Read imaan%202.pdf text version

Maana Halisi ya

Kimetolewa Na

First addition.

All rights reserved.

Toleo la kwanza

Copy 1000. Dec, 2007. i.

MWENYEZI DAWAMU:

Kwa jina lako Jahali, nalo ninalokadimu. Tukufu na la awali, Rahmani na Rahimu. Shabihi wala mithali, hana mfano adhimu Mwenye Enzi ya Dawamu, katukuka Maulaya. Uliyoumba arishi kubwa iliyo adhimu, Kursiyu na Firashi, na Lawhi na kalamu. Matukufu hayaeshi, Fi-Shani kulla yomu. Mwenye Enzi Dawamu, katukuka Maulaya. Kauni na vilivyomo, toka Alifu na Mimu. Jumla na waliyomo, katika kila Isimu. Kisicho na kilichomo, ni vyote vyako Halimu. Mwenye Enzi Dawamu katukuka Maulaya Ewe unao Sabihiwa, na kila kitu Dawamu. Pia na kuhimidiwa, na vitu vyote Ayamu. Kattu usiawe na malaika kiramu. Mwenye Enzi Dawamu katukuka Maulaya. Ndiwe unayefariji, daima unayekimu. Kadhiya na hawaiji, zote hutatukirimu. Bila ya wewe haiji, neema kila msimu. Mwenye Enzi Dawamu Katukuka Mauyalaya Penye haki Mola pako, tufutie maathiu. Penginepo wajawako, hatupajui adimu. Tumeeelekea kwako Molla wetu ya Alimu. Mwenye Enzi Dawamu katukuka Maulaya Tajiriba na fadhaa, kwa mja hilo lazimu. Moyoni weka rajaa, kwa Mola ukizimu. Usikatie tamaa Rabi atakukirimu. Mwenye Enzi Dawamu Katukuka Maulaya Kwashauku na vipaji, vikubwa vilo timu. Vipi visitoe maji vidole vyake Hashimu. Mola kampa faraji, mpenzi wake Karimu. Swalawatu wa salamu mpenzi wa Maulaya.

Zinaandama athari, kwa bwana mwenye ulumu Alieacha dahari, nyoyoni mwa wanaadamu. Jumla na Asrari, ziloondoa zidi hamu. Swala watu wa Salamu, Mpenzi Maulaya. Dhati ya nyoyoni mwetu, Mola anatufamu. Juu ya Mtume wetu, mwenye Badru tamamu. Kumpenda haki yetu, ilo kubwa Adhimu. Swala watu wasalamu, Mpenzi Maulaya. Rabi Sala zenye Huba, mfikizie Hashimu. Kadhaali na sahaba, pia wote Maimamu. Pasiwepo na hijabu, hapa mpaka kiyamu. Ndie Shafii Anamu, Mpanzi wa Maulauya

iii

Yaliyomo:

No. 1. Dibaji. 2. Utangulizi. 3. Imaani. 4. Undani wa Ngome ya Kwanza. 5. Ufafanuzi juu ya Moyo. 6. Ufafanuzi wa Roho. 7. Ufafanuzi juu ya Nafsi. 8. Nafsi, Roho, Moyo na Akili kuingia ndani ya kiwiliwili 9. Majaribio katika Uhai. 10. Mabadiliko ya Nafsi hadi kuungana na roho. 11. Insaan. 12. Kumalizika Mwili. 13. Neema za Dunia na Neema za Akhera. 14. Malipo ya Pepo kwa wapendanao Lillahi. 15. Askari na Adui za Moyo. 16. Mnyezi Mungu, Binadamu na Maumbile. 17 Undani wa Kutekeleza Faradhi. 18. Uislamu ndani ya Swala. 19. Undani wa kutekeleza wajibati. iv. Ukurasa.

Dibaji:

Kitabu hiki kilichoandikwa na Mtoto wetu kimekusanya mengi yenye maana kubwa na ya msingi wa Kiislamu. Amejulisha Umoja wa Mwenyezi Mungu na Mapenzi yake juu ya Mtume Muhammad Saw. Aya alizozitia katika kitabu hiki zinathibitisha kuwa yeye Sayyidna Muhammad ni Mjumbe wa mwisho kabisa wa pekee ambaye hapana njia yoyote nyingine ya kumjua Mwenyezi Mungu, ya Kumtii na kujisogeza kwake ila yeye Mustafa, aliyechaguliwa. Ahmad amefanya vizuri kutaja baadhi yalolazimu juu ya Uislamu na yaloharamishwa, na kuonyesha alama za kweli za Muumini, katambulisha umuhimu wa kutengeneza Moyo, kwani vitendo vya viwili wili, ijapokuwa Muislamu hana budi navyo. Havitoshi ikiwa Moyo umeachiwa uwe Mchafu. Moyo ukiwa safi ndipo vitendo vitapokubaliwa, hapana shaka kuwa tabia njema ndio lengo la Dini ya Kiislam, na kitabu hiki kimewacha wazi hayo. Alhasili atayekisoma kwa Insaafu na kuzingatia atapata faida ni nyingi zilohusu Islamu, Imaani na Ihsan. Mwenyezi Mungu ambariki aliyekitunga

Omar Abdallah.

v.

Dibaji

vi.

Dibaji

vii.

Utangulizi:

"Kullu-dhibalin la-yabdau fihi bil Basma-Llah fahuwa aqtwau ayil galilil-barka'' "Kila lenye kutuka minghayri ya kutangulizwa jina la Mnyezi Mungu, jambo hilo huwa lenye kukatika, au kama halikukatika basi huwa na barka chache). Imaani, zaidi kuliko kuamini Mnyezi Mungu, na Malaika wake na Vitabu vyake, na Mitume yake kuamini siku ya Mwisho na Kudra - kheri na shari zote zikiwa zinatokana na ­ Mnyezi Mungu, aliyetukuka ni yenye uzito zaidi. Na tumekiita (Maana halisi ya Imaani ­ ii) tukiamini ya kuwa, mara baada Mtu kukisoma hatakosa kujiona ana lile jicho la tatu ambalo, kwa wengi huwa haliwadhihiriki mapema katika uhai.na hasa ukizingatia maanani asri (karne) yetu hii, ya ishirini, ambapo Dini inachukuliwa kama kitu cha kudharauliwa na kisichokuwa na maana yeyote wala maendeleo kwa ujumla, na badala yake ikiwa nyimbo za Souls, Bolingo, na Mipira ambavyo ni vitu vya upuuzi mtupu ndio vyaonekana muhimu mno. Al habib Seyyid Umar bin Abdalla (Mwinyi baraka) katika nyingi ya hotuba (khutba) zake alizozitoa Ulaya, juu ya Uislamu, mfano wa ile alioitoa Amerika (1984/85) "The real meanings and teachings of Islam" ambao Majaalis imeshapata idhini yake Alhabib, ya kuitoleshea kitabu, ambayo ndani yake ameelezea kuwa, ameenda Amerika, lakini hakuona wana Sayansi wakinywa pombe (ovyo) na kujishughulisha na michezo na upuuzi. bali aliwakuta katika kazi kubwa za kujenga maendeleo ya binadamu, hawana habari kabisa juu ya madansa, pombe vilevi vya kudhuru akili (Drugs and Merijuana etc). Wengi wamo ndani ya Maktaba zao, na ndani ya Maabara zao, wakitafuta matukufu. Akili ya Mtu hukuwa kwa kufanza wingi wa majaribio (Experimentation) mbali mbali. Bwana Mtume SAW amesema:viii.

"Man amila bima alima waratha-hul Lahu ilman lam yaalam'' "Mwenye kutumiya (kufanzia majaribi, kufanza kazi) kwa yale aliyoyajuwa (basi) Mnyezi Mungu Humrithisha Ilimu (ambayo) hakuwa (Mtu huyo) anaijuwa (hapo awali)". Na hiyo ndo Fur-qan - yaani Ilimu ambayo Mnyezi Mungu humfundisha mja wake bila wasita wowote katikati ili tu aweze kupambanuwa baina ya mambo ya haki (mambo yanayofaa na yasiofaa). Qur an:Baqara: 2:53.

"Na (kumbuka) Tulipompa Musa kitabu (kilichokusanya kila wanayohitajia) na cha kupambanua baina ya haki na yasiyokuwa ya haki ili mpate kuongoka". Akili hupata raha na kujiweka tayari kupokea na pia kutoa mambo ya maana kwa kupata utulivu. Na hata Imaani yenyewe kwa upande mwingine, hukaa vizuri kifuani kwa Mtu kutokana na utulivu. Tazama Nabii Ibrahim ASW alipoomba aonyeshwe vipi Mnyezi Mungu ahushavyo wafu, alijibiwa (kwa suala) "Kwani huamini?" Akasema "Laa, bali ili utulie Moyo wangu..." (Na humo Moyoni ndimo mahali ilimo "Nuru ya Akili"). Basi halikadhalika sisi tukitaka tufanikiwe ni lazima tuelewe ya kuwa humo mwenye Madansi, Pombe, Uasharati na mambo ya upuuzi, Moyo haupati wasaa wa kutulia. Aghlabu watu huzusha ugomvi vilabuni, mwenye mipira, na kwengineko mfano wa humo. Sehemu kama hizo mwenye Akili ni lazima ajiepushe nazo ikiwa ameazimia kuendelea kihakika. Tunamtakia Rehma na Amani mbora wa viumbe, ambae hana kasoro hata chembe Bwana Mtume Muhammad SAW ambae juu ya kusifiwa kwake na Mnyezi Mungu Mwenyewe (Sub hana wa Taala) tena kwa njia ya heshima kabbisa kama vile:Qur an:Al Qalam:68:4:

ix.

"Na bila shaka una tabia njema kabisa" Pia: Qur an: Al Inshira:94:4.

"Na tukautukuza utajo wako"

Mnyezi Mungu Ameutukuza utajo wa Bwana wetu Muhammad SAW kwa kumpa Utume, na kumfanya bora kuliko Mitume yote; Ee! Sisi Mnyezi Mungu anatwambia katika: Qur an:Al Imraan: 3:110.

"Nyinyi ndio Umma bora kuliko Umma zote zilizodhihirishwa watu (Ulimwenguni), mna Amrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamwamini Mwenyezi Mungu. Na kama wale waliopewa kitabu wangaliamini (kama walivyoamrishwa) ingalikuwa bora kwao. (Lakini) miungoni mwao wako wanaoamini, na wengi wao wanatoka katika Twaa ya Mwenyezi Mungu" Sikwambii ambae ameletwa na Mwenyezi Mungu juu yetu ili atuhidi katika Dini, na ili awe Rehma kwetu!. Qur an:Al Ahzab:33:21.

x.

"Bila shaka mnao mfano mwema (Ruwaza nzuri) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na kumtaja Mwenyezi Mungu sana".

Qur an: At-Tawba:9:103.

"Chukua Sadaka katika mali zao, uwasafishe kwa ajili ya hizo (Sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) ­ na Uwaombee Dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu (watengenekewe), na Mwenyezi Mungu ndiye asikiaye na ajuaye". Na jaha ya Bwana Mtume SAW pamoja na kutawassuli nae kunaonekana wazi katika Ayah ii iliopo kwenye Juzuu ya tano: Qur an:Annisa: 4:64.

"Na hatukumleta Mtume yeyote ila atiiwe kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Na lau wangalijua walipojidhulumu nafsi zao (kwa kwenda kuhukumiwa,

xi.

kwa njia isiyokuwa ya sheria) wakaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na (yeye) Mtume pia akawaombea msamaha, bila shaka wangemkuta Mwenyezi Mungu ni mwenye kupokea toba na mwenye kurehemu". Mnyezi Mungu kaipanga Qur an kwa chungu ya mithali ili ipate kutufundisha kwa njia ya wepesi wote wale tangu zama za Bwana Mtume SAW hadi kufikia mwisho wa Dunia, kwani yeye amehusishwa kwa watu wote (He is meant as Divine Prophet for the entere man-kind to the last day). Kwa hiyo hatuwezi kusema: Eti o! Aya hiyo iliwahusu walopita, na kwamba sisi, na wengine wote watokuja miaka alfu baada ya leo 2001 ­ 3001, haiwahusu kitu aya hiyo. Bila shaka ingekuwa ni sahihi kuchukulia mambo kinamna hiyo, basi hatungehusika kamwe na kusali na kufunga kwani, amri zake zilitoka miaka 1400 iliopita. Masikini wanaisoma Qur an kila siku, huku wakiyakinisha kua mambo ya Mnyezi Mungu hayafanani na ya Viumbe, na kuwa siku yake moja ni sawa kwa makadirio na miaka alfu moja tunayohisabu sisi hapa duniani, kwa hiyo tangu iteremshwe aya hiyo, haijapita hata siku moja unusu. Masikini!! Tunasoma, tunayakinisha hakika zake lakini tunakataa kukubali!! Basi kwa Ulamaa, hakuna mjinga wa kumzidi mtu kama huyo.Tumekuwa kama tuloghafilika na Aya: Qur an:Nisaa:4:115.

"Na atayemwasi Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu na akafuata njia isiyokuwa ya Waislamu; tutamgeuza alikogeukia mwenyewe na tutamwingiza katika Jahannam; napo ni pahala pabaya kabisa pa mtu kurudia". Mnyezi Mungu Awahidi wale ambao katika kufwata kwao bila ilmu, yale madhehebu ya (Muhamma Abdul Wahhby)Wahbi na xii.

Muutazila, wametokea kuwa na mahabba machache sana kwa yule aliyependwa na kila kiumbe ukiacha mtu kando kabisa, Bwana Mtume Muhammad SAW, kwani bila ya Uwongofu wake (Mola) mfano wa watu hao umo hatarini kwa mujibu wa Aya hiyo ya An Nisaa:4:115. Basi juu ya kusifiwa huko wapo baadhi ya watu (tena Waislamu ­ maana Makafiri wengi wamemsifu Bwana Mtume Muhammad SAW katika njia nyingi za maisha (They glorified Muhammad in various and multitudinous aspects of life) na ndani ya vitabu vinene vinene na kwa sifa nzuri nzuri za ajabu. Vitabu ambavyo vimekuwa sababu ya wengine miungoni mwao kuukumbatia Uislamu (basi wapo baadhi ya watu hao ambao hawakubaliani na sifa kama hizo, apewe Bwana Mtume Muhammad SAW. Na waulizwapo sababu, eti husema: "a! Mtume si kama wewe tu? Utafikiri wao huweza kwenda kwa Raisi wao kama wajavyo kwangu. Binadamu aghlabu huwapenda viongozi wao (na hata kama ni wabaya kama Firauni) na hufikia kuwapa sifa kubwa na hata kupita hiyo ya Bwana Mtume SAW ­ ya kuitwa "Bwana Sayyid", mfano wa sifa hizo ni kama "Mtukufu Fulani bin Fulani", "Mawlana Fulani", Jalal Fulani bin Fulani", "Aya na hoja ya Mnyezi Mungu" (Allah), na kadhalika minghairi ya kuzikemea, Jee tujiweke wapi katika hadith ya Bwana Mtume SAW isemayo: "Laa Yuumin ahadukum hatta akun khayrun ilayhi min Nafsihi wa malihi wad-duni-ya kulliha". "Hawi ameamini mmoja wenu yeyote, mpaka niwe mimi ni bora kwake kuliko Nafsi yake na mali yake (Hata ahly zake) na Duniya yote" Aidha: "Laa yuuminu ahadukum hatta yakun hawa-hu tabian jiitu-bihi minal-lahi". "Hawi ameamini mmoja wenu yeyote, mpaka iwe mapenzi yake ni yale ambayo nimekuja nayo toka kwa Mnyezi Mungu". Ni wapi na wapi tulivyo kwa Bwana Mtume SAW, na wale ambao kwa wingi wa mapenzi yetu juu yao huwatungia mashairi mfano wa : xiii.

"Apendae hana dawa". "Mwenye kupenda haoni". "Sili silali nakuwaza wewe". "Kufa afadhali kuliko kukukosa wewe". Bila shaka ipo tofauti kubwa, lakini vipimo vya Imaani yake Mtu ina yeye mwenyewe mtu, kwani hakukosea Mnyezi Mungu kusema: Qur an: Al Qiyama:75:14. "Bali mtu ni shahidi juu ya Nafsi yake, ingawa anatoa nyuzuru zake za uongo".

Maana Halisi ya Imaani ­ ii, hatukuweza kuitoa pamoja katika kitabu cha kwanza kwa sababu ya uwezo wa kifedha hasa katika gharama za kupanga herufi (type setting) na gharama za kuchapisha kwa vile sahifa (pages) zilibidi ziwe nyingi ambapo tulikua tushindwe. Lakini kwa uamuzi wa pamoja na washauri tuliamua kutoa pole pole kwa kadiri ya uwezo wetu, na huenda pia tukapunguza, ili tujaalie kuepo kitabu cha iii. Tumekwisha onyesha katika sehemu ilotangulia vipi Imaani ilivyokusudiwa kuemo mwenye Ngome sita ambazo ni muhimu sana: 1. Yaqini. 2. Ikhla-s. 3. Kutekeleza fardhi. 4. Kuacha yaliyo haramishwa. 5. kutekeleza wajibati na 6. Kutekeleza Sunna. Na mwisho wa yote ni Kutekeleza Adabu. Katika Ngome 6 ambazo Imaani imezungushiwa nazo, hii Ngome ya Saba, nayo ni muhimu kama zilivyo hizo sita. Bwana Mtume SAW ameonyesha sura ya Adabu katika Wajihi chungu nzima ndani ya maisha; na ni yenye kuonyesha wazi kua bila ya Adabu, Imaani ya Mtu huenda ikawa dhaifu. xiv.

Mifano ya Adabu kwa kifupi ni kama ifuatavyo: Kutawadha mara tatu, wakati mara moja tu inatosha. Kusimama mbele ya Mzazi, Mwanachuoni na yeye mwenyewe SAW, na kadhalika. Kuna kurai Adabu kwenye Ilmu, kwenye kutarazaki, kwenye Kusali, na mfano wake ; kwenye Milahaka, kwenye Kula, kunywa, Kulala, kuamka, kuoga hadi Kuzungumza Mtu na Mkewe. Basi itafaa pia Mtu ajifunze ili aweze kujipamba kua Muumini alie bora mbele za Mnyezi Mungu. Vile vile katika kitabu hiki "Maana Halisi ya Imaani ii" ambapo tumeonyesha undani wa baadhi ya Ngome za Imaani pia tunazungumzia suala zima la "Nafsi" ambalo Al habib Sayyid Omar Ibn Abdallah (Mwinyi Baraka) pia amelichangia vizuri sana kwa maelezo ya kadiri katika Muhadhara wake. Na hata hivyo, tumehisi kuwa hatumudu kumalizia humu kwa hivyo huenda uwezo (Fedha) ukiruhusu tutamalizia suala zima la "Maana Halisi ya Imaani" katika namba Tatu au Nne ­ Insha Allah itakuwa kheri. Tunatumaini kuwa msomaji ambae hakupata mengi yalo madhubuti katika Uislamu, atakuwa amepiga hatua ndefu sana mara baada ya kusoma kitabu hiki- Insha Allah. Suala la kukumbuka ambalo hatukua tumeliona muhimu hapo awali, kwa vile wengi wa wasomaji ni wenye kuelewa mara moja, ni wapi Muallif amedharifia (ameegemeza kumbukumbu) kwa maandishi Fulani, sasa tumeona ipo haja ya kufanya hivyo. Kwa hiyo tumeonyesha hapo chini baadhi ya vitabu ambavyo tumevitumia ili kuandika suala zima la "Maana halisi ya Imaani" kwa kadiri ya bidii na Ilmu yetu. Alokamilika ni Mnyezi Mungu tu pekee, basi huenda yakawepo makosa pia katika kazi yetu hii, ambapo kutokana na Mnyezi Mungu anavyowapa watu Ilmu. Qur an:Yusuf:12:76. "Na juu ya kila ajuaye yuko ajuaye zaidi" Ingependeza sana kama tungekosolewa na kuelekezwa. Vitabu tulivyotumia ni hivi vifuatavyo:1. Tafsiri za Qur an za: a) Abi Twahir bin Muhammad Ash-Shiraz ­ Tanwi-ril Miqbas. xv.

b) Jalaleyni (Maarufu Afrika Mashriki). c) Al Farsy (Mungu Amrehemu pamoja na wenzie). d) Abul alla Maududi. e) Yusuf Ally. 2. Imamu Ghazzali ­ "Ahyal 3". 3. Imam Ahmed bin Sumeyt - "Minhal". 4. Imam Ahmed Bin Sumeyt - "Kawkabuz-zahir". 5. Al Allam Sh.Twantwawi. 6. Afi-f Abdul Fat-ha ­ "Ruhud-dinil Islamy". 7. Seyyid Ahmed El-Mash-hur ­ "Miftahul Jannat". 8. Sherehe ya Imam Nawawy ­ "Arbain" ­ Ya Kiarabu. 9. Zubad ­ Nadh-m. 10 "Hadithi 40" ­ Sherehe ya Imam Nawawy (Ya Kiswahili). 11 . Bukhary iii. 12. Tabarak Dhul-ula ­ Sheikh Hassan Bin Ameir. 13. "Swahihi Muslim" ­ Vol. i. 14 . Zawajir ­ Ibn Hajar. 15. " Min-tawaj-jiha-tin Nabawiyya" ­ Sheikh Minshawi na AbdulKarim. 16. "Seratin Nabawiyya" - Ibn Hisham. 17. "Fuyu-dha-tir-rabba-niyya" 18. "Maisha ya Nabii Muhammad- SAW" ­ Sheikh El Farsy. 19. "Umur Swalat El-Kubra" ­ Sheikh Mzee Bin Ally. 20. "Forty Hadith Quds" ­ Ezzeddin na Davis. 21. Rampa ­ "You Forever", "Beyond the tenth", "Ancient Cave", "Doctor from Lhaso", "Lighting the candles" Etc. 22. "The Occult". 23. "Problem of the Dual". 24. "Al Koran". 25. Kamusi za: i. Kiarabu - Kiingereza. ii. Kiingereza ­ Kiswahili. 26. "Muhadhara wa Al Habib Seyyid Omar Bin Abdalla (Mwinyi Baraka). Juu ya Nafsi na Insaan". Nachukua tena nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wote wale ambao wameshirikiana nami bega kwa bega hasa saa za usiku katika kuzichambua Nuskha za kitabu hiki:i. Habib Swaleh. ii. Al Akh Mahdy. iii. Al Akh Ali Dodo. xvi.

iv.

v. vi. vii. viii. ix.

