Read final-jarida1.pdf text version

Jarida la 001 Aprili - Juni 2010

Sanaa WA NA UFUNDI

WASWAHILI

2010 Mwaka wa Matarajio Mengi kwa TUSIMA Lamu

Tamasha za Kitamaduni Lamu na Mombasa

Uundaji wa Istllahi katika Lugha ya Kiswahili

TUSIMA NI KURUGENZI YA MAKAVAZI YA KITAIFA YA KENYA.

RISSEA NEWSLETTER LAUNCHING

The exalted welcome, of stature and respect In this congregation, of our good heritage In Lamu Mombasa, serving the public The purpose and objective, is to make you aware In our coastal stations, a newsletter we initiate Thanks to our sponsors, their generosity is sustained Lets join our hands, this institute we drive Students you bring, our heritage we teach Customs and culture, all we teach To indigenous and strangers, all are welcome Anyone who comes to the institute, with joy we take I HeR reads of culture, of the life of Swahili R I

H CR A E S E ESEARCH

A C I R F A N R E T S A E F O S E I D U T S I L I H AW S F O E T U T I T S N

NSTITUTE OF

S WAHILI S TUDIES

OF

E ASTERN A FRICA

From the arena we depart, his poem is enough And now look a play we show Amira and Nabhany, this composition they end

R ESEARCH I NSTITUTE

OF

S WAHILI S TUDIES

OF

E ASTERN A FRICA

Neno kutoka kwa Mwenyekiti

BODI YA WAKURUGENZI YA MAKAVAZI YA KITAIFA YA KENYA

" kutimiliza lengo la Kiswahili kuwa lugha (ya taifa) rasmi katika katiba mpya iliopendekezwa. "

wa niaba yangu na ya Bodi ya Wakurugenzi ya Makavazi ya Kitaifa ya Kenya, nachukua fursa hii kuipongeza Taasisi ya Utafiti wa Waswahili ya Mashariki mwa Afrika (TUSIMA) kwa toleo la kwanza la jarida lao. Naamini kwamba hatua hii muhimu itasaidia pakubwa kujuza kazi na mafanikio ya Taasisi bali pia kufahamisha ummah juu ya kazi za taasisi hii muhimu ya Makavazi ya Kitaifa ya Kenya hasa wakati huu wa majadiliano ya Katiba. Fauka ya hayo, twatarajia taasisi itaongeza maradufu juhudi zake kutekeleza wajibu wake kwa kuja na utafiti muafaka na kuleta washika dau wote pamoja ili kufikia na kutimiza lengo la Kiswahili kuwa lugha (ya taifa) rasmi katika katiba mpya iliopendekezwa. Hili liende sambamba na kuendelea kufanya utafiti wa kitaaluma na kuyatangaza matokeo hayo katika makongamano na maonyesho yatakayoleta ufahamu wa tafsili wa jamii ya Waswahili na utamaduni wao.

K

Nikimalizia, haya yote yataruka patupu ikiwa matokeo ya tafiti na shughuli zingine hazitafaidisha jamii moja kwa moja. Kwa hivyo, twatarajia TUSIMA itabuni miradi ambayo itawahusisha wanajamii sio kupata ilimu yao tu bali pia kuwafaidi wao moja kwa moja. Aidha, ni matumaini yetu kwamba hatua hii ni mojawapo ya hatua za kuifanya TUSIMA kuwa taasisi ya kimataifa kama ilivyoruwazwa katika utumishi wake.

Bw. Issa A. Timamy Mwenyekiti, Makavazi ya Kitaifa ya Kenya.

FAIRDEAL

u p v c , a l u m i n i u m & g l a s s

MOMBASA

P. O. Box 91045-80103, Mombasa ,Kenya. Mombasa: Tel: 041 47168,1. Mobile Tel: 0721 786430 Email: [email protected] Nairobi Tel: 0726 826 752 P. O. Box 15309-00509, Nairobi, Kenya. Email :[email protected]

3

Neno kutoka kwa Mkurugenzi mkuu

MAKAVAZI YA KITAIFA YA KENYA " Mikakati mujarab ya mawasiliano ni lazima kwa kufaulisha na kuendeleza taasisi na jarida hili ni hatua muhimu kwa TUSIMA. "

K

aribuni nyote katika toleo hili la kwanza la jarida la TUSIMA. Naipongeza TUSIMA kwa kuwa mstari wa mbele kutangaza shughuli zake na miradi yake. Mikakati mujarab ya mawasiliano ni lazima kwa kufaulisha na kuendeleza taasisi na jarida hili ni hatua muhimu kwa TUSIMA.

muhimu na kujikusuru kwao kukubwa kuhakikisha uhifadhi bora na usimamizi mzuri wa turathi zetu za kitaifa. Yote tuliyoyataja hapo juu yanaonyesha umuhimu tunaowekea uhifadhi wa turathi ya kitamaduni ambao ni kiini cha utambulisho wa jamii na hadhi yake. Kwa mintarafu hii, taasisi zetu za utafiti ikiwamo TUSIMA, itafanya tafiti na kuyaeneza matokeo yake katika jarida kama hili, juu ya njia muafaka za kuwafaidisha kiuchumi jamii husika kupitia tamaduni zao. Hili litaafikiana vilivo na Ruwaza ya 2030 na Malengo ya Maendeleo ya Karne Kumi.

TUSIMA, idara mojapo katika Makavazi ya Kitaifa ya Kenya (MKK), ilibuniwa ili kuziba mwanya ulioko wa utafiti na masomo ya utamaduni ya Waswahili, mapishi, historia, na turathi majenzi ambayo ni kiini hasa cha majukumu ya MKK. Jarida hili kwa hivo ni hatua muhimu katika kutekeleza jukumu hili. Mwaka wa 2010, ukiwa ndiyo mwaka tunaosherehekea karne moja ya uhifadhi wa turathi, shughuli kama hizi huangazia si tu tafrija nyingi tulizoziandaa kusherehekea mafanikio yetu bali pia husaidia kutuweka karibu na jamii kwa kuonyesha michango

Dkt. Idle O. Farah, Mkurugenzi Mkuu.

