Read Microsoft Word - K-HISTORIA YA MKOA WA MBEYA - MIAKA 50 YA UHURU_FINAL DRAFT text version

YALIYOMO; Yaliyomo ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ....i ....iv ....v ....1 ....2

Orodha ya Majedwali... ... Vifupisho 1.0 1.1 2.0 ... ... ... ...

UTANGULIZI:...

Historia Fupi ya Mkoa

MUUNDO WA MKOA WA MBEYA KUANZIA MWAKA 1961 HADI MWAKA 2011 ... ... ... ... ....4

3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 4.0 5.0 5.1 5.2 6.0

DIRA, DHIMA, MAJUKUMU NA MALENGO YA MKOA WA MBEYA... Dira ... Dhima ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ....7 ....7 ....7 ....7 ....7 ....8 ...13 ....13 ....14 ....14 ....14 ....16 ....17 ....19 ....19 ....19 ....19 ....21

Majukumu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Malengo ya Mkoa ...

HALI YA UONGOZI NA UTAWALA KUANZIA MWAKA 1961 HADI SASA... ... MABADILIKO YA MFUMO WA KIUCHUMI NA KIJAMII... Mabadiliko ya Mfumo wa Kiuchumi ... Mabadiliko ya Mfumo wa Kijamii ... MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA MKOA WA MBEYA KISEKTA HADI SASA... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

6.1 6.2 6.3 6.4

Hali ya Uchumi wa Mkoa... Hali ya Kisiasa Sekta ya Elimu ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... Hali ya Ulinzi na Usalama

... ... ... ... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ... ... ...

6.4.1 Elimu ya Awali 6.4.2 Elimu ya Msingi 6.4.4 Elimu ya Juu

6.4.3 Elimu ya Sekondari

-1-

6.4.5 Elimu ya Ufundi ... 6.5 Sekta ya Kilimo ... 6.5.1 Mfumo wa Kilimo...

... ... ...

... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

....22 ....22 ....22 ....24 ....25 ....25 ....26 ....26 ....27 ....27 ....29 ....31 ....32 ....33 ....35 ....36 ....37 ....37 ....38 ....40 ....43 ....45 ....45 ....46 ....49 ....49 ....50 ....51 ....51 ....51 ....52

6.5.2 Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Biashara... ... 6.5.3 Kilimo cha Umwagiliaji... 6.5.4 Matumizi ya Pembejeo 6.5.6 Huduma za Ugani... 6.6 6.7 6.8 6.9 Sekta ya Mifugo... ... Sekta ya Ushirika... Sekta ya Ardhi... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... 6.5.5 Matumizi ya Zana za Kilimo

6.5.7 Usindikaji wa Mazao ya Kilimo... Sekta ya Maliasili na Utalii... ...

6.10 Barabara... ...

6.11 Nishati na Umeme... 6.13 Mawasiliano... 6.14 Uchukuzi... ... 6.15 Sekta ya Maji... 6.17 Sekta ya Afya... ... ... ... ...

6.12 Sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji... ...

6.16 Sekta ya Biashara...

6.18 Rasilimali watu na Utawala Bora... ... 6.18.2 Mapambano Dhidi ya Rushwa 7.0 7.1 7.2 7.3 7.4 7.5 7.6 CHANGAMOTO ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

6.18.1 Hali ya Utumishi katika Mkoa wa Mbeya ...

Utawala na Rasilimali Watu Kilimo Mifugo Viawanda ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

Maliasili na Utalii ...

Maendeleo ya Ushirika ...

-2-

7.7 7.8 7.9

Nishati Elimu ... Afya ...

... ... ...

... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

....53 ....53 ....54 ....54 ....55 ....55 ....56 ....56 ....56 ....58 ....58 ....58 ....59 ....59 ....59 ....59 ....60

7.10 Sekta ya Maji 7.12 Barabara 8.0 ...

7.11 Maendeleo ya Jamii

7.13 Ardhi na Maendeleo ya Makazi MIAKA 50 IJAYO ... 8.1 8.2 8.3 8.4 8.5 8.6 8.7 8.8 8.9 Sekta ya Elimu Afya ... Ushirika Barabara Maji ... Umeme ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...

MATARAJIO YA MKOA WA MBEYA KATIKA

Hali ya Ulinzi na Usalama Biashara na Viwanda

Maliasili na Utalii ...

-3-

TAARIFA YA MKOA WA MBEYA MAADHIMISHO YA MIAKA HAMSINI (50) YA UHURU

1.0 UTANGULIZI Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa minne (4) iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa mingine ni Rukwa, Iringa na Ruvuma. Mkoa wa Mbeya ulianzishwa mwaka 1961 na ulikuwa ukijulikana kwa jina la `Southern Highland Province' kwa kujumuisha baadhi ya maeneo ya mikoa ya Iringa na Rukwa. Mkoa una eneo la km. za mraba 63,617 Kati ya hizo km. za mraba 61,783 ni za nchi kavu na km. za mraba 1,834 ni eneo la maji. Kulingana na Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 1967 mkoa

ulikuwa na watu 969,053, Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 Mkoa wa Mbeya ulikuwa na jumla ya watu 2,063,328. Kufikia mwaka 2010 mkoa ulikadiriwa kuwa na watu 2,662,156. Mkoa wa Mbeya upo kusini magharibi mwa eneo la Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mkoa upo katika Latitudi kati ya 7º na 9º 31' kusini ya Ikweta na Longitudo kati ya 32º na 35º mashariki ya Greenwich. Mkoa unapakana na nchi za Zambia na Malawi upande wa kusini, Mkoa wa Rukwa upande wa magharibi, Mikoa ya Tabora na Singida kwa upande wa kaskazini ambapo kwa upande wa mashariki unapakana na Mkoa wa Iringa. Mji wa Tunduma katika Wilaya ya Mbozi na Kasumulu katika Wilaya ya Kyela, hufanya milango ya kuingilia na kutokea nchi za Zambia na Malawi.

-1-

Ramani inayoonesha Mkoa wa Mbeya na Wilaya zake.

1.1

HISTORIA FUPI YA MKOA WA MBEYA

Katika enzi za ukoloni wa Waingereza, Mkoa wa Mbeya ulikuwa ukijulikana kwa jina la `Southern Highland Province'. Mkoa ulikuwa ukiunganisha baadhi ya maeneo ya mikoa mitatu ya sasa ambayo ni Iringa na Rukwa. Jina la Mbeya limetokana na neno la kisafwa "Ibheya" ambalo maana yake ni chumvi, kutokana na wafanyabiashara kufika na kubadilishana mazao yao kwa chumvi. Mji wa kisasa wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni Waingereza mnamo mwaka 1927. Wakati huo dhahabu ilianza kupatikana katika milima iliyopo karibu na Mbeya hadi Chunya hivyo Mbeya ulikuwa ni mji wa mapumziko kwa Wazungu kutokana na hali yake nzuri ya hewa. Mkoa huu ni moja kati ya mikoa mikongwe tisa (9) iliyokuwepo mpaka wakati wa uhuru mwaka 1961.

-2-

Katika kipindi hicho, makabila makuu katika Mkoa wa Mbeya yalikuwa ni Wasafwa, Wanyakyusa, Wandali, Wasangu, Wamalila, Wanyiha, wakimbu na Wanyamwanga. Kijiografia, Mkoa ulianzishwa katika maeneo yanayojulikana hivi sasa kama Uhindini, Uzunguni na Majengo. Mji ulipangwa kufuatana na kawaida ya miji ya kikoloni ya Afrika Mashariki kuwa na sehemu tatu zifuatazo; (i) Uzunguni kama sehemu ya nyumba za Wazungu na kando yake ofisi za serikali (Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Polisi na Mahakama) (ii) Uhindini kama mtaa wa biashara uliokuwa mikononi mwa

wafanyabiashara wenye asili ya Kihindi na Kiingereza; (iii) Majengo kama sehemu kwa ajili ya wafanyakazi Waafrika na familia zao. Kwa upande wa masuala ya kiimani, Mkoa ulikuwa umegawanywa kama ifuatavyo; (i) Kanisa Anglikana lililokuwa dhehebu rasmi la Uingereza ambalo lipo chini ya eneo la Uzunguni karibu na ofisi za kiserikali kama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mahakama. (ii) Kanisa la Moravian la mjini lilijengwa eneo la Majengo iliyokuwa sehemu kwa ajili ya makazi ya Waafrika. (iii) Kanisa Kuu Katoliki lililokuwa maeneo kati ya Uzunguni na Uhindini karibu na Majengo ambalo lilihudumia Wazungu wachache hasa Waeire na Wahindi kutoka Goa na Waafrika wachache. Kwa upande wa masuala ya uchumi Mkoa wa Mbeya ulitegemea kilimo cha mazao ya chakula yakiwemo mahindi, viazi vitamu, mtama, mpunga na ndizi. Shughuli nyingine zilikuwa ni biashara na viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza zana za kilimo.

-3-

Kielimu, shule zilizokuwepo zililenga hasa kutoa elimu kwa watoto wa machifu, wazungu na wahindi. Shule hizi zilikuwa zinamilikiwa na serikali na mashirika ya dini. Shule za serikali zilijulikana kama `Native Authority' na za mashirika ya dini ziliitwa shule za wamisionari. Waalimu wazalendo walikuwa wachache, wengi wao walikuwa ni wazungu. Misheni ya Rungwe ndiyo pekee iliyokuwa na Chuo cha Elimu katika Mkoa wa Mbeya baada ya uhuru. Kuhusu huduma za afya, jamii kwa kiasi kikubwa ilikuwa inatumia tiba za kienyeji. Hospitali zilikuwa chache zikitoa huduma bure isipokuwa hospitali za wamisionari.

