitunguu. Aina ya kwanza ndiyo ilimwayo katika nchi za tropic. Aina Red Creole Red Bombay Texas Grano Siku za kukomaa 150 160 165 Umbile Rangi ya la ganda kitunguu Nusu Nyekundu bapa Nyekundu Duara angavu Njano Duara (Kaki) Rangi ya ndani Nyekundu kahawia Nyeupe kahawia Nyeupe

Kusiha mbegu kwenye kitalu

Mbegu zinasiwa kwenye kitalu kilichoandaliwa vizuri. Mbegu hupandwa kwenye kina cha sentimita moja kwa kumiminwa polepole kwenye mistari/mifereji iliyoandaliwa vizuri. Kisha mbegu hufukiwa kwa kunyunyizia udongo juu ya mbegu zilizoko kwenye mifereji. Mbegu huota baada ya siku 7 hadi 10. Lakini hii hutegemeana na hali ya hewa. Kwani mbegu huweza kuechelewa kuota hadi mpaka siku 21 udongo unapokuwa wa baridi. Hali ya hewa ikiwa nzuri, mbegu uota mapema zaidi, hata ndani ya siku 4.

Kupandikiza vitunguu shambani

Miche hupandikizwa inapokuwa na urefu wa sentimita 15 na unene 1 /2 au 3/4 ya penseli kwenye shina. Miche hii huwa imetimiza umri kati ya wiki 7 hadi 9 kulingana na matunzo. Miche inapandikizwa kwenye nafasi ya upana wa sentimita 20 hadi 30 na nafasi ndani ya mstari ni sentimita 10 hadi 15.

Umwagiliaji:

Umwagiliaji mzuri unahitajika ili kupata vitunguu bora. Umwagiliaji wa maji yanayokwenda chini kiasi cha sentimeta moja au zaidi kwa wiki ni mzuri kwa kupata vitunguu vikubwa. Epuka umwagiliaji kupita kiasi au pungufu kwani hali hii huweza kusababisha mipasuko.

Kuandaa shamba

Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa. Kisha matuta au majaruba hutengenezwa ili kurahisisha umwagiliaji.

Udhibiti wa magugu

Ukuaji na mavuno yanaathirika sana endapo magugu hayatadhibitiwa mapema. Magugu yanadhibitiwa kwa kutumia madawa ama jembe dogo la mkono. Wakati mwingine ni mchanganyiko wa madawa, jembe la mkono na kungolea kwa mkono.

Mbolea

Vitunguu maji vinamahitaji makubwa ya rutuba ya udongo. Hukua vizuri vinapopata samadi ya kutosha kiasi cha tani 25 hadi 40. Kwa hekta. Mbolea isambazwe shambani baada ya kupandikiza, lakini ni vizuri zaidi kama ikichanganywa kwenye udongo kabla ya kupandikiza. Kwa kuzingatia mazao ya tani 18 kwa hekta, vitunguu huchukua kutoka katika udongo, kiasi cha wastani wa kilo 66, 11 na 70 za virutubisho aina ya Nitrojeni, Fosiforasi na Potasiam. Hivyo kiasi cha mbolea kinachopendekezwa ni kilo 450 hadi 565 za mbolea ya NPK (10-10-20) kwa hekta. Mbolea huwekwa siku 7 hadi 10 kabla ya kupandikiza. Kisha, inapendekezwa kuweka kiasi cha kilo 13 hadi 18 za Nitrojeni baada ya wiki tatu hadi nne, ili kuongeza ukuaji wa mimea. Upungufu wa kirutubisho cha Nitrojeni unaharakisha ukomaaji na unapunguza ukubwa wa kitunguu. Kirutubisho hiki kikizidi kupita kiasi huongeza ukubwa wa kitunguu na unene wa shingo ya kitunguu, tabia ambayo upunguza ubora.

Udhibiti wa magonjwa

1. Ugonjwa wa doa la pinki (Purple blotch) Uanza kama doa dogo linalozama ndani ya jani na kisha linaongezeka ukubwa na kufanya rangi ya pinki. Kiini cha ugonjwa huu huanzia kwenye mbegu na pia hubaki kwenye maozo ya majani ya vitunguu. Aina ya Red Creole inaonyesha kutoshambuliwa sana na ugonjwa huu.

Ugonjwa wa doa la pinki

Kuoza kwa kitunguu

Mbinu za kudhibiti ugonjwa huu ni kuendesha mzunguko (crop rotation) wa muda mrefu wa mazao pamoja na kuzuia kutuama kwa maji shambani. Kupunguza msongamano wa mazao shambani na matumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate and potassium hupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Kwa upande mwingine, matumizi ya mbolea ya nitrojeni kwa wingi au kwa kiasi pungufu uongeza mlipuko wa magonjwa. Viatilifu kama vile Mancozeb hutumika kuzuia mashmbulizi ya ugonjwa huu. 2. Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) Magonjwa haya hushambulia majani ya mimea shamabani na hata miche michanga. Kwenye majani kunaonekana vidoa vyeupe hasa kwenye majani makuu ya mimea michanga. Ukungu mweupe unatokea na kuongezeka kwa haraka kwenye sehemu au nyakati za baridi. Viini huishi kwenye mabaki ya mimea ya vitunguu na huweza kupeperushwa mbali na upepo. Kwenye mimea michanga ugonjwa unaweza kudhibitiwa na madawa kama mancozeb. 3. Kuoza kwa vitunguu (bulb rots) Hali hii inaweza kutokea shambani au wakati wa hifadhi ghalani. Ugonjwa huu ni hatari zaidi kwenye sehemu za joto na zenye kutuamisha maji. Ni vyema kuhakikisha kwamba shambani hakuna hali ya kutuamisha maji na pia kwenye ghala kunakuwa na hali nzuri ya mzuunguko wa hewa.