FAIRDEAL

f u r n i t u r e

MOMBASA

P. O. Box 88156, Mombasa Kenya Mombasa: Tel: 041 2230403. Malindi: Tel: 020 2136576 Email: [email protected] Nairobi: Tel: 020 829051 Nakuru: Tel: 020 2351166 Website: www.fairdealgroup.biz

4

TUSIMA: KITUO CHA ILIMU NA UTAFITI KWA MAENDELEO YA LUGHA YA KISWAHILI NA UTAMADUNI

Prof. Mohamed Hassan Abdulaziz, Mwenyekiti, Bodi ya TUSIMA

"Kimekubaliwa kama miongoni mwa lugha rasmi za majadiliano katika Umoja wa Afrika, na kimependekezwa kama miongoni mwa lugha za kazi za Umoja wa Mataifa. "

T AASISI

YA

U TAFITI

WA

W ASWAHILI

YA

M ASHARIKI

MWA

A FRIKA

K

ulingana na muhtasari wa shughuli zilizopendekezwa za TUSIMA, napendelea kusisitiza masuala ya ilimu na utafiti katika maendeleo na usasaji wa lugha ya Kiswahili. Amali kuhusu utamaduni wa Waswahili, sanaa na ufundi zajitokeza kwingine katika jarida hili na mapendekezo kadhaa ya taasisi hii. Kuundwa kwa taasisi hii umekuja katika wakati muafaka kabisa katika eneo hili la Mashariki ya Afrika. Huku Kenya, mbali na Kiswahili kuwa ni lugha ya kitaifa sasa imependekezwa katika Katiba Kielelezo kuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza. Kutokana na kuenea kutumika kwake katika sehemu hizi za Afrika Mashariki, Kiswahili kimetambulika kama hazina kubwa ya lugha, na pia lugha tajika itakayoleta maendeleo katika fungamano la kiuchumi, kijamii, kisiasa,na kitamaduni. Kwa dhumuni hili, Tume ya Kiswahili ya Afrika Mashariki imeundwa ili kuendeleza lugha hii katika Afrika Mashariki. Fauka ya hayo, Chuo cha Lugha za Kiafrika kimekitaja Kiswahili kama chombo muhimu mipakani. Kimekubaliwa kama miongoni mwa lugha rasmi za majadiliano katika Umoja wa Afrika, na kimependekezwa kama miongoni mwa lugha za kazi za Umoja wa Mataifa.

makamusi mahsusi, orodha za maneno na misamiati katika nyanja mbalimbali kama sheria, utawala, uchumi, matibabu, viwanda na kilimo. Taasisi hii itawahimiza wataalamu wa kitaifa na kimataifa kuja na kukitumia chombo hiki wakati wa mapumziko yao (mafupi au marefu). Taasisi kinapanga kuanzisha mafunzo kwa wanafunzi wa humu nchini au wa kutoka ng'ambo ambao wangependelea kukaa muhula mmoja wakijifunza mengi kuhusu lugha na utamaduni wa Waswahili. Amali kama hii itahitaji kuanzisha usajili na uwasilianaji na vyuo vya eneo hili, vya kiafrika, vyuo vya kutoka ng'ambo na taasisi zinginezo wastani. Wanafunzi wanaofanya utafiti wa Uzamifu watahimizwa watumie baadhi ya muda wao hapo TUSIMA. Taasisi hii kama taasisi nyingine tajika ya utafiti itabidi ianzishe jarida la utafiti ili iweze kuchapisha makala katika nyanja mbalimbali za masomo ya Kiswahili na makala mengineyo muhimu. Ili kufikia malengo yaliopendekezwa, lazima kuwako na sera na mikakati bayana. Kuendelezwa miundo msingi ya taasisi, vifaa vyake na wafanyakazi yanaweza kupangwa katika awamu yakinifu za mhula mfupi, wastani na mrefu. Taasisi ina mipango ya kujitengezea mapato kwa kukodisha nafasi kwa sababu ya mihadhara ya kijamii na makongamano. Bidhaa zitakazotengenezwa na Idara ya Sanaa na Ufundi zitanunuliwa na wateja anuai wakiwamo watalii. Kuandaa mapishi ya Kiswahili pia yataleta mapato mazuri kwa taasisi. Inatarajiwa kwamba rai hizi zitajadiliwa rasmi wakati wa mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi ya TUSIMA unaotarajiwa kufanywa mnamo wiki ya tatu ya Aprili 2010.

Kupanda ngazi kwa Kiswahili na kuwa lugha ya kisasa ya kimataifa kunahitaji uendelezaji na upangaji wa kina kama lugha ya kisayansi na kiteknolojia, na pia kama lugha mujarab ya mawasiliano hapa Afrika. Hapa ndipo taasisi kama TUSIMA inahitajika kuendelezwa kama taasisi ya utafiti ili kutekeleza sera za maendeleo na mipango za nchi husika za Afrika Mashariki. Ili kutimiza malengo ya utafiti, taasisi hii inahitaji vifaa msingi na wafanyakazi. Kwa hivi sasa, taasisi inalo jengo la kisasa lenye nafasi kundufu linaloweza kubeba vifaa vya utafiti kama:a) Chumba shehena cha filamu na radio b) Maktaba ya vitabu vya Kiswahili c) Mahala pa kuhifadhi miswada na stakabadhi zinazohusiana na lugha, fasihi na utamaduni wa Kiswahili d) Mahala pa kusoma na kutafiti e) Madarasa na chumba cha tarakilishi TUSIMA itafanya kazi na taasisi nyingine katika Afrika Mashariki zinazojihusisha na uendelezaji wa Kiswahili hasa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam. Taasisi hii ina tajriba kuu katika uendelezaji wa Kiswahili. Mawanda ya ushirikiano yatakuwa pamoja na uandishi na urejeleaji wa

5

Shughuli zinazoendelea na maono ya mbele katika TUSIMA

Bw. Kassim M. Omar, Kaimu Mkurugenzi,TUSIMA.

" harakati za kukifanya lugha rasmi pamoja na Kingereza katika Katiba Kielelezo, "

T

aasisi ya Utafiti wa Waswahili Mashariki mwa Afrika (TUSIMA) ilibuniwa mwaka 2000 na kustakiri katika mwaka 2004. TUSIMA ilianzishwa ili kuratibisha utafiti juu ya Waswahili. Makavazi ya Kitaifa ya Kenya ndilo shirika stahiki la kuendeleza juhudi hizi kwa vile lina sifa kuu katika utafiti kwenye nyanja mbalimbali na muhifadhi wa turathi za kitamaduni za Kenya. Makao makuu ya TUSIMA yako Mombasa na mwane chuo kiko Lamu. Kutokana na uenezi na maendeleo ya Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano katika eneo hili na harakati za kukifanya lugha rasmi pamoja na Kingereza katika Katiba Kielelezo, taasisi hii inatarajiwa kuwa mahala pa marejeleo yote kuhusu maendeleo ya lugha kwa serikali, mashule na taasisi za masomo ya juu. Humu mwetu, taasisi hii ilitarajiwa iwe ndiyo mahala pa murajaa kwa Baraza la Kiswahili la Afrika Mashariki. Na katika Afrika, Kiswahili kimependekezwa kuwa moja kati ya lugha tano zitakazopigiwa debe katika Umoja wa Afrika kwa fadhila za Chuo cha Lugha cha Afrika ,hivo Kiswahili kinaweza kutumika kama wasila wa tangamano la kiuchumi, kisiasa, na kijamii barani. Hili litakuwa na athari ya kuleta utulivu zaidi na masikizano zaidi kama yanavyoruwazwa katika Ruwaza ya 2030 na makala mingineyo ya maendeleo.