Al Akh Sleiman Dodo na wale ambao wamesababisha kutoka kwa sura ya kitabu chenyewe kwa safari hii: Ahmed S. Bamgha. Muhammad Adan ­ Hodhan International. Ibrahim I. Juma. Muhammad Is-Haq ­ Scandinavia Bus Service (kwa mara ya pili). Na Ahlil Majaalis El Qadiriyya wote kwa Jumla chini ya Ukhalifa wa Sheikh Aly Mzee Comorian, na mwisho Sheikh Ally Said wa Agip Dar es salaam kwa msaada wake wa kuzichapisha Nuskha zetu.

Wafaqana Llahu limaa yuhibbu wa-yardhwa.

Mnyezi Mungu awanufaishe nacho kitabu hiki kila msomaji Wasalla-Llahu wa salaam ala Seyyidna Muhammad wa alihi walhamdu-lillahi Rabil Ala-meen.

Wabillahit-Tawfeeq.

Al Faqeer, Ahmed Sheikh, Majaalis El Ulaa El Qadiriyya, P. o. Box 15170. Dar es salaam.

xvii.

IMAANI.

Amesema Bwana Mtume Muhammad S.A.W:"Al Insaan hadithun baada-hu fakun hadithan ahsana liman-dha-a". "Mtu hua ni hadithi tu (mazungumzo) baada yake, (basi) kua hadithi nzuri kwa watakaoipiga baada yako."

Bila shaka katika mazingatio ya kweli juu ya hadithi hii ni lazima Maneno: "Hadithi Baada yake" yatupatie upana wa maana zaidi ya vile tunavyodhani katika daraja ya kawaida. Kwa kawaida na mazoea, neno: "Hadithi" tunalielewa kua ni masimulizi ya jambo au tukio lililopita au linaloendelea. Ni sawa sawa ikiwa masimulizi yake ni mafupi, ya kadri au marefu. Na neno "Baada yake" katika daraja la kawaida husema: "Ni nyuma yake mtu", amma alikuwepo mahala, halafu aliondoka na kadhalika. Amma kuondoka, ni namna mbili:1) kuondoka kwa safari fupi na ndefu, na kurudi. 2) kuondoka safari ya moja kwa moja, na bila ya kurudi. Kuondoka kulikokusudiwa mno, ni kwa pili ambako kuna maanisha: "Kufa" na sio rahisi kurudi (labda kwa njia ya miujiza. kama alivyofanza Naby i Issa bin Maryam, zama alipofufua baadhi ya waliokwisha kufa, kwa idhini ya Mnyezi Mungu, wakarudia kwenye uhai mara ya pili, lau kwa muda mfupi). Neno hilo ukilitamka kwa sauti ya ndani yako ili ujisikizishe wewe mwenyewe, "Kuufaa" huenda ukahisi kumiliki moja ya hali mbili hizi: 1. Chuki: Yaani kama ambae hupendi, wala kupendelea kuiacha duniya na starehe zake, mambo ambayo yalikupumbaza kwa kila hali ya raha. hupendi kuachana na wapenzi maridhawa; watoto mali zako na mafedha uliorun uliyorundikisha - benki kwa muda mrefu. 2. Woga: Unadhani labda huenda ukatokewa na kifo kweli pengine saa hiyo hiyo, au punde kidogo hivi. katika hali hiyo unaanza kujiuliza masuala mengi mengi, mfano wa haya; "Vipi itakuwa hali yangu nikifa?, Ni amali gani ambazo nimeshazitanguliza huko niendako" (yaani akhera ambako kwenye uhai wa milele?), na kadhalika. 1.

Qur an: Luqman. 31:33.

"Wala asikudanganyeni yule mdanganyifu mkubwa, (Iblisi) katika (mambo ya) Mwenyezi Mungu". Amesema msanifu mmoja wa kizungu:"As we are in the midst of death we are in the nist of life". "Kama vile tukiwa katikati ya mambo ya kifo ndivyo hapo hapo tunavyokua kindibwa ndibwa katikati ya maisha". Amesema Al marhu-m Sheikh Hassan bin Ameir Ash-shirazi katika sherhe yake ya "Tabaraka dhul-ula" (hiyo mada-rijil-ullah) katika fasiri ya ubeti nambari 5-6, kua; "Ala ayyuhal maghruri ma lakatal- abu, tuammilu a-ma -lan wa mawtuka aqrabu" . "Oh! ewe mdanganyika vipi kucheza kumekusibu umezipa tamaa fika na mautiyo yako karibu". "Kam min mustaqbalin - la - yastakmilihu wa muntadhwirun - ghadan la yablughuhu walaw nadhwartum ilal ajal wa masiriruhu - la ­ abghadhtumul amala wa ghururahu". "Wangapi siku waloifikia wala hawajaikamilisha na wangapi walotegemea kufika kesho, haikuwafikisha na falau Ajali mwendoe mungeuangalia, basi tamaa na ghururi mngezichukia". Amesema Bwana Mtume S.A.W;"Man ahabbad dunya adhwarrabi a-khiratuhu" "Mwenye kuipenda dunia hudhuru akhera yake". Na pia amesema:2.

"Hubbud duniya raas kullu khati-a" "Kupenda dunia ni kichwa cha kila dhambi (makosa)". Na ma-damu unapenda dunia, basi lazima utakua na tamaa (Tul amal). Kuna msemo unaosema hivi:"Tamaa mbele mauti nyuma" Mara nyingi watu hufikia kufa wakiwa wameacha mambo mengi sana nyuma yao hayajamalizwa. (Man proposes, God opposes). lakini wapi! mauti yakishawadia, hua hayamsaili mtu. humhujumu tu, yakaacha kiwiliwili nyuma yake kikililiwa. Daima tungekua watu wa kujiandaa na mauti lau tungetia maanani kauli ya hakika kama hii, iliyofunuliwa katika: Qur an: Al-muna-fiqu-n. 63:11.

"...Lakini Mwenyezi Mungu hataighairisha Nafsi yeyote inapokuja ajali yake; na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda (yote)". Pia Anasema: Qur an: A`araf. 7:34.

"Na kila watu wana muda wao (wa kuondoka ulimwenguni utakapofika muda wao huo, hawatakawia (hata) saa moja, wala hawatatangulia (kabla haujafika)" Na hatari zaidi ni kwamba hakuna ajuaye lini atakufa au wapi atafia. Kama alivyosema Mnyezi Mungu katika: Qur an: Luqma-n. 31:34.

".....Na nafsi yeyote haijui ni nini itachuma kesho, wala nafsi haijui itafia ardhi gani". 3.

Qur an: Nisaa. 4: 78.

"Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa Katika ngome madhubuti". "Out brief candle, life is but a walking shadow". "Uhi ni kama kivuli cha kupita tu, mshumaa mfupi, mara moja, hun`gaa kisha huo, haupo tena". Ghururi za dunia, mwisho wake hua kama hivyo kama mtu asipojirudi nafsi yake, ambayo haizeeki ikachakaa ikaonekana, lakini huzeeka kiwiliwil, mara ukawa huwezi tena; juu ya kujikusuru kwako. kila siku mtu hujiona mtoto tu, shauri ya ghururi, basi usisubiri mpaka ukafikia hali ile iloelezewa ndani ya: Qur an: Muuminun. 23:99.

"Hata yanapomfikia mmoja wao Mauti husema "Mola wangu nirudishe (ulimwenguni)". Basi kama ni lazima (kwa mtu ) kuifwata dunia, basi nasaha ya maana juu yake, na iwe kama ile alioelezea Bwana Mtume S.AW:"Mwenye kuitaka dunia basi juu yake awe na ilimu, na mwenye kuitaka akhera, juu yake awe na ilimu, na mwenye kutaka yalioko kati ya dunia na akhera basi juu yake awe na ilmu". Zipo na chungu ya hadithi mfano wa hiyo, juu ya dunia na mambo yake ya khadaa, bali tumefupisha tu. pia zipo beti zinazoelezea mwenye "Taba-ra ka dhul ulaa. Uk. 75" zinasema:"Inna lil lahi iba-dan futwana tarkuud-dunya wakhaful fitana". (Hakika Mnyezi Mungu Anao waja, wenye akili kweli kweli, 4.

(ambao) wameiacha dunia kwa ajili ya kuchelea fitna yake). "Nadharuu fiha falamma alimu anna laysat lil hayyifi-ha watwa -nun". (Wameiangalia (na kuichunguza ) ndani yake, na pindi walipojua, kwamba haimpi makazi (makao ya kudumu) yeyote (yule) alie hai). "Jaalu-ha luj-jatan wat-takhadhu swali-hal aamal fi-ha sufunun". (Walijaalia kua ni kama wimbi la kupita (la bahari ) tu na Wakafanza amali njema ndani yake ni kama meli (za kuwanusuru na gharka)". Ni mafanikio yalioje lau tungepatikana miongoni mwetu kwa maelfu elfu wa mfano huo!. Mweyezi Mungu hampendi mtu ambae hujifanyia mambo bila ujuzi, na hata kama amali yenyewe ni nzuri yenye thawabu kubwa kweli mfano wa "Swala" basi haitatosha kitu. "Waman bighayri ilmin yaamalan Aama-luhu mardudatan lan taqbalan" (Na ambae bila ilmu yuwajifanyia tu (mambo yake )basi amali zake zote ni zenye kurudishwa hazitapokelewa hata kidogo). Na anaefanya amali kwa ujuzi basi Mola Sub-hana wa Taala humpenda sana na angaa amali yenyewe ni chache.Tazama nini anasema Bwana Mtume S.A.W. juu ya jambo hilo: "Innal Laha Taala yuhibbu kullu man atqana bi amalihi". (Hakika Mnyezi Mungu alietukuka, humpenda kila ambae huifanza amali yake vizuri sana (yaani kwa Ilimu). Katika hadithi hiyo pana hikaya ambayo, kwa thamani iwaa yeyote lazima tuipate kwani si yenye kutoka katika zungumzo letu - Wenye kuipenda dunia na kuchukia mauti - Hikaya yenyewe ni hii na inaanza hivi:"Katika zama za Naby Mussa As palikuepo Mtaabad (yaani mcha Mungu sana) aliekuwa akifanza ibada zake, kwa muda wa miaka 80 nje ya mji, penye jabali. Hata pale alipokuwa akisujudu, palifanza 5.

athali ya kishimo hasa. Kwa upande mwengine alikuwepo mlevi wa kupindukia, hakua na amali nyengine yeyote zaidi ya pombe. Mtihani kati yao ulikuwa juu ya uwezo wa Mnyezi Mungu katika kumpitisha Ngamia mzima ndani ya tundu ya sindano (hii haina uhusiano wowote na aya 40 katika Suratil Aara-f ambapo Mnyezi Mungu anasifia juu ya roho za makafiri kua hazitapenya mbinguni labda hata atapopenya ngamia ndani ya tundu ya sindano. Aya hiyo ilikua mbali na aya hii). Basi matokeo ya mtihani wao yalikua hivi: Yule mcha Mungu kwa muda wa miaka 80 alizingazinga moyoni mwake akasema (nafsini mwake) "Amma Mitume hawasemi urongo, lakini!! Aa!! hii habari ya kupitishwa ngamia mzima mzima ndani ya tundu ya sindano!!!!. Amma kwa yule mlevi ilikuwa hivi: Mara baada ya kuelezwa kisa kile, yeye alijibu kwa kutaassaf na kuhuzunika: "Yaani kalimal lah (ewe mwenye kusemezana na Mnyezi Mungu) Mnyezi Mungu ni muweza wa kuipitisha dunia nzima ndani ya tundu ya sindano, nini ngamia katika ukubwa?". Na kwa upande wa pili wa zile hisia mbili ziwezazo kuta-athari kutokana na kujiuliza mtu juu ya KUFA - ikiwa utapata woga mara tu baada ya kujisikizisha binafsi yako, basi itaonyesha wazi kua iko tamaa kwako kurejea kwa Mola wako na kuiacha dunia na ghururi zake, kwani hiyo ni dalili ya kuipa nyongo. Bwana Mtume S.A.W amesema: "Iz- had fid - dunya yuhbibkal llah" "Ipe nyongo dunia atakupenda Mnyezi Mungu". "waz - had ma - fin nas yuhbibkan - na-s". "Na yape nyongo yalo na watu watakupenda watu". Na hii huenda ikawa ni kumbusho kwako, toka kwa Mola wako basi, fanza haraka kwani, huenda hiyo ikawa ndo nafasi yako ya pekee na sio rahisi kwa nafasi kumjia mtu mara mbili (opportunity never comes twice and misfortune never comes single). Kwa yote hayo, yafikirie mauti vipi yanavyomuhujumu mtu, iweje wewe kughafilika nayo? Bwana Mtume SAW anasema: "Hayakumbuki mtu mauti illa atazidisha mambo mema, na atapunguza maasi" Kwa hivyo, kwa muumini kuyakumbuka mauti ni ibada kubwa sana. 6.

Na ambae anajitia hamnazo, akidhani kua atayakwepa au atayakimbia, basi Mnyezi Mungu anatwambia na kutukumbusha katika: Qur an: Suratil Juma - a: 62:8.

"Sema: Hakika mauti haya mnayoyakikimbia bila shaka yatakutana nanyi kisha mtarudishwa kwa mjuzi wa siri na dhahiri hapo atakujulisheni yote mliyokuwa mkiyatenda". Basi katika aya ambazo ni za kumkatisha tamaa yule adhaniae kua atadumu hapo duniani kwa ujanja wake akifaulu kuyakimbia mauti ni hayo na juu ya hivyo Mnyezi Mungu hapendi desturi ya kukata tamaa kwani hiyo ni tabia ya makafiri. yeye humpendelea mja wake matumaini ya hakika. kwa hivyo Bwana Mtume SAW ametufundisha njia nzuri ya kuishi nayo ni kama hii; njia nzuri ya kuishi kwa sababu dunia inatubidi na akhera pia inatubidi ni hii: "Jishughulishe na dunia kama kwamba utaishi milele na ujishughulishe na akhera kama kwamba utakufa kesho". Na vile vile amesema: "Hakua mbora wenu ambae anaacha dunia kwa ajili ya akhera yake, wala yule mwenye kuacha akhera kwa ajili ya dunia yake, bali mbora wenu ni yule mwenye kushikamana na vyote hivyo kwani dunia ndio kiwasilisho cha akhera''.

7.

UNDANI WA NGOME YA KWANZA.

Yaqini:

Qur an: Waqia: 56:81 ­ 96.

"Je! Mnabeza hadithi hii? (Mnayapuuza yaliyo katika kitabu hiki?)".

"Na mnafanya kuikadhibisha ndiyo (shukrani ya) pato lenu (alilokuruzukuni?)"

"Basi mbona (roho) ifikapo kooni, na nyinyi wakati ule mnatizama".

"Nasi tunakaribiana naye zaidi (huyo anayetoka raho) kuliko nyinyi, wala nyinyi hamuoni. Kama nyinyi hamuoni katika mamlaka (yangu)"

8.

"Kwa nini hamuirudishi (hiyo Roho) ikiwa mnasema kweli (kua hamumo katika mamlaka yangu)".

"Basi akiwa (mtu huyo anayekufa) ni miungoni mwa wale walio karibishwa (na Mnyezi Mungu) basi ni raha (kubwa) na manukato (mazuri) na mabustani yenye neema (zinamngojea)".

"Na kama akiwa ni miungoni mwa watu wa kheri. Basi ataambiwa. Ni salama kwako (daima) (uliye) miungoni mwa watu wa kheri".

"Na kama akiwa ni miungoni mwa waliokadhibisha, wapotofu (wapotevu), basi karamu (yake) ni maji ya moto yachemkayo na kuwaka motoni".

"Bila shaka hii ndiyo haki yenye yakin (yaqini) Basi litukuze jina la Mola wako mwenye Utukufu". Tumeanza kufahamisha undani wa Yakini (Yaqini) kwa kunasibisha hakika yake kwa kuopoa baadhi ya aya ziliopo mwisho wa Suratil Waqiah (56) katika fungu la Qur an, kuanzia aya ya 81 hadi 96, ambazo zina utajo mzuri juu ya neno hilo ­ Yaqini ­ Zipo sehemu, nyinginewe ndani ya kitabu hicho ambako pia, limetajwa si hasha. Kwa upande mwingine Yakini (Yaqini) hua na maana ya kifo hakika yake imeelezewa mwisho wa Sura Al-Hijr 15: 99. pale inaposema. 9.

Qur an:Al Hijr: 15:99.

"Na Umuabudu Mola wako mpaka ikufikie hiyo yakini (Yaqini) (nayo ni mauti)". Katika maelezo tu, tulionyesha huko nyuma (kwenye ukurasa wa 18 ya ­ MAANA HALISI YA IMAAN ­ I). Vipi yakini (Yaqini) ilivyo sadifu (ilivyotokea) kua ngome ya nguvu kabbisa. Na ni kama hivi imekuwa ndo Usu-l, nyanja ya Imaani, na Amal ni matawi yake. Pia tulionyesha kua Yakini (Yaqini) ni Imaani yote kutokana na hadithi ya Bwana Mtume SAW. Lakini yote hayo sio undani wake. Kufahamu undani wa Yakini (Yaqini) kuna tutupia miangaza yake kutoka hadithi ya Bwana Mtume SAW isemayo:"Hakika ndani ya mwili mna pande la damu, Likitengemaa hilo kimetengemaa kiwiliwili kizima, na likiharibika hilo umeharibika mwili mzima. Haitoshi kua ni Moyo (kitu hicho?). Tafsiri ya maneno hayo ya Bwana Mtume SAW. Yaani ufafanuzi wake na uchambuzi, kwa kadiri ya maarifa yetu kwani katika kufanya hivyo walipatikana Mujitahidina, zikapatikana fikra za Maimamu na Masheikh tangu zamani had leo hii, lau milango ya Jitihadi imeedhoofika), ni kama huu:

1. NDANI YA MOYO:

Yakini (Yaqini) tuizungumziayo undani wake imo ndani ya kichambuliwa hicho "Ndani ya Moyo". Ni yenye kuonyesha wazi ya kuwa hapo ni mahala pa maana sana. Kadhalika humo humo ndani ya Moyo mna chungu ya mambo muhimu ambayo ujuzi wetu juu yake ni wa juu juu tu: i) Roho na stesheni (Markazi) ya ii) Nafsi. iii) Akili na kituo cha hisia (Asasi). iv) Nguvu ya Fikra na Maono ya ajabu, v) Nguvu ya kutamka. vi) Ubinaadamu. 10.

Kwa vile kuna mkusanyiko wa mawazo mabaya, Chuki, Mapenzi, Husda, Tamaa na Unyimi, Ubakhili na kadhalika Sukhaa, na Ndimo alimoweka Imaani, Yeye Mnyezi Mungu. Jumla ya mambo yote hayo yamo ndani ya Moyo, na takriban yote ni maalumu kwako, hakuna lililo geni kwako hata moja. Lakini hebu jiulize Nafsi yako katika Aya mbili hizi zifwatazo, ili ujitazame kama dai lako katika kuyajua mambo yote tuliyochambua hapo nyuma, ni kweli au babaisha tu?. Qur an: Ar-Rahman: 55:14.

"Amemuumba Mtu kwa udongo wa Mfinyanzi (Utoao sauti) kama vyombo vya udongo". Qur an: Suratil Twa-riq: 86:5 ­ 7.

"Hebu na ajitazame Mtu ameumbwa kwa kitu gani? Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa (Yatokayo katikati ya mifupa ya mgongo na kifua".

Ufumbuzi: Ikiwa jawabu lako ni kutokana na aya ya kwanza, basi bado kujijua Nafsi yako, na ikiwa jibu lako ni kutokana na aya ya pili, basi maana ni sawa. Kwa nini iwe hivyo? Kwa sababu, Mtu ambaye ametajwa katika aya ya awali Ni baba yetu Naby Adam Asw, ambaye ndiye pekee wa kwanza kuumbwa moja kwa moja, (Directly). kutokana na udongo. Wa pili, kufuatia alikuwa mkewe, ambaye katika masalia ya udongo ule ule aliumbwa yeye (Mama Hawwa). Na wa tatu, lakini katika njia ambayo iliwashangaza watu tangu siku hizo hadi leo, ni Naby Isa As ambaye Mnyezi Mungu Muumba alitwambia jinsi alivyowaumba wote wawili ni mfumo mmoja tu: Qur an: A`al Imran: 3:59. 11.

"Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam: Alimuumba kwa udongo kisha akamwambia "kuwa" basi "Akawa". Lakini: Waliobaki wote (katika jamii ya Mtu) ni walioumbwa kutokana na maajabu ya Aya ya pili - "Tumeumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa" (yakitoka bila mchupo pana mashaka kuwa ni yenyewe, au kuwa ni mazima) ­ Bila ya shaka yeyote hayo ni manii ( Mbegu ya uzazi). Wana Sayansi wamechunguza na kugundua ndani ya hiyo mbegu ya uzazi wako wadudu wa uhai - Waitwao Amoeba (Amiba) ambao hawana umbo maalumu, kwa hivyo siyo rahisi kuchoreka. Vidudu hivyo visivyoweza kuonekana kwa macho matupu ni vyenye kubadilika umbo hadi umbo kila dakika huku vikiongezeka idadi yake mpaka kufikia kujenga umbo kamili. Qur an: Al Muminuun: 23:13 - 14.

"Kisha tukamuumba kwa tone la manii (mbegu ya uzazi) lililowekwa katika makao yaliyohifadhika kisha tukalifanya tone hilo kuwa pande la damu.........." Upo ushahidi mzuri wa kuweka mkazo juu ya hakika hiyo ndani ya:

Qur an: Al-furqa-n:25 : 54.

12.

"Naye ndie aliyemuumba Mwanadamu kwa maji, kisha akamfanyia nasabu (ya damu) na ujamaa wa ndoa, Na Mola wako ni mwenye uwezo (wa kila jambo)". Basi, ukizingatia ufafanuzi mfupi kama huu kuhusu majibu yako katika aya mbili hizo: "Ameumba mtu kwa udongo wa ufinyazi (utoao sauti) kama vyombo vya udongo". (Ar-Rahman 55:14). Na "Hebu na ajitazame Mtu ameumbwa kwa kitu gani? ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa, yatokayo katikati ya mifupi ya mgongo na kifua". (Twa-riq: 86: 5-7) Hutakosa, kuona ya kwamba kwa njia moja (direct) au nyengine (indirect) vijidudu hivyo (amoeba) ambavyo hupatikana: a. Mwenye Udongo wa maziwa ya maji, na b. Mwenye manii (mbegu ya uzazi) ni vyenye kuingia huku (kwenye umbo la mtu wa kwanza) na huku (kwenye umbo la mtu wa pili mfano wako wewe na mimi). Kiasi ambacho mwenye akili hawezi kupata taabu ya kusarifu mambo ya ajabu ya muumba: ambayo yametapakaa mno, sio kwetu tu (kama alivyosema Mnyezi Mungu katika: Qur an: Suratil Rom: 30 : 20.