2.0

MUUNDO WA MKOA WA MBEYA KUANZIA MWAKA 1961 HADI 2011

Muundo wa Mkoa Mbeya umekuwa ukibadilika kutokana na mabadiliko ya kiuongozi na kiutawala ikihusisha kuanzishwa kwa Mikoa mipya, Wilaya na Halmashauri, Tarafa, kata, Vijiji, Mitaa na Vitongoji. Wakati wa uhuru mwaka 1961, Mkoa wa Mbeya (Southern Highland Province) ulikuwa na jumla ya Wilaya 7 ambazo ni Chunya, Sumbawanga, Mbozi, Rungwe, Njombe, Iringa na Mbeya. Mwaka 1974 mabadiliko ya kiutawala yalifanyika ambapo Wilaya ya Sumbawanga iligawanywa na kuwa sehemu ya Mkoa wa Rukwa, baadae Wilaya za Njombe na Iringa ziligawanywa na kuwa sehemu ya mkoa mpya wa Iringa. Baada ya mabadiliko hayo ya kiutawala, Mkoa wa Mbeya ulibaki na kuwa na eneo la kilometa za mraba 63,617 ambalo linaundwa na Wilaya 7, Halmashauri 8 za sasa ambazo ni Chunya, Ileje, Kyela, Mbarali, Mbozi, Rungwe, Mbeya na Halmashauri ya Jiji, Tarafa 27, Kata 218, Mitaa 181, Vijiji 829 na Vitongoji 4,349. Mamlaka za Serikali za Mitaa zilianzishwa kabla ya Uhuru na mabadiliko yalikuwa ifuatavyo; (i) Mwaka 1972; Mamlaka za Serikali za Mitaa zilivunjwa na kuanzishwa kisheria Madaraka Mikoani.

-4-

(ii)

Mwaka 1982 chini ya Sheria Na.7 na Na.8 ya mwaka 1982; Mamlaka za Serikali za Mitaa zilirejeshwa tena na kuzirudishia madaraka ya kumiliki watumishi na rasilimali zilizokuwepo.

(iii)

Mwaka 1997; Sekretarieti za Mikoa ziliundwa chini ya Sheria Na.19 ya mwaka 1997 na kuwa na washauri wataalam wa sekta mbalimbali. Idara ya Serikali za Mitaa katika Sekretarieti ya Mkoa imekuwa ni kiungo kikubwa kati ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na Serikali Kuu. Idara hii inabeba majukumu ya kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Mamlaka zote za Halmashauri za Mkoa.

Kwa mujibu wa Muundo ulioidhinishwa na Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Januari, 2011, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ina Sehemu tano, vitengo vikuu vitatu na Hospitali ya Mkoa kama inavyooneshwa katika Kielelezo Na. 1; a) b) c) d) e) f) g) h) i) Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu; Sehemu ya Mipango na Uratibu; Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji; Sehemu ya Huduma ya MiundoMbinu; Sehemu ya Huduma ya Jamii; Kitengo cha Uhasibu na Fedha; Kitengo cha Ununuzi na Ugavi; Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani; Hospitali ya Mkoa;

-5-

Kielelezo Na. 1; MUUNDO WA OFISI YA MKUU WA MKOA

(Umepitishwa na Mhe. Rais tarehe 03 Juni, 2011)

MKUU WA MKOA KAMATI YA USHAURI YA MKOA KATIBU TAWALA WA MKOA

KITENGO CHA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Mkuu

KITENGO CHA FEDHA NA UHASIBU Mhasibu Mkuu KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI

KITENGO CHA MANUNUZI

Mkaguzi wa ndani Mkuu KITENGO CHA HUDUMA ZA SHERIA Mwanasheria Mkuu

Afisa Ugavi Mkuu

SEHEMU YA MIPANGO NA URATIBU

SEHEMU YA AFYA NA HUDUMA ZA JAMII Katibu Tawala Msaidizi

SEHEMU YA HUDUMA ZA ELIMU

SEHEMU YA UCHUMI NA UZALISHAJI

SEHEMU YA UTAWALA NA RASILIMALI WATU

SEHEMU YA MIUNDOMBINU

SEHEMU YA HUDUMA ZA MAJI

SEHEMU YA HUDUMA ZA SERIKALI ZA MITAA Katibu Tawala Msaidizi

Katibu Tawala Msaidizi

Katibu Tawala Msaidizi

Katibu Tawala Msaidizi

Katibu Tawala Msaidizi

Katibu Tawala Msaidizi

Katibu Tawala Msaidizi

HOSPITALI YA MKOA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA

MKUU WA WILAYA KAMATI YA USHAURI YA WILAYA

KATIBU TAWALA WA WILAYA

Mganga Mkuu

AFISA TARAFA

6

3.0 3.1

DIRA, DHIMA, MAJUKUMU NA MALENGO YA MKOA WA MBEYA Dira:

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ina majukumu ya kuweka mazingira mazuri ya kiutendaji kazi na kusimamia maendeleo katika Mkoa. Usimamizi huu unaongozwa na Dira ya Sekretarieti ya Mkoa ambayo ni kuwa "Taasisi yenye uwezo wa hali ya juu yenye kujituma katika kuwezesha shughuli za maendeleo na ukuaji wa uchumi wa Mkoa kwa kuzingatia misingi ya uongozi bora na utawala wa sheria". 3.2 Dhima: ni "Kuwezesha na kujenga uwezo wa watumishi wa

Dhima ya Mkoa

Sekretarieti ya Mkoa na Serikali za Mitaa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi; na kutoa msaada wa kitaalamu katika sekta mbalimbali za uchumi ikiwa ni pamoja na mawasiliano na Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na wadau wengine katika maendeleo ya Mkoa". 3.3 Majukumu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliyoelezwa hapo juu, Mkoa unatekeleza

Ili kufanikisha dira na dhima majukumu muhimu yafuatayo: (i) (ii) (iii) (iv)

Kuzijengea Halmashauri uwezo wa kutekeleza majukumu yake; Kutoa ushauri wa kitaalam kwa Halmashauri ili ziweze kutoa huduma bora kwa Wananchi; Kuhakikisha kwamba kunakuwepo amani na utulivu katika Mkoa; Kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali na Sera za kisekta katika Halmashauri.

3.4 (i)

Malengo ya Mkoa Kusimamia utekelezaji wa shughuli za utawala bora na uwajibikaji

Malengo ya utekelezaji yaliyowekwa ni:

-7-

(ii) (iii) (iv) (v) (vi) (vii)

Kusimamia ushirikiano na uhusiano kati ya Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na wadau wa maendeleo; Kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali na nyenzo muhimu za kuhudumia umma; Kuhakikisha masuala mtambuka yanaingizwa katika mipango ya maendeleo ya wadau wote; Kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi ili kuwepo kwa huduma na ufanisi unaotarajiwa; Kuratibu na kutoa ushauri wa kitaalam kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na wadau mbalimbali wa maendeleo; Kuboresha huduma za kinga ili kupunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI kwa wananchi wa Mkoa;

4.0

HALI YA UONGOZI NA UTAWALA KUANZIA MWAKA 1961 HADI SASA

Katika kuhakikisha kwamba shughuli za maendeleo, Usalama na Usimamizi wa masuala yote muhimu ya Mkoa yanatekelezwa kikamilifu, Mkoa umekuwa ukiongozwa na Wakuu wa Mikoa tofauti. Orodha ya Wakuu wa Mkoa wa Mbeya ni kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 1;

-8-

Jedwali Na. 1; Orodha ya Wakuu wa Mkoa wa Mbeya kuanzia mwaka 1961; Na. 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. Jina la Mkuu wa Mkoa Mhe. Selemani Kitundu Mhe. Waziri Juma Mhe. John B. Mwakangale Mhe. Aaron Mwakang'ata Mhe. Oswald Marwa Mhe. Peter Siyovelwa Mhe. John Shija Mhe. Richard Wambura Mhe. Kingunge Ngombare Mwiru Mhe. Chrisant M. Mzindakaya Mhe. Michael Baruti Mhe. Meja Jenerali (Mst) Makame Rashid Mhe. Nalaila Kiula Mhe. Zakhia Meghji Mhe. Azan Aljabri Mhe. Paulo P. Kimiti Mhe. Basil P. Mramba Mhe. Mateo T. Qaresi Mhe. John L. Mwakipesile Kipindi 1964 ­ 1964 1964 ­ 1965 1965 ­ 1967 1967 ­ 1971 1971 ­ 1973 1973 ­ 1975 1975 ­ 1977 1977 ­ 1982 1982 ­ 1982 1982 ­ 1983 1983 ­ 1989 1989 ­ 1990 1990 ­ 1990 1990 ­ 1990 1991 ­ 1995 1995 ­ 2000 2000 ­ 2006 2006 ­

-9-

Jedwali Na. 2; Orodha ya Makatibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya kuanzia mwaka 1972; Na. 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. Jina la Kiongozi Bw. Solomon Ole Saibulu Bw. C. Y. Mpupua Bw. Michael Danford Mapunda Bw. Matiku T. Nyitambe Bw. Meshack Mkumbwa Dr. Bismark U. Mwansasu Bw. Bruno Mpangala Lt. Col. Tilumanywa P. Magere Bw. S. Majaliwa Bw. Damsoni Badi Bw. Fredy R. Mwaisaka Asumpta F. Ndimbo (Bibi) Beatha O. Swai (Bibi) Kipindi 1972 ­ 1975 1975 ­ 1976 1976 ­ 1981 1981 ­ 1984 1984 ­ 1987 1987 ­ 1990 1990 ­ 1991 1991 ­ 1994 1994 ­ 1994 1994 ­ 1996 1997 ­ 2004 2004 ­ 2008 2008 ­

- 10 -

Kielelezo na. 2; Picha za Viongozi wa Mkoa wa Mbeya. Mkuu wa Mkoa Katibu Tawala wa Mkoa

Mhe. John L. Mwakipesile Mkuu wa Mkoa Mbeya

Beatha O. Swai (Bibi) Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya

Kielelezo na. 3; Picha za baadhi ya Viongozi waliowahi kuwa Wakuu wa Mkoa wa Mbeya

Hayati Mwl. J. K. Nyerere akiwa katika picha pamoja na John S. Malecela, Njelu Kasaka na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Marehemu Peter Siyovelwa (1971 ­ 1973)

Mhe. Kingunge Ngombare Mwiru Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa (1977 ­ 1982)

- 11 -

Mhe. Chrisant M. Mzindakaya Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa (1982 ­ 1982)