Malengo Wakati wa kubuniwa kwake, malengo ambayo ilitarajiwa kuyafikia ni pamoja na: · Kuhakikisha uwasilianaji , utangamano wa tafiti na masomo timilifu kuhusu uswahili na jamii ya Waswahili. · Kufufua mafunzo na utengenezaji wa kazi za asili za sanaa na ufundi kwa sababu ya kutoweka ufundi na usanii asli wa Kiswahili na kusababisha maafa kwa hadhi na historia ya Kiswahili · Kuvumbua na kutekeleza mikakati maalumu ya kuzitangaza bidhaa na huduma za taasisi. Haswa haswa kutangaza sanaa na ufundi wa kiasili wa Kiswahili, mafunzo na miradi ya utafiti pamoja na tamasha na masuala ya waswahili. · Kushinikiza na kutetea utunzi na utekelezaji wa sera afiki za TUSIMA zenye kulenga kuboresha utoaji wa huduma na utafiti bora kutoka idara hii. Kufaulisha uhusiano na ushirikiano na taasisi nyingine za humu nchini na za kimataifa katika nyanja za utafiti na mafunzo. Mafanikio yetu Tangu ilipobuniwa taasisi hii, kwa muda mchache wa kuwako kwake na ari yake ya kutaka kutimiza shabaha zake, imejaribu kupata mafanikio yakiwamo: 1. TUSIMA imefanya mkataba na Chuo Kikuu cha London, ambapo wanafunzi wao wanakuja kutekeleza baadhi ya masomo yao na TUSIMA. Watafiti wengi wamegundua taasisi hii na kukifanya chuo chao na wengi wanaongezeka. 2. Ujenzi wa jumba la hazina ya Kiswahili litakalowashawishi watafiti wengi kuja na kufanya utafiti wao na kujifunza mengi kuhusu uswahili. 3. Taasisi ilishua tamasha la utamaduni wa waswahili katika mwaka wa 2008 na la pili likafanyika 2009. Tunatarajia kuliendeleza kadri tunavyosonga mbele. 4. Taasisi hii pia imefanya vikao vya mihadhara na majadiliano wakati wa tamasha za Lamu na Mambasa ambapo jamii inapawa fursa ya kujadili masuala muhimu yanayowaathiri maishani kama ilivyofanyika 2009 kwa kupatikana Azimio la Fort Zahidi Ngumi lililohusu ujenzi wa bandari mpya Lamu.

...endelezo uk.7

Hii ni moja wapo wa kazi zinazofanyika katika kitengo cha usaramala na kuchonga mbao

6

Siku za usoni Ajenda kubwa ambayo taasisi hii muhimu katika eneo hili inayo ni kuitangaza kupitia mifumo yote ya mawasiliano ili ipate kujulikana. Matumizi ya mtandao utatusaidia kukifunua kwa walimwengu wakiwamo watafiti, wateja anuai, wanafunzi wa sasa na wa zamani ili huduma zetu zijulikane na kutakwa na kila mtu au shirika. Haya yatakwenda sambamba na kukitilia nguvu chuo pamoja na kiwanda cha ufundi cha bidhaa za mbao na ufumaji wa Kiswahili.

wao, and mambo mengi mengine. Hali kadhalika twataraji kuendelea kuifanya tamasha la utamaduni ya Mombasa na pia kushiriki katika tamasha la kitamaduni la Lamu na tamasha la Maulidi ya Lamu. Ili kupata wateja wengi wenye kutuzuru sisi, kama wajibu wake wa kufufua usanii na ufundi wa Waswahili, taasisi itafufua na kukikarabati kiwanda cha usanii na ufundi wa Waswahili katika siku za hivi karibuni na kuendelea kuendesha masomo ya mbao kwa wavulana na kushona na kufuma kwa wasichana. Mwakani tutajaribu kutia vifaa zaidi kiwandani ili kuhuisha utengenezaji wa vyombo asli vya Kiswahili na kupata fedha zitakazotusaidia na pia kuwapa mafunzo ya hapo kwa hapo vijana wa mitaani ili wanufaike. Halafu kutatengenezwa ukumbi wa maonyesho ya vyombo hivi ili wateja zaidi watambue bidhaa zetu. Ukumbi mkubwa wa jumba la Swahili Centre pamoja na nafasi zilizoko zitakodishwa kwa watu kama kumbi za mikutano na makongamano.

Taasisi hii itabuni mikakati shikamanifu ambayo itafungamana na idara nyinginezo za Makavazi ya Kitaifa ya Kenya ili ipate mafanikio makubwa katika rasilimali zilizoko sasa na ushirikiano baina yao ili kutimiza wajibu wake. Katika muhula wa sasa tutajaribu kuunda na Wanafunzi wa SOAS kutoka chuo kikuu cha kutilia nguvu maktaba ya kisayansi London wakiwa safarini kuzuru Kisiwani Wasini na kiutamaduni kwa watafiti, Mustakbali wa TUSIMA ni mzuri tena wanafunzi na ummah kwa jumla. Maktaba hii itakapokamilika adhimu walakini ukiona vyaelea juwa vimeundwa na safari ya kesho itakuwa na vyombo mahsusi vya Waswahili na benki ya vitu kama hufunganywa leo. Mikakati lazima iwekwe kuona kwamba mipango vitabu muhimu, miswada, santuri, picha, kanda za tepu na vitu yote ya kuirutubisha taasisi imetiwa kazini na usaidizi wa kila vinginevo kuhusu utamaduni na historia ya Waswahili. mfadhili lazima utafutwe ni kutokana na ushirikiano baina yetu na wahisani wa kiserikali na kibinafsi ndiyo utakaofaidi taasisi hii na Taasisi pia itaendeleza na kutilia nguvu miradi yake ya kuwafikia kuifanya ifikie malengo yake. wananchi katika maudhui mahsusi ya Waswahili kama tamasha la kitamaduni la uswahili, chakula chao, mavazi yao, majenzi yao, uvuvi

u p v c , a l u m i n i u m

FAIRDEAL

&

g l a s s

MOMBASA

P. O. Box 91045-80103, Mombasa ,Kenya. Mombasa: Tel: 041 47168,1. Mobile Tel: 0721 786430 Email: [email protected] Nairobi Tel: 0726 826 752 P. O. Box 15309-00509, Nairobi, Kenya. Email :[email protected]

7

T

TAASISI YA UCHUNGUZI WA WASWAHILI YA MASHARIKI MWA AFRIKA (TUSIMA) NA BI. RUKIYA HARITH SWALEH

aasisi ya uchunguzi wa Waswahili ya Mashariki mwa Afrika ni taasisi iliyo chini ya Makavazi ya Kitaifa ya Kenya yenye dhima ya kutafiti, kukusanya na kuandika mambo yanayohusiana na Kiswahili. fursa ya kujumuika na kukaa na Waswahili ili washuhudie maisha halisi ya Waswahili. Safari fupi za kuzuru makazi/maeneo ya kale ya Waswahili zinaandaliwa kama vile magofu ya Jumba-la-Mtwana, Gede, Shimoni, Wasini na kadhalika. Katika kufanikisha mafunzo, taasisi imeandika kitabu cha kufunzia Kiswahili na Kitabu cha mazoezi kwa wanafunzi wa Kiswahili.