"Na katika ishara zake za kuonyesha uwezo wake ni huku kukuumbeni kwa udongo, kisha mumekuwa watu mnaonea (kila mahala)". Na kama vile ilivyo kwenye: Qur an: Dh-dha riyat: 51 : 21. 13.

"Na katika nafsi zenu (pia zimo alama yaani zenye maajabu ya mambo ) je hamuoni?". Bali ajabu hizo zimetapakaa kila mahali katika ujudi, mfano wa Mbingu, Sayari, Upepo, Hewa, Milima ambayo utadhani imesimama, lakini ni yenye kuzunguka na hali kadhalika. Na yote hayo yalomuhusu Mtu na mtoto mtu, yamo ndani ya kichambuliwa, Moyo jee haikustajabishi? Katika undani wa yakini (yaqini) Moyo ni chombo muhimu chenye kuendesha uhai na maslahi ya maisha yetu hapa ulimwenguni na ndo maana Bwana Mtume SAW akasema kwa mkazo sana juu yake;

"...Likitengemaa kimetengemaa kiwiliwili kizima....."

KUWEMO NDANI YA KICHAMBUO - MOYO:

kumbuka tena kwa mazingatio ya hali juu kabbisa sio vile ulivyozoea tu, laa, haitoshi kwani suala hilo ni lenye kukuhusu wewe suala, hilo ni la kukutayarisha wewe kuipokea na kuisarifu vile ipasavyo - Amana (Toka kwa Mnyezi Mungu - ukiwa ni Muislam au si Muislam). Basi pengine huenda baada ya kwisha pata fununu yake ukaona ya kua ulipoteza muda mrefu ukijifanyia mambo ambayo sivyo kabbisa, Huenda wewe mwenyewe ukatwaa uamuzi mpya kuanza upya. Na tuanze na Aya ifuatayo ambayo iko katika: Qur an: Suratul Fus-swilat: 41 : 53.

1.

"Tutawaonyesha (ukweli wa) maneno yetu haya katika nchi za mbali, na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainike kwamba haya ni kweli. je! Haitoshi kwa 14.

Mola wako kua yeye ni mjuzi wa kila kitu?". Na tuangalie: Qur an Al Haj: 22:46.

2.

"Je hawatembei katika ardhi ili wapate nyoyo, (akili) za kufahamia, au masikio ya kusikilia? Kwa hakika Macho hayapofuki (yakadhuru katika dini), lakini nyoyo ambazo zimo vifuani ndizo zinazopofuka (zikadhuru katika dini)".

3. 4.

Qur an: 51:21.

"Na katika Nafsi zenu (pia zimo alama hizo, yaani: zenye maajabu ya Muumba) je hamuoni?".

Utaona ipo tofauti zaidi na zaidi juu ya neno Nafsi kwa maana yake jinsi ilivyotumika hapo, na jinsi ilivyotumika katika Suratil Fusillat 41:53. Tutazame katika Aya hiyo ya: Qur an: Bani Israel - 17 : 36.

15.

4.

"Wala usifuate (ukipita ukisema au kuyafanya) usiyo na Ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na Moyo, hivyo vyote vitaulizwa".

Tupate kuzingatia mapema mapema suala la Moyo huo. Tuangalie katika: Qur an: Suratin Nnass: 114:1 - 6.

5.

"Sema najikinga kwa Bwana mwenye kuwalea, Mfalme wa watu muabudiwa wa watu, na shari ya mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma, atiaye wasiwasi nyoyoni mwa watu (ambaye ni) katika majini na watu".

Nini muradi wa Mnyezi Mungu kwa mkusanyiko wa kauli zote hizo kutoka katika Sura mbali mbali? Naam, mkusanyiko wa aya zote hizo na nyingi mfano wa hizo, zimekusudiwa huo Moyo ili utayarishike sawa sawa katika yakini (yaqini); na lengo lake ni kumtambua Mnyezi Mungu mmoja. Na huko ndiko kumuabudu. Kuabudu au Ibada ni neno ambalo waarabu haliwapi taabu, lakini kwa kiswahili unaposema kuabudu ni kuabudu, au kufanza ibada inakua bado hatujafasiri kitu, na pengine huenda tukakwama tukilifasiri kua ni kuswali au kumuomba Mnyezi Mungu. Wakati tukiulizwa juu ya mfano wa ndugu zetu Mabaniyani wanapolikabili jua saa likichomoza, hua wanafanza nini?. Kuabudu ni kutambua, tena kwa yakini (yaqini) kua Mnyezi Mungu ni mwenye kupatikana na ni ambae Hapasi kuabudiwa kwa yakini (yaqini) Asiye kuwa yeye. Na sasa tunaanza na ufafanuzi ambao, Inshallah utatufikisha katika kudhihirikiwa kua huo Moyo sio ni wewe tu, bali ndio Nafsi 16.

yako, Roho, Akili na Mnyama alo muovu kupita wote ulimwenguni! Na yote hayo yamo ndani ya Qur ani, na kukubalika akilini.

UFAFANUZI JUU YA MOYO:

Wamehitalifiana Maulamaa katika hakika yake, kua, ni kitu gani? Madaktari wanaamini kua Moyo ni ule ulioko ndani ya kifua kwa upande wa kushoto kidogo, ambao hupiga vishindo vyake kama vile saa na hasa baada ya kukimbia masafa marefu au kufanza kazi ya harubu ndipo vishindo vyake vinapozidi, Saa hio hua inasukuma damu kwa kasi sana (speedy blood circulation-BP ). kwa hivyo hakika yake ni pande la nyama lenye matundu ndani kwa ndani ambamo hupitia damu chafu na safi. Shughuli zake katika kudumisha uhai wa kiumbe, (mtu) ni kubwa sana kwani, lau utasimama falau kwa dakika chache tu, basi kiumbe ni budi afe. Pengine maiti angepasuliwa ukatolewa Moyo wake kwa ajili ya utafiti ili kuelewa sababu ya kifo cha marehemu, nae (maiti) akazikwa bila moyo wake ndani ya kiwiliwili. Moyo ulodhibiti chungu ya ilimu na maarifa mbalimbali na nguvu za kuinua uzito, umesababisha mwili kuanguka kama gogo halina kazi tena, je huyo maiti atajibu vipi maswali ya malaika kaburini hali ya kuwa moyo wake umeachwa Hospitali kwa uchunguzi?. Ndani ya moyo m na mishipa ya hisi ambayo imekamatana na hisia zote Tano za akili ili kusaidiana katika kutambua vyenye kumkini kutambulika. Na iko sababu maalum kwa kusema vyenye kumkini kutambulika; Kwani katika upande wa ladha, mathalani akili haiwezi kutambua zaidi: i. Tamu. ii. Chungu. iii. Chachu - gwadu iv. Kali na v. ya chumvi Viongozi wa Dini (hasa Islamu) wamechunguza (Tazama mfano wa Imaam Ghazzali katika kitabu chake "Ahya-u iii" katika habari za Moyo ) na wengine mfano wa Seyyid Ahmad Bin Abubakkar Bin Sumeyt katika kitabu chake "Min Hal" ambapo 17.

hawakuhitilafiana sana katika jitihada zao: wao wameona mbali zaidi ya madaktari: Kwanza: Wameona kua katika kiwiliwili kizima hakuna ambako panamvutia na kumuhimu mno Mnyezi Mungu kama hapo, na kwa sababu gani mpaka iwe hivyo? Kwa sababu: Ndo mahala pekee anapopatizama Mnyezi Mungu, Hadithi inathibitisha hayo: "Mnyezi Mungu hatizami sura zenu wala mali na watoto wenu. Lakini Mnyezi Mungu anatizama nyoyo zenu na matendo yenu". Mnyezi Mungu anaupitia moyo wa kila mtu mara 360 kila siku. Na ukiwa mtu wa akili na mazingatio utaona kua inastahili iwe hivyo ushirikiano ulioko baina ya Moyo, Akili na Roho, ndani ya mwili wa mtu wa ajabu. Na hasa inapofikia Roho kutaka kuueleza moyo ambao ndani yake ndo kwenye Nuru ya Akili kutaka kuelezea juu ya Siri ya uhai. Pili: Ndio utaulizwa (mas-uwl) na Mnyezi Mungu, kama ilivyoonyesha hapo nyuma katika aya namba 4 katika sura ya 17 aya ya 36 (Bani Israel). Ikiwa hiyo ndo hakika ya mambo yatavyokwenda, mtu ungeweza kufikiria njia yake mwenyewe jinsi vile ungejibu suala la kuulizwa ambae alizikwa bila moyo wake ndani ya kiwiliwili. Tatu: Ndio utaoonja Raha au Mateso hiyo siku ya hesabu. Nne: Ndio wenye Nuru ndani yake ambayo kwayo mtu husarifu chungu ya mambo muhimu. Kwayo (hiyo akili) Mtu hua mukalif (mkalifiwa au mbidiwa na jukumu la sharia (Islam). Aya nambari 2 ambayo imenukuru Surat Hajj 22: 46 inahusika. Angalia kwa makini jinsi gani Mnyezi Mungu amejaalia huo huo Moyo kua na akili ndani yake. Hii ni fununu tu kwako, basi ikiwa ni yenye kulingana na kupewa funguo mikononi, juu yako ni kufungua kila unapopataka Wewe!. Tano: Ndio ambao huwekwa (na mwenyewe Mnyezi Mungu) Imaani ndani yake, na ikiwa ndio hivyo basi mfano wa waumini wa dini mbalimbali ni wenye kututosha. 18.

Sita: Ndio mahala ambapo huanza habari zote mpya mpya na zile ambazo Mtu anataka zitekelezwe na kiwiliwili. Na ni katika hakika hii ambapo Moyo umenasibishwa na Arshi ya Mnyezi Mungu. Basi ikiwa matakwa yenyewe ni mfano wa kuswali au kufunga, kumtusi mtu, kufanza nini na nini. Ukweli ni kwamba viungo havina shauri ila kufwata tu yanayoamriwa utafikiri Malaika (na hiyo ndo sehemu ya maana ya Uislamu) ukitupa uzito wa fikra juu ya tahkiki hizo utaona haimkiniki kua Moyo huo ndio uliotolewa na daktari, ambao, vyovyote itakavyokua, mwisho wake utarudi kuwa mchanga. Ni yenye kueleweka ya kua kila ambacho ni sehemu ya ardhi hatimae kitarudi ardhini. Ni kwa sababu hiyo ndipo pumu ilipopata mkohozi, kwa upande wa makafiri (na mfano wa wenye fikra ndogo kama wao) walipo kiwauliza Mitume masuala ambayo Qur ani imeyadhibiti kama hivi: Qur an: Al-waqiah: 56 : 47.

"Tutakapokufa na tukawa udondo na mifupa tutafufuliwa? (Ni uwongo huo)". Katika jumla ya mkusanyiko wa Mtu, Udongo toka ardhini unachukua sehemu kubwa, na baada ya kufa Mtu, sehemu hiyo inarudi ardhini pia, Ardhi ni kiumbe (Tumeelezea hakika hiyo katika kitabu chetu "El Makhluq"). Na tumesoma au tumeshapata kusikia jinsi vile Bwana Mtume SAW alivyoiona katika Sura ya msichana kwanza, na Sura ya Aju-z (mwanamke mzee) Mara ya pili. ikiwa ni miungoni mwa ajabu aloonyeshwa usiku wa Miraji. Kwa hivyo, moyo ulotolewa na daktari kwa ajili ya utafiti utakuemo ndani ya Aju-z (mwanaamke mzee) huyo Yawmul Qiyama. Kwa mwenye kufikiri mbali ataona hakuna sababu kwa Mnyezi Mungu kuuliza Moyo wakati mioyo yote itakuwemo ndani ya Bi Dunia; Angeiulizwa Dunia tu badala yake. kila jambo alilosema Mnyezi Mungu (mfano wa kuulizwa masikio, na macho na moyo, kulikoelezewa ­ lau si hapo tu peke yake katika Qur an mzima, Katika Bani Israel 17:36) Lazima likubaliane na akili, aghlabu, Na angaa itatumika miujiza tu juu yake au ndani ya jambo lenyewe ­ lakini Akili lazima ikubali. Mfano wa uwezo wa Mnyezi Mungu katika kufanza atakalo baina 19.

ya "Kafu" na "Nuni" tu, yaani ­ "Kun Fayaku-n", angeweza bila shaka yeyote kumtumbukiza Mtu mzima mzima ndani ya moyo mdogo kama ule ulotolewa na Daktari; na kwamba siku ya kiyama akamtoa tena Mtu yule yule toka kwenye mchanga (Bi Dunia) lakini Hajaagiza hivyo. sio rahisi aende kinyume na alivyokwishapanga. Qur an: Surat Fa-tir: 35 : 43. ..... "....Wala hutapata mabadiliko katika kawaida ya Mwenyezi Mungu". (Na kadhalika hutapata kuona zikihama ­ kawaida hiyo ni tangu zamani imetangulia kuwepo kwake). Na kama ndo hivyo, kwamba mambo yake Mnyezi Mungu hayawezi kubadilika badilika ovyo ovyo tu, basi - Moyo lazima uwe na sura nyengine zaidi ya ile tuliyoizoea, haijakudhihirikia tu, kua, huu Moyo, nini hukmu yake?.

MOYO NI WEWE:

Bila shaka yeyote Akili inakubali bila upinzani wowote na ingawaje Mtu amekipita kila kitu kwa ubishi, kwamba ikiwa (ni Moyo) ndo unaotamka. ndio wenye Imaani na Uislam, ndo Unofikiria, ndo Unaoamrisha mpaka matendo yakafanzika, ndo utaoonja raha na kumiliki yote miongoni mwa neema na fadhila kubwa zilizoahidiwa kupewa, mfano wa isemayo aya hii katika Qur an: Wa-qian: 56 : 22-24.

"Na wanawake wenye macho mazuri na makubwa (ya vikombe) (wanapendeza na safi) Kama kwamba ni lulu zilizofichwa (katika machaza yake ndio kwanza zinapasuliwa), ni jaza ya hayo waliyokua wakiyatenda". Ikiwa ndo hivyo basi, ni kweli na yakini (kua ndio mimi ndie yeye). 20.

UFAFANUZI WA ROHO:

"War ru-h maa-akhbara an-hal mujtaba fanumsikul maqala an-ha adaba" "Na Roho hakuielezea juu yake mteule mtegemewa (Bwana Mtume SAW kwa hivyo ni uzuri ) kujizuia kusema chochote juu yake, Kwa ajili ya kurai adabu!!". Na falau Mnyezi Mungu amesema kua ametupa ujuzi kidogo juu yake. "Na wanakuuliza habari ya Roho. sema: "Roho ni Jambo lililokhusika na Mola wangu (Mnyezi Mungu) Nanyi hamkupewa katika (ujuzi) ila kidogo kabisa. (Nayo ni ilmu ya vitu visivyokhusika na roho)". Na juu ya kufunuliwa kiduchu tu, ambacho sio hasa hasa kihusikacho na Roho yenyewe, mtu amefanza ya kushangaza kabisa jee? ingekuwa kiduchu hiyo hiyo ni juu ya Roho halisi labda ungefikia kusema ulamaa hawangekufa. Wazoefu juu ya mambo ya kiroho (practical spiritual Experts) nao hufanza mambo mengi ya kiajabu ajabu kiasi cha kushindwa mtu wa kawaida kuyabeba ndani ya Tasdike (kukubali). Kwa upande mwengine tuangalie mfano wa Mwanachupa (The taste tube baby) mtu amefikia hadi hio ya kutoa mtoto bila kupitia njia yake ya ada (bil kul sio kwamba wao wameumba laabali ni kwamba wamijitahidi katika kufanzia majaribio chungu ya aya mbazo Mnyezi Mungu Mtukufu ameonyesha waziwazi jinsi vile anavyotoa mtoto kutokana na tone la manii kama ndani ya kitabu hiki (Tulivyokwisha elezea huko nyuma tukanukuru aya ya 13-14 ya Surat ya 23 Al Muuminun). Na pia katika Surat Zumar 39:6. "Amekuumbeni katika nafsi moja kisha akamfanya mwenzie (mkewe) katika jinsi ile ile, na akakuteremshieni (akakuumbieni) wanyama wanane (hawa wenye nafuu kubwa kwenu) madume na majike. (Ngamia, Ng'ombe, kondoo na mbuzi) ( Huumba) hukuumbeni matumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo - katika viza vitatu huyu ndie Mnyezi Mugu wenu: ufalme ni wake hakuna 21.

aabudiwaye kwa haki illa yeye basi nyinyi mnageuzwa -wapi?"

PANDE LA DAMU:

wakati Bwana Mtume SAW alipojulisha juu ya hilo pande la damu, bila ya shaka yeyote alimaanisha Roho - kwani hiyo damu chafu ndio chanzo cha Roho (Man-bair-ruh) Na huenda kiwiliwili kizima mfano wa Nuru ya taa inavyozagaa katika chumba. Si rahisi kuashiria kwa mkato nuru-iko sehemu gani khususi, ndani ya chumba hicho. Hiyo Roho iliumbwa zamani, kabla ya kiwiliwili, haipungui miaka alfu nne kabla; ila miaka yote hiyo huenda ukashangazwa kuona kua ni makadirio ya siku nne mbele za Muumba Sub-hana wa Taala. Hiyo, katika kutafutiana, na kutofanana na yeyote amenasibisha siku yake moja kwa hisabu zetu za hapa duniani ni, kadiri ya miaka Alfu moja; imeonyeshwa katika: Qur an: Surat As-sajada: 32 : 5.

"Anapitisha mambo yote yaliyo baina ya mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku moja tu ambayo kipimo chake ni miaka elfu mnayotumia nyinyi katika kuhisabu kwenu" Na katika makadirio hayo Mnyezi Mungu alitangulia kuumba Riziki na akaitanguliza hapa duniani ambako alikwisha panga kumleta khalifa (Viceregent) kama ilivyo katika: Qur an: Sura ya 41:10.

22.

"Na akaweka humo milima juu yake (ya uso wake), na Akabariki humo na akakadiria humo chakula chake (cha kuwatosha watakao kaa humo, amefanya haya) katika siku nne, (mida mine). Haya ni sawa kabisa kwa hao wanaouliza (mambo wakataka kuyajua)". Hiyo Roho, Maulamaa wengine wanakubali kuwa ndiyo Nafsi na baadhi yao wanakubali kuwa ni sehemu ya Roho iliyojitenga siku ilipoumbwa. Na ni kutokana na tendo hilo ndipo ilihutubiwa kwa jina la Nafsi. Roho imeshikana na Moyo, (lau siyo Moyo ule uliotolewa na Daktari) wa Mtu katika kiwiliwili chepesi ambacho ndiyo hakika ya Mtu mwenyewe. Siyo mwili wenye manyama ambao Asili yake ni udongo huu huu wa ardhini. Katika kuufahamu undani wa yakini (yaqini) ni jambo la busara kuzingatia suala la Moyo ambao ni: Kiwiliwili chepesi chenye Roho ya Mola, ambacho ndani yake lipo hilo pande la Damu ambalo ni chanzo cha Roho ikiwa humo ndani ya Moyo ndio ilikoanzia. Katika Moyo wa Roho, na Moyo wa kawaida pana uhusiano fulani ambao kwa ajili ya kurai adabu, ingekuwa bora kutokuingilia suala lake.

UFAFANUZI WA AKILI

Kila mwenye Akili hakosi kua na fununu ya kitu ambacho kimeweza kumpambanua yeye na Mnyama ni nini? Ni Akili. Taba-an lakini wakati ukiulizwa "Iko wapi hiyo akili?" Huenda ukajibu iko kichwani utafikiri labda unajua kua yule "Mwenda wazimu" kichwani mwake hakuna kitu, au imepungua kidogo. Na imekwenda wapi? Au wakati ametibiwa na kupona na huwa imeingia kutoka wapi? Je mtoto mchanga, mdogo na kijana wa miaka kumi na mbili utaeleza nini juu ya akili zao? Ikiwa mtoto mchanga ni hana akili basi labda atakua kama mwenda wazimu?. Hayo yote ndio miungoni mwa harakati za kutafuta jibu halisi; lakini bila shaka umeanza kulitilia wasi wasi jibu la kuemo akili 23.

ndani ya kichwa. Akili imo ndani ya Moyo, na ndo Johari yake hasa. Akili ni kitu azizi sana, ambacho Mnyezi Mungu humuhukumu mja wake kwa kadiri ya akili yake. Na ambae hanayo basi hua hana hukumu yeyote juu yake. Na hapo ndo mfano wa mwenda wazimu na mtoto unapovutika. Wa kwanza (mwenda wazimu) mas-ala yake yanajulikana; kwani kuhisabiwa kwake ni kabla ya kupata ugonjwa huo. Amma mtoto atahesabiwa kuanzia miaka 9 hadi 15. miaka tisa, kama ametokewa na manii katika umri huo au hadi kufikia miaka kumi na mitano. Kuhusu kukua kwa akili ya mtoto kila miaka inapomsogea mbele sio rahisi kuelezea, lakini ukweli ni kwamba inasaidiana na Ubongo. wa mbele ya kichwa (ambao wanasayansi wanauita ­ Cerebrium) na pia kusaidiana na ubongo wa katikati ya kichwa (Cerebellum) na ule wa uchogoni (medula oblongata). Na huzidi na kupungua. Amma kuzidi kwake ni kwa kadri ya majaribio (Experimentations), na pia kwa kusoma Qur an kama alivyosema Bwana Mtume SAW.