Mhe. Meja jenerali (mst) Makame Rashid Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa (1983 ­ 1989)

Mhe. Nalaila Kiula Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa (1989 ­ 1990)

Mhe. Zakhia Meghji Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa (1990 ­ 1990)

Mhe. Paulo P. Kimiti Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa (1991 ­ 1995)

Mhe. Basil P. Mramba Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa (1995 ­ 2000)

- 12 -

5.0 5.1

MABADILIKO YA MFUMO WA KIUCHUMI NA KIJAMII Mabadiliko ya Mfumo wa Kiuchumi

Katika miaka hamsini ya uhuru, Mkoa wa Mbeya umeshuhudia mabadiliko makubwa katika kuendesha mfumo mzima wa uchumi wake. Katika kipindi baada ya Uhuru, Uchumi wa Mkoa ulijikita zaidi katika kilimo cha mazao ya chakula na wananchi katika baadhi ya maeneo walijishughulisha na kilimo cha mazao ya biashara. Maeneo hayo ni Rungwe (Chai), Chunya (Tumbaku) na Mbozi (Kahawa). Kwa upande wa mazao ya chakula, Jamii ilijishughilisha sana na kilimo cha Mahindi, viazi, maharage, karanga, ulezi, viazi mviringo, ndizi, mbaazi, ufuta na mtama. Jamii ilikuwa ikipata ushauri wa kilimo kutoka kwa wataalam wachache wa kilimo waliokuwepo. Wakulima walikuwa wakitumia samadi kwa ajili ya kuboresha rutuba ya udongo na majivu kwa ajili ya kuondolea wadudu waharibifu wa mazao. Wadudu waharibifu katika kipindi hicho walikuwa ni nzige na viwavijeshi. Zana za kilimo katika kipindi hicho ilikuwa ni jembe la mkono. Mavuno yalikuwa ni kidogo sana kwa sababu kilimo cha kipindi hicho kilikuwa kimelenga kutosheleza familia, koo au kaya fulani. Mabadiliko makubwa yaliyoshudiwa katika sekta ya kilimo ni pamoja na ongezeko la eneo la kilimo, uzalishaji, matumizi ya zana bora za kilimo (Matrekta makubwa na madogo ­ Power tillers), mbolea na mbegu bora, miundombinu ya umwagiliaji, ujenzi wa mabwawa ya kuhifadhia maji, hali inayofanya Mkoa kuwa kati ya Mikoa sita ya kilimo Kitaifa inayotegemewa kuzalisha mazao mbalimbali ya chakula kutosheleza mahitaji na ziada. Mfumo wa soko la mazao haukuwa rasmi. Wakulima waliuza mazao yao katika gulio kwa kubadilishana na bidhaa nyingine kama vile mifugo. Ili kuhifadhi mazao ya kilimo yaliyopatikana, wakulima walihifadhi kwa njia za asili zikiwemo kutumia majivu, kuvukiza kwa moshi, n.k.

- 13 -

5.2

Mabadiliko ya Mfumo wa Kijamii

Katika miaka hamsini ya uhuru, Mkoa wa Mbeya umeshudia mabadiliko makubwa kijamii ikiwa ni pamoja na muingiliano wa makabila, dini, kupungua kwa mamlaka ya viongozi wa kijamii (Machifu na Mamwene), Mila, desturi na tamaduni. Mabadiliko haya kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na mabadiliko ya sheria za nchi ikiwemo kufutwa kwa utawala wa kichifu katika mfumo wa utawala wa nchi, kukua kwa miji, teknolojia, biashara na upatikanaji wa huduma za jamii. Mfano mabadiliko makubwa katika mila na desturi yamechangiwa na kuwepo kwa dini nyingi katika Mkoa. Ufafanunuzi wa mabadiliko haya umeelezwa katika katika mafanikio ya Mkoa Kisekta.

6.0

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA MKOA WA MBEYA KISEKTA HADI SASA

6.1

Hali ya Uchumi wa Mkoa:

Katika kipindi cha miaka hamsini ya Uhuru yaani kutoka mwaka 1961 hadi 2011 Mkoa umepata mafanikio makubwa katika nyanja za uzalishaji mali, utoaji huduma za kiuchumi na kijamii, utawala bora, ulinzi na usalama. Mafanikio hayo ni matokeo ya ushirikiano wa kila hali kati ya wananchi na serikali yao, Serikali za Mitaa, Sekta binafsi, Mashirika ya dini, Mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine wa harakati za kuuletea Mkoa maendeleo.Aidha kwa kipindi cha miaka 50 Mkoa umefanikiwa kuunganisha nguvu za wadau i. hao wa maendeleo na kufikia malengo ya kuimarisha na kuboresha uchumi wa mkoa kama ifuatavyoo; Kujenga uchumi wa kisasa na wenye misingi ya kujitegemea na kuwawezesha wananchi kiuchumi. Shilingi 723,391 milioni 335,305 2009. Kwa mfano, pato la wastani la mwananchi limekuwa kutoka Shilingi 89,726 kwa mwaka 1995 hadi mwaka 2009.Pato la mkoa limekua kutoka Shilingi mwaka 1995 hadi Shilingi milioni 1,867,644 mwaka

- 14 -

ii.

Kuongeza fursa za ajira, kujiajiri, kuimarisha menejimenti ya rasilimali watu na fursa zote zilizopo katika mkoa na kukuza mitaji ya sekta binafsi na sekta isiyo rasmi. Hii ni pamoja na kuimarisha ushirika hasa vyama vya msingi vya kuweka na kukopa, mifuko ya mikopo na vikundi vya uzalishaji mali, kama vyombo vya wananchi vya kuwawezesha kubaini na kumiliki agenda ya maendeleo na kushiriki kikamilifu kuondoa umaskini kwa wananchi.

iii.

Kuimarisha, kutunza na kuendeleza huduma zote za kiuchumi kama vile; barabara, nishati, mawasiliano, uchukuzi, Elimu, Afya, Maji na Ustawi wa Jamii ambavyo vyote vina mchango mkubwa katika uchumi wa Mkoa.

iv.

Kuwepo kwa uongozi bora na utawala wa sheria na kuona kuwa masuala mtambuka yanaingizwa katika mipango na kutekelezwa kikamilifu na wadau wote.

v.

Kuimarisha utoaji wa huduma za kifedha kwa wananchi kutoka katika Taasisi mbalimbali za fedha. Huduma za Kibenki zilizopo katika Mkoa ni pamoja na Benki ya Posta, CRDB, Stanbic, NMB, NBC, Exim, Akiba na CBA. Taasisi nyingine za kifedha zinazotoa huduma katika Mkoa ni pamoja na Bayport Finance, Faidika, Pride Tanzania, Finca Tanzania, Platinum, Blue Finance, Brac Tanzania n.k.

Huduma za Benki

vi.

Masuala hayo ni haki za binadamu, jinsi, Menejimenti ya mazingira, menejimenti ya maafa na kudhibiti VVU/UKIMWI.

- 15 -

vii.

Katika mwaka 1961 Mkoa ulikuwa hauna kiwanda lakini mpaka kufikia mwaka 2011 Mkoa umefanikiwa kuongeza idadi ya viwanda na kufikia viwanda 1,179 ambapo kati ya viwanda hivyo, viwanda vikubwa ni 11, vya kati 14 na vidogo ni 1,154. Baadhi ya viwanda vilivyopo katika Mkoa ni pamoja na Mbozi Cofeee Curing, Lima Coffee Curing, Wakulima Tea Company, City Coffee, Wella Millers, Kapunga Rice Farm, Highland Seeds, Family Loaf, Kiwanda kidogo cha kutengeneza unga wa sembe, Viwanda vidogo 7 vya kukoboa mpunga eneo la Ubaruku, Kiwanda cha kutengeneza bia (TBL), Afri Bottlers na Mbeya Cement.

6.2

Hali ya Kisiasa: TANU chini ya uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Chama cha

Tunaposherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara tunakumbuka pia historia ya Chama cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere..Hivyo kitu cha kwanza kukienzi katika sherehe hizi ni Chama cha TANU na Hayati Mwalimu Nyerere. TANU ndicho kilicholeta ukombozi na kujipatia Uhuru tarehe 9 Desemba 1961. Baada ya Uhuru sera ya kudumu imekuwa ni kudumisha Uhuru wa Watanzania. Kwa kuimarisha Uhuru wetu, Mwalimu J. K. Nyerere aliona nchi jirani zikiwa bado chini ya ukoloni hivyo uhuru wa nchi yetu ungekuwa mashakani. Kufuatia hali hiyo, nchi yetu ikawa mwenyekiti wa kudumu wa ukombozi kusini mwa bara la Afrika jambo ambalo lilifanyika kwa mafanikio makubwa. Hivi leo tunapoadhimisha miaka 50 ya Uhuru, hata nchi hizo tulizozisaidia kujikomboa zinasherehekea kwani historia ya uhuru wa nchi hizo unajivunia jitihada zilizofanywa na nchi yetu. Imani ya wananchi tunapoadhimisha miaka 50 ya uhuru imejikita zaidi katika kuulinda na kuudumisha uhuru wa nchi yetu. Ulinzi wa taifa letu ni wa kila Mtanzania mzalendo.