Ni taasisi isiyo na lengo la kupata faida bali ina lengo la kufikia daraja ya juu katika utafiti na mafunzo ya Kiswahili. Ina makao yake makuu Mombasa, ina chuo kidogo Lamu na afisi katika makao makuu ya Makavazi ya Kitaifa ya Kenya.

Wanafunzi wa kimataifa na Mkufunzi Rukiya(Katikati)

Vijana wakiterema kwa bashasha na ngoma ya shabwan wakati wa tamasha la tatu mjini Mombasa

Taasisi hii hutekeleza majukumu yafuatayo katika chuo cha Mombasa: Mafunzo: Kwa sababu ya kukua kwa lugha ya Kiswahili hadi kimataifa wageni wengi wanaoipenda lugha ya Kiswahili, wanafunzi na watafiti wanapenda kujihusisha na kushirikiana na TUSIMA katika kutafiti zaidi juu ya historia, utamaduni na lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo wanafunzi wa taaluma mbali mbali kama vile akiolojia, anthropolojia, elimu jamii (sosholojia), sheria na jenetiki waja ili wasome Kiswahili waweze kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili au kuwawezesha kufanya utafiti wao. Hadi leo wanafunzi wengi wamepitia katika taasisi hii wakifanya shahada zao za kwanza, za uzamili au za uzamifu. Taasisi hii pia inajitahidi kuwa na ushirikiano na taasisi nyingine au vyuo vikuu ili kuiwezesha taasisi kufikia malengo yake ya kufunza na kufanya utafiti. Chuo Kikuu cha London kupitia `School of Oriental and African Studies' walifanya makubalilano na TUSIMA, ambapo wanafunzi kutoka SOAS huja kusoma masomo ya Kiswahili wanayoyaita "Swahili Year Abroad Programme". Wanafunzi wa kwanza walikuja TUSIMA mwaka wa 2005, wakiwa wanafunzi tisa (9) na mwaka wa 2010 ni mwaka wa sita (6), SOAS inaleta wanafunzi wake TUSIMA. Wanakuja kwa wiki kumi na moja kuanzia Januari hadi Machi kila mwaka. Wanapokuja wanafunzwa historia na maendeleo ya Bi.Rukiya Harith Swaleh Kiswahili, lugha, fasihi na Mkufunzi Mkuu,TUSIMA- Sehemu utamaduni. Pia wanapata

ya kisomo cha Kiswahili

Mwaka wa 2008, TUSIMA ilianzisha Tamasha za Kitamaduni za Waswahili Mombasa, na ni sherehe za kila mwaka. Hii ni katika kuhifadhi na kutunza tamaduni za Waswahili. Katika tamasha ya mwaka jana (2009) kulikuwa na ngoma za Waswahili, mashindano ya heena, mashindano ya mashairi na mihadhara inayoongeza ladha ya kitaalamu kwa tamasha hizo. Katika miaka ya baadaye, taasisi ina miadi ya kupanua tamasha hizi kwa kuongeza mambo mengi ya kitamadunI, ili kuweza kufikia malengo ya tamasha. Katika kutimiza malengo ya kiakademia na pia kuhakikisha taasisi inafikia kiwango cha Kimataifa, maktaba ya kisasa yenye vifaa vyote muhimu iko karibu kukamilika ambayo itaifanya taasisi kutoa huduma bora za utafiti na masomo. TUSIMA pia inajizatiti kuwa na ushirikiano na vyuo vikuu vya hapa Kenya na vya kimataifa katika nyanja za utafiti na mafunzo. Uhusiano huu utaendelezwa kwa njia inayostahiki baina ya taasisi na taasisi hizo nyingine. Kama taasisi changa inayokua, changamoto kubwa inayoikumba ni ukosefu wa vifaa vya kutosha ili kuifanya itekeleze lengo lake kuu la utafiti, ushirikiano huu na taasisi nyingine itaifanya TUSIMA kufaulu.

8

USIMA mwane chuo Lamu kimefanya maendeleo mengi ili kutekeleza wajibu kama taasisi. Mafanikio ambayo yamepatikana mpaka sasa ni pamoja na kufanyika mihadhara katika tamasha zote mbili za Lamu na pili, kupatikana kwa Azimio la Ngome ya Zahidi Ngumi wakati wa tamasha la Maulidi ya Lamu. Azimio hili lilikuwa natija kubwa kwa kazi iliojumuisha wataalamu wakubwa wa masuala ya kijamii na kiuchumi waliojumuika kupiga darubini suala la ujenzi wa bandari huku Lamu iliopendekezwa na serikali. Azimio hili lilitayarishwa kama Mkataba na alipawa Waziri Chirau Ali Mwakwere ambaye aliupokea kwa niaba ya serikali na kuahidi kushughulikia masuala yaliomo. TUSIMA Lamu ilifuatisha mapendekezo ya azimio hili na mjadala kuhusu utandawazi na namna gani wanati wa sehemu hii wanatarajiwa kuuchukua na kuupiga pambaja wakati wa maendeleo ya haraka sana. Fauka ya hayo, TUSIMA Lamu ikishirikiana na Kuliya ya Riyadha iliweza kufanya maonyesho ya ushauri wa kazi uliohusisha vyuo vikuu na vyuo vya kati vya humu nchini. Haya yalifanyika Jumamosi ya tarehe 28 Machi 2009 ikiwa na nia ya kuamsha wanafunzi juu nafasi za kazi zitakazojitokeza wakati bandari iliopendekezwa itakapoanza kufanya kazi.

T

2010 MWAKA WA MATARAJIO MENGI KWA TUSIMA LAMU

NA BW. MOHAMMED KARAMA

kutayarisha na kuonyesha kipindi cha chakacha na ilhali hii ni ngoma tukufu kwa Waswahili. Mwaka wa 2010 waonekana utakuwa na shughuli nyingi na mafanikio mengi. Kwa hivi sasa mgeni wetu katika taasisi yetu ni Bwana Darren Ray ambaye ni mtahiniwa shahada ya Uzamifu katika Chuo Kikuu cha Virginia, nchini Marekani. Yeye anamili utafiti wake katika historia na mambo yote yanayohusiana na maulidi. Pia wanafunzi wa chuo cha SOAS kutoka Uingereza wamewasili tayari Mombasa na wanatarajiwa wakati wowote kufiika Lamu na kukamilisha mafunzo yao. TUSIMA Lamu ikishirikiana na Idara ya Elimu ya Makavazi ya Lamu imepanga mwaka huu kuita wataalamu na maafisa wa serikali kuja na kutoa mihadhara katika mfululizo wa mihadhara iliopangiwa kufanyika kila baada ya miezi miwili. Mihadhara hii inanuia kufaidi watu wote wakiwemo wanafunzi na wafanya kazi kwa jumla.

