Read Sitapungukiwa%20na%20kitu%20-2010%20pg%201-12%20hp.pdf text version

Sitapungukiwa

na kitu

Kimeandikwa na Mchg. Fredrik Wislöff Kimetafsiriwa na Askofu William E. Mwakagali

Soma BiBlia

1

Sitapungukiwa na kitu

© SoMA BiBliA na Askofu William E. Mwakagali 1996 Kimeandikwa na Mchg. Fredrik Wisloff Kimetafsiriwa na Askofu William E. Mwakagali originally published as "Mig fattes intet" by Mchg. Fredrik Wisloff and o. lohse, København, Denmark, 1938.

Kimetolewa na: SoMA BiBliA P.o. Box 12772 Dar es Salaam, Tanzania

Toleo la kwanza: 1997, nakala 3,000 Toleo la pili lililosahihishwa: 2010, nakala 2000

iSBN 9987 8836 7 2

Kimepigwa chapa na: Colour Print Tanzania lTD. S.l.P. 76006, Dar es Salaam

2

Yaliyomo

Dibaji ya Mfasiri kwa Toleo la Kwanza ............ 4 Neno la watoaji ............................................................. 5 Utangulizi ............................................................................. 5

1.

Sitapungukiwa na kitu .................................................. 7 Heri Walio Maskini wa Roho ...................................................... 9 Yesu Anaokoa Kabisa ................................................................ 11 Hali ya Ajabu ............................................................................. 13 Kupungukiwa Yote .....................................................................16 Kando ya maji ya utulivu ........................................ 20 Hali ya Kuona Uchovu .............................................................. 21 Kushikwa Mno na Matokeo ....................................................... 22 Maisha ya Mtu Aliyechoka ........................................................ 24 Kweli Nne kuhusu Majaliwa ya Kupumzika ............................. 26 Bonde la uvuli wa mauti ............................................ 37 Kivuli cha Dhambi ..................................................................... 38 Kivuli cha Mateso ...................................................................... 43 Kivuli cha Mauti ........................................................................ 47 Kikombe changu kinafurika .................................... 51 Sote Tunaweza Kupokea Maisha Tele ....................................... 52 Tutapataje Haya Maisha Tele? ................................................... 54 Yule Aishiye Maisha Tele Anayasikiaje Yeye Mwenyewe? ...... 56 Kutiririka kwa Roho .................................................................. 59 Wema peke yake ............................................................. 62 Fumbo la Mateso ....................................................................... 63 Yaliyo Mema Hasa .................................................................... 65 Shabaha ya Maisha .................................................................... 67

2.

3.

4.

5.

3

Zaburi 23 Bwana ndiye mchungaji wangu,

Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza. Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.

6

1. Sitapungukiwa na kitu

Maneno yanayotumiwa hapa ni mazito kweli. "Bwana ni mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu." Mtu akiyafikiri sawasawa maneno haya anaanza kujaribiwa kuona mashaka juu ya maana yake iwapo ni kweli. Je, ni kweli kwamba mtoto wa Mungu hapungukiwi kitu? Siku zote kuna maono ya ndani ya mioyo ya watoto wa Mungu walio wa kweli na wanyenyekevu, kwamba wako mbali na ilivyowapasa kuwa. Kati ya hisia zote alizo nazo Mkristo katika maisha yake, hisia ya umaskini ina nguvu sana. Ni vema kusoma maneno kama haya, "Sitapungukiwa na kitu." lakini, nani anathubutu kuyatumia kabisa maneno haya juu yake mwenyewe, akisema, "Sipungukiwi kitu"? Kwa maana, kweli ninajiona kupungukiwa mengi: Katika ukristo wangu ningependa sana kwamba Mungu na mambo yake yashike kwa nguvu nia na mawazo yangu. Pia ningependa kujitoa kwa Mungu kwa moyo wote. lakini hata nikijitoa kabisa, sifanikiwi. Ni kana kwamba siku zote kuna kitu ambacho hakitaki kufa kabisa. Ni mwili wangu mwenyewe, tamaa ile mbaya na ubinafsi wangu mwenyewe. laiti ningeweza kufanya yale ambayo nataka, Kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote! Pamoja na hayo, yanipasa kukiri pia kwamba hata nia yangu ina upungufu mwingi. lingekuwa ni jambo rahisi kama ningeweza kumpenda Mungu kabisa na kuelekeza nia yangu yote kwake. Ningekuwa tu mtu ambaye siku zote hupata ushindi - si ushindi katika matendo peke yake, bali hata katika mawazo na njozi zangu zote, na ushindi juu ya maneno yote maovu, ya uzembe na yenye chuki. Nikiangalia maisha yangu yote ya utakaso, yanipasa nikiri kwa aibu kwamba sijaenda mbali. Basi, nani athubutuye kusema, "Mimi sipungukiwi kitu"? Mungu na wanadamu wenzangu, nadhani wote wanakubaliana na mimi kwamba kuhusu utakaso ninapungukiwa mengi. Kisha huzungumzwa juu na kujaa Roho, juu ya ule uwezo mkuu na ile 7