- 16 -

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika vazi rasmi la mila za kinyakyusa alipotembelea Mkoa wa Mbeya mwaka 2009

Katika Mkoa wa Mbeya mbali na kuwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), vyama vingine vinavyofanya kazi katika Mkoa wa Mbeya ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), National Convention for Construction and Reform (NCCR-MAGEUZI), The Civic United Front (CUF), United Democratic Party (UDP), Progressive Party of Tanzania (PPT-Maendeleo), National League for Democracy (NLD), Union for Multiparty Democracy (UMD), Tanzania Labour Party (TLP), Chama cha Haki na Ustawi Peoples Democratic Party (UPDP), Tanzania (CHAUSTA), Alliance Democratic Party (DP), Jahazi Asilia, Chama Cha Demokrasia Makini, United Democratic (TADEA),National Reconstruction Alliance (NRA) Sauti ya Umma (SAU) na The Forum for Restoration of Democracy (FORD). 6.3 Hali ya Ulinzi na Usalama:

Mwaka 1961 hali ya uhalifu mkoani Mbeya ilikuwa chini sana. Takwimu za uhalifu ziliongezeka kutokana na ongezeko la watu, shughuli mbalimbali za kiuchumi, mwingiliano wa makabila na watu kutoka nchi jirani pamoja na imani za kishirikina. Matukio makubwa yaliyojikeza katika Mkoa ni pamoja na

- 17 -

utengenezaji wa silaha za kuwindia na baadaye kutumika katika uhalifu na unyang'anyi, wimbi la uchunaji ngozi na tukio moja la mauaji ya mlemavu wa ngozi (Albino). Matukio haya yalijitokeza zaidi katika Wilaya ya Mbozi, Ileje, Rungwe na Chunya. Wimbi la uhalifu lilipungua kutokana na juhudi za makusudi za uongozi wa mkoa ambapo kuanzia mwaka 2004 matukio ya uhalifu hususani unyang'anyi, ujambazi wa kutumia silaha, wizi wa magari, magendo, ajali za barabarani, uchunaji ngozi na unyofoaji wa viungo vya binadamu ulitokomezwa. Matukio haya ya uhalifu kwa ujumla yamepungua hadi kufikia asilimia 50 hadi sasa. Mkakati wa kukabiliana na uhalifu kwa sasa ni kwa njia ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi. Uongozi wa Polisi wa Mkoa unazunguka katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha na kuelimisha wananchi kuhusu wajibu wao katika kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuwabaini wahalifu na uhalifu katika maeneo yao. Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imeshiriki kwa pamoja katika kuimarisha usalama mkoani na utunzaji wa mazingira. Aidha viongozi mbalimbali wa kitaifa waliowahi kutembelea mkoa wetu wamekuwa wakiridhishwa na hali ya usalama wa mkoa na kutaka hali hiyo iendelee. Hali ya Mkoa wa Mbeya kwa sasa ni shwari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Advocate Nyombi

- 18 -

6.4

SEKTA YA ELIMU

6.4.1 Elimu ya Awali Baada ya uhuru kulikuwa na vijana wengi wenye umri mkubwa zaidi ya miaka kumi ambao walikuwa hawapo shuleni. Aidha, baadhi ya vijana walibahatika kuanza madarasa ya awali kwa mfumo wa zamani walianzia shule za Jumuia ya Wazazi (Tanzania Parents Association ­ TAPA) ambazo hazikuwa katika mfumo rasmi. Mfumo huo ulioendelezwa kwa ajili ya vijana wadogo, hivi sasa unafahamika kama madarasa ya awali. Tofauti kubwa ya mfumo wa zamani na mfumo wa sasa ni umri wa vijana kuanza madarasa ya awali, ambapo inaonesha kuwa tumepiga hatua kubwa kwani vijana waliopo katika madarasa ya awali kwa sasa wana umri chini ya miaka 7. Serikali imeendelea kuboresha mfumo wa Elimu ya Msingi kwa kuhakikisha kwamba kila shule ya msingi inakuwa na madarasa ya awali. Mpaka kufikia mwaka 2011 Mkoa umefanikiwa kuwa na shule za Msingi 1,057 zenye madarasa ya awali kati ya shule 1065.

6.4.2 Elimu ya Msingi Maendeleo ya Elimu ya Msingi yamekuwa makubwa katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Shule za msingi zimeongezeka kutoka 50 mwaka 1961 hadi kufikia shule 1,065 mwaka 2011. Kati ya hizo, shule za binafsi 15 na serikali 1,050. Ongezeko hili ni kutokana na mipango mbalimbali ya serikali ya kupanua elimu ya msingi na kuboresha miundombinu kama vile Mpango wa Maendeleo ya Elimu Msingi (MMEM). 6.4.3 Elimu ya Sekondari Elimu ya sekondari imepata mafanikio makubwa katika Mkoa wetu kwa kipindi cha miaka 50 ya Uhuru. Sekondari. Wakati nchi inapata Uhuru mwaka 1961, Mkoa ulikuwa na shule za Sekondari 4 za Loleza, Iyunga, Rungwe na Sangu Wanafunzi wengi wa mkoa wa Mbeya walikuwa wanapata elimu

- 19 -

katika shule za Sekondari za Bweni zilizoko nje ya Mkoa. Hata hivyo, idadi ya wanafunzi waliopata fursa ya kusoma katika shule hizo ilikuwa ni ndogo. Katika kipindi cha mwaka 1961 hadi 2011, Mkoa umefanikiwa kuwa na jumla ya shule za Sekondari 298. Kati ya hizo, shule za binafsi zipo 73 na serikali 225.

Baadhi ya majengo ya Shule za Sekondari zilizopo Mbeya.

Sera ya Serikali kuhusu Elimu ya sekondari ni kuwa na Shule moja ya kidato cha kwanza hadi kidato cha nne katika kila Kata na shule moja ya kidato cha tano hadi sita katika kila tarafa. Katika kutekeleza sera hiyo, Mkoa una shule za sekondari za kidato cha kwanza hadi nne katika kila kata na ujenzi wa shule za kidato cha tano hadi sita kwa kila tarafa tayari umeanza katika baadhi ya tarafa. Hadi kufikia mwaka 2011 Mkoa una shule za sekondari 19 zenye kidato cha tano na sita kati ya hizo, shule 15 zimejengwa chini ya mpango maalum wa serikali kuwa kila tarafa iwe na shule ya kidato cha tano na sita kwa kila tarafa kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 3; Jedwali Na. 3; Idadi ya Shule za sekondari zenye kidato cha tano na sita.

Na. Halmashauri Idadi ya Idadi ya Jina la Shule Tarafa Shule

1. 2. 3.

Chunya Ileje Kyela

4 2 2

2 1 2

Kiwanja na Maweni Ileje Matema Beach na Kyela

- 20 -

4. 5. 6. 7. 8.

Mbarali Mbeya (J) Mbeya (V) Mbozi Rungwe Jumla

2 2 3 8 4 27

1 2 2 5 15

Madibira Iwalanje na Usongwe Vwawa na Mwl. J K. Nyerere Tukuyu, Mwakaleli, Lufilyo, Isongole na Lwangwa

Baadhi ya majengo ya madarasa na maabara yaliyo katika hatua mbalimbali za ujenzi

6.4.4 Elimu ya Juu katika kipindi cha uhuru, mkoa haukuwa na chuo kikuu. Kutokana na jitihada za serikali katika kuinua elimu ya juu na kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika elimu ya juu, Mkoa umefanikiwa kuwa na Chuo kikuu kimoja cha Teofilo Kisanji (TEKU) na matawi ya vyuo vikuu vya Mzumbe, Ushirika na Stadi za Biashara Moshi (MUCCOBs), Tumaini na Chuo Kikuu Huria. Mkoa pia una Taasisi ya Sayansi na Teknolojia (Mbeya Institute of Science and Technology ­ MIST) chuo cha Uhasibu (Tanzania Institute of Accountancy ­ TIA) na Vyuo vya Elimu vitano (5).

- 21 -

Moja kati ya majengo ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Mt. Teofilo Kisanji (TEKU)

6.4.5 Elimu ya Ufundi Katika kuboresha elimu ya kujitegemea mkoa umefanikiwa kuwa na vyuo vya ufundi 45 vilivyo chini ya Chuo cha ufundi (VETA). Kati ya vyuo hivyo, vyuo 8 ni vya Serikali, 3 vinamilikiwa na mashirika yasiya ya kiserikali na 16 ni vya binafsi. Hii ni mafanikio makubwa sana ikilinganishwa na miaka ya 1960 ambapo mkoa wa Mbeya haukuwa na chuo chochote cha ufundi. 6.5 SEKTA YA KILIMO:

6.5.1 Mfumo wa Kilimo Kabla ya uhuru kilimo cha mazao hususan ya biashara kiliendeshwa na wakulima wakubwa. Kilimo cha wakulima wadogo kilianza baada ya Uhuru mwaka 1961. Mwaka 1967 kulianzishwa Azimio la Arusha la Ujamaa na kujitegemea. Mwaka 1974 vijiji vya ujamaa vilianzishwa ambapo wananchi walilima mashamba yao kwa pamoja kupitia vyama vya ushirika. Mfumo wa kilimo kwa sasa umeboreshwa zaidi ambapo wakulima wakubwa na wadogo wanashiriki katika kilimo cha mazao ya chakula na biashara. Mazao makuu ya chakula ni mahindi, mpunga, maharage, ndizi, mihogo, ngano, mtama, ulezi, karanga, ufuta, manunuzi, vitunguu na mboga mboga. Mazao ya biashara pamoja na Kahawa, Chai, Tumbaku, Kokoa, Pareto na alizeti. Kilimo cha zao la pamba halilimwi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Kilimo cha pamba hususan wilayani Chunya kilizuiwa na Serikali kuanzia msimu wa 1994/1995 kutokana na kutokea kwa funza wekundu (Diparopsis Castanea)

- 22 -

wanaoshambulia zao hilo na kupunguza tija ya uzalishaji. Hadi sasa udhibiti wa funza hao haujapatikana. Mabadiliko makubwa yamefanyika katika kilimo kwa kuwa na kilimo kinachozingatia utaalamu, kupanuka kwa maeneo ya kilimo na ongezeko la tija katika uzalishaji, udhibiti wa visumbufu na magonjwa ya mazao na mimea.

Baadhi ya mazao ya chakula na Biashara yanayolimwa Mkoani Mbeya

Takwimu halisi za hivi karibuni zinaonesha kuwa Mkoa wa Mbeya una eneo la kilomita za mraba zipatazo 63,622 ambapo kati ya hizo kilomita za mraba 61,868 ni nchi kavu na zilizosalia yaani 1,754 ni eneo la maji. Katika eneo la nchi kavu, km2 4,122 ni misitu na mbuga za wanyama, km2 746 ni milima na majabali na km2 57,000 ndizo zinazofaa kwa kilimo.