Umahiri wa wanafunzi kwenye tamasha la maonyesho ya Lamu

Kazi ya kutia darizi katika kitengo cha kushona cha Lamu wakionyesha ustadi wao wakufuma kwa mkono

Jambo jingine kuu lililotukia mwaka jana ni kuzinduliwa tena sherehe ya kufuzu kwa wanafunzi wa Kituo cha Utamaduni wa Waswahili katika Lamu mnamo Novemba 26. Wanafunzi kumi na tano walipawa shahada zao na kupawa ijaza ya kuenda kujenga taifa watakapokuwa nje. Kabla ya hapo walikuwa wamemili katika masomo ya ushonaji nguo na ufumaji wa vitambaa kwa miaka miwili. Mgeni wa heshima katika hafla hii alikuwa mhadhiri wa Swafaa Academy ndugu Zeinab. Kituo hiki pia kiliwakilishwa katika tamasha la kitamaduni hapa Lamu na wanafunzi waliweza kuonyesha ufundi wao wa kushona na kufuma. Wakati wa Kongamano la Kisayansi la Pili la MKK TUSIMA Lamu iliwakilishwa na Mohamed Karama ambaye aliwasilisha karatasi yenye tasnifu ya kutumia Kiswahili kama chombo cha kuunganisha makabila yote hapa Kenya baada ya yaliyotokea humu nchini baada ya kura za 2007. TUSIMA Lamu ilidhihirisha ukakamavu wake wa kulinda na kutetea hadhi ya utamaduni wa Kiswahili wakati ilipoandikia Shirika la Utangazaji la Kenya kuhusu utovu wake wa

Lamu inajinaki kwa ushairi na TUSIMA Lamu inafanya kila jitihada kuanzisha chombo ambacho kitajihusisha zaidi na ushairi wa mapokeo. Chombo hiki kitahusisha washairi wa kutoka huku na pia kukuza vipawa vya washairi chipukizi. Pia chombo hiki kitakuwa kama kamusi la marejeleo yote kuhusu uswahili. Kuambatana na haya, TUSIMA Lamu itajaribu mwaka huu kuanzisha kilabu cha wanasayansi wachanga katika shule za upili hapa Lamu. Hii ni kwa sababu wanafunzi hawa tunawakuza ili waje wafaidi jamii yao na vile vile tunawatia motisha ya kusoma zaidi na kufanya bidii katika masomo yao.

Bw. Mohammed Karama

9

UUNDAJI WA ISTILAHI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI NA: PROF. AHMED SHEIKH NABHANY

Uundaji wa Istilahi katika lugha ya Kiswahili si jambo geni tokea zamani. Waswahili wa kipata neno katika lugha nyingine la kiulimbe au la kitaalamu lolote ambalo laweza kuwafaa kulitumia katika lugha yao na wao hawana. Kwanza kabla ya kuliunda hulitafuta katika ndimi za Kiswahili ambazo ni zaidi ya kumi na Tano (15) ikiwa halikulipatikana hapo ndipo wakae katika jopo lao waliunde neno hilo kulingana na sharia zake, nazo ni:(1) Utenda kazi (2) Umbo (3) Sauti Hapo kale Waswahili walilipata neno la Risasi ambalo ni neno la Kiarabu (Bullet) hapo walitizama utendakazi wake nao ni:Risasi ikitiwa katika mrau (Bunduki) ikifetuliwa hutowa cheche kwa pamoja, cheche kwa lahaja ya kiamu ina maana tatu (3) (1) Tete (2) Kialia (3) Kiyandi Wakapendelea kuchukua kiandi nakutizama utenda kazi wake, nao ni kutowa cheche kwa pamoja wakakiita kiyandi pota na maana (1) Kiyandi ni cheche (2) Pota kutoka cheche kwa pamoja Kifetuliwa risasi inatowa cheche kwa pamoja, kwa hivyo lilitumika jina hilo katika lugha ya Kiswahili. Hapa tizama shairi la Bwana Bakari Bin Jabir kwa niaba ya chama cha Soud kujibu shairi la Bwana Zahid Mngumi aliyekua Raisi wa Lamu katika vita vya Kuduhu au (Battle of Shela) katika ubeti wa tatu (3) alitumia neno kiyandi P'ota: NAAPA KWA MOLA YANGA NASI TULI NA MIZINGA SUUDI TWALINA APANGA TURADHI SAMBO KUTOTA DHULI SIYENYE TUPATA MIVI ZIYANDI POTA WATAE WENYE KUZITA SUTE TUKAWA MAINI

(OGW) FULBRIGHT UCLA - USA

PROF. AHMED SHEIKH NABHANY

Kwa sasa kuwa lugha ya Kiswahili imeenea ulimwenguni na inazidi kukuwa na kupanuka, ipo dharura ya kuunda jopo la kuunda istilahi, na jopo hilo lazima wapatikane wajuzi wa ndimi mbali mbali: Kama kiamu, kipate, kisiyu, kimvita, kijomvu, kivumba, kimtangata, kingare, kipemba, kitumbatu, kimagao, kingazija na kibarawa na iwapo kuna zaidi ya hizo tuweze kuwa na wataalamu kama hao. Kwa hivyo tutaweza kukikuza Kiswahili kwa njia nzuri sana. Lakini kabla ya kuunda neno ni lazima neno hilo liwe halipatikani katika lahaja hizi za Kiswahili. Hapo ndipo liundwe neno hilo la utaalamu au ulimbe kulingana na sharia zake ambazo nimezitaja huko nyuma. Kuunda neno lazima liwe linatokana na Kiswahili chenyewe na lisiwe lakuchuliwa neno la kizungu, na hali Kiswahili lipo. Wanaofanya hivyo ni wavivu hawana bidii na wanataka Kiswahili, kuwa wao wameunda neno wapate jina. Wengine tayari wamebuni maneno aina hiyo kwa mfano:(1) Historia (2) Saikolojiya (3) Fizikia (4) Bayolojia

Windows Aluminium Partitions Frameless Glass System Alucobond Cladding Structural Glazing Stainless SteelBalustrade