1. Utitiri wa vitunguu (Onion thrips) Hawa ni wadudu wadogodogo sana ambao hula kwa kukwaruza juu ya jani na kunyonya majimaji ya kwenye mmea. Hali husababisha kutoka kwa mikwaruzo meupe kwenye majani ya vitunguu. Mashambulizi yakizidi majani huanguka na kunyauka. Ukubwa wa vitunguu hupungua. Hili ni tatizo kubwa zaidi hasa wakati wa ukame kuliko wakati wa unyevu.

Utitiri wa vitunguu

Madhara ya utitiri

Udhibiti wa wadudu

Utitiri wa vitunguu (Onion thrips), Funza wa vitunguu (Onion maggots) na Minyoo wa vitunguu (Onion wireworms) ni miongoni mwa wadudu wasumbufu kwenye zao la kitunguu.

2. Bungua weupe (White grub) Huyu ni aina ya funza mkubwa. Hutaga mayai yake kwenye uozo wa majani na samadi na hivyo mashamba ya vitunguu yaliyoko karibu au kwenye maeneo ya jinsi hiyo huwa kwenye hatari zaidi. Hushambulia mizizi na kusababisha kukauka kwa mimea. Kutifulia shamba na kuwaweka wazi wadudu hawa kunapunguza idadi yao.

huwa na shingo iliyonywea vizuri na ganda kavu. Kama shingo ya kitunguu haikukauka sawasawa kutatokea hali ya uozo.

Soko la vitunguu

Ukubwa wa vitunguu ni sifa ingaliwayo na wanunuzi. Vitunguu vidogodogo sana au vinene sana huwa havipendwi. Vitunguu vinavyopendwa ni vile vyenye wastani wa unene wa sentimita nne. Vitunguu vilivyochubuka, mapacha na vyenye shingo ya chupa huwa havipendwi. Vitunguu vilivyooza na vile vilivyobabuka na jua pia havifai. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza vitunguu kwa vipimo vya magunia na ama ndoo za plastiki. Kwa miaka kadhaa vitunguu vimekuwa vikiuzwa kati ya shilingi 20,000/= hadi 30,000/= kwa gunia.

Bungua mweupe Funza wa Kitunguu 3. Minyoo ya vitunguu (Onion wireworms) Hawa ni funza ambao mayai yao hutagwa kwenye maeneo yenye magugu. Wadudu hawa huwa ni tatizo kubwa kwenye sehemu zenye kutuamisha maji. Kutifulia udongo ili upitishe maji vizuri pamoja na udhibiti wa maguu ni njia nzuri ya kuwadhibiti wadudu hawa.

Uvunaji

Inapowezekana mwezi mmoja kabla ya kuvuna udongo uanze kuondolewa polepole ili kuviacha wazi vitunguu kwa ajili ya ukaukaji mzuri. Zoezi hili linalenga kufanya angalau theluthi moja ya sehemu ya kitunguu kiwe hakijafunikwa na udongo kwa siku kati ya 7 hadi kumi kabla ya kuvuna ili kuharikisha ukaukaji. Vuna wakati asilimia 75 ya shingo za vitunguu zimelala. Mara nyingi vitunguu hung'olewa na kurundikwa kwenye matuta na baadaye kukusanywa na kuwekwa kwa ajili ya kukata shingo. Mizizi pia inapunguzwa na vitunguu vinajazwa kwenye magunia tayari kwa kusafirishwa nyumbani kwa ukaushaji zaidi na kisha kuwekwa galani au kuuzwa.

Hifadhi ya vitunguu

Vitunguu vipya vilivyovunwa huwa havioti upesi. Hifadhi sahihi hurefusha muda wa kutoota. Kwenye hifadhi ni vizuri vitunguu vipate hewa yenye mzunguuko mzuri na ndiyo maana maghala ya kuhifadhia vitunguu yanajengwa kama vichanja ili kuruhusu hewa kuzunguuka hata kwa kupitia sehemu za chini. Ndani ya ghala vitunguu humwagwa na kusambazwa kama inavyonyesha kwenye picha namba.. Vitunguu vinaweza kuhifadhiwa kwa miezi sita au zaidi bila kuharibika.

Mavuno

Mavuno ya vitunguu yanategeme huduma za shamba pamoja na hali ya hewa. Vitunguu pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya kitunguu. Kwa wastani vitunguu vinaweza kutoa mavuno kati ya tani 10 hadi 18 kwa hekta moja.

Ukaushaji

Madhumuni ya kukausha ni kuvifanya vitunguu visiweze kuota kwa muda na pia kuvifanya visiharibike. Vitunguu vilivyokauka vizuri

Information

Microsoft Word - Onion Brochure in Swahili.doc

5 pages

Report File (DMCA)

Our content is added by our users. We aim to remove reported files within 1 working day. Please use this link to notify us:

Report this file as copyright or inappropriate

55775


You might also be interested in

BETA
matunda na mboga-book 3
Microsoft Word - Onion Brochure in Swahili.doc