- 23 -

Sehemu ya maeneo ya Uoto wa Asili Mkoani Mbeya (Ziwa Ngosi, Mlima Loleza na Kawetere)

Eneo linalolimwa kwa sasa ni km2 13,000. Eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni km2 870 kati ya eneo hilo linalomwagiliwa ni km2 197.94. 6.5.2 Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Biashara Uzalishaji wa mazao ya chakula umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na hali nzuri ya hewa, matumizi ya pembejeo za ruzuku, kilimo cha umwagiliaji, ongezeko la matumizi ya mbolea, mbegu na zana bora za kilimo. Eneo la kilimo kwa mazao ya chakula limeongezeka kutoka hekta 261,685 mwaka 1961 hadi hekta 821,381.8 mwaka 2011 na mavuno kutoka tani zinazokadiriwa kufikia 210,500 mwaka 1961 hadi tani 3,290,055 mwaka 2011. Kwa upande wa mazao ya biashara eneo la kilimo limeongezeka kutoka hekta

- 24 -

zinazokadiriwa kufikia 10,300 mwaka 1961 hadi hekta 124,479 mwaka 2011 na mavuno kutoka tani zinazokadiriwa kufikia 30,700 mwaka 1961 hadi tani 77,941 mwaka 2011.

Baadhi ya maeneo yanayoendesha Kilimo cha mpunga, Mahindi na Maharage 6.5.3 Kilimo cha Umwagiliaji Mabonde yanayofaa kwa umwagiliaji yanajumuisha skimu za umwagiliaji zipatazo 159 zilizoendelezwa na kuboreshwa na zile ambazo hazijaendelezwa. Mkoa una hekta 90,190 zinazofaa kwa umwagiliaji. Kufikia Juni 2011 jumla ya hekta 55,225 zilimwagiliwa zikiwemo hekta 30,034 zilizoboreshwa na hekta 25,191 zilizomwagiliwa kwa teknolojia za asili.

Moja kati ya miundombinu ya skimu za umwagiliaji. 6.5.4 Matumizi ya Pembejeo Wakati wa Uhuru matumizi ya mbolea na mbegu bora yalikuwa kidogo. Rutuba ya udongo iliendelea kupungua mwaka hadi mwaka. Kuanzia wakati

- 25 -

wa uhuru hifadhi ya udongo imeboreshwa kwa kuzingatia kanuni za kilimo ikiwemo kilimo cha makinga maji. Aidha rutuba ya udongo inaendelezwa kwa kutumia mbolea za asili na viwandani. Matumizi ya mbegu bora pia yameongezeka ili kuongeza tija ya uzalishaji. Kwa mfano matumizi ya mbolea yameongezeka kutoka tani 28,457 mwaka 1990 hadi tani 131,294 mwaka 2011, mbegu bora kutoka tani 2,009 mwaka 1990 hadi tani 7,861 mwaka 2011. Elimu ya umuhimu wa matumizi ya pembejeo bora na Ruzuku inayotolewa na Serikali ni mojawapo ya sababu zilizochangia ongezeko la matumizi ya pembejeo hizo. Mbolea ya ruzuku imeongezeka kutoka tani 12,700 mwaka 2005/2006 hadi tani 32,028 mwaka 2011 na mbegu bora kutoka tani 1,170 mwaka 2008/2009 hadi tani 3,189 mwaka 2010/2011. 6.5.5 Matumizi ya Zana za Kilimo Matumizi ya zana bora za kilimo yameongezeka ikilinganishwa na kipindi cha kabla na wakati wa uhuru ambapo jembe la mkono lilitumika kwa kiwango kikubwa. Kwa mfano mwaka 1990 mkoa ulikuwa na matrekta makubwa 262 na plau 42,389. Kufikia Juni 2011 mkoa una matrekta makubwa 387, matrekta madogo 988, maksai 56,215 na plau 28,807. 6.5.6 Huduma za Ugani Utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima na wafugaji umeongezeka kwa kutumia mbinu mbalimbali zikiwemo mashamba darasa, mashamba ya mfano na waganikazi. Mbinu hizi zimeboreshwa zaidi ili kuweza kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima wengi zaidi. Kwa mfano kupitia shamba darasa, afisa ugani mmoja anaweza kufundisha wakulima kati ya 25-30 badala ya kutembelea mkulima mmoja mmoja katika kaya/shamba. Mbinu ya shamba darasa ilianza mwaka 2005; idadi ya mashamba darasa imeongezeka kutoka 37 mwaka 2005/2006 hadi 268 mwaka 2010/2011 yakiwemo ya mazao 204 na ya mifugo 64 na kuweza kunufaisha wakulima 5,494 wakiwemo wanawake 3,125 na wanaume 2,369.

- 26 -

6.5.7 Usindikaji wa Mazao ya Kilimo Kuna viwanda vinavyotumika katika kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na mifugo. Aidha mashine mbalimbali zinatumika kwa mazao ya alizeti, kahawa na usindikaji wa maziwa unaofanywa na vikundi vya wafugaji vya MVIWAMBO -Mbozi, Faraja ­ Tukuyu, Mbeya Milk na katika Chuo cha Kilimo Uyole. Pamoja na shughuli zinazoendelea za kuongeza thamani ya mazao, bado kuna hitaji kubwa la kupanua viwanda vya kisasa zaidi ili kukabiliana na ushindani uliopo katika soko la kimataifa ambalo linahitaji mazao bora na yaliyosindikwa katika madaraja mbalimbali. Soko la mazao limeimarishwa ambapo wakulima wameunganishwa na masoko ya ndani na nje ya mkoa kwa kupata tarifa za bei, kuunganishwa na mfumo wa Stakabadhi ya Mazao Ghalani na kutumia vipimo ili kuweza kuuza kwa kupata faida.

6.6 (i)

Sekta ya Mifugo: Mkoa una jumla ya Ng'ombe 652,627 wa asili na ng'ombe wa kisasa 53,055. Pia mkoa una Ng'ombe wa nyama (beef cattle) 2,045. Mkoa una Mbuzi 272,811. Mkoa pia una Mbuzi wa maziwa wapatao 7,926 na Mbuzi wa nyama 1,763.

Mkoa umepiga hatua katika sekta hii kama ifuatavyo;

- 27 -

Ufunguo; 1. Mbuzi 3. Kondoo

2. Ng'ombe 4. Kuku wa asili

Baadhi ya Mifugo inayofugwa na Wananchi Mkoani Mbeya

(ii)

Mkoa pia una kondoo 8,441, nguruwe 174,749, kuku wa asili 2,216,735 na kuku wa kisasa 84,480.

Moja ya madume bora ya nguruwe Mkoani Mbeya

(iii)

Mkoa umefanikiwa sana katika kuendeleza sekta ya mifugo kwa kuhuisha teknolojia bora ya uhamilishaji kwa ng'ombe na pia kuwa na madume wananchi bora ili kuhakikisha kwamba sekta hii inakuwa na tija kwa wa Mkoa. Kufikia - 28 mwaka 2011 ng'ombe 10,460

wamehamilishwa. Madume bora yameongezeka kufikia 5,719 mwaka 2011. Pamoja na juhudi mbalimbali zilizofanyika, changamoto mbalimbali

zimejitokeza katika kuendeleza sekta hii. Changamoto hizi ni pamoja na upatikanaji wa kliniki za mifugo kutoka kijiji ambapo maeneo mengi yanayojihusisha na ufugaji yapo umbali wa kilomita 15 kutoka kliniki ya mifugo, uwepo wa wataalam wa kutosha wa mifugo, maradhi ya mifugo kama vile minyoo, homa ya mapafu na nguruwe, ugonjwa wa miguu na midomo na upatikanaji wa masoko yaliyoimarika ya mazao ya mifugo ambapo asilimia 15 ya kaya zipo mbali ya masoko makuu ya mifugo zaidi ya km. 15; wakati asilimia 19 ya kaya zipo zaidi ya km.15 kutoka masoko ya msingi (minada). 6.7 Sekta ya Maliasili na Utalii: Katika sekta ya Wanyamapori Mkoa ulitenga mapori ya akiba mawili na kuyahifadhi. Mapori hayo ni ya Usangu wilaya ya Mbarali na Lukwati Wilaya ya Chunya. Pori la Akiba la Usangu limepandishwa hadhi na kuwa Hifadhi ya Taifa kwa kuunganishwa na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Baadhi ya Wanyama wanaopatikana katika hifadhi za Mkoa wa Mbeya

Vile vile katika sekta ya misitu, misitu ya hifadhi imetengwa na kuhifadhiwa. Mkoa ulikuwa na misitu ya hifadhi 77 ambayo imeongezeka na kufikia takribani 137 baada ya Programu ya Usimamizi Shirikishi kuwezesha vijiji kuhifadhi misitu 60. Misitu mikubwa ya Kawetere na Kiwira imepandwa miti

- 29 -

na kutunzwa na inaendelea kupandwa miti. Usimamizi wa misitu unafanyika kwa kuzingatia Sera ya misitu ya mwaka 1998 ambayo inafanyiwa mapitio kwa lengo la kuiboresha. Ipo pia Sheria ya misitu Na. 14 ya mwaka 2002 iliyoboresha tuliyorithi wakati wa uhuru. Miti imepandwa kwenye vyanzo vya maji na mashamba ya watu binafsi. Dhana ya ushirikishwaji wananchi katika kuhifadhi misitu imeanzishwa na inaendelea kutumika. Zipo programu mbili za usimamizi shirikishi wa misitu na matumizi endelevu ya ardhioevu ambazo zinahimiza vijiji kuhifadhi maeneo kwa maendeleo endelevu. Mkoa umetayarisha sera ya kuhifadhi mazingira na inatumika. Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira limeanzishwa na linafanya kazi na Elimu ya kutunza na kuboresha mazingira inatolewa kwa wananchi. Misitu ya miombo, iliyoenea katika maeneo mengi ya mkoa, inawezesha wananchi wengi kufuga nyuki kwa ajili ya asali na nta ambavyo huongeza vipato vya wananchi. Wilaya za Chunya, Mbozi na Mbarali zina fursa ya kuzalisha zaidi na wananchi wanatumia fursa hiyo kuzalisha zaidi. Elimu ya kuzalisha asali na nta bora inatolewa ili kukidhi matakwa ya soko la ndani na nje ya nchi. Katika sekta ya uvuvi, sera ya uvuvi imetayarishwa na inatumika na pia wananchi wanahimizwa kuanzisha vikundi vya wavuvi na vipo vinafanya kazi ya kuvua na kuuza samaki na vile vile uchimbaji wa mabwawa ya samaki umeanzishwa na unaendelea. Mkoa una jumla ya mabwawa 959 na crater lakes 9. Kati ya mabwawa hayo, Chunya (24), Mbozi (85), Kyela (8), Ileje (264), Rungwe (429 na crater lakes 9), Mbarali (5), Halmashauri ya Mbeya (124) na Jiji (20).