Great [email protected] Fairdeal

10

Kwa hivyo nikaona kuna umuhimu wa kuunda istilahi ya lugha yetu kulingana na sharia zilizowekwa na wenyewe Waswahili. Ndipo nilipo anza kubuni maneno na lilonifanza nibuni niliposikia limeundwa. Nalo ni (Television) kuita kiona mbali au kisanduku cha masanamu. Kwa hivyo nikaona mimi nina haki ya kuunda maneno kama hayo kwa kuwa mimi mwenyewe ni Mswahili na mila na dasturi na nimeilimishwa katika lugha hii yangu ya mama. Niliunda neno la kuwakilisha (Television) kulingana na mbinu na taratibu za Kiswahili na kuyavuta maneno ya kale kuyatia katika matumizi. Nikafikiria neno la khabari ya kutoka mbali Waswahili waliita Rununu na Waswahili wana itikadi khabari ile inaletwa na majini kutoka nchi ya mbali, vile vile Waarabu wana itikadi hiyo hiyo wao wanaita khabari hiyo kwa jina la (Hatif ). Wakati zilipokuja (Telephone) kuwa wapata khabari kutoka mbali waarabu wakaita (Hatif ) nami nikaona kuiita (Telephone) Rununu. Nakuwa bado msingi wake ni Rununu ni kaweza kutumia pia ni khabari kwa njia ya pili kutoka mbali na kungia katika kisanduku na kuweza kuziona khabari zile kwa macho. Sasa nikaunganisha maneno matatu ili kupata neno moja la kuwakilisha (Television) nayo:(1) Rununu Khabari kutoka mbali (2) Kuenga Kuona (3) Maninga Kwa macho Maana yake:RU ya wakilisha ­ NG ya wakilisha ­ NGA ya wakilisha ­ Likawa Rununu ­ Kuenga ­ Maninga ­ Rununu Kuenga Maninga Ru Nga Nga

Na ndio kinanawiri ulimwenguni na sisi tukiungana pamoja tutafaulu. Leo tumewaletea makala haya ya Istilahi ya Kiswahili na tutaendelea ambayo tuliyoandika. (1) Runinga (2) P'ataninga (3) Nyakaso (4) Nyakaso P'ataninga Kwa mwanafunzi wa Kiswahili anaotaka maelezo zaidi mwimo wetu uko wazi. Research Institute of Swahili Studies of Eastern Afirca (RISSE-A) Mwimo wa (Taasisi) Utafiti wa Waswahili ya Mashariki mwa Afrika (TUSIMA) Mombasa Hospital Road ­ Old Town Mombasa Kenya UGUNDUZI WA JARIDA LA RISSEA Watukufu karibuni Katika hafula hini Lamu mombasa mjini wa daraja na hishima ya turathi zetu njema kuutumikia umma nyinyi kuwafahamisha jarida kulianzisha uzuri kuudumisha chuo hiki kuchendesha urathi kuwafundisha yote tuna yasomesha nyote twawakaribisha twamtwaa kwa bashasha ya uswahili maisha shairi hili latosha mchezo kuwaonesha utungo waukomesha

Kusudi na madhimuni Vituo vyetu vya pwani Pongezi kwa wa dhamini Mkono tuunganeni Watoto muwaleteni Mila na utamaduni Kwa wanati na wageni Ajao hapa chuoni asome utamaduni Twaondoka uwanjani Na sasa tutizameni Amira na Nabhani -

Likawa Rung, kulitia utamu liweze kutamkika vizuri likawa Runinga. Tamko lingine la kizungu ( Video) kwa hivyo ( Video) haiwezi kufanya kazi bila ya kuunganishwa na (Television) kuwa ni mapacha kwa hivyo nikatumia tamko la pacha kwa lahaja ya kiamu nalo ni pata liwe na maana ya pacha ya runinga nikapata neno la kuwakilisha ( Video) nalo ni P'ataninga. Ni pacha ya Runinga haliwezi kufanya kazi mpaka liunganishwe na Runinga. Neno lingine ni la kuwakilisha (Camera) nilitowa kulingana na utenda kazi wake kusudi nikukilekeza chombo ili kichukue sura za mtu hulekezwa usoni, chombo chenyewe kikachukua sura au uso. Kwa hivyo nikakiita chombo hicho Nyakaso maana yake nyaka uso limewakilisha neno (Camera). Na neno ( Video Camera) limewakilishwa na neno Nyakaso pataninga. Tumebuni maneno haya kuonyesha Kiswahili ni lugha yajitosha kama lugha nyinginezo ulimwenguni. Na urongo kabisa kwa wanao sema hakijitoshi hao wanataka Waafrika wasende mbele na kwa sababu ya umasikini hatuwezi kusonga mbele. Lakini tukiwa na fedha za kutosha tunaweza kusonga mbele sana. Kiswahili kinakuzwa na Mwenyezi-Mungu, hakipati msaada wowote kama lugha nyingine za ulimwenguni. Hakuna lugha iliokuwa masikini kama Kiingereza kilikua na maneno mia tatu (300) lakini walipokua na fedha sana wana zaidi ya makamusi thalathini (30) na kinazidi kukuwa kwa njia wanayoitaka wenyewe.

Sherehe za kuanzisha jarida la TUSIMA Mombasa na Lamu

11

SANAA NA UFUNDI WA WASWAHILI NA: NAJASH AHMED,KHADIJA RIDHWAN,HOKKAH

K

itengo hiki cha sanaa na ufundi wa Waswahili kwanza kilijulikana kama Kituo cha Utamaduni cha Waswahili kilichozaliwa kutokana na ushirikiano wa kiufundi baina ya mashirika ya Makavazi ya Kitaifa ya Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Miradi ya Maendeleo, Shirika la Kimataifa la Ajira pamoja na ushirikiano wa watu wa Mombasa na Lamu. Mradi huu ulishuliwa Septemba 1991 huko Mombasa na halafu 1994 huko Lamu. Kituo kilibuniwa ili kufufua na kuendeleza utamaduni wa Kiswahili na pia kutoa nafasi za ajira kwa vijana wa miji hii miwili. Baada ya muda wa kuanzisha kituo hiki kuisha mashirka haya ya kimataifa yaliondoka na Makavazi ya Kitaifa ya Kenya ilichukua usukani wa kuendeleza kituo hiki na hivi sasa kiko chini ya usimamizi wa TUSIMA. Wanagenzi hawa walifunzwa mengi kuhusu ujenzi, uashi, useremala na wasichana walifunzwa ufumaji vitambaa. Kwa hivi sasa wanagenzi hawa wanafunzwa useremala tu na wasichana ushonaji na ufumaji pekee.

Sehemu ya Ushonaji na Darizi

Mbali na mafunzo ya lugha ya Kiswahili na useremala Taasisi ya Utafiti wa Waswahili ya Mashariki mwa Afrika (TUSIMA) pia inatoa mafunzo ya ushonaji nguo na kudarizi kofia na vitambaa kwa kutumia mitindo ya Kiswahili.