amani tulivu vinavyoweza kuonjwa kwa njia ya Roho Mtakatifu tu. Tena hapo lazima nikiri kwamba ninapungukiwa mengi sana. Hisia hii juu ya umaskini aliyo nayo Mkristo moyoni mwake, si madanganyo ya unyenyekevu, bali ni ya kweli na ya kusikitisha. Hali halisi ndiyo kwamba hata Mkristo aliye bora zaidi, anapungukiwa mengi kwa ndani, katika kujitoa kwa moyo wote, katika kupenda, katika kujitumikisha, katika utakaso, katika ushindi, katika nguvu na mengine mengi. Hata hivyo imeandikwa katika zaburi hii iliyo sehemu ya Maandiko ambayo hayawezi kamwe kusema uongo, "Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu." licha ya hayo yaliyotajwa kabla, na licha ya kupinga kwa nguvu kwa moyo wangu, ni kweli pia kwamba mimi kama mtoto wa Mungu sipungukiwi chochote. Hisia hii ya ndani ya umaskini inayojaza mioyo ya watoto wote wa kweli wa Mungu, kwa bahati mbaya imewapotosha wengi. Na imetumika kuwatia mashakani watu wengi waaminifu na kuwakwaza kiroho. Kwa mfano, watu hawa hukumbwa na hoja na maswali kama haya, "Hakuna jambo fulani unalopungukiwa? Una hakika kwamba umeuona wokovu wote? Una furaha na ni imara kama vile ambavyo ungeweza na kupaswa kuwa? Na je, unapata ushindi halisi juu ya dhambi? Kama sivyo, ni lazima nikuambie kwamba unapungukiwa furaha ya Roho Mtakatifu. Ndiyo, umepata furaha ya wokovu, na kwa kweli ni Mkristo, lakini wa kiwango cha chini. Yakupasa uinuliwe juu zaidi. Haikupasi tu kumpokea Kristo bali pia Roho. Umepata kujifunza ya kutosha tunda kuu la ijumaa Kuu, lakini kuna lililo la utukufu zaidi: Kipawa cha Pentekoste. Hata hili yakupasa kulionja." Akisikia hivyo, huenda Mkristo mwaminifu ambaye hajaimarika kiimani, ataungama kwa unyenyekevu kwamba ni sawa, yaani kwamba anapungukiwa Roho. Ndipo anaanza kuomba, naam, kumsihi sana Mungu juu ya furaha ya Roho, kwamba kwa mara moja afikishwe kiwango cha juu na kuepuka mashindano ya kila siku dhidi ya mwili. Hufanya kila linalowezekana kuibidiisha roho yake: Anasoma, anaomba, anafunga na kuendelea na mazoezi mengine yote ya kidini ambayo anaweza kuyafikiri yatamsaidia kuyaonja hayo mapya. 8