- 30 -

Shughuli za Uvuvi katika Ziwa Rukwa Wilaya ya Chunya Katika sekta ya Nyuki, wananchi wamepewa mafunzo ya jinsi ya kufuga nyuki kwa njia za kisasa na kuvuna mazao ya nyuki kama Nta na Asali kwa njia za kisasa na pia maeneo ya kufugia nyuki yametengwa.

Shughuli za Ufugaji wa nyuki na Uvunaji wa Asali katika Wilaya ya Chunya

6.8 Sekta ya Ushirika: Kabla ya Uhuru wanachama wenyewe katika sekta ya ushirika ndio waliokuwa wakianzisha na kuendesha ushirika wao. Kazi ya serikali ilikuwa ni kutoa Ushirika leo umerithi habari, uhamasishaji, elimu, mafunzo, ukaguzi na usimamizi. Ushirika ulikuwa huru na ulizingatia kanuni ya kujitegemea. n.k. Baada ya Uhuru, kutokana na mafanikio ya ushirika katika sehemu chache nchini, serikali ilichukua jukumu la kuanzisha na kuendesha ushirika. Serikali ilisimamia uanzishaji wa ushirika. Ushirika ulijumuishwa moja kwa moja kwenye malengo ya kitaifa badala ya kufuata matakwa na malengo ya mali nyingi za ushirika huu wa kabla ya Uhuru kama vile majengo, mitambo

- 31 -

wanachama wa ushirika. Hii ilichangia kwa kiasi kikubwa kukosekana kwa mitaji kutoka ndani ya ushirika na hivyo ushirika kuwa tegemezi kwa serikali na kuendeshwa kwa mikopo. Sheria ya Ushirika imekuwa ikibadilika mara kwa mara tangu Uhuru kama ifuatavyo:(i) (ii) Sheria ya kwanza baada ya Uhuru ilitungwa mwaka 1968. Mwaka 1975 ilitungwa sheria iliyojulikana kama sheria ya kuandikisha vijiji na vijiji vya ujamaa. Baada ya sheria hii iliyotambua kuwa vijiji vyote ni Vyama vya Ushirika iliashiria kufutwa kwa Vyama vya Ushirika vya mazao vyote vilivyokuwa vimeandikishwa chini ya sheria ya 1968. (iii) Mwaka 1982 ilitungwa sheria Na.14 ya Vyama vya Ushirika ambayo nayo ilitaka vijiji vyote viandikishwe kuwa vyama vya ushirika wa uzalishaji mali. (iv) Sheria Na.15 ya 1991 ilitungwa sheria na vyama vya mazao. (v) Mwaka 2003 ilitungwa sheria nyingine Na. 20 ambayo imeweza kutambua uwepo wa vikundi vya ushirika (Pre-Co-operatives). Katika hatua zote hizi za mabadiliko kumekuwepo na kuandikishwa na kufutwa SACCOS ambazo hazikuweza kuhimili ushindani wa biashara ya fedha. Hata hivyo kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa hali ya SACCOS katika kipindi cha Sheria ya Ushirika ya 1968 uandikishaji wa SACCOS 2003 kumekuwepo na ambapo hadi kufikia mwaka 2010/2011 mkoa Vyama vya Akiba na Mikopo vijijini iliyovitaka vyama vya Akiba na Mikopo vijijini viandikishwe tofauti

unazo SACCOS zipatazo 318,vyama vya mazao 151,na vyama vingine 121. 6.9 Sekta ya Ardhi:

Katika kipindi hiki cha miaka 50 ya uhuru sekta ya ardhi imeendelea kuboreshwa katika Mkoa ambapo serikali imeendelea kuimarisha Idara ya ardhi, upimaji na ramani. Viwanja mchanganyiko 49,604 katika mkoa

- 32 -

vimepimwa,

mashamba

ya

ukubwa

mbalimbali

1,800

katika

mkoa

yamepimwa. Vijiji 765 vimepimwa na kati yake vijiji 437 vina vyeti vya vijiji. Wilaya ya Mbozi ni moja ya maeneo ya majaribio ya matumizi ya hati za kimila ambapo mashamba 24,250 ya wananchi yalihakikiwa ili kupewa hati miliki za kimila hadi Julai, 2011 hati miliki 21,330 za kimila za mashamba yaliyohakikiwa zimetolewa. Jumla ya mipngo ya matumizi bora ya ardhi 47 iliweza kuandaliwa kwa kutumia fursa mbalimbali kama vile Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Wetlands management, DADPS na WWF. Katika kutekeleza sheria namba 5 ya Ardhi ya mwaka 1999 Mkoa unajumla ya Vijiji 800 kati ya Hivyo vijiji 607 vinamabaraza ya Ardhi,Katika mabaraza hayo ni mabaraza 506 ndio yanayofanya kazi kwa sasa. Vilevile mkoa unakata 173 ambapo jumla ya mabaraza ya Ardhi ya kata ni 173 na yote yanafanya kazi.vilevile kuna masjala za Ardhi za vijiji 189 katika kati ya vijiji 800 6.10 Barabara: Hali ya miundo mbinu ya barabara katika Mkoa kabla na baada ya Uhuru ilikuwa si ya kuridhisha kwani kulikuwa hakuna barabara za lami na pia hakukuwa na mtandao wa barabara zilizokuwa zinaweza kupitika mwaka mzima. Maeneo mengi hayakuwa yameunganishwa katika mtandao wa barabara hali iliyopelekea suala la usafiri kuwa gumu kwani ililazimu kutumia muda wa siku mbili kusafiri kutoka Mbeya kwenda Iringa na ililazimu kupitia barabara ya mlimani Makete. Hali ya mtandao wa barabara kwa sasa ni nzuri ikilinganishwa na wakati wa uhuru. Mkoa kwa sasa una barabara zenye urefu wa kilomita 10,512.68. Kati ya hizo km 833.95 zimejengwa kwa kiwango cha lami km 6,160.08 zimejengwa kwa kiwango cha changarawe na km 3518.65 ni za udongo.

- 33 -

Mtandao wa barabara za Mkoa wa Mbeya

Mtandao mkubwa na ubora wa barabara umekuwa ni kichocheo cha shughuli nyingi za kiuchumi na maendeleo ya mkoa kwa ujumla. Miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara inayotekelezwa katika Mkoa kuanzi kipindi cha mwaka 2005 hadi sasa ni pamoja na; (i) (ii) (iii) (iv) Ujenzi wa barabara ya Rujewa ­ Madibira ­ Kinanyambo (KM 152.1) Ujenzi wa barabara ya Katumba ­ Mbambo ­ Tukuyu (KM 83) Ujenzi wa barabara ya Mpemba ­ Isongole ­ Tz/Malawi Boarder (KM 51.15) Ujenzi wa barabara ya Kikusya ­ Ipinda ­ Matema (KM 39.5)

- 34 -

(v) (vi)

Ujenzi wa barabara ya Mbeya ­ Chunya ­ Makongorosi ­ Rungwa (KM 115) Ujenzi wa barabara ya Tunduma ­ Ikana ­ Laela (KM 127.9)

Baadhi ya Miundombinu ya Barabara iliyopo na inayoendelea kutekelezwa 6.11 Nishati ya Umeme; Kabla na baada ya uhuru mwaka 1961, mkoa haukua na mtandao wa umeme katika Makao Makuu ya mkoa, Wilaya na miji. Hadi kufikia mwaka 2011 mkoa umepata mafanikio makubwa katika miundombinu ya umeme ambapo mahitaji ya umeme katika mkoa yamefikia megawati 29 na watumiaji wa umeme waliopo ni 47,920. Mkoa umefanikiwa kuunganisha umeme katika makao makuu ya Wilaya zote, Miji na baadhi ya maeneo ya vijijini. Hadi kufikia mwaka wa fedha 2011/2012, Mkoa una jumla ya miradi 13 ya umeme vijijini ambayo hivi sasa ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Miradi hii itakapokamilika, jumla ya watumiaji 650 wataunganishwa. Miradi hiyo

- 35 -

inatekelezwa katika Halmashauri za Wilaya ya Mbeya (4), Mbozi (3), Chunya (3), kyela (3) na Rungwe (2). Pia baadhi ya miradi inatekelezwa katika Jiji la Mbeya.

TANESCO Mwakibete Sub-station 220/33KV iliyopo eneo la Sae, Mbeya Jiji

6.12 Sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji; Katika kuboresha huduma mbalimbali za usafiri na uchukuzi, Mkoa unashirikisha Serikali na sekta binafsi. Mkoa umefanikiwa kuwa na miundombinu imara ambapo kuna viwanja vitatu vya ndege vya serikali ikiwamo kiwanja cha kati cha Mbeya Mjini, Kiwanja cha kimataifa Songwe kinachoendelea kujengwa na Serikali ya Tanzania na kiwanja kidogo cha ndege Chunya. Aidha, kuna viwanja vinavyomilikiwa na watu binafsi kama vile kiwanja cha ndege Tukuyu na viwanja vya ndege vitano vilivyopo Wilaya ya Mbarali.