UISLAMU NDANI YA AKILI:

Mnyezi Mungu alipoiumba Akili aliiamrisha kugeuka nyuma (mfano wa askari kwenye mafunzo-about-turrn, Right-turrn- nyuma geuka, kulia geuka, na kadhalika) ikageuka - Mnyezi Mungu alifurahikiwa nayo na kusema: "Sikuumba baada ya Mohamad (Nuru yake) Kitu bora kuliko wewe, na sitakuweka ila kwa wale wenye kupendeza sana mbele zangu". Na ni kutokana na sababu hiyo leo kila mwenye akili hupendwa sana na watu. Kitendo cha Akili katika Utu wake mbele ya Mnyezi Mungu, kwa mujibu wa misingi ya uislamu (principales of Islam) ni chenye kuonyesha Uislamu. Kwa hivyo kila mwenye akili hatokosa kuwa mnyenyekevu. Hatokosa kua mwenye kumuogopa Mnyezi Mungu, nako ni kufwata maamrisho yake. Mpaka sasa hakuna alielezea Akili ni kitu gani hasa na juu ya kuzidisha uchunguzi juu yake. Wana Elimu ya viumbe (Biologists) 24.

baada ya jitihada hizi na hizi katika kutafuta hakika ya akili wameandika hivi (katika kitabu "Exploring Biology"): "We know from Experimentation that the cerebrum is the centre of intelligence, but we DO NOT as yet KNOW just what intelligence is. ONE great advance step we have made is in discovaring that consciousness and intelligence are centred in th cerebrum. Intelligence is a function of the cerebrum just as life is a function of Protoplasm". Maana yake: "Tuna jua kutokana na majaribio tulokwisha yafanza, kua cerebrum (sehemu moja katika tatu, ya ubongo) ni ilioko katikati ya akili (ni kitovu cha akili yote ) lakini bado hatujafikia kujua hiyo akili ni kitu gani. Hatua moja kubwa tulioipiga katika maendeleo ni iliopo katika kugundua ya kwamba akili mahiri (tambuzi) na hio akili yenyewe ni ziliopo kati kati ya cerebrum. Akili ikiwa matenda kazi yake ni yenye kutokana na hio cerebrum, kama ilivyo kua uhai kua matenda kazi yake ni yenye kutokana na misingi (ya tabiya) ute (wa uhai)". Basi kutokana na kushirikiana pamoja (Nuru ya akili ilioko ndani ya Moyo) (na Bongo zote tatu zilizoko kichwani) ndipo mtu anapomudu kuswarifu mambo sawa sawa. Amma ikizimika Nuru ya akili Ubongo peke yake haumudu kufanza kazi zote pekee. Kwani huonekana mtu ni mwenda wazimu, na kusamehewa mambo mengi juu yake. Ni hiyo akili kutokana na kua kwake kitu cha ajabu, angalia jinsi tunavyo weza kujua na kusarifu mambo hata mingha-iri ya kuyaona kwa macho, katika hali kama hizi, mathalan: 1. Maji yamiminikao chini toka nyumba ya tatu ambayo ina kuku pia. 2. Nyama ya mbuzi inachomwa jirani yako; na nguru jirani yako mwingine, na kuunguliwa na nguo toka kwa jirani yako wa mbele. 3. Uko mbele ya umati lakini katikati ya mgongo wako yuko chawa au ndorobo. 25.

Akisema Bwana Mtume SAW: "Usimlilie aliekufa, mlilie aliepungua akili yake. Basi kwa kadiri ya upungufu katika hisia tano, Ndipo pia mazingatio ya upungufu wa akili yake kwa jumla. Hisi zote tano hushindwa kufanya kazi kama mtu akilala usingizi. Kila kitu kina sifa, na akili nayo ina sifa zake. Katika hadithi iliopokelewa kwa Bi Aisha (R.a) hakika amesema Bwana Mtume SAW: "Akili inayo sehemu kumi, kati ya hizo zimegawanyika ndani ya mafungu mawili:1. Dhwa-hiri na 2. Ba-tini. Sifa tano zilizomo ndani ya kundi la: Dhwa-hiri ni hizi:1. Samt. Yaani ukimya kwani amesema Bwana Mtume SAW: "Mwenye kuzidisha maneno yake huzidi kuanguka (kuporomoka) kwake"(Speech is silver silence is gold) kusema sema ni fedha, kunyamaza ni dhahabu. 2. Hilm: Upole. 3. Tawa-dhui: Unyenyekevu ikiwa ni ile hali ya kujitupa chini na hata kama Mnyezi Mungu amekufanza mfalme, kwani hapo ndipo hasa pahala pake, kasema Bwana Mtume SAW:"Mwenye kujiweka chini, Mnyezi Mungu humrufaisha (Humnyanyua, Humpandisha cheo juu)". 4. Kuamrisha mema na kukataza maovu: Maana yake ni dha-hiri kabisa kwani kilicho toa ubora kwa Umat Muhammad SAW mbele za Mnyazi Mungu ni sifa hiyo. 5. Amal swa-lih: Kuwa na amal njema ipendeleayo kheri kila mara.

Sifa tano za Ba-tin:6. Tafakkur: Hali ya kufikiri fikra hasa mambo mengi mengi tu ya ajabu, ambayo Mnyezi Mungu ameyaumba, 26.

mfano wa mbingu, Ardhi na kadhalika. Bwana Mtume SAW alikua mtu wa kufikiri mno, hasa juu ya jamaa zake na yale waliokua wakiyafanya ambayo yalikua ni ya kinyume badala ya Insania. Sayyidna Ibrahim ASW nae alikua na khulka kama hiyo ya Bwana Mtume SAW katika upande wa tafakur kujadiliana na baba yake juu ya kuyatambua masanamu kua miungu, halikua jambo la sawa kwa mzazi. 7. Ibra: katika maajabu mazito ya Akili sifa hii ni yenye kutia fora, kwa kua katika maisha yao huenda wenye akili ndogo wakakuelewa vibaya kukutabiri ambavyo sivyo ulivyo. 8. Khofu: kumkhofu Mnyezi Mungu peke yake. Kumkhofu zaidi, ambaye hamkhofu Mnyezi Mungu - Kwani haachi kutomuogopa Mnyezi Mungu ila mwenda wazimu, na asiemuogopa mwenda wazimu, basi ipo hatari kua yeye ni zaidi. 9. Kuyaadhimisha madhambi; Uyaone kua ni mazito, sio kila dhambi ni gunia la sufi. Kumbuka, Moto mkumbwa usababishwavyo kutokana na cheche ndogo ya moto. 10. Kuidhalilisha Nafsi: Nafsi kila siku inataka makuu na kutambuliwa na wewe kua inayo haki kwako. Ni kama vitimbi vya mtoto pale nyumbani na hasa anapokuwepo mgeni. Na kama iliyo maalumu, Nafsi ukiitukuza basi lazima itakuliza, kwani daima haikutizamii ya maslaha kwako abadan. Kwa kifupi mwenye akili hua na mfano wa sifa hizo.

UFAFANUZI JUU YA NAFSI:

Mnyezi Mungu aliposema katika: Qur an:Suratish-shams: 91:7 - 10. 27.

"Na kwa Nafsi (Roho) na aliezitengeneza. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake. Bila shaka amefaulu alietakasa (Nafsi yake) Na bila shaka amejihasiri alieiviza (Nafsi yake)". Alimaanisha kuuhusisha wakati wa kabla ya kuingia ndani ya viwili wili vya udongo. Akili inapiga picha (khayal) kiasi cha kuona labda ulikuepo hapo awali na kwamba hivi sasa unajishughulisha kufikiri, ambaye anapata shauku ya misemo ya Mnyezi Mungu yenye mifano kama hiyo. Basi mfano mwingine ni kama ule uliomo mwenye: Qur an: Sura Al-a`araf: 7:172.

"Na (kumbuka) Mola wako alipowaleta mwanadamu kutoka Migongoni mwao kizazi chao na akawashuhudisha Juu ya nafsi zao (akawambia) "je mimi siye Mola wenu? Wakasema" Ndio, tunashuhudia (kuwa wewe ndiye Mola wetu) (Akawaambia Mwenyezi Mungu ) "Msije mkasema siku ya kiyama kuwa sisi tulikua tumeghafilika na haya (hatuyajui)". Aya hiyo inashadidia siku ya Ahadi na Mithaki wakati ambao viumbe vyote havikua vimevaa miili ya udongo. Na kama ilivyoashiria Suratish-shams, Ukweli ni kwamba:-

"Kisha akaifahamisha (Nafsi uovu wake na wema wake)". Maelezo ya aya zote mbili hizi ni yenye kuonyeha wazi wazi 28.

uhakika mzito kweli kweli kwamba tulikueko kabla. Siri ya Ibin Adamu ajuae ni Mnyezi Mungu peke yake, lakini kwa shuhuda nyingi zilizotapakaa mote mwenye Qu ran, inaonyesha wazi wazi kua Ibin Adamu mbele ya Muumba anayo nafasi mahsus na ya pekee juu ya viumbe wengine. Moja ya kiungo kikubwa cha siri hio na ajabu zake ni Nafsi ambayo imo ndani ya miili yetu.

NAFSI, ROHO, MOYO NA AKILI KUINGIA NDANI YA KIWILIWILI CHA UDONGO:

Qur an:Ad-dahr: 76:1.

"Hakika ulimpitia Binaadamu wakati mrefu katika Dahari hakua kitu kinachotajwa (Binadamu ndie kiumbe cha mwisho kuletwa ulimwenguni)". Baada ya kuumba dunia na kuweka kila kinachohitajiwa, Mnyezi Mungu aliweka viumbe mbali mbali kwa madhumuni ya Ibada lakini walishindwa.Viumbe hivyo vilomtangulia mtu kuishi hapa duniani vinaonyesha kua ni Majini, kutokana na uchunguzi wa kauli ya Mnyezi Mungu, tazama: Qur an: Al Hijr:15:27.

"Na Majini tuliwaumba kabla, kwa moto wa upepo wenye joto (kubwa kabisa)". Hiyo ni hakika ya wazi wazi kua tulitanguliwa na viumbe wengine walio tofauti kabisa na sisi. Lau sio Binadamu kama wanavyodai watu wa Elimu ya machimbo (Archeologists) mfano wa Dr. Leacky 29.

ambaye ni mashuhuri zaidi Afrika Mashariki (Tumeelezea kwa kirefu katika kitabu chetu "El-makhuluq") Mnyezi Mungu alipendelea kuweka kiumbe kingine, tena kutokana na Ardhi hii hii, na ndipo aliposema: Qur an Al Hajr:15:28.

"Na (kumbaka) Mola wako alipowaambia Malaika: "Hakika mimi nitaumba mtu kwa udongo mkavu unaotoa sauti, wenye kutokana na matope meusi yaliyovunda". Qur an:Hijr:15:29.

"Basi nitakapomkamilisha na kumpulizia Roho inayotokana na Mimi basi mumuangukie na kumtii". Na ijapokua Malaika waliingilia kati kutaka kufupisha azma ya Mnyezi Mungu juu ya kuumbwa Mtu, lakini mwishoe walisujudu (lau sijda hiyo siyo kama ile ya kwenye swala. Hii ni kuinamisha kichwa tu, kuonyesha kumtukuza huyo umsujudiaye). Kwa heshima na taadhima hiyo Mnyezi Mungu anatukumbusha katika sehemu nyingi mfano wa hii, mwenye: Quran:Israh:17:70.

"Na hakika tumewatukuza wanadamu na tumewapa vya kupanda bara na baharini, na tumewaruzuku vitu na tumewatukuza kuliko wengi katika wale 30.

tuliowaumba, kwa utukufu ulio mkumbwa (kabisa)". Hiyo ndio hakika ya Nafsi, Roho, Moyo na Akili zilivyoingizwa ndani ya miili yetu kwa wasta- (kupitia) kwa watu wawili wa kwanza (Seyyidna Adam Asw na Mama Hawwa Asw).

MAJARIBIO KATIKA UHAI:

Mnyezi Mungu alimleta Mtu duniani kwa majiribio ili afaulu kua kiongozi wa kufaa. Na tofauti na Malaika, amemuekea matamanio ndani ya hiyo Nafsi. Kwa upande mwingine tumeona vipi Nafsi ilivyoandaliwa kwa kutambua mambo maovu na mambo mema na hiyo ni Ilmu. Ilmu bil kulli ilitanguliwa na akili. Tabia ya Nafsi yenye matamanio ni yenye kuamrisha mabaya daima. Qur an inasema hivi juu ya Nafsi: Qur an: Surat Yusuf 12:53.

"Nami sijitakasi Nafsi yangu, kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha Sana maovu, isipokua ile ambayo Mola wangu ameirehemu. Hakika mola wangu ni mwingi wa kusamehe (na ) mwingi wa kurehemu". Na Bwana Mtume SAW ameisemea Nafsi hiyo hiyo: (a). Alipokua akitoka Katika vita ya jihadi (Uhud). "Tumetoka katika vita ndogo tunaiendea jihadi kubwa. Maswahaba wakamuuliza: "Ni ipi tena hiyo jihadi kubwa e mjumbe wa Mnyezi Mungu? Akasema: "Ni jihadi ya Nafsi" pia amesema : (b) "Nafsi ni khabbithi kuliko mashetwani sabini". 31.

Kwa hivyo baada ya Nafsi hiyo kuwekwa ndani mwetu imekua ni majaribio tosha kwetu kumtafautisha Mtu na Mnyama, na Mtu na Malaika. Vipi habari hiyo? Mtu anakua Mnyama akiifwata Nafsi yake na pengine Mnyama akawa afadhali kwa sababu ya akili. Na Mtu anakua kama Malaika, akiipinga Nafsi yake akatekeleza yote aliyoamrishwa na Mnyezi Mungu bila kuasi, na papo atamzidi Malaika kwa sababu ya matamanio, ambayo Malaika hakupewa. Kwa hiyo wakati ukhabithi wake (Nafsi) ni zaidi ya Mashetwani sabini, basi ni wazi kabisa kua Shetwani mmoja hawezi lolote juu ya Mtu. Ndo, sawa na kusema afanzapo mtu kosa, si rahisi kukubalika kua amezidiwa nguvu na Shetwani kuliko kua ni Nafsi yake mwenyewe. Nafsi hiyo inaweza kubadilika kama mtu mwenyewe anataka.

MABADILIKO YA NAFSI HADI KUUNGANA NA ROHO:

Kama tulivyoona ya kua asili ya Nafsi ni Roho, na kwamba ilipata usugu baada ya kuchangukana nayo, basi inaweza kurudia kuungana na Roho. Qur an:Ash-Shams:91:9 -10 . "Bila shaka amefaulu alieitakasa (Nafsi yake) na bila shaka amejihasiri alieiviza (Nafsi yake )". Safari ya kujitakasa inaanza pale anapokwisha tenda kosa na kuanza kujuta. Kwani ni lazima ajilaumu. Basi anapofikia hadi hiyo, hua amebadilika toka: 1. Amma-ra ­ imeingia katika Nafsil: 2. Law-wama ­ Amma anapotubia mtu akarudi kwa Mola wake, pamoja na kuazimia kufanza kheri tu, basi hua ni mwenye Nafsil: 3. Mul-hama ­ Hii ndiyo Nafsi ambayo Mnyezi Mungu aliikhitari 32.

Kuifahamisha ule uovu wake Nafsi na wema wake. Na akizidi Mtu kujitakasa kwa kuongeza mambo mema, basi huingia kwenye utawala wa Nafsil: 4. Mut-mainna ­ Ambayo huwa ni ile ilotulizana kabisa. Pengine huitwa Moyo, Pengine huitwa Roho, pengine huitwa Akili, (hizi ni jitihada za Ulamaa). Nafsil Mut-mainna imetajwa ndani ya Suratil Fajr: Qur an:Fajr:89:27.

"Ewe Nafsi yenye kutua". Mtu hupata utulivu mzuri sana ambao husababisha Moyo, Akili, na Roho kutua kabisa kama siye alokua na vituko. Badilika badilika hii inaenda toka hapa mpaka kuingia katika: 5. Ra-dhiya ­ Ambayo ni hali ya kurudi kabisa kwa Mola wake Mtu, na zaidi ya kuridhiwa pia na Mola wake Mtu hapo hua: 6. Mardhiyya ­ Ambayo ndiyo iko katika kukwea sana. Na Nafsil: 7. Kamila au Swafiyya ­ Ambayo ni Nafsi ilosafika kabbisa. Na zama ikishafika hali hiyo hurudi ikajiunga na Roho, na ikishafika hali hiyo basi haitazamiwi kutoka tena hapo. Na hapo ndipo Mtu anapokua "Minal fa-izina". ­ Qad aflah man zakkah. Ipo Falsafa kubwa sana katika jambo zima la Nafsi, lakini na tutosheke na lile la kupatikana nguzo ya sita ya Imaan ndani ya hali ya Nafsi Mar-dhiyya: "Khayri-hi wa Sharri-hi Mina Llahi Ta`ala". Na haimkiniki kuyakatia tamaa majaribio ya Mnyezi Mungu wakati Mtu anafahamu wazi wazi kua maisha ya hapa duniani yamepangwa sehemu kubwa ya mitihani ambayo ili kuifaulu, basi misuko suko yake ni mingi ambayo anatakiwa Mtu kuifungia kibwebwe. Qur an:Al-A`nkabuut:29:1 -2.

" Alif Lam Mym, je watu wanadhani wataachwa 33.

(wasitiwe katika misukosuko) kwa kuwa wamesema "Tumeamini", basi ndiyo wasijaribiwe (wasipate mitihani?)". Zaidi ya mfano huo ni aloutoa Mnyezi Mungu ndani ya: Qur an: Suratil Baqara:2:214.

"Mnadhani kuwa mtaingia peponi, na hamjajiwa na mfano wa (yale yaliyowajia) wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara na wakatetemeshwa sana hata mitume na walioamini pamoja nao wakasema: "Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika lini? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu iko karibu". Ipo sababu moja tu ya maana katika taabu taabu zote hizo, nayo ni ile iloambatana na hadithi ya Bwana Mtume SAW kua: "Hakika ya Mnyezi Mungu anapompenda mja wake, basi humtia mabalaa, akisubiri basi humkinga, na akiridhia humchagua". Hakuna njia ya kututhibitishia lile penzi la Mnyezi Mungu juu ya mja, kama katika hadithi hii. Ni kitu wazi wazi kabbisa lakini Mtu anapofikwa na mashaka na misuko suko kama hiyo, basi hutokwa na Imaani mara moja na kuanza kuelekea kwenye Ishraki Kama kwamba siye Bwana Mtume SAW aliyemuelezea hadithi hiyo ilopita. "Basi Ad-duniya (Dunia) sijnul Muumin, ni jela ya walioamini (Mnyezi Mungu mmoja ­ Allah) Wa Janntul kafir. Na ni pepo ya kafiri". 34

"Na law thamani ya Dunia mbele za Mnyezi Mungu Ingelingana na thamani ya ubawa wa mbu, basi (kila ) kafiri asingekunywa funda la maji". Kwa hivyo kila taabu zinavyozidi kwa Muumini ndio kuthubutika kwa maneno ya Bwana Mtume SAW na ndio kukamilika kwa neno Insaan. ".....Likitengemaa hilo, kimetengemaa kiwili wili kizima, na likiharibika hilo umeharibika mwili mzima". Ni wazi kuwa katika kulitengeneza hilo pande la Damu chafu ambalo ndo chanzo cha Roho na Nafsi panahitajika matendo ya wema katika kila njia. Na yote hayo yatekelezeke na Ikhlas. Katika mlango ufwatao zipo nasaha zote zile ambazo zitamnufaisha mwenye mapenzi ya kweli katika kujitakia maslahi ya Nafsi yake, vile alivyotupendelea Bwana Mtume SAW.

35

INSAAN

Qur an:Al Infitar:82:6.

"Ee Mwanadamu! Ni nini kikudanganyacho na Mola wako Mtukufu (hata ukamuasi)". Ewe Insaan, Mtu bila ya kutazamwa viungo vyake au Ubinadamu wake, lakini ni Insaan. Wala Mayyiz zake namna anavyomili, tabia alizopewa mara asimange mara afurahi, haya sio yanayotizamwa hapo. Wala haitazamwi Aadami ­ Mara kachoka, mara usingizi, lakini - Insaan. Haya ni maneno matatu tofauti. Insaan ni yule Mtu, yule "yeye" au "wewe" au "mimi"; anaeazimia, anaekusudia, anaechagua. Anapochagua Insaan kwenda pahala aliechagua ni nani? Insaan. Sehemu ya Ubinaadamu imetumwa tu. Miguu imetumwa tu, na viungo vingine vimetumwa tu. Inaweza na Ubashari ukawa umekuja kati, labda kuna mkate na mchuzi Ubashari unatamani mkate na mchuzi ukazidi kukutia hamu uende. Lakini Insaan yule anaependa, anaehusudu, anaechukia, anaetakia watu wema, anaekumbuka Uungu, anaekumbuka kiyama. Hata mwili ukifa "yeye" yuko na yeye, ndiye anaeulizwa kaburini, anaeulizwa Barzakh. Kwa hiyo Qur an inapotaka kusemea Mtu namna hiyo humwambia "Insaan" ­ Mtu, humwambia Insaan ­ Haikuambiwa "Ya Adami", "Yaa ayyuha Adam" au "Yaa ayyuha Bashari". "Yaa ayyuhal Insaan" ndo inamtofautisha baina yake yeye na Malaika, baina yake yeye na Wanyama wenginene, ni kua Insaan ­ Wewe Insaan si kwa Mwili (bali) kwa Roho.

KUMALIZIKA MWILI

36.

Kutumikia Mwili upatie matamanio yake, uupe nguvu, basi uuhudumie Mwili, uwe na nguvu tu au starehe zake mwili tu. "Atat lubur rib hu fiima fiihi khusran nu..." "Unatafuta faida katika kitu ambacho ndani yake mna khasara." Kila unapomuona mtu mzima, hakuwa namna hiyo alikua kijana, na ujana wake ulitumika kwa sehemu ya Ubinadamu, sehemu ya Ubashari na Insaan ndio aliesemezwa akaongoza mwili, sasa unatumika mwili tu. Na mwili unapotea kila siku kidogo kidogo na kwa bahati kijana akifika utu uzima ni lazima siku moja mwili utamtoka. "...Atat lubur rib hu fiima fiihi khusran nu aqbil alan nafsi au ruhu..." "Kaabil juu ya Nafsi au Roho". ".....Was-takmil fadha-iluha" "Ukamilishe fadhila zake (virtues) zake". Uwe una Sa-ir, iwe kitu cha Nafsi au Roho, Fadhail uwe karim, hichi kitu cha Roho uwe unawapendelea watu wema, iwe unampenda Mtume SAW , unajishughulika na kumtaja Mnyezi Mungu na kumtumikia Mnyezi Mungu, hayo yote ni mambo ya Roho. Shughulika na hayo "Aqbil alan Nafs". Usiwe nawe ni mtu wa kujipima nguvu (Exercise) tu, unatizama Nafsi inakuaje kila siku unajipima; unashindana kuvuta kamba, kua shujaa: "Washujaatus sabri saa" "Unavutwa na matamanio wewe ukapigana na matamanio ukasubiri". Na Twariqa yote ukisikia kuna, Twariqa ni kumtengeneza Insaan yule anaeitwa Insaan, tena sehemu ya Ubinaadamu. Mikutano ya kheyri, ya Dhikri, macho yanatizama njia ya kupita. Lakini hasa Twariqa inamuongoza Insaan imfanye ana mahaba katika Moyo wake. Anampenda Mnyezi Mungu na Mtume wake SAW na viumbe vya Mnyezi Mungu. Awe karimu, asiwe Mwizi, asiwe mjanja si madhambi ya Nafsi, madhambi ya Roho. Madhambi 37.

ya Nafsi yanakuwa makubwa sana, mbali kuliko madhambi ya mwili. Hata Mtu akiiba unaokwiba si mkono, unatumwa tu, ndio maana Mtu asiekua na uaminifu hana Imaan: "Laa Imaan liman laa amanata Llahu" "Hapana Imaani kwa Mtu ambae hana uaminifu". Kwa sababu uaminifu si kitu cha mkono, wala cha kichwa, wala cha miguu. Ni Nafsi ni Roho, ndio inaovunja Uaminifu. Mkono unatumwa ufanye lisilo la twaa: "Laa Imaan lima laa amanata-Llahu" . Yaa ayyuhal Insaan, Aqbil alan Nafsi was sstqbil fadhailiha fa-anta bin-Nafsi au bi Ruhi laa bil jismi Insaan". Si kwa kiwiliwilli Insaan, usidhani kuwa wewe ni kwa kiwiliwili Insaan .

