Read TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO text version

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KATIKA VYUO VYA MAFUNZO YA MIFUGO (Livestock Training Institutes - LITIs) NA VYUO VYA MAFUNZO YA UVUVI (Mbegani Fisheries Development Centre - MFDC na Nyegezi Fisheries Institute - NFI ) KATIKA MWAKA WA MASOMO 2011 / 2012.

1.

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi inatangaza nafasi za mafunzo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kama ifuatavyo: A. Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo · Stashahada ya Afya ya Mifugo (Diploma in Animal Health - DAH) · Stashahada ya Uzalishaji wa Mifugo (Diploma in Animal Production - DAP) · Stashahada ya Uendelezaji wa Nyanda za Malisho na Udhibiti wa Ndorobo (Diploma in Range Management and Tsetse Control -DRMTC) · Stashahada ya Ufundi Sanifu wa Maabara Mifugo (Diploma in Veterinary Laboratory Technology DVLT) na · Astashahada ya Afya na Uzalishaji Mifugo (Aimal Health and Production Certificate - AHPC). B. Vyuo vya Mafunzo ya Uvuvi · Stashahada ya Ubaharia (Master Fisherman Diploma (DMF ­ NTA 6) - Mbegani · Stashahada ya Uchakataji, Masoko, Udhibiti na Ubora wa Samaki (Fish Processing, Quality Assurance and Marketing Diploma (DFP ­ NTA 6) - Mbegani · Stashahada ya Ufugaji Samaki (Aquaculture Diploma (DAQ - NTA 6) - Mbegani · Stashahada ya Sayansi na Teknología ya Samaki (Fisheries Science and Technology Diploma (DFST­ NTA 6) ­ Nyegezi · Stashahada ya Usimamizi na Teknología ya Samaki (Fisheries Management and Technology Diploma (DFMT ­ NTA 6) ­ Nyegezi · Astashahada ya Teknología ya Samaki (Fisheries Technology Certificate (FTC) NTA 4 &5) Mbegani · Astashahada ya Uchakataji na Masoko ya Samaki (Fish Processing and Marketing Certificate (CFP) ­ NTA 4 &5) - Mbegani · Astashahada ya Ufugaji Samaki (Aquaculture Certificate (CAQ - NTA 4 &5) - Mbegani · Astashahada ya Sayansi na Teknología ya Samaki (Fisheries Science and Technology Certificate (CFST­ NTA 4 &5) ­ Nyegezi · Astashahada ya Usimamizi na Teknología ya Samaki (Fisheries Management and Technology Certificate (CFMT ­ NTA 4 &5) ­ Nyegezi

2.

Katika mwaka wa fedha wa 2011/2012 Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi itagharamia mafunzo kwa sehemu kubwa na wazazi / walezi watachangia kidogo. Mafunzo yatatolewa kwenye Vyuo vyake sita (6) vya Mifugo na viwili (2) vya Uvuvi, na inakadiriwa kutoa nafasi za mafunzo zipatazo 800.

3.

Wizara inakaribisha maombi kutoka kwa vijana waliomaliza Kidato cha Sita na wale wenye Astashahada katika fani zinazohusiana na kozi wanazoomba kwa ajili ya kujiunga na mafunzo ngazi ya Stashahada. Pia vijana waliomaliza Kidato cha Nne kwa ajili ya kujiunga na mafunzo ngazi ya Astashahada. Vyuo vitakavyohusika na mafunzo hayo ni kama inavyooneshwa hapa chini: No 1 2 3 4 5 6 7 8 Chuo LITI Tengeru LITI Buhuri LITI Mpwapwa LITI Morogoro LITI Madaba LITI Temeke MFDC Mbegani NFI Nyegezi Anuani S.L.P 3101 Arusha S.L.P 1483 Tanga S.L.P 51 Mpwapwa S.L.P 603 Morogoro S.L.P 568 Songea S.L.P 9254 DSM S.L.P. 83 Bagamoyo S.L.P. 1213 Mwanza Simu 027 255 3187 au 0754 313617 0754 091461 au 0712 398064 026 2320884 au O712 581367 023 2604366 au 023 2604367 0784 716219 0713 441829 au 0768 156625 0754 688099 0754 650996 Kozi zitolewazo DAH, DAP & AHPC DAP DAH, DAP & AHPC DAH, DAP, DRMTC & AHPC DAP & AHPC DVLT (Kutwa) DFM, DFP, DAQ,CFP, CFT na CAQ DFMT, DFST, CFST na CFMP

4.