Kismu ya Kazi za Mbao

Mkufunzi Khadija Ridhwani (mwisho kulia) na wanafunzi wake wakiwa katika shughuli za kukata mishono

Mkufunzi Abeid Hokkah akiwaonyesha wanafunzi wake jinsi ya kuchonga mbao

Kitengo hiki kilianzishwa ili kiwafunze wavulana kazi za mbao. Vijana wajiunga na kituo hiki katika Januari ama Februari na kiliazimia zaidi wanafunzi waliomaliza shule za msingi na hawakupata nafasi ya kuendelea na masomo ya shule za upili. Ada ndogo hutozwa kwa wanafunzi ili kukimu mahitaji ya kununua vifaa vya kutumia kwa mafunzo. Wanafunzi hawa hushughulikia zaidi utumizi wa mikono kama asilimia thamanini na asilimia ishirini hutumiwa kwa masomo ya nadharia na biashara. Hufanyiwa tamrini kila baada ya muda ili kujua uwezo wa ufahamu wao. Muda wa kozi hii ni miaka miwili na mwanafunzi akikamilisha hupawa shahada na barua ya upendekezo kutoka kwa kituo na ana khiari ya kujiunga kufanya mtihani wa kitaifa unaoandaliwa na Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia. Kituo hiki cha ufundi pia kimeanzisha kiwanda ili kujikimu na kuwanufaisha wanagenzi hawa. Hutengenezwa vyombo vingi vya thamani na vimepata umaarufu mwingi mkoani. Milango, viti, vitanda na mabao ya nakshi hutengenezwa na mipango iko tayari kukipanua kiwanda hiki mwakani pamoja na kuongeza vifaa na ala za kazi.

Mafunzo haya ni katika hali ya kuhifadhi mila na desturi za Waswahili na kutoa nafasi za ajira kwa wasichana. Tunafunza mapambo mbali mbali ya nyumbani kama mapazia ya milango na madirisha, shuka zenye darizi za mikono na vitambaa vya meza, kanzu za darizi (Kanzu za Kiume), mabuibui ya wanawake. Kuna somo la kufuma kofia za Kiswahili (kofia za vito), msakara (Kofia ya kushona kwa mashini) mdongea (kofia ya kuchoma kwa moto vitundu vidogo). Wanapewa mafunzo ya historia ya mavazi ya Kiswahili na jinsi yalivyoingiliana na desturi za makabila mengine kama wahindi, waarabu na wenyeji wa kanda la Bahari ya Hindi.

Mr.Najash Ahmed

12

Nafasi za kujiunga zinatangazwa mwezi wa pili kila mwaka. Wanaofuzu kujiunga na chuo ni walohitimu elimu ya msingi au ya upili au yeyote yule mwenye hamu ya ushonaji. Kuna mafunzo ya mda au mchana kutwa pia wanapewa mafunzo na ushauri wa kuanzisha biashara. Wanafunzi walomaliza wanapewa muda wa miezi sita kufanya mazoezi kabla ya ajira au kuwa na uwezo wa kufungua biashara. Baadhi ya wanafunzi wamefungua biashara mjini na wengine majumbani mwao.

Mwaka jana wasichana kumi na nane walihitimu. Tuna mpango wa kufungua sehemu ya mazao ili kuongezea mapato na kutoa ajira kwa wanafunzi waliohitimu. Mwaka huu 2010 tuna matarajio ya kupata wanafunzi zaidi pia tuna mpango wa kuboresha huduma zetu hasa kwa upande wa wasichana.

TAASISI YA UTAFITI WA WASWAHILI YA MASHARIKI MWA AFRIKA WASILA WA AFISI KUU, NAIROBI NA: BI. MUNIRA MOHAMMED

apo makao makuu ya TUSIMA yako Mombasa, afisi ya wasila iliundwa ili kujibu masuala mengi yanayohusu mafunzo ya Kiswahili na TUSIMA kwa jumla hapa Nairobi. Wateja wa kila aina kutoka mashirika mbalimbali walimiminika hapa. Wasila wa TUSIMA hapa Makao Makuu ya Makavazi ya Kitaifa ya Kenya hufunza wanafunzi masomo ya lugha ya Kiswahili. Mabadiliko yanayoletwa na utandawazi pamoja na usasa yamesababisha Bi.Munira Mohammed kutoweka kwa sanaa na ufundi wa asli wa Waswahili hivo kuathiri vibaya hadhi na historia ya Waswahili. Afisi hii hukusanya kwenye kanda za santuri, majarida, magombo, na hupeperusha habari katika tovuti yake kuhusu utamaduni wa Waswahili. Hivi karibuni tovuti ya TUSIMA itazinduliwa upya ambayo itakuwa na habari za tafsili zaidi pamoja na hazina ya data ya maktaba yake yakiwemo majarida, ya kisayansi, vitabu, masomo ya Kiswahili na kanda za DVD. Pia kutakuwa na faharisi ya vyombo vya nakshi na ufumaji. Tovuti hiyo mpya itamuwezesha mteja kufanya biashara kimtandao ili kumrahisishia kujua na kununua bidhaa zetu na pia kuchangia blogi yetu pamoja na kujifunza Kiswahili cha awali kupitia tarakilishi. Afisi hii pia inanuia kufufua na kupa nguvu sanaa na ufundi wa Waswahili kupitia maonyesho ya utamaduni. Mkusanyiko wa ngoma za Waswahili k.m Kirumbizi, Msondo, Goma la Siyu uko katika kubuniwa na wafadhili wanatafutwa ili mradi huo ufaulu. Mwaka huu tunatarajia kufanya maonyesho ya Harusi ya Waswahili ili kuitangaza na pia kuiuza. Vile vile pana mipango ya kufungua duka katika mlia wa Makumbusho ya Nairobi ili kuuza vyombo vya samani vya Kiswahili asli. Katika eneo hili la Afrika Mashariki, Kiswahili kinaweza kutumika kama wasila wa tangamano la kiuchumi, kisiasa, na kijamii. Hili litakuwa na athari ya kuleta utulivu zaidi na masikizano zaidi baina ya watu katika eneo hili na zaidi kama yanavyoruwazwa katika Ruwaza ya 2030.

J

13

TAMASHA ZA KITAMADUNI LAMU NA MOMBASA NA: MOH'D ZEIN

Shabaha za Tamasha

1. Kuhimiza ummah kujihusisha na sherehe za kitamaduni 2. Kufanya jamii za Lamu na Mombasa kuifahamu, kuithamini na kuienzi turathi ya kitamaduni 3. Kuendeleza masemezano baina ya tamaduni na ustaarabu tafauti 4. Kuweka msingi thabiti kwa vijana wa leo na wa siku zijazo ili warithi ratiba madhubuti ya kitamaduni 5. Kuipembejea sekta ya utalii

Mashindano ya upakaji Henna.