MTU MNYAMA:

Kwa kiwiliwili wewe ni kama Ng`ombe, Mbuzi Sungura, Panya; wao ndio sehemu ya kiwiliwili ulionacho wewe "Mammal" (Biologists - wanawaita). Lakini Insaan Twariqa iko hapo. Katika Sulu-k kupata njia kijitengenezea njia ya Dini, ukatafuta ubora kwa njia ya Dini. Ukatafuta mali kwa njia ya Dini, njia kwa kumtaja Mnyezi Mungu, na huku unayo yako ya kidunia. Insaan hapo anakuwa katika hatari. "Ee Mwanaadamu ni nini kikudanganyacho na Mola wako Mtukufu (hata ukamuasi)". Una wazee wawili huwatii una mke humtizami inavyolazimu, mke ana mume hakai nae kwa Insaafu. "Nini kilichokukhadaa na Rabu wako wewe ni karimu, kakukarimu wewe Insaan kakupa Ubinaadamu huo, una macho, una miguu, una viungo, una mambo kadhaa wa kadhaa. "Alladhi khalaqaka" "Ambaye kakuumba (akakupa mwili huo)" 38.

"Fasaw ­ waaka" "Akakufanya sawa, (mikono imekaa sawa na miguu, macho kila kitu kakiumba kimekaa sawa)". Ingeweza ukawa miguu mirefu, mkono mmoja mrefu mmoja mfupi. Na yote hajakufanyia haya. Kakutengeneza bara-bbara. "Faadalaka" "...Akakufanya ulingane". "Fi-ayyi suratin maa ­ sha-a". "...Katika sura yeyote anayotaka yeye Mnyezi Mungu". "Rak-kabaka". "...Kakutengeneza (kakupandanisha)" (Kakupa sura unyoitaka, watu wangapi kuna mamilioni Waislamu tu duniani, wanaambiwa leo wako milioni alfu, na kila mmoja ni namna yake na sura yake na wewe una yako. Fikiri, kaa ufikiri usende kinyama, mnyama anakwenda kwa mwili tu - mambo ya kimwili). Sasa kinchokuzuia baada ya kuwa umeonywa, baada ya kuwa umeshazinduliwa, baada ya kuwa umezaliwa katika Uislamu, baada ya kuwa umesikia mambo ya Mungu na mambo ya tabia nzuri na Roho zinazotakiwa Mtu awe nazo ­ Wema Insaaf, nini ufikiri kilichokuzuia usiwe hivyo? "Bal tukadh dhibuna bid-diin". "Mnakanya Mnakadhibisha hukumu siku ya kiyama". Ungekuwa una Yaqini, mimi ntahukumiwa, kwa ninoyafanya ungeyakimbia yaliokatazwa. Yakikufika utafwata Qur an inavyokwambia (yalokatazwa) mbio unarejea kwa Mnyezi Mungu.

KUREJEA KWA MNYEZI MUNGU:

"Wastagh firul Laha innallah Ghafuwrun Rahi-m". Wanaomtaka Maghfira Mnyezi Mungu­Innallah­Ghafurun-Rahim. 39.

Hakufukuzi sasa mbona umeshindwa, laa.

"Innal ladhi-nat-taqaw". "Hakika watu wenye Taqwa". "Idhaamas-sat humut twaifun minash shaytwani". "Wakiguswa na sehemu katika Shaytwani". "Tadhakkaruw" "Wanakumbuka" Khalafu Sheytwani anaweza kukuta sehemu ya Basharia ya Insaan anapita kwa njia ya basharia, anaingia katika Insaan, anamukhadaa katika njia ya matamanio, katika njia ya majivuno ya kujiona, njia ya kughafilika. Usifanye hivyo, ukifanya hivyo ukamsahau Mungu kabisa, umekhadaika na Mungu, mambo ya Mungu umeyaachilia mbali. Huna Sala tano, huna saumu, huna chochote huna kutumikia walo kulazimu uwatumikie, huna Insaaf, huna uaminifu Mungu hatambui, inaonyesha nini: "Tukadh- dhibuna bid-dini". "Mnakanya, Mnakataa, mnakadhibisha hukmu na kila kitu kinaandikwa". Kuna Malaika kazi yao kuandika: "Wainna alay kum laha-fidhii-na". "Na hakika juu yenu (wako) wenye kuhifadhi hayo mnayoyafanya (na kila kitu)". "Kira-man ka-tibi-na". "Waandishi". "Maa yalfidh min qawlin illa laday-hi raqib-un atiid". "Hatamki mtu neno ila mbele yake yuko Raqib na Atid". Raqib anaandika mema. Ati-d anaandika maovu. Akifanya ovu Atid, kwanza huzuiwa. "Mwache labda atakumbuka, atarejea kwa Mnyezi Mungu". Na ni mwepesi ikiwa mambo yenyewe hayajakamatana na 40.

haki ya binaadamu, Mnyezi Mungu hukusamehe.Ikiwa haki ya Binaadamu, kakosea mtu - kaharibia mtu nyumba, ameharibia watu watoto wao majumbani. Haki ya binaadamu inakuwa taabu. Lakini yako wewe Nafsi yako na Mnyezi Mungu, ukikumbuka ukarejea Mnyezi Mungu anakupokea: "Wal ladhina idha faalu fa-hishatan " "Na wale watu wema wanapofanya (Fa-hishatan) uchafu (Aw-dhala-mu anfusa-hum) ­ au wakadhulumu nafsi zao (dhakarul Lah) Wanakumbuka Mnyezi Mungu. "Fastaghfiru li-dhunubi-him". "Wanataka maghfira kwa Mnyezi Mungu kwa dhambi zao". "Waman- yaghfiru dhunu-b illa Llahu". "Na nani mwenye kughufiria madhambi ila Mnyezi Mungu". Anakutaka Mnyezi Mungu wende kwake wakakutakie maghfira, ukijiachia basi, Malaika wataandika wala hapana kua: "Aa miye Mungu ananighufurilia kwa hivyo ntaasi", wakati huo upate yanotakiwa uwe nayo Majuto na Tawba, kua ndo sababu ya wewe kughufuriliwa. Hiyo ni kua tabia (Environment) pahali palipokuzunguka, dunia yako ulonayo mambo kadhaa wa kadhaa yamekuvuta, umefanya silo- sio umezoweya kusema uongo ulipokuwa mdogo unakutoka vile vile kwa sababu ya mazoeya ya uongo, hayo ndiyo yanosemwa sio kua "Aa, Mungu yupo atanisamehe, ntastaghfiru ". Huwezi, Istighfari sio kusema "Astaghfirrullah", ni kutaka akughufirilie, na hakughfirilii mpaka ajue kwa kweli umejuta ikiwa ndo hivi, hata ukichupa mpaka vipi kwa ubaya, unaingia katika anaowaambia: "Yaa iba-diyal ldhina asrafu ala- anfusi-himu". "Enyi waja angu ambao wamechupa mpaka juu ya Nafsi zao". Pengine Mtu kakulia pamoja na kikundi cha watu wabaya, kaingia ulevini, akazoeya uongo - anaongopa - kazoeya kufwatia mbio 41.

wanawake au wanawake wanojiweka kutafuta wanaume akakumbuka "Inna lillahi" "Ninafanya nini haya ndo ya motoni". Haya ndo ya Insaan anoambiwa ­ "Nini kinakukhadaa, yaa Insaan" , haya ndo yale ya unyama, si ya Uinsaan, si ya Insaania, ya Unyama. Anataka kuepuka nayo moja kwa moja yamesha mvaa kila yakimjia anajuta anatamani yamtoke kabisa anaambiwa" "Laa taqnatwu" Watu wa namna hao wanaambiwa: "Msikate tamaa na Rehema ya Mnyezi Mungu". Iwe basi, Mnyezi Mungu Sub hana wa Taala, madamu nimemuasi ndo lazima atakutia motoni - hakusema labda ­ Laa la hasha. "Innal Llaha yaghfiru dhunu-ba jami`a". "Mnyezi Mungu anaghufirilia madhambi yote". "Innahu huwal ghafuw - rur rahim'. Yeye anaghufirilia (hapana hata kubwa vipi linalomshinda kughufirilia) Anarehemu sana lakini: "Waaniibu ilaarabbikum". Rejeeni bila kurejea kwake hapana tamaa inataka urejee kwa kujuta na Tawba, ikiwa mali ya watu kwa kiasi unavyoweza kurejesha. Ikiwa umemtukana mtu au umemsema mtu, ukamtake radhi kwa kiasi ya kupata salama ukiona mambo yatazidi tena haki ya binaadam hii nikisema mambo yatazidi hapo hatari: "Waaniibu ila Rabbikum". "Rejeeni kwa Rabbu wenu (makafiri hawana pa kurejea)".

"Dhaalika biannal ladhiina aa-manut tabaul haq

wa annal ka-irina laa mawla lahum". Kumbuka kuna Malaika wanaandika. Na kufanya makosa si ajabu kwa Insaan madam anao Ubashiria na Uadamiyyi. Ukifikwa 42.

"ni kua mazoea tu yamemfika na anapigana na nafsi yake anaisemeza nafsi:"Yaa nafsi walihubbik, mtawaani" "E! Nafsi nakuonea huruma mpaka lini unajiakhiri kuniakhirika namna hii". Na kila ukiacha mapema na ukenda mwendo mzuri mapema ndo inakua wepesi kwako wewe, ukikawia, inakua kama mti umeuacha umetia mizizi ukitaka kuung'oa taabu, na ni uzito kuung'oa mti ule, Na raha sana kuwa mwema mtu, na utakua ukijambia:"Yaa ayyuhal ashbaan, maa gharraka birabbikal karim al ladhi khalaqaka fasaw aaka faadalaka fi ayyi swu-ratin maashaa-arak ­kabaka, kalla bal tukadh-dhibuna bid-diini wa inna alaykum lahaafidhina kiraaman ka-tibina yaalamuw-na maa tafaluna-innal abraala lafii naiim a (wa Innal fujja-ra lafi-jahiim). Hakika watendaji wema wako katika neema kubwa wawe ndani ya Neema (hapa duniani kabla ya Akhera, sikwambii watakapofika Akhera).

NEEMA ZA DUNIANI NA NEEMA ZA AKHERA:

"Wainnal fujjaara la fii jahiim".

WATU waovu wachafu matata mifujjaari, mijitu matata (malaghai Imaani zao za ujanja) la fii jahim ­ wako ndani ya moto hapa duniani. Inawataabisha - Conscious ­dhamiri yao. "Yas - lawnaha yawmad -diin".

43.

"Jahiim" hiyo wataingia siku ya hukumu, watakwenda wakahukumiwe wakutikane na maovu mengi kuliko mema, maovu yale hayajafutwa kwa Toba, hayajafutwa kwa Istighfaar - kwa kumtaka Maghfira Mungu, hayajafutwa kwa iitiraaf - kukubali kua mtu ni muovu, anataka Mungu amtengenenze. "Laa ­ ilaha ­ illa ­ Llah". "Yas- lawnaha yawmud-din". Wataingia siku hiyo (ambayo mambo yote yanategemea uzito wa amali zikiwa nyepesi yuko katika hatari mtu). "Fa-amma man thaqulat mawaazii-nuhu" "Mtu ambae amali zake zimekua nzito". "Fahuwa fii iishatin raadhiya" "Yuko katika maisha yenye kuridhiwa atayaridhia yeye mwenyewe". Amali nzito kama kukutana pahala (kama pale penye Dhikri) amali zinaongezeka zinakua nzito. Unakwenda Msikitini unaswali unatumwa nyumbani unatumika katika mambo ya kheri. Unawapenda (Mawalii) Wa a`malas-swa-lihati-waudi ilal ladhina aamanuw - Watatiwa watu ambao wenye kuamini wakafanya mema - Jan-naatin ajri min tahtihal an-har Mabutsani katika pepo inapita chini yake mito - lakini inataka kila mmoja kwa kiasi chake, njia zake - Wa udkhilal- ladhina amanu wa amilus swa-liha-ti janna-tin ajri min tahthal an har Siku hiyo ambayo watu wengine watakuamo katika hatari. "yawmud- diin" - Siku ya hukumu , ndo maana katika Alhamdutunaita: Maliki yawmid-diin - Mwenye (kumiliki) siku ya hukumu - ndo Yawmud Diin. "Wainna alaykumu laha-fidhi-na kira-man katibun na wama-hum an ­ha bigha-ibin". "Wala hawakua wao na moto ni wenye kua hawapo, hata siku moja ( They are never absent from the fire)". 44.

Kila ikija list ya kuitwa majina "fulani fulani" "Labbeka" yupo ­ hathubutu kukimbia akawa (absent). "Wa ma-hum anha bigha-ibina wa ma-adrakaMaa yaumud-diin". "Nini kitachokujulisha kitafanya ujue nini hiyo siku ya hukmu". "Thuma ma-adra-ka ma-yawhud diin" "Nini baada ya hapa kitacho kujulisha nini siku ya hukmu". "Yawm-laa tamliku nafsi linafsi shay-an". "Hapana nafsi itomiliki kumiliki nafsi nyingine kwa kitu chochote. (Hapana nafsi yoyote itathubutu kuja bila Amri ya Mnyezi Mungu na kukubaliwa na Mnyezi Mungu, "Aa, mimi namuombea huyu mtu wangu". "Huyu Swahiba wangu", "Huyu mwanangu", "Huyu Muriidi wangu", Sharti Mnyezi Mungu Ampe ruhusa kwanza). "Walaa yash-fauw-na illa limanir tadhaa" Wala hawashufii ila wale Mungu alowaridhia kwanza, kua "huyu anaweza kuwashufaiya; a" huyu alikua mtu; unaambiwa kachupa mipaka, katoka kwenye (cycle) ya kushufaiwa". Si mambo ya kuyafanyia maskhara, inataka mtu akae afikiri na mambo yanamngojea kila mtu. "Yawma laa tamliku nafsi linafsi shay an wal amru yawmaidhin lillah." "Na amri-jambo siku hiyo lina Mwenyezi Mungu". Al hayyul qayyumu Mnyezi Mungu hakuna Mola ila yeye (na) ndiye mwenye Uhai wa maisha msimamia kila jambo, Anayejua yote - Laa- taakhudhuhu sinatu walaa-nawm - Haumchukui usingizi, kusinzia wala usingizi. Yaalamu ma-bayna aydi-him Anayajua yalo mbele yao watu wote - Wamaa-khalfahum - na yalo nyuma yao - Walaa yuhiitwuna- Wala hawazungukii akiwajua 45.

Vilivyo. Bi shay- in min ilmihi - Katika yaliyo katika IImu yake, llla bima-sha-a - Illa anachokitaka, Wasia kursiyyuhus-samawa-ti wal ardh - kiti chake cha ufalme kimeenea mbingu zote na ardhi, Walaa yauw-duhu hifdhuhuma wa huwal aliyyul adhi-m Hakumchoshi kuhifadhi Samawati wal ardhi. Siku hiyo watu wa mwanzo watostahiki watopata kheri kubwa siku hiyo watu wenye kupendana kwa ajili ya Mnyezi Mungu.

46.

MALIPO YA PEPO KWA WAPENDANAO LILAHI:

Itanadiwa:"Aynal muta-ha-bbi-na- lijala-li adhilluhum tahta dhilli yawma laa dhillu illa dhili". "Wako wapi wanaopendana kwa ajili ya Utukufu wangu niwafunike chini ya kivuli changu, siku ambayo (leo) hapana kivuli illa kivuli changu" "Wajabat mahabbati lilmutahabbi-na-fiiya" "Yamepasa mapenzi yangu kwa wenye kupendana kwa sababu yangu". "Al-mutajali-sin fiiya" "Wenye kukaa pamoja kwa ajili yangu" Na kuna watu saba: "Yudhillu-humu llah tahta dhilluhu yawma la dhillu-hu". Mmoja Imam -A-adil - Waja wake wenye kufanya uadilifu. Na katika hao waliotajwa, "Shabun Nashaa fii twa-atii laha". Kijana kakulia katika twaa, fi ibadatil-laha ­ katika ibada ya Mnyezi Mungu (kama vijana ambao wana Swala zao tano, wanakutana kwa ajili ya Mnyezi Mungu Al-hamdu-lillah inataka washukuru. Na alama kubwa ya kushukuru ni kuepukana na kumuudhi Mnyezi Mungu kadiri unavyoweza. "Sha-bbun nasha-a fii twa-ati llahi warajula-ni tahabba fil-la-hi" "Watu wawili wamependana kwa ajili ya Mnyezi Mungu "

"ljtamaa alay-hi". "Wamekusanyika kwa sababu ya Mnyezi Mungu"

"Wa-tafarraqa alay-hi". "Wamefarikiana kwa sababu ya Mnyezi Mungu". 47.

"Wa-rajulun" Na mtu" "Da-at-hu" "Amemuita mtu yule" "Mra-atun" "Mwanamke" "Dha-tu Mansibun" "Mwenye cheo", "Wa jama-lin" "Na uzuri" "Faqala inni akhafu Llah", "Akasema mimi namuogopa Mnyezi Mungu". (Hapana kusema wanavyosema vijana wa kisasa "Aa, si kataka mwenyewe" ­ inatosha wapi umuogope Mnyezi Mungu). Na mwengine kutoa mkono wake wa kulia, mkono wa kushoto hauna habari. Yaani katoa sadaka kafanya kwa lilah hatta hapana anaejua. Mradi, wote saba, watu ambao Mnyezi Mungu atawaambia siku ya kiyama"Tahiyyatu-hum fii-ha sala-m" Maamkio yao ­ Mnyezi Mungu kuwaamkia ni "Sala-m". Hawa wanatokota motoni, na hawa Mnyezi Mungu anawaamkia "Sala-m qawlan min rabbi rahiim". Na wao wenyewe wanaamkiana "Salam tahiyyatu-hum fii-ha sala-m". Wanaamkiana wenye "Sala-m" kuna salama tu ­ (peace) basi. Pepo ya Kiislam ina amani, hapana mtu atosikia neno la kumuudhi, Hapana chochote ­ La-ila-ha-illa llah. Yaa Rab Amani Salam - bali wanaanza kuipata tangu wanapoondoka duniani. Malaika wanawafisha na huku Malaika wanawaambia: "Salam aleykum al-ladhi-na tawaf-fata humul Mala-ikat 48.

tayyibi-n Sala-mun alaykum -ud-khulul jannat". "Ingieni peponi", pepo gani? Pepo ya Barzakh, kiyama bado (haijafika) hakijaja. "Ud-khulul jan-nat" ­ "ingia Peponi" Na mwengine Barzakh wanataabika, kama Firawni na watu wake "Anna-ru yuuradhu-na alay-ha (him)". "Moto unakabilishwa juu yao asubuhi, na jioni". "Ghuduwan wa ashiyyan, wa yawma taquw-mus-sa-ati" - Na siku (ya) kiyama kitaposimama. "Ad-khilu ­ watieni-Alafir-awni". - Firauni na watu wake. "Ashad-dal adha-ba" - Adhabu kali kabisahii wapi ­ "Sab-han, wa Masa-an". "Ghuduw-wan au "Wa shiyyan" ­ Barzakh. Ukipita kwenye makaburi unaona bas. Kuna watu wako katika taabu kubwa, na wengine wamo katika raha kubwa inategemea umetengeneza nini huko. Basi, muhimu ni Sulu-k kujaribu kujitengeneza, uwe na tabia nzuri, hata ukionekana uwe unajulikana.

49.

ASKARI NA ADUI ZA MOYO:

Mfano wa Mtu (wewe) ni wa ajabu kupita yote ambayo Mnyezi Mungu ameieka mbele ya macho yetu. Na tuchukue mfano wa viumbe vidogo sana kama vile Nyuki jinsi walivyo. Umma wa kutosha wenye nguvu na umoja, (a perfect Emperial Kingdom). Amesema Mnyezi Mungu katika: Qur an: Surat Al-Muddath-thir: 74:31.

Basi ni vyake yeye Mnyezi Mungu vyote viliomo Nyoyoni na Rohoni na kwingineko, katika ulimwengu wa majeshi (yalowekwa tayari tayari kwa wingi). Tukijihusisha kwa majeshi ya Nyoyoni, tutaona kua yako mawili jeshi ambalo linaonekana kwa macho jeshi ambalo halionekani kwa macho ­ ila kwa wale wenye kuona kweli kweli. Amma katika hukmu, ni kama mfano wa nyuki, ambako kuna Mfalme, Majeshi, Watumishi, Mawaziri, Hal-mashauri, na wasaidizi. Hii ndo maana ya jeshi. Jeshi (l) ni kama lifuatalo: Mkono

Mguu Jicho Sikio

50.

Ulimi na viungo vingine vya dhahir. vyote hivyo vinatumikia Moyo kwa sababu Mnyezi Mungu ameshavisakhirisha kwa ajili yake (Moyo) na katika kutekeleza amri vinafanana na Malaika wa Mnyezi Mungu ambao hawaasi hata siku moja na hufanya yale ambao wameamriwa. (Tafauti na itikadi za baadhi ya watu ambao wanaamini kua Malaika wanaweza kukhini, na wakafikiliza amri tofauti na vile walivyoamriwa na Mola wao). Kiwiliwili ni Marikebu ya Moyo, na ndicho ambacho hukipanda, na kuuzidisha ilmu na kumakinisha sawa-sawa. Basi mwenye kujifanzia zawadi Moyo wake, maslahi yake baadae ­ hua ametimia Akili. Miongoni mwa askari wa (ii) Ba-tini ambao hawaonekani kwa macho ni matundu ya ubongo ­ Dima-gh (Cerebruim, cerebellum na medula Oblongata). 1 . Mtu baada ya kuona kitu (jambo) hukifutika na (kuipata) kuijua sura ya kitu kile ndani ya nafsi yake kwa njia ya khayali (mfano wa mwenye kutoa) sura ile hubaki nayo katika kumbukumbu. Anaeisababisha kua hivyo ni askari wa kuhifadhi. 2 . Kisha hufikiria kile alokihifadhi ambapo hua mwenye kukipandanisha baadhi kwa baadhi. Ikiwa iko haja anaweza kurejea sura yote akaikusanya pamoja ili ajenge maana kamili yenye kuweza kuhusika ndani kwa ndani au kuzishirikisha vile apendavyo katika tandhimu (utungo) hii inapatikana:Tafakuri. Kumbukumbu. Hadithi. Na Kupinga picha (khayali). Na lau Mnyezi Mungu hangeumba Askari khao, basi ubongo (Brain) ungeachia, si ajabu kila kitu cha maana ambacho kingeachiwa kwa muda.