- 36 -

Moja kati ya Viwanja vidogo vinavyopatikana Mkoani Mbeya

6.13 Mawasiliano Katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru, mkoa umefanikiwa kuboresha huduma za mawasiliano ambapo mkoa umeunganishwa katika mtandao wa mawasiliano kwenye ngazi zote za Wilaya, miji na baadhi ya Vijiji. Mitandao ya mawasiliano inayounganisha sehemu mbalimbali za mkoa ni pamoja na TTCL, TIGO, VODACOM, AIRTEL and ZANTEL. Pia, mkoa umeunganishwa kwenye mtandao wa mawasiliano wa Kitaifa (Mkongo wa mawasiliano).

6.14 Uchukuzi Hali ya huduma ya uchukuzi katika mkoa haikuwa ya kuridhisha wakati wa uhuru kutokana na kutokuwepo na miundombinu yenye kukidhi viwango. Kuanzi mwaka 1968 hadi 1973 mkoa uliunganishwa kwenye mtandao wa barabara ya Kitaifa (TANZAM Highway) iliyojengwa kwa kiwango cha lami lengo ikiwa ni kuunganisha mkoa wa Mbeya na mikoa mingine pamoja na nchi jirani ya Zambia. Aidha, mkoa umeunganishwa na reli ya TAZARA iliyojengwa kati ya mwaka 1970 ­ 1976. uwepo wa miundombinu hii muhimu umechangia kwa kiasi kikubwa kukua haraka kwa sekta ya uchukuzi ambapo kwa sasa hali ya uchukuzi na usafirishaji wa mazao, malighafi na bidhaa za viwandani umekuwa rahisi hali inayopelekea kuwepo na kampuni mbalimbali za uchukuzi katika maeneo yote ya Mkoa Mjini na Vijijini.

- 37 -

Stesheni ya TAZARA ­ Mbeya na treni ya TAZARA.

6.15 Sekta ya Maji: Katika Sekta ya Maji, mkoa umepiga hatua kubwa sana katika kuwapatia wananchi wake huduma ya maji safi na salama tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961. Pamoja na idadi ya wakazi kuongezeka kwa wastani wa asilimia 2.4 kwa mwaka, asilimia ya wananchi wanaopewa huduma ya maji iliendeleea kukua kwa mtiririko ufuatao:(i) (ii) (iii) Mwaka 1961 huduma ya maji safi na salama ilikuwa asilimia 5 ya wakazi wote. Mwaka 1980 huduma ya maji safi na salama ilikuwa asilimia 20, Mwaka 1995 huduma ya maji safi na salama ilikuwa asilimia 48, aidha, huduma ya maji safi na salama hadi kufikia mwaka 2005 ilikuwa asilimia 54 vijijini na asilimia 73 mijini. (iv) Hadi kufikia Machi, 2011 huduma ya maji safi na salama ilikuwa asilimia 57.8 vijijini na asilimia 89.6 Jijini Mbeya. Mwaka 1961 Mkoa ulikuwa na miradi midogo 5 tu iliyokuwa ikitoa huduma kwa watu wachache katika miji ya Mbeya, Tunduma, Kyela, Tukuyu na Chunya. Wananchi wengi walitegemea vyanzo vyao vya asili vya maji vya mito na chemichemi ambavyo havikuwa safi na salama.

- 38 -

Baada ya uhuru Serikali ilianzisha mkakati wa kuwapatia wananchi wake maji kwa matumizi yao. (i) (ii) Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru ni kama ifuatavyo; Mkoa unayo miradi ya visima vifupi na virefu 723 hadi Desemba 2010 inayohudumia miji na vijiji katika Wilaya zote 7 za Mkoa; Mkoa ulitekeleza mradi kabambe wa maji kwa ufanisi mkubwa kwa kushirikiana na DANIDA kati ya mwaka 1980 ­ 1985 ambapo vijiji 170 vilipewa huduma ya maji kwa dhana ya ushirikishaji wananchi (iii) (iv) Upatikanaji wa maji katika Jiji la Mbeya umepanuliwa hadi kufikia asilimia 89.6 ukilinganisha na asilimia 5 tu mwaka 1961; Ushirikishwaji wa wananchi katika upatikanaji wa huduma ya maji umeimarishwa vijijini na mjini. Kwa upande wa vijiji kamati za maji 514 na mifuko ya maji 470 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 150 zimeundwa. Aidha mamlaka za maji 11 chini ya Bodi za Ushauri zimeundwa kisheria ili kusimamia huduma ya maji katika Mkoa, Wilaya na Miji midogo; (v) Mkoa unashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira katika wilaya zote za mkoa kuanzia mwaka 2006/2007 ikiwa ni juhudi ya kufikia malengo ya milenia yanayoelekeza kuwa na asilimia 74 ya wananchi wapatao huduma ya uhakika ya maji safi na salama hadi mwaka 2015; (vi) Mkoa tayari umebaini zaidi ya vyanzo vya maji 5500 kwa lengo la kuhifadhiwa kama sehemu ya mkakati wa kuhifadhi mazingira ya Ardhi na vyanzo vya maji; (vii) Mkoa pia umeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendelelo katika sekta ya maji katika kufanikisha lengo kuu, hawa ni pamoja na SIDA, ELCT ­ Dayosisi ya Konde, DFID na Japan.

- 39 -

6.16 Sekta ya Biashara: Katika sekta ya biashara nchi yetu ilipokuwa inapata Uhuru, tarehe 09 Desemba 1961, mkoa ulikuwa na maduka machache sana; hasa Makao Makuu ya Wilaya. Sera za Taifa zilitetea sana wanyonge na kupelekea kuanzishwa kwa maduka ya ushirika ambapo watu waliungana na kuchanga kuanzisha maduka ya ushirika. Maduka hayo hayakudumu kwa muda mrefu sana kufuatia uongozi mbaya pamoja na kukosa mtaji mkubwa wa kuyaendesha. Hali ya biashara imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, ukizingatia kwamba Mkoa wetu ni wa kuzalisha mazao aina mbalimbali ambayo huwapatia wananchi wake fedha baada ya kuyauza. Uchimbaji wa madini ni shughuli muhimu pia katika Mkoa wetu. Kuna mgodi wa makaa ya mawe Kiwira ambao kwa hivi sasa shughuli zake zimesimama pamoja na dhahabu inayochimbwa Chunya na wachimbaji wadogo-wadogo wasiotumia teknolojia wala utaalam wa kihandisi.

- 40 -

Uchimbaji wa Madini Mkoani Mbeya

Mbali na makaa ya mawe na dhahabu, Mkoa unayo madini mengine kama Gemstone, Dimensional stones, kama vile marble, Industrial minerals kama gypsum, ulanga, chumvi, mineral water (hot springs), gesi ya Kyejo (Liquid Carbondioxide), pamoja na chokaa, udongo wa mfinyanzi na kokoto kwa ajili ya ujenzi. Katika sekta ya viwanda wakati wa Uhuru mkoa ulikuwa na viwanda vichache sana. Viwanda vilivyokuwepo vilikuwa ni vya Chai katika Wilaya ya Rungwe pamoja na sabuni Rungwe na Kyela. Mjini Mbeya tulikuwa na Mbeya Industries, kilichokuwa kinakamua mafuta ya kula.

- 41 -

Moja ya Viwanda vya Chai, Uzalishaji wa gesi ya Carbondioxide, Cement na TBL Mkoani Mbeya

Katika miaka ya 1970 na 1980, Mkoa ulishuhudia ujenzi wa viwanda vingi, hasa katika mji wa Mbeya. Viwanda vilivyoanzishwa katika kipindi baada ya uhuru ni pamoja na Kiwanda cha Zana Za Kilimo (ZZK), Mbeya Textile, Hisoap, Kiwira Coal Mine, Mbeya Cement, Mbozi Coffee Curing, Lima Coffee Curing, Wakulima Tea Company, City Coffee, Wella Millers, Kapunga Rice Farm, Highland Seeds, Family Loaf, Afri ­ Bottlers, Maji Rungwe, SBS na CocaCola Bottlers. Hali ya uzalishaji katika viwanda vyetu sio nzuri sana kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo ya uchakavu wa mitambo, upatikanaji mdogo wa malighafi, viwango vikubwa vya gharama za umeme na kukosekana kwa soko la kuaminika. Baada ya kutambua umuhimu wa masoko, Mkoa sasa una masoko na magulio katika Wilaya zote ambayo yanafanyika katika siku mbalimbali kwa kila Wilaya. Mfano, mkoa umejenga masoko ya kisasa katika Wilaya za Mbozi (Soko

- 42 -

la Tunduma), Ileje (Soko la Isongole), Kyela (Soko la Kasumulu na soko la Samaki - Matema), Mbeya Vijijini (Soko la Inyala). Pia, ujenzi wa soko la kimataifa la Mpunga ­ Igurusi Mbarali upo katika hatua za awali, Ujenzi wa soko la kimataifa la kisasa unaendelea katika Jiji la Mbeya (Mwanjelwa City Market) na ujenzi wa One Stop Boarder ­ Tunduma upo katika hatua za usanifu. 6.17 Sekta ya Afya: Katika sekta ya Afya, Mkoa umepata mafanikio kadhaa katika utoaji wa huduma za Afya Tiba na Kinga kwa wananchi wake katika nyanja mbalimbali za utoaji wa huduma husika. Baadhi ya mafanikio yaliyoweza kupatikana ni kama ifuatavyo; i. Kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma ambapo kwa hivi sasa tuna Hospitali 18, Vituo vya Afya 38 na Zahanati 331 hadi kufikia mwaka 2011; ii. Kuanzishwa kwa huduma za Mama na Mtoto ili kupunguza kasi ya vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 (mitano); iii. Kiwango cha wajawazito wanaojifungua kwenye vituo vya afya vyenye wahudumu wenye ujuzi kimeongezeka hadi kufikia asilimia 54 mwaka 2010; iv. Kupungua kwa vifo vya akina Mama vinavyotokana na uzazi kutoka vifo 508/100,000 mwaka 1998 hadi 181/100,000 mwaka 2005 na kwa watoto kutoka vifo 147/1000 hadi vifo 88/1000; v. Mkoa umefanikiwa kuwa na jumla ya vituo 261 vya kutoa huduma za kuzuia maambukizi ya VVU/UKIMWI mwaka 2010 na kuandaa mpango kabambe wa kudhibiti UKIMWI; vi. Kuanzishwa na kuimarika kwa mfumo wa taarifa za uendeshaji wa huduma za Afya ambao umewezesha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za Afya kwa uhakika zaidi;