lakini mara nyingi sana bidii hizo huishia kuleta masikitiko, na pamoja na kusikitika huja kudhoofika. Mkristo huyo maskini amechoka, naam, na pengine amepata dhara lisilotibiwa. Maana sababu ya jitihada zake zote imetokana na kufahamu vibaya injili yenyewe. Pasipo yeye mwenyewe kujua, na bila kutaka hata kidogo, amebadilisha neema kwa sheria. ilitegemea kwamba sheria ilijigeuza vizuri hata hakuitambua. Kama akisoma maneno hayo mtu aliyechoka na kuchanganyikiwa kiroho, kwa hakika Mungu atamwonyesha mtu huyo utajiri wa injili kwa njia ya maneno hayo na kumrudisha kwenye neema ile isiyostahiliwa. Sikiliza haya, ndugu yangu uliyechoka: Bwana ni mchungaji wako, hupungukiwi kitu. Kwa maana unayo yote katika Kristo.

Heri Walio Maskini wa Roho

Unayo yote katika Kristo. Tuangalie kwa makini maana ya ukweli huu wa kiinjili kwa hali yetu wenyewe! Ni mara kabla ya Yesu kutoa hotuba kubwa na ya maana. Anakaa mlimani na wanafunzi wake wakimzunguka. Yesu anajua jinsi walivyo wadhaifu, na ni maonyo ya namna gani ambayo wanayahitaji. Anajua kwamba atazungumza nao juu ya amri ya tano na ya sita hasa, na kuwaonya wasiafikiane na kila upande wala kuwatumikia mabwana wawili. Anajua vizuri jinsi mioyo yao inavyopenda kufanya hivyo. lakini hata hivyo Yesu anaanza hotuba yake kwa maneno haya, Heri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao (Mt 5:3). Watu hawa walikuwa ni wenye upungufu na wadhaifu waliohitaji maneno yote mazito ya mahubiri ya mlimani, hata hivyo walikuwa heri! Walikuwa na hisia ya umaskini ndani yao, na wakaona njaa na kiu ya haki. Hawakuwa na kitu chochote walichoweza kukionyesha kama kitu hasa cha kuwastahilisha. Hata hivyo walikuwa ni heri. Basi, kuwa heri, maana yake ni nini? Aliye heri anakosa nini? Neno "heri" huonyesha furaha ya juu sana na utajiri. Ndiyo, ni jambo la kupendeza sana hata kuelekeza mawazo yetu kwa hao waliosimama nyumbani mwa Mungu hali wameokolewa. Hata hivyo ni watu wanaopigana 9

na kushindana kila siku na maisha ya dunia hii wanaosifiwa kwa neno hili "heri". Yesu anaona Wakristo wana hisia ya umaskini katika mioyo yao, na ni wakati wanapokuwa na hali hiyo anawahesabu kuwa matajiri, naam, na wenye heri. Kuwa Mkristo ni mtu kuwa na hisia hii kwamba mimi siwezi kuwa ninavyotakiwa, na kwa hiyo anatafuta haki na nguvu yake katika Kristo. Mtu huyo yu heri. lakini mtu yule anayeuangalia ukristo wake, anajiangalia mwenyewe. Na mara anaporidhika kwa sababu ya mafanikio anayoyaona kwake mwenyewe, anakuwa Farisayo. Mtu huyo si heri, maana mtu yu heri wakati tu anapoona njaa na kiu. Mfano mwingine wa jambo hilo ni yule mtoza ushuru hekaluni. Mwulize kama alipungukiwa kitu, naye atajibu, "Ndiyo, napungukiwa kila kitu." Na kisha atajipiga kifuani na kusema, "Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi."