MFANO WA MTU NDANI YA KIWILIWILI:

Mtu anapokuwa ndani ya kiwiliwili anakua na mfano wa Mfalme katika Mamlaka yake ametulia kabisa. Jina ki - wili-wili peke yake linamfahamisha kila mwenye Akili ilosalimika kua ni vitu viwili, Sio kimoja. Ni umbo lenye jingine ndani yake. Na ndo maana siku ya kufa Mtu akaachana na kiwiliwili chake, kiwiliwili 51.

huanguka na yeye Mtu hujitenga akenda kwengine (Barzakhyaani pahali pa mapumziko na mateso ya muda tu hadi kufika siku ya kiyama na siku ya hukumu). viungo na nguvu za ndini: Hivi, kwa upande hua ni silaha, lakini kwa kweli ni wahandishi (San-nai) kwa mambo. Kiwiliwili: Ni mfano wa Mji, Marikebu, ambayo Moyo imependa. Mfalme mwelewa, na nguvu zake zinatokana na hawasi za dha-hiri na ba-tini ambazo ni kama Askari wake, na Viungo ni kama Raiya.

Akili:

Na hata Bwana Mtume Saw alikua na maana kubwa aliposema juu ya viungo kama:"Kullukum ra-in-wa kullu ra-ni mas-uw-lun an raiyyatihi". "Nyote ni wachunga (khalifa) na kila mchunga ni mwenye kuulizwa kwa vichungwa (raiya ) vyake". Nguvu za Akili Nguvu za kufikiri. Matendo ­ A`mali

Hao ni halmashauri na ni Mawaziri wake Mtu.

ADUI ZAKE MTU

Shah-wa: Yaani matamanio ya Nafsi, ni mtumishi muovu sana ambaye kila mara anaazimia kumuhilikisha Mtu. Hana wema hata mara moja juu ya Mtu, na daima husubiana na Sheytwan-rajiim.

Ghadhabu na joto lake: Ni kama Askari muongo, hadaa zimejaa tele na ni khabithi kweli kweli. Daima hujifunza Mtu mzuri 52.

wa nasaha wakati chini ya nasaha yake ipo sumu kali yenye kuweza kuua mara moja. Ujinga: Fidhuli ndani ya mji na nje yake ­ yeye huharibu kila hatua yenye sura ya kuendelea. Na daima hua peke, kwani kila anaemsogelea humkwepa.

Bwana Mtume Saw amesema: "Ja-hil ni adui wa Nafsi yake mtu, vipi atakua rafiki wa mwengine?". Chuki na husda: Hawa ni katika maadui ambao hua ni ugojwa wenye madhara mazito yenye kufwatiliza kuhiliki kwake mtu mara moja. Na mwisho ni:Nafsi: Ambayo kama isipotayarishwa vile ipasavyo hasa, basi haiwezi kuitwa Mtu mwanaume alie Kamilika yaani: Rijaal.

WATU WA KWELI KWELI:

Amma wanaofaa kuitwa Rijaal si (kwa ajili ya) ghasia tu urijali ni kuweza kupigana na Nafsi yako ukiwa umo ndani ya (mapambano ya) kupigana ili mwishoni uwe Mtu unaekwenda mwendo mwema. Hata Mtu mmoja anawataja watu wakubwa Anasema : "Humur rijaal" Wao hao ndio Rijaal ­ (Wanaume) wa kweli" "Wa-ayb-an yuqa-lu liman-lam yattaswif fi maani waswfihir rijaalu". "Aybu kusema kwa mtu asie sifika na sifa zao, kua yeye ni Rajul (Mwanaume)". (Kafiri awe Rijaal, Fa-sik awe Rijaal, Mujrimu awe Rijaal ­ Itakuwaje!!). Rijaal wanoshughulika na Mnyezi Mungu na Iqamu Swala-ti na kusimamisha Swala. Yakha-funa yaw-ma - Wanaogopa siku, 53.

"Tataqallabu fii-hil qulub wal-abswa-r". "Zitageuka ndani yake (ndani ya siku hiyo) nyoyo na maoni".

"Liyajzia ­ humu-Llahu kulla nafsin ma-amilat" "Mungu apate kuilipia kila nafsi kilichochuma (kila nafsi italipwa kilichochuma)". "Fa-man yaamal mith-qala dhar-ratin khayran yara-hu" "Mwenye kufanya uzito wa chembe ndogo ya kheri ataiona". "Waman yaamal mith-qala dhar-ratin shar-ran yara-hu". "Na mwenye kufanya uzito wa chembe ndogo ya shari ataiona" Anasema Mnyezi Mungu katika Hadithil Quds:"Hakika si vingine, ni vitendo vyenu nyie wenyewe ­ Nakuthibitieni ­ Faman wajada khyran fal - yahmidul Lah ­ Mwenye kukuta kheri na amshukuru Mnyezi Mungu­Waman wajada ghyra dha-lika falaa yalumu Illa nafsiha. Mwenye kukuta kisichokua kheri asilaumu ila nafsi yake" Kila Mtu atapewa chuo chake, "Iqra-a kita-baka" "Soma chuo chako - Soma daftari lako". "Kafa binafsikal yawma alayka hasi-ba" "Utatosha leo wewe kujifanyia hesabu, huna haja hata ufanziwe hisabu na mwenginewe (utatizama mwenyewe)". "Manih tadaa fa-innama yahtadi linafsih". "Mwenye kuongoka (akiwa sehemu nyingine) ndo anaongoka kwa sababu ya nafsi yake". "Waman dhal-la innama yadhil lu alayhi". "Mwenye kupotea anapotea juu ya Nafsi yake mwenyewe". "Walaa taziru wa-ziratu" "Habebi mwenye kubeba". 54.

"Wizra ukhra" "Mzigo wa Mtu mwingine". Kila mmoja atakuwa na yake. Lakini tuamrishwa tukionyana, na tukikumbushana na tukisaidiana katika kheri. (Mafanikio yako katika kheri yatategemea) kufwatia (kwako) kheri (na) kua pamoja na watu wema: "Ya-ayyuhal ladhina a-manut-taqul- laha" "(Enyi ambao mumeamini), mcheni Mnyezi Mungu" "Wa-kunu ­ maa-swa-diqi-na" "Muwe pamoja na wakweli".

55.

MNYEZI MUNGU, BINAADAMU NA MAUMBILE:

Mnyezi Mungu aliyetukuka ametengeneza na kujaalia kitu kwa ajili ya Binaadamu, na Amemtengeneza Binaadamu kwa ajili yake yeye. Na ajaribu Mtu kuhisabu, kuanzia popote pale alipo ataona kua kila kiliopo mbele yake kimekusudiwa yeye. Hiyo ajabu kubwa na neema isiokua na kipimo maalum. Ukiacha hayo yote ukatizama yaliokaribu zaidi, utaona Mnyezi Mungu pia amekuumba, akakuekea macho, na maono (Baswari) na jamii ya viungo ambavyo si mgeni navyo kwa sababu viko mwilini mwako. Na wako ambao Mnyezi Mungu mwenyewe amewanyima, basi ni kwa Hikma yake amefanza hivyo, sio kwa dhulma. Kwani yeye hawi mwenye kudhulumu Mtu, au kiumbe. Basi baada ya kuumba kila kitu kwa ajili ya Mtu (Mwanaadamu) Amemuumba Mwanaadamu kwa ajili ya Mnyezi Mungu (Mwenyewe) na ndo maana akasema katika: Qur an: Suraul Bayyinah: 98:5.

" Wala hawakuamrishwa ila kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawache Dini za upotofu na wasimamishe Sala na kutoa Zakah ­ Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. (Nao wameikataa)". Kwa ushahidi huo, ni yenye kuonyesha kua saa yeyote ile anapokengeuka na yule ambaye kwa ajili yake ndo ameumbwa anakua katika makosa ya kuchukiza kabisa, na hasa ikiwa anajua (sio mjinga ambae anaishi mbali na mji au jijini). Umekwisha pata fununu nzuri ya kujijua wewe ni nani na kuja kwako hapa duniani ni kwa madhumuni gani. Kwa hivyo, mpaka kufikia hapa wewe sio mjinga tena. Na ikiwa haya yaliomo ndani humu si yenye kutoka kichwani mwangu kwa matamanio ya Nafsi, yangu bali ni 56.

mafundisho walofundisha maulamaa ambao ndo warithi wa Mtume Saw. Basi kitabu hii kitatosha kua shahidi juu yako Yawmul Qiyama (Qiyama). Sasa ilobaki ni kuzidi kujiendeleza na kuyatia majaribuni yale ulokwisha yajua ikiwa ni pamoja na haya yafuatayo hapa:

KUACHA YALOHARAMISHWA:

Undani wa suala hili si mzito sana, kwa sababu:i. Mnyezi Mungu hakuamrisha jambo lolote ila linafaida na maslahi na Mwanaadamu; na ii. Hakukataza jambo lolote ila lina hasara na madhara na Mwanaadamu. Mfano wa Kamari - Ukicheza ukapata basi kwa vile ni tendo lilokatazwa na Mnyezi Mungu pato lake litakua ni haramu na kula yake, vaa yake, na zaa yake itakua ni haramu. Na twaa ya Mtu ambae vitu vyake ni vya haramu haisimami. Hukumu yake ni kama kuweka msingi juu ya maji ya bahari. Maafa ya kamari ni makubwa, na zaidi hua si ya khasara tu peke yake, bali yana madhara, wenye kufutwa (Kuliwa) aghlabu hupigana na pengine huua, kwa ghadhabu. Katika kamari nyingine wenye kufutwa huwarubuni wake zao wakawaacha siku mbili tatu mpaka kumudu kuwakomboa, huo ni Udayuthi. (yaani ni kukosa ari), na kila Dayuthi mwisho wake ni kuingia motoni. Mnyezi Mungu hakumuumba Mwanaadamu akampenda, akamtukuza juu ya viumbe vyote, ili aje amtie motoni ­ Hasha. Mfano mlevi - Amekatazwa kuukaribia wacha kuunywa; kwani gha-lib huharibika akili ya Mtu, ukiwa Mtu hujui nini usemalo. Na pengine ukazusha ugomvi na kuumizana. Na mwisho ukipata usingizi hujui nini lipitalo, na hata ukijua unabaki kupayuka payuka tu. hayo yote ni maafa makubwa. Mnyezi Mungu anasema katika: Qur an: Suratil Baqara: 2:219.

57.

"Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari, sema: katika hivyo mnamadhara makuu na (baadhi) ya manufaa kwa (baadhi) ya watu. Lakini madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: "Vilivyokuzidieni." Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya (zake) mpate kufikiri". Na kwa nini amali mbili hizi zina madhara makubwa mno? Sababu si nyingine isipokua ile ya kua kwake fungu katika mambo ya sheytwani, Mnyezi Mungu anabainisha hivyo katika: Qur an: Suratil Ma-idah 5:90.

"Enyi Mliomini! Bila shaka ulevi na kamari, na kuabudiwa (kuombwa ) asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kutazamia kwa mishare ya kupigia ramli (Na kwa vinginevyo) (yote haya) ni uchafu (na) katika kazi ya sheytani. Basi jiepusheni navyo. Ili mpate kufaulu (kutengenekewa)". Mfano wa Kuzini: katika kijishughulisha na wanawake tu kwa kuzini nao, badala ya kuoa ukatulizana au na baada ya kuoa pia ukawa unazini ­ basi huko ni kuutumia mwili vibaya, na kuudhoofisha afya na nguvu hupungua sana. Kwani walopima mchupo wa manii, wamegundua kua katika kila tone moja kuna matone sabini ya damu. Damu ni kitu azizi ndani ya mwili, nayo ili ipatikane kwa wingi unotosha kutuweka katika hali ya afya, tunapaswa kutumia vyakula vizuri ambavyo tunavinunua toka 58.

sokoni na madukani. Zinaa ni za namna mbili Ya kwanza: Ni ya mwenye kufanza hali ya kua na Mke (au Mume) na ile ya mjane (Bechula) au (Aazib). Ya kwanza ndo yenye dhambi zaidi na hata adhabu yake ni nzito zaidi, kwani ni lazima apigwe kwa mawe ndani ya handaki mpaka afe. Ya pili: Ni ya kupigwa mijeledi Mia moja. Na zinaa ya macho, katika kutizama Mwanamke asie kuhusu. Lakini vyovyote itavyokua, Bwana Mtume Saw anasema: "Azzinaa Yuw rithul faqr". "Zinaa inarithisha ufukara". Na ukichunguza kwa uadilifu hutokosa kuthibitisha kauli yake hiyo kuwa ni kweli. Mfano wa Liwati na Kusagana (Maji ya ndimu). Liwati ni aina ya fiili kati ya Mume na Mume. Badala ya kuoa Mke ambapo ndo iloruhusiwa na sheria, Mtu huoa Mume mwenzake pasina manufaa yeyote bali kumwaya damu tu na kudhoofisha afya. Na maafa yake nayo ni makubwa, kwani wote hao hua na Laana za Mnyezi Mungu. "Ra-kib wal Marku-b" Mwenye kupanda na mwenye kupandwa ­ wote hao. Amali mbaya hii ilianza wakati wa Naby Lut As. Haipungui miaka elfu sita nyuma, na ndo maana ikapewa jina hilo ­ Qawmu Luut- Basi watu wake waliangamizwa kwa kupinduliwa, chini juu pamoja na nchi yao. Amma kusagana ni kati ya Mke na Mke. Vitendo ambavyo havielekei hata kidogo. Lakini kwa vitu vya Sheytani ndo hupamba moto kati ya watu. Ni mambo hata wanyama hawafanzi, kwa hivyo, Mtu mwenye akili inataka afanze ­ jitihada aviache vitendo hivyo. Mfano wa kula Nguruwe Mnyama huyu mwenye mafuta mengi mwilini na wadudu puani, anayo tarikh ndefu. Na hapa hatuna makusudio ya kumbainisha hivyo (Kitabu chetu: "Jua na miezi 24 ­ juu ya ujao wa Mitume 25" - Tumeelezea habari zake huenda kikatoka ­ Insha Allah). Nguruwe ni namna mbili: Wa kwanza: Ni Mwenye kutokana na ubichi ubichi wa kinyesi. Wa pili: Ni Banii Israel (Binaadamu) walogeuzwa Nguruwe Maafa yake ni makubwa, lakini yenye madhara sana hakuna kama 59.

Udayuthi (yaani kuondokewa na ari). Na inatosha kumchunguza Nguruwe mwenyewe katika maisha ya ngono. Nguruwe wanaweza kufanza fiili mbele ya Nguruwe mwenzao bila kuingiliana kati kama walivyo wanyama wengine, ambapo huzuia kufanzika kwake ­ labda waende mbali huko wasikoonekana na wenzao. Basi na kila mwenye kumtumia mwisho wake hivyo na Mnyezi Mungu hapendi Mtu akose Ari. Kwa hivyo katika kuacha yalo haramishwa kutapatikana fursa nzuri, si ya kujitakasa tu bali ya kujenga Taqwa. Mfano mdogo tu unaonekana katika: Qur an Suratil Maidah: 5:93

"Si dhambi juu ya walio amini na wakatenda mema kwa vile walivyovila (kabla ya kuharimishwa) madamu wakimcha (kwa vile alivyowaharimishia wakati huo) na wakiamini (alivyowaamrishawakati huo) na wakitenda mema..." "Thummat taqaw wa-amanu thummata-qaw wa ahsanu wal Lah yuhibul muhsiniina!". "Tena wakamcha (vile vile alipowakataza makatazo mengine) na wakafanya mema (mengine alivyowaa mrisha) na Mungu huwapenda wafanyao mema) Huo ni mfano mdogo tu ambao unaonyesha vipi hali ya Masahaba ilivyokuwa ya khofu kubwa kwa Maswahaba wenzao waliokwisha kufa kabla kutelemka Aya hiyo, hali ya kua wakinywa pombe. Ni katika mwaka wa sita wa Al hijra zama ilipokatazwa mno kunyewa pombe, lakini Mola Sub hana wa Taala ni muadilifu alibainisha wazi kua: Laysa jun-ahun ­ Si dhambi - kwao ambao hawakudiriki amri ya makatazo. Na katika mabaya yaloharamishwa ni mfano wa Riba, yaani kukopesha kwa masharti ya kulipa zaidi baadae, ambapo daima huiliki mkopaji. Mnyezi Mungu ameiharamisha amali hiyo na ameikaripia sana sana kiasi cha kusema yeye yuko katika vita na 60.

Yeyote alae Riba, kwani makamio yake ni katika daraja moja na wanyang`anyi wa kuuwa na maharamia. Suala hili ni refu na zito sana, lakini inatosha kulielewa kwa ufupi, kiasi kile ambacho Mnyezi Mungu mwenyewe amekielezea katika baadhi ya Sura za Qur an kama ile ya: Qur an: Baqara: 2:275 ­ 280.

"Wale wanaokula Riba, hawasimami (kuendesha yao) ila kama anavyosimama yule ambae Shetani kamzuga kwa kumsawaa ­ (Wao mbioni tu hawana kituo). (Na) haya ni kwa sababu wanasema Biashara ni kama Riba hali Mnyezi Mungu amehalalisha Biashara na ameharamisha Riba. Na aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake (ya huku kukatazwa Riba ), kisha akajizuia, basi yamekwisha mthibitikia yale (mali) yaliyopita (aliyokwisha yapata: na hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu . Lakini wanaorejea (kula Riba) basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele".

"Mwenyezi Mungu huyafutia (baraka mali ya) riba; na huyatia baraka (mali yanayotolewa) sadaka, na Mwenyezi Mungu hapendi kila kafiri (na ) afanyae dhambi.

61.

"Hakaika wale walioamini na kufanya vitendo vizuri na kusimamisha Sala na kutoa Zaka, wao watapata ujira wao kwa Mola wao, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika"

"Enyi Mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni yaliyobaki katika Riba, ikiwa mmeamini".

"Na kama hamtafanya (hivyo), basi fahamuni mtakuwa na vita na Mwenyezi Mungu. Na mkiwa mmetubu, basi mtapata rasilmali zenu; msidhulumu wala msidhulumiwe".

"Na kama (mkopi) ana dhiki, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na kama nyinyi (mnaodai mkizisamehe deni zenu) mkazifanya sadaka, 62.

basi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua haya (basi fanyeni)". Katika utawala wa Kiislamu amal hii hupuuzwa na kuondoshwa kabbisa kabbisa; na kufikia hata kuuawa ambae anakopesha kwa faida au kufungwa jela mpaka atoe maelezo ya kukoma kufanza kazi hiyo (Tazama maelezo yake katika tafsiri ya Qur an kwa kiingereza, ya Abul Ala Maudud. Vol: 1. Page: 72). Na miungoni mwa mambo matatu ambayo Bwana Mtume Saw alipendelea apate miangaza zaidi juu yake - Ribaa ni moja wapo. Lakini hakuwahi ­ (Tazama pia maelezo yake, katika tafsiri ya kiingereza ya Sheikh Yusuf Aly. No. 324, sahifa No. 111). Kadhalika na katika mifano mikubwa ambayo ni maarufu kwako, lakini unaipita bila ya nadhari ni ile ya: Kuuwa bila kukusudia (Fatal Accidents/Manslaughter). Amma kuua kwa makusudi tena Muislamu mwenzako, jazaa yake ni Jahannam, kama ilivyoelezea aya 93, ya Suratil Nnisaa ambayo Sheikh Abdallah Swaleh El Farsy ameielezea vizuri khabari zake katika ukurasa wa 124 wa Tafsiri yake. Lakini kuua bila kukusudia, mfano wa waendesha magari au wawindaji na kama hivi, wajue ya kwamba watatakiwa kuacha huru mtumwa mmoja, au kama hana anunue, kisha awalipe Diya watu wa marehemu. Na hiyo Diya ilokusudiwa na Mnyezi Mungu ni Ngamia mia moja, au thamani yake kama hazipatikani. Laa ikwa aliyemuua akiwa ni Muislamu, lakini jamaa zake ni makafiri wanaopingana na Waislamu, basi itampasa ile haki ya Mnyezi Mungu tu ya kumfanya mtumwa huru. Tafauti na ikiwa makafiri wenyewe si wenye kupigana na Waislamu (haya yalihusika zama za vita vya Uhud, wakati Waislamu walipofadhaishwa na makafiri baada ya kuzungukwa ikawa hawajui Waislamu wepi na makafiri wepi, kwa hio walitokea kuuana kwa bahati mbaya). Bwana Mtume Saw alikadiria diya kua Ngamia 100, au Ngombe mia mbili au Mbuzi Alfu mbili au Dinari 800 za Dhahabu au Dirham ya Fedha Alfu Nane.(tazama Maududi katika tafsiri yake ya kiingerezapage 157). Na anapokosekana mtumwa, basi ni kufunga miezi miwili ya kufwatana, ambapo udhuru wa kufunga Swaumu ya kawaida hautatosha katika Swaumu hii ya toba. Na akiacha basi italazimu aanze upya. Basi lazima tuelewa ya kua faini zinazotolewa mahakamani 63.

Hazitatosha kumkomboa mtu na dhima mbele ya Mnyezi Mungu. Ni lazima pia tutoe na faini ya Mola. Mifano ya mambo ya haramu mingine ni ile ya Uongo na Kudanganya ­ Ghushi, ambayo Bwana Mtume Saw amesema juu yake kama vile: "Man ghaash-sha falaysa min-na". "Mwenye kudanganya (ghush - Cheating) si pamoja na sisi (si katika ­ sisi).

64.

UNDANI WA KUTEKELEZA FARDHI:

Qur an: Baqara:2 : 110.