T

amasha la kitamaduni la Lamu na Mombasa hufanyika kila mwaka ili kufufua turathi za Waswahili. Tamasha la Mombasa huandaliwa na TUSIMA ambacho ni kitengo cha utafiti katika Makavazi ya Kitaifa ya Kenya ilhali lile la Lamu huandaliwa kwa ushirikiano wa Makavazi ya Kitaifa ya Kenya na Kikundi cha Kuendeleza Utamaduni cha Lamu. Mwaka huu tamasha Mohamed Zein hizi zitafanyika Novemba na TUSIMA MOMBASA Disemba zikiwa ni za 10 na za 3 katika Lamu na Mombasa mtawaliya. Hivi sasa tamasha hizi mbili zimekuwa maarufu na zimeratibiwa katika takwimu ya sherehe katika Makavazi ya Kitaifa ya Kenya. Tamasha hizi hufurika watu wa matabaka mbalimbali na huvutia sana kwa sababu ya furaha inayoonekana kote. Sherehe hizi zina wajibu mkubwa katika kudhibiti turathi zetu na kuwaonyesha desturi zetu za Kiswahili. Sherehe hizi pia hujenga jina la miji hii miwili, mikongwe kwani wanasayansi wa timbo, ramani ujenzi, wanamazingira, na waalimu hukutanika hapa.

Tamasha hizi huhusisha aina za ngoma za waswahili kama mdurenge, kirumbizi, uta, goma la Siyu, tari la ndiya, goma la barani, taarab na kadhalika. Pia huwa kuna mashindano ya mashua, vidau, kuogelea, punda na mashairi. Katika sherehe hizi ufundi wa kusuka mikeka, makuti, kushona kofia, kutema milango na ufumaji pia hushirikishwa. Wanawake hawakuachwa nyuma kwani huwa na maonyesho ya bi harusi kupaka hina, kuonyesha mishono na mavazi ya kale ya akina mama wa Kiswahili na pia ngoma za vugo na lelemama huchezwa. TUSIMA kama chuo cha kitaaluma kimeweza kutia uhondo wa kiakademia ili kupa nguvu sherehe hizi kwa kuandaa mihadhara yenye nia ya kuwafunza na kuilimisha wananchi juu ya majukumu yao katika jamii. Wataalamu watajika katika Kenya wameshaalikwa kuwasilisha karatasi zenye uzito wa kimataifa katika kongamano hizi na wengi wamefurahia kitengo hiki cha mihadhara ndani ya sherehe.

Washiriki wa mashindano ya bao mjini Mombasa wakati wa tamasha

Mwenyekiti wa Bodi wa Makavazi ya Kitaifa ya Kenya Bwana Issa Timamy akikabidhi zawadi kwa washindi wakati wa hafla ya tamasha ya kitamaduni mjini Mombasa

14

M

RISALA KUTOKA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MASOMO YA MASHARIKI NA AFRIKA (SOAS), CHUO KIKUU CHA LONDON NA: WAFUNZI WA SOAS

ombasa, kwetu sisi wanafunzi saba wa SOAS, ilikuwa kipumbazi mwanana baina ya London mji wa harakati na zahma nyingi na mji wa kale wa Zanzibar wenye utulivu na ukimya. Mombasa ilitupa yote mawili: mazoweya ya London na sawia ni mji wa utulivu na historia kuu.

Punde tu tulipowasili tulilakiwa vizuri na wafanyakazi wa TUSIMA. Katika vitu vya kwanza kufanya ni kutembelea mji wa kale wa Mombasa. Tulipendezewa sana na majenzi ya majumba na miundo ya milango ya mji wa kale pamoja na barabara zake na mazingira yake tulivu. Tulibahatika sana kusoma hapa kwa vile kufikia madarasa yetu yalitupitisha karibu na ngome adhimu ya Fort Jesus. Ilikuwa tamu sana kugubikwa na historia namna hii na pia kuwa karibu na njia kuu kama Barabara ya Digo, Barabara ya Biashara ambazo tuliziona kuwa zenye harakati nyingi pamoja na kupambika vizuri. Twashukuru sana kwamba tuliishi karibu na jingome la Fort Jesus. Kuta zake nzuri nyekundu tuliziona kwa urahisi kutoka nyumbani mwetu kwenye ufuo wa bahari. Tulitamani sana kujua mengi kuhusu ngome hii na walimu wetu wa TUSIMA walitupangia ziara yake mapema sana katika maisha yetu ya wiki nne mjini Mombasa. Ijapokuwa ngome hii ilijengwa katika miaka ya 1500 na imepokezanwa mara kadhaa katika utawala wake, bado ni thabiti na imara tangu ilipojengwa, yenye kusimulia hadithi nyingi kuhusu maumbile ya historia ya kisiasa ya mji wa Mombasa. Baadaye katika kukaa kwetu tulizuru Mapango ya Shimoni karibu sana na mpaka wa Tanzania. Tulirauka kuwahi feri ya Likoni kuelekea Kusini halafu tukaenda mpaka Shimoni kupitia Ukunda na Kwale. Mwanzo tuliona jumba la kizamani la kikoloni ambalo Makavazi ya Kitaifa ya Kenya inaliregesha upya. Halafu tuliabiri kidau kidogo na kuvuka mkanda mdogo wenye kufarikisha kisiwa cha Wasini na bara. Huko tuliona mabustani ya matumbawe na jela ya zamani. Baada ya kuandaliwa wali mtamu kwa samaki tulienda kuona hayo mapango pamoja na mapopo nyundo wanaoishi humo. Kuna nadharia nyingi kuhusu matumizi ya mapango hayo lakini kwa sasa kuna koma dogo la kuombeya afya njema. Tulirudi Mombasa wachovu lakini sote tumeridhika. Ni taadhima kubwa kukutana na kufundishwa na gwiji la Kiswahili -- Sheikh Nabhany. Sote tulifurahia kuandika, kutunga na hata kuimba mashairi tuliotunga wenyewe kutumia miundo ya Kiswahili. Ilikuwa tajriba nzuri sana iliotupa nguvu katika masomo ya Kiswahili. Tungependelea kuwashukuru khususan walimu Rukiya, Ali Wasi, Zein, Sheikh Nabhany, Amira na yoyote aliyetukarikibisha kwa moyo mkundufu.

AUTHORISED DEALERS OF MAROO PAINTS:

FAIRDEAL

P.O. Box 88156 Mombasa. Tel: 041 2315210/2, 2318589. Mobile: 0722841406, 0721 591265. Fax: 041 2315204, 2318588. Email: [email protected] , [email protected]

h a r d w a r e

15

Information

15 pages

Report File (DMCA)

Our content is added by our users. We aim to remove reported files within 1 working day. Please use this link to notify us:

Report this file as copyright or inappropriate

308623


You might also be interested in

BETA