10

lakini mtoza ushuru aliposema hivyo, wakati uohuo Mungu alipitisha hukumu yake mbinguni juu yake na hiyo ilijibu, "Wewe ni mwenye haki!" Mtu huyu aliyeelemewa na dhambi na kusikia hisia ya umaskini na mashtaka katika moyo wake, alirudi nyumbani hali amehesabiwa haki. Alipungukiwa nini basi? Hakupungukiwa kitu! Ukweli huu unaonekana hata vizuri zaidi tunapomwangalia yule mhalifu msalabani. Alikuwa mbaya miongoni mwa watu. Hakuwa na uwezekano wowote wa kurekebisha uhalifu wake, wala hakuwa na udhuru kwa matendo yake maovu. Hata kama tungeona matunda ya kwanza ya imani tukichanganua hali yake ya kiroho, hatukosi kuona kwamba hakuwa amekomaa kiroho na alikuwa mbali na mtu aliyekamilika. lakini hata hivyo aliingia Paradiso! Basi, alipungukiwa nini? Ebu fikiri kama tungeliweza kumwona wakati alipokanyaga mbele ya lango la Paradiso. Tungelimwona aking'aa kuielekea ile nuru na kufunikwa na utukufu mwingi wa pale juu. Tungeliona maumivu ya mapigo yake yakigeuzwa kuwa furaha wazi, kuona mikono yake iliyotobolewa ikiponywa na kunyoshwa kuelekea utukufu wa Mungu unaomzukia kama mwangaza mkuu pande zote. Yeye aliyepungukiwa kila kitu hakupungukiwa kitu! Maana alikuwa na uheri wote wa mbinguni. Huu wote ulikuwa uheri wake kufumba na kufumbua. Haya yote aliyapata kwa sababu hii tu ya kumwomba Yesu. Ndivyo ulivyo wokovu wa Mungu usiostahiliwa. Ndivyo ilivyo karama ya Kristo isiyo na mipaka. Yeye aliye na Bwana kama mchungaji wake hapungukiwi kitu!

Yesu Anaokoa Kabisa

Mara nyingi yanibidi kuiuliza na kuihoji nafsi yangu mwenyewe hivi, "Kwa nini unakwenda ukilemewa dhambi na kukata tamaa namna hii? Kwa nini unasikiliza mashtaka ya moyo yasiyokoma na kukubali lawama za dhambi zilizopita kukuibia furaha yako? Dhambi iliyotubiwa kwa moyo 11

wote mbele za Mungu imesamehewa. Na dhambi iliyosamehewa haipo tena. Badala yake unahesabiwa haki ya Kristo na u mtakatifu kamili na safi katika yeye! Uzima wako umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kwa kweli hupungukiwi kitu. Kumbuka kwamba Kristo Yesu alifanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi" (1 Kor 1:30). Yote ninayohitaji sasa na wakati ujao, ikiwa ni wakati wa kufa, wakati wa hukumu au milele; yote yamefungamanishwa katika Kristo. Katika yeye kuna kufurika kwa milele kwa msamaha, haki, upendo, ufahamu, nguvu, ushindi, hekima na ukombozi. Hujaokolewa nusu tu wala si Mkristo kwa sehemu tu. Huishi maisha ya kikristo kwa namna iliyo tofauti. Kwa maana imeandikwa, "[Yesu] aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye" (Ebr 7:25). ikiwa umefuata mwongozo huu wa kumjia Mungu kwa njia ya Kristo, basi umeokolewa kikamilifu. Hupungukiwi kitu! Maelezo haya yana uzito mkubwa. Ni karibu hayaeleweki. Hata hivyo ni kweli. Katika Kristo Yesu sijaokolewa sehemu au nusu kipimo tu, bali nimeokolewa kikamilifu. Vilevile hata katika imani isiyo kamilifu kuna wokovu mkamilifu. Siku zote Mkristo huona huzuni sana moyoni mwake, lakini pia yu mwenye furaha. Siku zote hujiona yu maskini, na hiyo humfanya mnyenyekevu. lakini Mkristo huyu mnyenyekevu na maskini anakwenda huko na huko na kuwafanya wengi kuwa matajiri. Mkristo kama huyo akifanya hesabu matokeo yake yanakuwa haya, Napungukiwa kila kitu! lakini Mungu huandika sahihi tarakimu zote, Unayo yote! Haya huelezwa katika 2 Kor 6:10 hivi, "Kama wenye huzuni, bali sikuzote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote." "Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu."

12

Information

10 pages

Report File (DMCA)

Our content is added by our users. We aim to remove reported files within 1 working day. Please use this link to notify us:

Report this file as copyright or inappropriate

75940


You might also be interested in

BETA
In the spirit and power of Elias.PDF
Microsoft Word - KITABU KIMEKAMILIKA final
UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI
ALIPANDU1