"Na simamisheni Swala, na toeni Zakaa na kheri mtakazozitanguliza, kwa ajili ya Nafsi zenu, mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu anayeona (yote) mnayoyafanya". Swala na Zakaa ni miungoni mwa Fardhi alizotuwekea Mnyezi Mungu, kama alivyowawekea waliotangulia kabla yetu wakati Uislamu haukua umekamilika. Baada ya Swala na Zakaa, zinafwatia Swaumu na Hajji. Amma Swala ni dua, au maombi kwa Mnyezi Mungu kiunganisho kati ya Mja na Mola wake. Na pia ni Ibada mahsusi ilioekewa nyakati zake mahsusi, na ndiyo ifarakishayo baina Muislamu na Kafiri. Anaeacha Kuswali ­ hua Kafiri wa kweli kwa hadithi ya Rasuli ­ Tahadhari nakwambia. Zakaa ni kutoa fungu maalumu katika mali iliyowajibikia zakaa juu yake. Na kuitoa kwa mwenye kustahiki. Fungu hilo linaweza kuchukuliwa kwa nguvu kwani sio lake Mtu, bali ni la Mnyezi Mungu. Na Hijja ni kuikusudia Nyumba ya Mnyezi Mungu (Makka) kwa Ibada walau mara moja katika uhai; kwa mwenye uwezo (hasa fedha) wa kwenda. Uchache wa Faradhi ni huo, na kwazo, unapatikana Uislamu. Lakini kwa vile hawezi asiyekuwa Muislamu, baleghe mwenye akili, kupokelewa amali (zake) zozote katika hizo. Imelazimika kutamka "Laa ilaha illal lahu Muhammada Rasulullahi" (Kwa wakati huu, kwani kwa zama za Nabii Isa As ingebidi iwe: "Laa 65.

Ilaha illal - lahu Isa Rasulu Llahi" au Yahaya, Zakaria, Musa,

hadi Adam ­ Rasulu Llahi). Katika tamko hilo ambalo hujulikanwa kama: "Shahada mbili" Ipo maana nzima ya "Tawhiid" yaani kumpekwesha Mnyezi Mungu (Divine Unity) Neno hilo ni zito sana na si kutamkwa kwa ulimi tu peke yake, bali kwa Moyo (ule ambao ndio wewe mzima mzima Roho, Nafsi na Akili). Na hivyo ndio kukira kwa kweli, ambako matokeo yake hua kama hivi: Kafiri hua Muislamu. Hupanda Daraja ya juu toka chini . Huwa Mrehemewa badala ya Mbughudhiwa. Huvuta mapenzi ya Muumba badala ya chuki zake (Sakhtwa). Humkimbiza Shetwani akawa mbali na Moyo wake Mtu. Lau baada ya tamko hilo unafikiwa na Mauti, basi kwa hadithi ya Bwana mtume Saw, unakwenda peponi duna shakki- pasi na shaka yeyote ile, kwa sababu neno hilo lina uzito katika mizani kiasi ambacho si mbingu na ardhi , wala Arshi na Kursi na Dunia zote, ambazo uzito wao unaweza kuinua "Laa Ilaha Illa Llahu". Mnyezi Mungu Anasema katika: Qur an: Suratil Qaariah: 110: 6-9.

Basi yule ambae mizani yake itakuwa nzito. Huyo yuka katika maisha yanayompendeza".

"Na yule ambaye mizani yake itakuwa nyepesi. Huyo maskani yake yatakuwa katika (huo moto ) Hawiya". Aya hii halikadhalika inawasaidia waumini kutatua mfano wa tatizo la waliokufa wawili bila kutambulikana majina anwani yao na Dini. Nguo sare, nywele sawa, na wote wamevaa vidani bangili na herein sikio moja (mfano wa vijana wetu wa kileo ambao wameacha nyendo za Jadi zao na Dini yao na kufuata utamaduni wa kigeni ambao lengo lao ni kuudhoofisha Uislamu unaoingia kwa kasi Duniani. Lakini hakuna wa kumudu kuuzuia au kuupiga vita (Basi inatumiwa mbinu za namna hiyo ili vijana wetu wawe 66.

Wenyewe waharibu nchi (Dini) lakini Dua za Waislamu zitawavuta Insha Allah wazinduke wao wenyewe waipiganie Dini yao zaidi ya vile wanavyopigania kuunga mkono mambo ya wageni ambayo hayawahusu ndewe wala sikio. Haimkiniki kuwa baada ya kujua kutokana na mafunzo ya Dini: Amelaaniwa Mwanamume anaovaa vazi la kike, na Mke avaae vazi la Kiume bila udhuru wa sheria, kisha awe yeye ndo wa mwanzo kupinga amri hiyo ya Mnyezi Mungu na Mtume Saw). Yule mzito ndo Mwislamu na kafiri hata akiwa Mnene vipi atakuwa mwepesi tu. Basi sharti ya Shahada Mbili itapatikana, ndo sasa inafwata utekelezaji wa Fardhi kwa vitendo. Amma fardhi iliyo kubwa sana katia Uislamu baada ya shahada mbili, hakuna kama Kuswali. Qur an Suratil Hud:11 : 114.

"Na simamisheni Sala katika ncha mbili za mchana (Nayo ni Adhuhuri na Laasiri) na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana (Nayo ni Magharibi na Isha ­ ziko karibu na mwisho wa mchana, na Al fajr ipo karibu na mwanzo wa mchana). Hakika mema huondoa maovu huu ni ukumbusho kwa wanaokumbuka. ( Haya ni mawaidha kwa wanaokubali kuwaidhika)". Katika kuswali umo Uislamu wote; kwa maana ya nguzo za Uislamu Tano:1. Shahada mbili, Sawa na kusema kwa Kiarabu "Ashhadu an laa ilaaha illal Lahu". Maana yake: "Nakiri kwa Moyo ( wewe binafsi yako na Roho na Akili yako) na kubaini kwa ulimi kuwa hapana wa kupasa kuabudiwa kwa haki illa Mnyezi Mungu "Wa Anna Muhammadun Rasulul Lah" ( Na ninakiri kwa Moyo na kubaini kwa ulimi kuwa) Hakika ya Muhammad ni Mjumbe wa Mnyezi Mungu.

2. Kusimamisha Swala Tano,

i. ii. Asubuhi Adhuhuri Rakaa mbili. Rakaa nne. 67.

i.) ii.) iii.) iv.) v.)

iii. Al asr Rakaa nne. iv. Magharibi Rakaa tatu. v. Ishai Rakaa nne. Wakati wake kwa siku za joto huingia saa 10.30. saa za msikiti (sio kwa saa ya Zone). Inaingia saa 6.30 ama saa7 mchana. Inaingia saa 9.30 ya Msikiti. Inaingia saa 12.10. Inaingia saa 1.30 usiku.

Na kila unapokurubia wakati wa Swala gha-lib huepo mwenye kuweta watu (Muadhini) kwenda Msikitini kwa ajili ya Ibada hiyo. 3. Kutoa Zakaa. ( Nayo ni fungu maalum) la mali na kuwapa wale wanaostahili miungoni mwa Mafakiri, Masikini, wapiti njia, wanaozitumikia kugawa mafungu, wageni katika Uislamu, walopewa Uhuru, Wenye madeni, Katika kuipigani (Dini) Uislamu. Mali zipasazo zakaa: 1. Mali ya biashara ( Rasilimali ndiyo itolewayo Zakaa Shs.2.50 katika Mia) Na baaada kupitiwa na mwaka, sio kila Ramadhani ( kama wafanzavyo wengi wa matajiri kwa uchache wa elimu) utafikiri wote walianzia biashra tarehe moja, pia faida. 2. Nafaka za punje punje zote kila gunia kumi, utatowa moja, na nusu yake kama umenyesheleza. 3. Tende na Zabibu kila mizo mitano ( kiasi cha kilo 1000). 4. Mbuzi na kondoo: zikifikia kiwango cha arubaini utatoa mbuzi jike wa mwaka mmoja (au Thaniyya mwenye miaka miwili). Na wakifikia 121 utatoa mbuzi wawili. Na 201 mbuzi watatu. Na 400 mbuzi wanne. Na wanaozidi kiwango hicho, basi kila mia utatoa mbuzi mmoja. 5. Ng`ombe ­ kiwango chake cha Zakaa ni zinapofikia 30 ­ (Thalathini) utatoa ndama wa mwaka mmoja. Wakifikia 40 ndama jike la miaka miwali. 6. Dhahabu na Fedha: (Madini sio Fedha ya sarafu) ) Na isiyokuwa ya pambo la mke iliyo halali). Itapofika Mithqali ishirini. Dhahabu itatolewa Robo ya kumi. - Sawa na 2.50%. 7. Zakatil Fitri: Hii hutolewa na kila Muslamu baada kumalizika Ramadhani na ambayo pia hujuzu hata kwa mwanzo wa Ramadhani. Lakini ilo bora ni kuitoa baina ya Magharibi ya 68.

Usiku wa Iddi hadi kufikia al fajiri na baadae kidogo, lakini isifikie hadi Kuswaliwa Sala ya Iddi ­ itakua haramu kuichelewesha hivyo. Kuitoa kwake ni Vibaba 4 kiasi ya Pishi au kilo 2 na Thuluth. Kwa kila anayekutegemea wewe chakula (wengine wamejuzisha - awe Muislamu). (Kwa yote hayo tazama "HidayatulAtfal" kurasa wa 53 cha Sheikh Al Amin bin Aly, na "Mahadi ya Fiqhi" juz 3 ukurasa wa 44 cha Sheikh Abdul Jabbar). 8. Madini na Rikazi: Utatolea baada kuuza, sio kungoja Mwaka

4. Kufunga Mwezi wa Ramadhani:

Siku Thalathini ­ Isipokuwa mtoto mdogo, Mwenda wazimu, Asiyekuwa Muislamu, Mwenye Edhi na Nifasi, Mzee, Mgonjwa na Msafiri.

5. Kuhiji Makka:

Kwa mwenye uwezo katika Waislamu, Mwenye Akili, Wakubwa na Huru ­ Kwani hizo ndio shuruti zake Hijja, Swaumu, Zakka na baadhi ya Ibada zingine ni miongoni mwa zenye kupasa kujifundisha wakati wa shida. Lakini Ilmu nyingi ni lazima saa yeyote uwe unajua amma sivyo itakuwa umemukhalifu Bwana Mtume Saw.....

Uislamu ndani ya Swala:

Amesema Bwana Mtume Saw: "Aswalatu Imaadud diin, faman aqa-mah aqaamad diniin, Waman adhaa-aha afaqad hadamad diin" "Swala ni nguzo ya Dini, (basi) mwenye kusimamisha Swala, huwa amesimamisha Dini, na mwenye kuicha (kuipuuza ­ kuipoteza) hua ameibomoa Dini". Hadithi hii inawafiki kiupande na maelezo yaliomo ndani ya Aya namba 42 ­ 49 ya Suratil Al Mudath thir ­ 74. 69.

Qur an: Al Mudath thir: 74: 42 - 49.

Tafsiri yake inafululiza kama hivi: "Ni kipi kilichokupelekeni motoni? Waseme: "Hatukuwa Miungoni mwa waliokuwa wakisali wala hatukuwa tukilisha masikini. Na tulikuwa tukizama (katika maasia) pamoja na waliokuwa wakizama. Na tulikuwa tukikadhibisha siku ya hukumu mpaka mauti yakatujia. Basi hautawafaa uombezi wa waombezi (wowote wale)". Basi kwa nini wanapuuza onyo hili!? Swala imethibiti kuwa Ibada kubwa sana, sio kwa vile ndio Ibada aliyoipenda sana kuifanza kwa wingi Bwana Mtume Saw, hasa saa za usiku hata ikamvimba miguu yake tu, bali kwa kusema kwake kua: "Amali ya kwanza kuulizwa mja siku ya hisabu ni Swala, ikikutwa imetimia, basi zitakubaliwa na pamoja na amali zake zote zilizobaki". Kwa hikma tu itakudhihirikia kuepo kwa Falsafa nzito ndani ya kauli hiyo na hakika yake. Anaposimama Mtu kuswali anahakikisha kuwa hana mabaki ya chakula kwenye meno yake, kwa hadhari kua, kula ndani ya Swala huivunja kufaa kwake. Kwa tendo hilo anaswiri mtu kuwa Swaim (Aliyefunga) nayo ndiyo Nguzo ya tatu ya Uislamu na Swala yenyewa ni Nguzo ya pili. Katika kurukuu, Kuitadili ( yaani kurudi kusimama baada ya kuinama) na kwenda Sijida hadi kukaa Tahiyyatu ­ ni moja amali zenye mfano wa Hijja, Nguzo ya tano ya Uislamu. Katika Atahiyyatu yapo matamko ya "Ash ­ hadu an laa ilaha illal Lahu wa ash-hadu anna Muhammadan Rasulullah". Hiyo ni nguzo ya kwanza ya Uislamu. Na katika Kumswalia Bwana Mtume Saw kutokana na hadithi yake kua: "Swalat alan Naby ni Swadaka". 70.

Na Sadaka ni mfano wa Zakaa inapatikana Nguzo ya nne ya Uislamu. Basi mpaka akitoa salam mwenye Kuswali hua ameutimiza Uislamu wote. Kwa hiyo ikikutwa Swala yake imetimia zitakubaliwa na Amali zake zote, inayo maana nzito. 1. Kusubiri na Kuswali ni Ibada mbili pekee ambazo ni ngumu na nzito sana. Bwana Mtume Saw amisemea "Subra" kua haina malipo ila pepo. Na mara kadhaa wa kadhaa Mnyezi Mungu amewasifu wenye kusubiri, kwani Yeye Mnyezi Mungu hua pamoja na wenye kusubiri. Basi mwenye macho haitaji kuambiwa "tizama". Mambo ya faida kama hayo hayafai kuyawacha, lakini pia katika kuyapapia haifai kujingikiwa nayo kwa hivyo ni vyema kuijua Subra ni nini, na pia Swala. Amma Subra kwa kifupi inatosha kuidala vyema baada yakuijua ilivyogawanyika kwake katika mafungu manne. Kusubiri katika Twaa ya Mnyezi Mungu Qur an Al Imraan: 3:200.

"Enyi Mlioamini subirini na muwashinde makafiri (katika kusubiri) na kuweni imara (nyoyo zenu) na Mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu (Kufuzu)". 2. Kusubiri katika maasi ya Mnyezi Mungu. Nafsi yako ina mili katika maasi, wewe ukapigana nayo ukaifunga. 3. Kusubiri katika kadhaa ya Mnyezi Mungu. Na utaacha wapi kusubiria yaliyokwisha kukadiriwa juu yako na hali una amini kuwa "Khayrihi wa Sharhrihi minal Lahi?". Mnyezi Mungu Anasema: Qur an Suratul Baqara: 2:155 ­ 156. 71.

"Na tutakutieni katika msukosuko wa (baadhi ya Mambo haya). Hofu na njaa na upungufu wa mali na wa watu na wa matunda. Na wapashe habari njema wanaosubiri. Ambao wapatapo msiba husema: "Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na yeye tutarejea ( atatupa jaza yake)". 4. Kusubiri katika Akhlake (Tabiya). Tafauti za viumbe vya Mnyezi Mungu, kwani wapo ambao hazipatani tabia zenu wala kulingana.

Amesema Bwan Mtume Saw: "Mcheni Mnyezi Mungu popote ulipo ­ Na uendeleze mema katika mabaya yako, yatafuta. Na ukae na watu kwa Khulka nzuri". Amma kwa upande wa Maarifa ya Swala inatosha kujua ya kwamba imejengewa katika usafi kama ulivyojengewa Uislamu mzima katika unadhifu. Kasema Bwana Mtume Saw: "Uislamu ni unadhifu, basi jinadhifisheni, kwani haingii peponi ila mnadhifu". Kwa hiyo ili iswihi Swala ya mtu ni lazima kuzingatia suala la:Twahara: Kutwahirika (kutokana) na Hadathi ndogo (mkojo) na kubwa (Mavi) mwilini na kwenye nguo na pahala pa kuswalia. Pia atwahirike najsi ipasayo kuoga (mfano wa Janaba) Hedhi na nifasi. Janaba: Ni lenye kupatikana kwa kumuingilia Mwanamke au Mnyama, kwa kadiri ya kichwa cha dhakar kiasi cha kupotea ndani ya ule mzungo wa kichwa. 72.

Hedhi: Nifasi:

Ni damu imtokayo Mwanamke mkubwa, kila mwezi (Monthly period) na Ni damu ya uzazi.

Mwenye Kuswali awe amesitiri uchi wake, ambao ni baina ya kitovu na magoti ­ na Mwanamke kiwiliwili chake chote isipokuwa uso na vitanga vya mikono. Wakati wa kuswali uwe umeshaingia, na ajue mwelekeo (Kibla) iko wapi na atambue kuwa Swala ni Fardhi juu yako. Ili uhakikishe kuwa umejitayarisha sawa ni lazima kujua hukumu ya maji aina saba: a. Ya mvua. b. Ya kisima. c. Ya mto. d. Ya bahari na Ziwa. e. Ya thaluji. f. Ya barafu. g. Na ya chem-chem. Hukumu yake ni kuwa: a. Kidogo: ambayo hayatimii madebe kumi na mbili (yaani Qullaten) ambayo yanaweza kunajisika kwa kuingiliwa na najisi, na ingawaje hayajaharibika rangi, harufu au tamu yake. b. Mengi: ambayo hayawezi kunajisika hata yakiingiwa na najisi ndani yake. Amma yakibadilika rangi, Harufu au tamu yake hapo yatakuwa mas-ala mbali.

Udhu:

Maandalizi ya Swala ikiwa ni madhumuni ya Mja kukutana na kuzungumza na Mola wake, ambaye pia ni Mola wa Dunia zote, yalotaalaki mno na usafi kwa sababu Mnyezi Mungu Mwenyewe sio mchafu. Kwa hivyo kabla ya kufikia, hatua hiyo, na baada ya Mtu kuepukana na iana zote za uchafu (najisi) mavi, mkojo,damu, usaha, 73.

matapishi, pombe hata tone dogo tu au mnuso wa Mbwa na Nguruwe ambao haisafishiki isipokuwa kwa kuoshwa mara saba (osha moja ikiwa limechanganywa na mchanga), janaba, hedhi na nifasi. Ataingia birikani kutawadha, na hata ikiwa ametoka kuoga. Na kutawadha kuna shuruti zake. Uislamu, na kujua halali na haramu (Mumayyizi) na ikosekane katika viungo vya kutawadha kitu chochote kizuiacho kufikilia maji kwenye ngozi (Mafuta, lami au zafarani) na asiitakidi kuwa ni Sunna yeyote katika Faradhi za Udhu ambazo ni Sita: i. Nia, hasa unapoanza kuosha mwanzo wa fungu katika uso. ii. Kuosha uso, ambao ni sehemu iliopo baina ya maoteo ya nywele hadi mwisho wa kidevu, na kutoka sikio hadi sikio. iii. Ni kuosha mikono miwili, au sehemu iliyobaki kama mkono ndo umekatwa labda. Kwa mkono mzima osha yako ifike hadi penye vifundo au kupita. Na kwa wenye makucha marefu ambayo yangemudu kumficha mdudu chungu ndani bila taabu, ataosha chini yake. iv. Ni kupaka kichwa kwa maji, na ni uzuri katika mipako mitatu uweze kuhisi kuwa maji yamegusa ngozi ya kichwa. Baadhi ya watu hupitisha dharau katika kupaka maji kichwa, na hasa wenye nywele ndefu ambazo kwa mujarrad hujitingisha tu nazo huweza zikajigawa ikawa katika mpako wa pili zile zilizojigawa hazipati tena nafasi ya kusibu maji ­ udhu hautafaa (swihi). Na usipofaa udhu haifai Swala. v. Kupaka maji miguuni, mpaka kwenye kifundo cha mguu. vi. Ni taratibu, yaani utawadhe kwa mpango sio kwamba mradi vipate maji vile viungo vinihusika tu basi ­ laa, haitatosha. Ni Sunna katika kutawadha kutanguliza mswaki, ila baada ya kulingana jua kwa mwenye kufungu. Kuosha vitanga viwili vya mikono ambavyo kwa nia pengine huchukua mahala pa kata, uoshe kabla kuitumbukiza ndani ya chombo chenye maji kidogo, (Nuia: SunnatiIghtirafi ­ Nanuia kuyachota maji kwa mikono yangu). Kupiga "Bismillahi" mbele ya kila kitu. Pia kusukutua, kupanza 74.

Maji Puani, kuosha kichwa chote na masikio mawili nje na ndani. Kuasua vidole vya mikono na miguu. Kuasua ndevu nyingi na kutingisha pete. Ni Sunna kutanguliza kulia juu ya kushoto, na kufanza mara tatu tatu pamoja na kufawatanisha matendo yote pamoja na kujisugua kabla kuleta Dua ya Udhu ambayo ni: "Allahumma jalni minal taw-waab-ii na. "Mola wangu nijaalie miungoni mwa waja wako wenye kutubia mbele zako. "Wajaalni minal mut-twah-irina. "Na unifanze mimi kuwemo miungoni mwa waja wako waliosafika". "Wajaalni minal Ibadikas-swa-lihiin" "Na unijaalie mimi kuwa miungoni mwa waja wako walio wema". Pengine udhu wako huweza ukavunjika kabla kuanza kuswali, kwa kudhihirikiwa na moja ya mambo manne haya: 1. Kutokwa na ushuzi au chochote katika tupu ya mbele au nyuma. 2. Kutokwa na akili hata kwa kitambo kidogo, imma kwa wazimu au kuzimia au ulevi au kwa usingizi. Tofauti na ambaye amekaa akiambatanisha makalizi yake (matako) kwenye ardhi. 3. Kugusana na mwanamke min-ghairi ya kuwepo kizuizi chochote katikati (tafauti na madhehebu mengine). 4. Kujigusa dhakar kwa matumbo ya vidole vya mikono. Lakini ikiwa umesalimika na hayo yote, basi utaingia kuswali bila taabu yeyote.

Swala

Ndani ya Ibada hii mabayo ni muhimu mno katika mzunguko au lile duara la Uislamu, ni lenye shuruti za kufaa kuziangalia sana kwa sababu bila ya kuzijua mbele huenda ukawa huna hata cha kulipwa 75.

chochote. Mnyezi Mungu anapendelea ufanze amal zako kwa ujuzi, kama tilivyokwisha tangulia kusema. Basi shurti zake ni kama zifuatazo, ambazo kwa idadi ni kumi na saba:

Shurti za Swala:

1. Kusimama kwa mwenye kuweza. 2. Nia, nayo ni kusema: " Uswalli fardhis-swalaatis sub-hi rakaa teyni". Ni Swala ya Sub-hi (laa Swala nyingine basi utaitaja hivyo Swala na Rakaa zake) 3. Takbira ya kuhirimia Swala, nayo ni kusema (baada ya neno Rakaa teyni au idadi yenyewe katika Swala) "Allahu Akbar" kwa sharti, usivute alifu tukufu kiasi cha kusikika kama "Aa-llahu". Wala usivute "Hee" kisi cha kusikika kama "Aallaahuuw" utafikiri iko "Waw" mbele yake. pia tamko la "Akbar" lisitamkwe ovyo ovyo, mfano wa kulegeza ulimi hata ikazaliwa "Waw" baina "Allaa" "Hu-wa-akbar" au usivute "Be" kiasi cha kusikika kama hivi: "Akbaa-ru". Swala haitasihi na kama u-maamuma basi jambo la maana ni kupitisha nia moyoni ya kumkhalifu (kuachana naye Imam nawe utakuwa hapo hapo safuni lakini unaswali peke yako ­ Utapa fadhila za jamaa kama kawaida). 4. Kusoma Suratil Fat-ha pamoja na "Bismillahi" ikiwa ni aya amma sivyo katika aya ya saba "Ghayril maghudhubi alay him" ­ Lazima uifanze ndo aya, na "Walaadh dhwaal-liin" aya, wakati pamoja na "Bismillahi" hizo zote hua ni aya moj tu.