5

Sifa za mwombaji

A. Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo i) Stashahada · Awe amemaliza na kufaulu elimu ya Kidato cha Sita na kufaulu masomo matatu ya Sayansi kati ya (Baiolojia, Kemia, Fizikia, Hisabati na Sayansi ya Kilimo). Ngazi ya chini ya kufaulu itakayomwezesha muombaji kukubaliwa ni kuwa na kiwango cha angalau subsidiaries mbili kwenye masomo ya sayansi. AU · Awe amemaliza mafunzo ya cheti (Astashahada) katika fani ya Animal Health and Production (AHPC), Agrovet au Certificate in Agriculture and Livestock Production (CALP) ii) Astashahada Awe amemaliza Kidato cha Nne na kufaulu masomo matatu ya sayansi kati Fizikia, Hisabati na Sayansi ya Kilimo) na kufaulu katika daraja la tatu. B. Vyuo vya Mafunzo ya Uvuvi i) Stashahada · Awe amemaliza na kufaulu elimu ya Kidato cha Sita na kufaulu masomo matatu ya Sayansi kati ya (Baiolojia, Kemia, Fizikia na Hisabati). Ngazi ya chini ya kufaulu itakayomwezesha muombaji kukubaliwa ni kuwa na kiwango cha angalau subsidiaries mbili kwenye masomo ya sayansi. AU · Awe na Astashahada NTA ­ 5 kwenye fani inayohusiana na kozi anayoiomba. ii) Astashahada Awe amemaliza Kidato cha Nne na kufaulu masomo matatu ya sayansi kati Fizikia na Hisabati) na kufaulu katika daraja la tatu. ya (Baiolojia, Kemia,

ya

(Baiolojia,

Kemia,

6. Masharti ya Uombaji · Mwombaji atume maombi ya kozi anayotaka kusomea akiambatanisha nakala (photocopies) za vyeti vyake pamoja na cheti cha kuzaliwa. · Watakaochaguliwa watatumiwa fomu za kujiunga na Chuo (joining instructions) zitakaozowajulisha tarehe ya kuanza masomo na masuala mengine muhimu. Ni muhimu kuweka anuwani sahihi katika barua ya maombi.

7.

Gharama za Mafunzo i) Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Mzazi / Mlezi atachangia Tshs 300,000 kwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza. Aidha, kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili aliyejiunga na Chuo 2010 / 2011 mzazi / mlezi watachangia Tshs 250,000. Mchanganuo wa fedha hizi umeainishwa kwenye fomu za kujiunga na chuo `Joining Instructions'. ii) Vyuo vya Mafunzo ya Uvuvi Mzazi / Mlezi atachangia Tshs 400,000 kwa kila mwaka kwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili. Mchanganuo wa fedha hizi umeainishwa kwenye fomu za kujiunga na chuo `Joining Instructions'.

8.

Utaratibu wa kutuma maombi Maombi ya kujiunga na mafunzo yatumwe kwa: Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi S.L.P 9152 Dar es Salaam AU Kwa Mkuu wa Chuo husika kwa kutumia anuani kama inavyooneshwa kwenye namba 4 hapo juu.

9

Mwisho wa kupokea maombi Mwisho wa kupokea maombi ya kujiunga na chuo ni tarehe 30.06.2011.

10.

Majina ya watakaochaguliwa Majina ya watakaochaguliwa yatatangazwa kwenye magazeti ya Habari Leo na Daily News na kwenye tovuti ya Wizara: www.mifugo.go.tz (Home page: Click: Livestock ResearchCoordi nation, or Training and Extension)

Information

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO

3 pages

Find more like this

Report File (DMCA)

Our content is added by our users. We aim to remove reported files within 1 working day. Please use this link to notify us:

Report this file as copyright or inappropriate

318277