Shuruti za kusoma Fa-tiha:

Nguzo hii ni yenye nguvu sana kwa sababu hata ukisoma Sura 113 uiwache Sura hii, Swala yako haitafaa, kinyume na kuwacha kusoma hizo (Sura zote 113) ukasoma Fa-thia, Swala itafaa. 76.

Herufi za Suratil Fa-tiha ni 156 pamoja na kusoma "Maaliki" kwa alifu (kama alivyoelezea hivyo Seyyid Abu Bakar bin Abdillahi bin Abdur Rahman bin Sumeyt el Alawy Sherehe ya "Tiryaaqin Naafii" - Babu ukurasa wa 32), kwani haijuzu kupunguza hata moja katika herufi hizo. Ni sharti ya nguvu sana kuzitoa "Tashididi" (au lama ya kukaza) zake zote 14. 1. katika Lam ya Bismillahi. 2. katika Ree ya Rrahmaani. 3. katika Ree ya Ar rhiim. 4. katika Lam ya Al-hamdulillahi. 5. katika Bee ya Rabbi. 6. katika Ree ya Ar rahmaani. 7. katika Ree ya Ar rahiimi. 8. katika Daal ya Yawmi-diin. 9. katiak Yee ya Iy-yaaka-naabudu. 10. katika Tee ya Iy-yaka nasta-iinu. 11. katika Swa-d ya Swiraatal mustaqiim. 12. katika Laam ya Lladhina. 13. katika Dhwa-d ya Dh-dhwaa. 14. katika Laam ya Lliina. Katika Sharti zake ni kukosekana kuisoma "Ddhaad" kwa "Dhwaad" amma sivyo haitaswihi kusoma kwake na isiposwihi, Swala pia haitafaa, na hiyo ndo khatari ikiwa atakusudia kusoma hivyo na hapo Swala yake haitabatilika. Ingekuwa jambo la maana sana lau Maimamu wa Misikiti wangekuwa wakichukua hata dakika tano kila siku kuwaelimisha watu mambo haya, kwani yule ambaye haipatii vizuri atakuwa ameilimika akipata mawaidha ya dakika tano hizo. Na imesunniwa baada Kuhirimia Swala, (Sharti ya tano) kuleta dua ya kufungulia Swala, kama hivi: "Waj jahtu Waj hiya lil-ladhi Fatwaras Samaawaati wal Ardhi, Haniifan Musliman wa maa ana minal mush-rikina anna S-swalaati wa nusuki wa mahyaa-ya wa mamatti lillahi Rabila a-lamiin laa shariika Llahu wa bidhalika umirtu wa anaa minal Muslimina. 77.

5. 6 7.

8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17.

Kurukuu. Kujituliza, kiasi cha kusema "Sub-hana Rabbi yal adhwimi wa Bihamdihi" x 3. Kuitadil, (kurudi wima) huku ukisema: "Samial Lahu limn hamida" x 3. (Maamuma atasema: " Rabbana lakal hamdi" kwa kifupi). Kujituliza, ndani yake. Kusujudu mara mbili. Kujituliza. Kitako, baina sijda mbili. Kujituliza, ndani yake. Kitako ajili ya Tashahudi. Tashahudi katika kitako cha mwisho (yaani kusoma Tahiyyatu). Kumswalia Mtume Saw. Kutungamanisha (Taratibu). Kutoa Salamu, kulia na kushoto unageuza uso wako.

Mwenye Kuswali akiacha nidhamu hiyo kusudi, mfano akitanguliza nguzo ya kitendo - kama Kusujudu kabla ya Kurukuu na kuitadili, basi Swala yake itavunjika. Basi ipo maana nzito na yenye hakika na ithibati kama mwenye kauli ya Bwana Mtume Saw: "Amali ya kwanza kuulizwa mja, siku ya hisabu ni Swala ikikutwa imetimia basi zitakubaliwa na pamoja na amali zake zote zilizobaki".

78.

UNDANI WA KUTEKELEZA WAJIBATI:

Ni wajibu wa kila mja, sio Muislamu tu kumjua Mnyezi Mungu. Lakini katika Kumtambua kikweli, hapo ndipo penye mfarakano baina waumini wa kweli. Wana Adamu huweza kuzusha ubishani mkubwa juu ya chombo kidogo mfano wa saa ­ huyu akasema: "Sanaa ya Japan" (made in Japan), mwingine akasema: "Laa ni U.K" (made in U.k). Lakini ajabu, si kawaida kufuma watu wakizoza katika suala la Bin Adam, kajiumba mwenyewe, (au kaumbwa na sheytwani na kadhalika). Katika kumjua Mnyezi Mungu ziko faida nyingi ambazo Mwanadamu hawezi kuzidhibiti zote. Inatosha (lau Mnyezi Mungu hafanani kinamna hiyo), kuangalia mfano wa Mtu anavyofanya rafiki mpya. Mwislamu anatosha kuitwa "A-llim" (yaani mjuzi sio ­ mjinga), kwa kuyajua majina (ya Mnyezi Mungu 99 - Tisinin na tisa) maarufu kwa "Asmaaul Lahil husna ­ Majina ya Mnyezi Mungu, yalio matukufu na mazuri mazuri". Twaba-an katika kujiandaa kumjua kwako, kama si kwa hayo Majina 99 ambayo yamekusanya Swifa chungu nzima, basi hata yale 20 au13 ambayo ndio Wa-jibu, hutakosa kujua kua yeye yupo, na haiwezekani kukosekana ­ kwa sababu kukosekana ni sifa pungufu ambapo si laiki yake (yaani na hazimstahiki hata kidogo). Sifa yeyote ya Mnyezi Mungu ambayo Akili ya Mtu (ikiwa ndo chombo pekee kilicho madhubuti kuweza kuhukumu majambo yote Mtu kwenye uhai kinjia ya miujiza ilokwea kabisa) haiwezi kuikubali, basi sio yake kweli. Na bila kuilisha kuilisha mfano wa masuala kama: "Mnyezi Mungu kakosekana. Jee kaenda wapi? "Nani badala yake alishika nafasi yake?" Na "Waja wake walikiabudu nini alipokosekana? Kwa hali yeyote ile sifa kama hizo akili haiwezi kuzikubali. Mnyezi Mungu sio mjinga kwa hiyo yeyote anayejiandaa kumjua ni wajibu kua na Ilimu ­ basi kwa uchache hata kwa kuuliza wale wajuzi ili wakueleweshe vizuri. Katika sifa za Mnyezi Mungu zilizoepukika na Upungufu (nuksani) 99 ndani yake muna kila jambo linalohusu (Manufaa) 79.

na maslahi ya Uhai wetu hapa duniani. Angalia vile alivyosema katika: Qur an: A`arafa: 7:180.

"Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri mazuri, muombe kwayo. Na wacheni wale wanaoharibu utakatifu wa majina yake. Karibuni hivi watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda". Neno: "Muombeni kwayo" si neno jepesi kwa wenye akili, kwa wenye Tadabbur kwa sababu Ulamaa wamegundua mengi ndani ya maneno machache kama hayo . Mathalan ukizingatia tangu pale aliposema: Qur an: Dhaariyaat: 51: 56.

"Sikuwaumba Majini na Watu ila wapate kuniabudu". Na aliposema: Qur an Banu Isra-el: 17: 110.

"Sema, muombeni (mwenyezi Mungu) kwa (Jina la) Allah au muombeni (kwa jina la) Rahmaan, kwa jina lolote mnalomwita (katika haya itafaa) kwani ana majina mazuri mazuri". Ni (hakika) yenye kuonyesha jinsi wazi kuwaMnyezi Mungu anapenda kuombwa (kinyume na sisi ambao huchukia kuombwa sana sana hata tukiwa matajiri au wakwasi vipi), na 80.

Anachukia asipoombwa. Na isitoshe kaonyesha jinsi (njia Method) ya kumuomba kwa kusema: "Muombeni (Mwenyezi Mungu) kwa (Jina la) Allah au muombeni (kwa jina la) Rahmaan". Ikionyesha kua kila tunapopatwa na shida yeyote ndani ya maisha yetu, basi tumuombe Mnyezi Mungu kwa jina lenye mnasaba na ile shida yenyewe; na lazima litakuepo tu jina lenye kunasibiana na shida hiyo , amma sivyo ingembidi Mnyezi Mungu aongeze majina mengine. Kwa hivyo katika mazingatio ya Maulamaa juu ya hakika hii wametupanua mawazo yetu kwa kuweka wazi njia za kuombea. Kwa ufupi tu njia mbili hizi zenye kutoshekeza mahitaji (au matakwa yetu). 1. Kumuomba kwa namna hiyo hiyo aloifahamisha yeye Mwenyewe wazi wazi kabisa "Allah ­ au ­ Rahmaan" Jina moja Allah ikiwa ndo kama Kubwa lenye kutosheleza kwa jumla inamaanisha kua kwa shida yeyote ile utafanikiwa tu ukilitumia jina hilo. Khilafi na Rahmaan ambalo linaweza kujihusisha na mambo ya Neema kubwa kubwa au Rehma. Kwa hivyo, kwa kufwata mfano huo pindi tukiwa na shida mfano wa "Ugonjwa" na tumeshindwa kuvumilia, tunahitaji kupona, basi tutatizama katika Majina 99 tuone ni Jina lipi la Mnyezi Mungu mahususi kwa tatizo letu? Bila shaka ni "Afuwwu" ­ "Mwenye Kuafu" au "Shaafi" ­ "Mwenye Kuponyesha" basi tutaomba uzima wetu kwa jina lake hilo. Mfano mwingine tuko hohe hahe, tunahitaji hali ya uwezo wa kifedha, basi bilkul Mnyezi Mungu ni "Ghaniyyi" tutamtegemea yeye kwa jina lake hilo. Au kama tunachohitaji ni matayassar tu, basi bila shaka yeyote Mnyezi Mungu pekee ndiye "Ra-zaq" Mwenye kuruzuku. Tutaomba kwa jina lake "Ra- zaq" au "Ba-switu" kwani ndiyo majina laaik kwa shida kama hizo.Amma Wakulima wanapokwisha kupanda wakawa wanategemea Mola awaletee Mvua ili kuotesha mbegu zao, basi 81.

wangestahiki wamuombe kwa Jina lake la "Muqiitu", na halkadhalika Wanafunzi wa Vyuoni au Shule, madamu haja yao ni Ilmu, basi Mnyezi Mungu ni "A-lim" na "A-liim" wangetaka wangeomba (pamoja na kujifunza kwao ­ sio kukaa nyumbani kuomba tu "Ya A-lim, Ya Aliim) kwa jina lake moja kati ya mawili hayo. Huo ni mfano mmoja tu ambao Mnyezi Mungu Ametuonyesha, basi sio atuonyeshe kwa kila namna tena. Katika Qur an ambayo imekusanya kila linalohitajiwa kwa njia ya mifano ya muhtasari. 2. Kuomba kwa Majina hayo hayo lakini kwa njia ya idadi. Kila jina lina idadi yake, na kila jina linwatumishi wake mahususi katika Malaika Ruhania. Tizama kwa ufinyu tu, Mnyezi Mungu alipoelezea: Qur an: Al Muddath-thir:74:30 - 31.

"Juu yake wako (walinzi) kumi na tisa. Na hatukuweka walinzi wa huo moto ila malaika, wala hatukufanya idadi yao (hiyo ya 19) illa kuwa mtihani kwa wale waliokufuru.......". Hadi mwisho wa aya hiyo ya 31. Na hizo idadi ziko ndogo, nazo ni zile zijulikanazo kama "Hijaiya" kwa kufwatana kwa "Alifu" ni moja "Bee" mbili, "Tee" Tatu hadi kufikia "Yee" ambayo ndo herufi ya mwisho katika "Hijaiya", sawa na 29 au 30 kwa pamoja na "Hamza"- ambayo ni sawa na "Alifu" kwa upande. Idadi kubwa ni "Abjadia" namna alivyoteremshiwa Naby Adam Asw, nayo ni "Alifu" ni moja, "Bee" ­ 2, "Jim" ­ 3, "Dal" ­ 4, na "Tee" ambayo katika "Hijaiya" ni ­ 3, katika "Abjadia" ni - 400 ­ Hisabu hizo utazikuta katika baadhi ya vijuzuu vya Sura Amma 82.

mwisho wa "Ka-ida" ambapo herufi ya mwisho ni "Ghain" nayo ni 1000. Na ambayo "Kihijaya" ni 19. Halafu katika hiyo hiyo njia kubwa ipo njia nyingine tofauti kidogo. Na inapoingia hiyo basi, hii ambayo ndo kubwa inarudi kuwa ya kati na kati. Njia hiyo ni ya kupatika herufi kama itamkwavyo moja moja. Mfano "Alif" ni ­ Alif, Lam, Fa. Kwa hiyo badala ya kua ni 1 (moja) inakua mia na kumi na moj (111) kwa sababu: Alif ni 1, Lam ni 30, na Fa ni 80. Kwa hivyo mfano wa Kumuomba Mnyezi Mungu kwa Jina lake "Allah" itatubidi tutimize idadi yake mara 66 (Sitini na sita). Kwa njia zote hizo, Mnyezi Mungu humpa kila anaetaka kupewa . Amesema Bwana Mtume Saw: "Mnyezi Mungu amekipa kila kitu silaha na silaha ya muumini ni Dua". Kwa hivyo kila mwenye akili lazima ajue matumizi ya Silaha vizuri kwani kisu kile kile ulichokinunua ili kikatiwe nyanya na vitunguu, kinweza pia kuhudhurishwa mahakamani kama kielelezo katika kesi ya kuua (Murder case). Vyovyote itavyokuwa, mategemeo yapo kwa muombaji mwenyewe, katika kua na moyo kwake pamoja na matumaini (Confidence) mbele ya Mola wake. Kila siku tu anatakiwa awe na matumaini ­ Asikate tama kwa sababu: "Hawakati tamaa illa watu makafiri". Ni kawaida kwa Mwanadamu kuelekeza mambo yake kwa yule ambae anajua ndie mwenye nacho kile akitakacho, na ana matumaini kua atampa au atapata tu kutoka kwake. Basi kuliko kiumbe, Mnyezi Mungu ndie ahakki wa kua na kila tunachokitaka, mradi tu tuweke matumaini ya hali ya juu kua tutapata. Kwa sababu tunamuomba Ambae hapungukiwi hata siku moja. Lakini inapotokea kukosa yale uliyoyaomba, basi jichunguze wewe mwenyewe kwanza kwa sababu Mnyezi Mungu si rahisi kuvunja alichoahidi ­ Huenda sababu ikawa ni yenye kutokana na wewe mwenyewe au ikawa umeyakosea mashrti ya kuomba. Basi jaribu tena utafanikiwa tu Insha Allah. Qur an: Baqara:2:186.

83

"Na waja wangu watakapo kukuuliza hakika yangu (waambie kuwa) Mimi niko karibu nao. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi na waniitikie na waniamini ili wapate kuongoka".

Sharti la Kwanza ni: 1. Kumuitikia Mnyezi Mungu kwani anaita katika wema. 2. Kumuamini Mnyezi Mungu. 3. Unyenyekevu (Tawadhu-i). 4. Woga (Khofu). 5. Tamaa (kua utapata tu ­ Confidence). 6. Kufanza mema haswa wazazi wawili (kwani Bwana Mtume Saw. Amesema: "Ambaye wazazi wake wawili hawako Radhi nae, basi asiwe na haja na mimi". Basi tuzingatie vizuri sharti kabla kujilaumu. Wengine hutanguliza Swadaka kwa kuwapa watoto (hasa yatima ambao wamekatikiwa kabisa), basi Mnyezi Mungu hufurahi na hujibu haraka haraka Dua ya mwombaji. Wengine hulisha masikini kwanza kabla ya kuomba Dua zao. Tuelewe kwamba masikini wako karibu sana kwa Mnyezi Mungu, na ndo maana Bwana Mtume Saw akiwapenda sana. Wao pia Wataingia mwanzo peponi. Bwana Mtume Saw ameeleza kua: "Ameonyeshwa Pepo akaona wengi ya wakazi wake ni masikini, na akaonyeshwa motoni akaona wengi ya wakazi wake ni wanawake". Maswahaba walipomuuliza juu ya wake zao ambao Wanaswali na kufanza khairati chungu nzima ­ Aliwafahamisha Sababu hasa ambayo ndo itofanza wengi waingizwe motoni, nayo ni: a) Kusahau Ihsani za Waume zao kwa kitu kidogo sana. b) Kuwakhini Waume zao. Waombaji wengine hueka Nadhiri kabla maombi yao. Lakini Mnyezi Mungu hakopeshwi, kuliko kutumia siasa ya watoto ya: "Nipe Nikupe". Wewe toa halafu uone utapata au laa? 84.

Ufunguo ndo huo, basi kila tuonapo mafanikio, na Tumswalie sana Bwana Mtume Saw, Kwani ndo Mwalimu Mkuu.

Allahuma Swalli Wasallim alaa Sayyidna Muhammad wa aalihi.

Wabillahi Tawfiq

85.

Vitabu vilivyokwishatoka ni: *1. Maana halisi ya Imaan. (i) (1st, 2nd & 3rd addition). *2. Njia nyepesi ya kuijua nafsi yako. *3. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya uongofu. *4. Knowledge vision & ecstacy. *5. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa Uislamu (i) . *6. Waislamu na Sayansi - Ulu-m. *7. Kuhifadhi Burda. *8. Maana halisi ya Imaan (ii). *9. Muhammad SAW katika ulimwengu wa ghayb. *10. Siri ya Balaa. *11. El makhlouq (Viumbe) *12. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya uongofu. (2nd addition) *13. Manaqib ya Al habbib Sayyeid Al Ma`aruf. *14. Some aspects of concepts of facility in medevial Islamic Philosophy by Mwinyibaraka. *15 maana halisi ya Imaani I (3rd. Addittion) *15. Njia nyepesi ya kuijua Nafsi yako. (2nd addition). *16. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa Uislamu ii. *17. Maana halisi ya Imaani ii (2nd. Addition).

Vitabu ambavyo tunategemea kuvitoa muda si mrefu

(Insha Allah) ni: *1. Mwinyi Baraka katika Ulimwengu wa Uislamu I (2nd. Addi.). *2. Muhammad SAW Bwana wa Mabwana *3. Muhammad SAW katika ulimwengu wa Ghayb. *4. Waislamu na Sayansi - Ulu-m. (2nd addition) Kwa maulizo kuhusu vitabu wasiliana nasi:

Majaalis El Ulaa - El Qadiriyya Sinza,

P.o. Box 15170, Tel: 0747 483553 Tel: 0748 595958. Tel: 0744 023703. Tel: 0741 235091. Tel: 0744 299597.

Dar es salaam.

86.

Ujumbe wa Ahly Majaalis:

Assalam Alaykum:

Ndugu Msomaji lengo la kitabu hiki siyo biashara; Madhumuni makubwa ni kuwa Waislamu wanufaike na mafundisho ya Dini yao, kwani si wengi waliobahatika kupata Ilmu ya madrasa eidha ukubwani au wakati wa utoto wao. Kutokana na gharama za uchapishaji kuwa kubwa ndiyo imetubidi tukiuze kitabu hiki ili kufidia gharama na tuendelee kutoa vitabu vingine. Kama Muislamu yeyote atakuwa yuko tayari kutoa gharama za uchapishaji ili avitowe bure hivi vitabu, basi sisi tuko tayari. Awasiliane nasi ili tufanikishe hilo kwa ajili ya Allah. Wabillahi Tawfiq.

87.

Al habib Al Faqeer Ahmed Sheikh Mohamed Sheikh Msiha, amezaliwa Singida mkoa wa Dodoma, mwaka 1938. Amepata elimu ya sekula Unguja na amebahatika kupata elimu ya juu katika chuo maarufu Afrika ya Mashariki Makerere Uganda. Elimu yake ya Dini ameipata hapo hapo Unguja toka kwa Masheikh mbali mbali, baadhi yao ni: Sheikh Sleiman Alwi (Muhib Rasul) (Al Marhum). Sheikh Seyyid Mansab. Maalim Himid (Al marhum). Maalim Hemed Muhamed El Buhry. Sheikh Mohammed Qamus. Sheikh Muawwiya Ibn Abdul Rahman. Sheikh Ally Muhamed Comorian. Sheikh Ibrahim Mzee Ahd. Sheikh Haj Mzee Ahmad Msiha. Amma Elimu ya Nafsi na Roho Amepata Ijaza yake toka kwa A`limu mkubwa Duniani Al Habib Seyyid Omar Bin Abdallah (Mwinyi Baraka). Sheikh Ahmad amewahi kufanya kazi katika jeshi la Polisi Tanzania Bara katika mikoa mbali mbali mpaka alipostahafu. Katika umri wake wote Sheikh Ahmad alijahid katika kuendeleza Uislamu kwa kusomesha na kuandika vitabu vya mada na maudhui mbali mbali katika Uislamu. Pia alianzisha Majaalis Sehemu mbali mbali ambazo ziko mpaka leo, Mtaa wa Pemba, Sinza, Bungoni, kijito nyama, Sadani (Ilala) na Kibaha (Misugusugu) ambapo ndipo ilipo Dhwariha lake (alipozikwa). Sheikh Ahmad ametwawafu 27. 8. 2001. ( Mwezi 7 jumadda thany 1421 H.R.). Akiwa na umri wa miaka 63, vile vile alivyokuwa akiomba aishi umri ule ule alioshi kipenzi chake Bwana Mtume Muhammad SAW. Insha Allah Mnyezi Mungu amjaze kheri na alizidishie Nuru dhwariha lake (Amin).

Majaalis El Ulaa El Qadiriyya, Sinza Dar es Salam.

Information

106 pages

Report File (DMCA)

Our content is added by our users. We aim to remove reported files within 1 working day. Please use this link to notify us:

Report this file as copyright or inappropriate

234689


You might also be interested in

BETA