- 43 -

vii. Kuwepo kwa vyuo vya mafunzo mbalimbali ya kada za Afya. Kwa sasa kuna vyuo 6 (Uuguzi 4, Udaktari 1, Meno 1). hapakuwa na chuo chochote; viii. uwepo wa watumishi wengi wazalendo wa fani mbalimbali za huduma za Afya wakiwemo wataalam waliobobea (Specialists) katika nyanja mbalimbali za afya; ix. x. xi. Upanuzi wa Hospitali iliyokuwa ya mkoa na kuwa Hospitali ya Rufaa; Mkoa umefanikiwa kujenga Hospitali mpya ya Mkoa inayotoa huduma za kisasa za matibabu, upimaji na chanjo; Kuanzishwa kwa mfuko wa afya ya jamii (Community Health Fund) katika wilaya zote na mfuko wa Bima ya Afya kwa watumishi; Kabla ya uhuru

Baadhi ya vituo vya kutolea Huduma na tiba ­ Mbeya (Hospitali ya Mkoa, Hospitali Teule ­ Ifisi, Jengo la Maabara na Kliniki ya Watoto Hospitali ya Rufaa Kanda)

- 44 -

6.18 6.18.1

Rasilimali Watu na Utawala Bora; Hali ya Utumishi katika Mkoa;

Hali ya utumishi wa Umma na Utawala Bora katika muda wa miaka 50 ya uhuru, mkoa umekuwa na mafanikio makubwa katika sekta zote. Jitihada mbalimbali zimefanyika katika ngazi ya mkoa katika kuboresha hali ya utumishi. Mkoa umeendelea mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa watumishi wake ili kuwaendeleza watumishi waliopo lengo ikiwa ni kuwa na watumishi wenye sifa zinazostahili kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa mkoa na wadau mbalimbali ili waweze kujiletea maendeleo. Katika Mpango Mkakati wa mkoa, lengo limewekwa kuhakikisha kwamba mkoa unaondokana na tatizo la uhaba wa watumishi wenye sifa stahiki ili kuwa na watumishi wanazingatia utawala bora. Hadi kufikia Juni, 2011 mkoa una watumishi wapatao 19,966. Haya ni maendeleo makubwa katika sekta ya rasilimali watu na utawala bora ikilinganishwa na wakati wa uhuru. Pamoja na mafanikio haya mkoa bado una upungufu wa watumishi 4,899 katika sekta mbalimbali Mchanganuo wa watumishi waliopo na upungufu katika mkoa ni kama ilivyooneshwa katika Jedwali Na. 4; Jedwali Na. 4; Hali ya Watumishi wa Umma katika Mkoa. Na. 1 2 3 4 5 6 7 8 9 Mkoa/Halmashauri Sekretarieti ya Mkoa wa Mbeya Chunya Kyela Ileje Mbarali Mbeya (DC) Mbeya Jiji Mbozi Rungwe Jumla Idadi 426 1,149 2,845 1,600 2,124 2,723 2,880 3,165 3,054 19,966

- 45 -

Baadhi ya majengo ya Kisasa ya Ofisi na nyumba za Watumishi pia majengo ya Ofisi za Vijiji na wananchi wakipata huduma.

6.18.2

Mapambano Dhidi ya Rushwa

Katika mapambano dhidi ya Rushwa, mkoa ulijiwekea malengo mbalimbali katika kuhakikisha kwamba mapambano dhidi ya adui rushwa yanafanyika kikamilifu; malengo hao ni; i. Kuongeza uwajibikaji katika usimaimizi wa fedha za Umma na ugawaji wa rasilimali ii. iii. iv. v. katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri kwa kuimarisha vyombo mbalimbali vya udhibiti wa matumizi ya fedha za serikali; Kuongeza uwazi katika utendaji kazi kwa kupitia Kamati za Ushauri za Mkoa na Wilaya (RCC na DCC); Kuimarisha uhuru katika kutoa maoni kwa wananchi kupitia sanduku la maoni na dawati la malalamiko; Kutekeleza majukumu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa; Kuongeza ushiriki wa wananchi katika mapambano dhidi ya rushwa;

- 46 -

Mikakati na Shughuli Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa Katika kutekeleza majukumu yake ili kupunguza na kutokomeza tatizo la rushwa katika Mkoa, mikakati mbalimbali iliwekwa na shughuli mbalimbali zilitekelezwa. Mikakati na shughuli hizo za mapambano dhidi ya adui rushwa ni kama ifuatavyo; i. Mkoa umeimarisha Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu za Ndani katika Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za Mkoa kwa kuwapatia mafunzo wajumbe wake mwezi Septemba, 2008. Kamati hii ina majukumu ya kupitia taarifa za hesabu za ukaguzi kila robo mwaka na kutoa ushauri. Kitengo hiki kimepewa mamlaka ya kupitia matumizi na kutoa ushauri jinsi ya kudhibiti matumizi na kuongeza tija katika utoaji huduma. ii. Mkoa unahakikisha unafanya vikao vyote vya kisheria ili kupata maoni na ushauri muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake. Vikao hivi (hasa Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Wilaya) hupokea taarifa mbalimbali za maendeleo na kuzitolea maoni na ushauri ili kuboresha utekelezaji wake. Hii ni pamoja na kujadili thamani ya fedha (Value of Money) katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa mkoani. iii. Katika kuongeza uwazi wa kutekeleza majukumu yake kwa kumeanzisha dawati la malalamiko la wananchi na sanduku la maoni. Hii huwapatia fursa wananchi kutoa maoni na malalamiko yao katika madawati/masanduku haya yaliyopo katika kila ofisi ya Serikali katika Mkoa mzima. Maoni haya hushughulikiwa kikamilifu katika kuboresha utoaji wa huduma. iv. Mkoa umeimarisha Kitengo cha Manunuzi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na Halmashauri kwa kuongeza idadi ya Maafisa Ugavi, kusiamia miradi ya maendele na kuongeza uwazi katika kutangaza ajira na kuajiri. Mkoa unayo Kamati ya Manunuzi ambayo majukumu yake ni kuratibu, v. kusimamia, kupitia na kupendekeza manunuzi yote yanayofanyika. Mkoa umeongeza ushiriki wa wananchi katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kutoa elimu kwa wananchi ili watambue athari za kutoa au

- 47 -

kupokea rushwa na pia kuwahakikishia kuwa huduma zinazotolewa katika Ofisi za serikali ni bure na haki ya kila mwananchi. Mafanikio katika Mapambano Dhidi ya Rushwa. Katika kupambana na rushwa, mkoa umefanikiwa katika yafuatayo; i. Mkoa na Halmashauri zake katika miaka minne iliyopita (2005/06 ­ 2008/09) zimefanikiwa kufuzu vigezo vya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 5 Jedwali Na. 5: Hati za Ukaguzi wa Hesabu za Fedha kwa Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri; Jina Sekretarieti ya Mkoa Halmashauri Chunya Ileje Kyela Mbarali Mbeya (W) Mbozi Rungwe Mbeya Jiji 2005/06 Hati ya Mashaka Hati safi Hati ya Mashaka Hati safi Hati Chafu Hati ya Mashaka Hati ya Mashaka Hati safi Hati Chafu 2006/07 Hati safi 2007/08 Hati safi 2008/09 Hati safi

Hati ya Mashaka Hati ya Mashaka Hati ya Mashaka Hati Chafu Hati safi Hati safi Hati safi Hati safi

Hati safi Hati ya Mashaka Hati safi Hati ya Mashaka Hati safi Hati safi Hati ya Mashaka Hati safi

Hati safi Hati safi Hati safi Hati safi Hati safi Hati safi Hati ya Mashaka Hati ya Mashaka

ii.

Mkoa umefanikiwa kuanzisha Dawati la malalamiko, sanduku na maoni na pia Mkoa umefanikiwa kuzindua makala ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja (Client Service Charter) ambao umeweka misingi muhimu na uwazi katika kutoa huduma kwa wateja na wadau mbalimbali.

iii.

Sheria na utaratibu wa manunuzi hufuatwa kikamilifu

- 48 -

iv. v. vi.

Kusambaza taarifa zote muhimu za kiserikali kati mabango ya matangazo na vipeperushi; Kuwahusisha wananchi kikamilifu katika kupanga na kutekeleza shughuli mbalimbali za kiserikali ikiwa ni pamoja na miradi ya maendeleo Mkoa umefanikiwa kuboresha huduma zitolewazo katika Ofisi na Taasisi za umma kama vile Hospitali, Zaanati na Vituo vya Afya.

vii. Ugawaji wa viwanja vilivyopimwa unazingatia sheria na unafanyika kwa uwazi na usawa. viii. Hati miliki za Vijiji hutolewa kwa wakati; ix. x. xi. Mkoa umefanikiwa kuondoa tatizo la kuvuja kwa mitihani ya kitaifa; Mkoa umefanikiwa kusimamia kikamilifu ugawaji wa pembejeo za kilimo na madawa ya mifugo; Mkoa umefanikiwa kutoa elimu ya udhibiti wa mianya ya rushwa kwa watumishi wote ili kuto huduma nzuri kwa wananchi na kuzingatia uadilifu katika kutekeleza majukumu yao;

7.0

CHANGAMOTO utekelezaji wa majukumu ya Mkoa changamoto mbalimbali

Katika

zimejitokeza.

7.1; Utawala na Rasilimali Watu; Changamoto; i. ii. iii. Upungufu wa watumishi wenye ujuzi hasa katika Hospitali ya Mkoa na Wilaya. Kukosekana kwa mipango mizuri ya rasilimali watu. Upungufu wa vitendea kazi.

- 49 -

Mikakati; i. ii. Mkoa unaendelea kutenga fedha na kujaza nafasi za wataalam wa kada za afya kwa kadri watakavyopatikana katika soko. Mkoa unakamilisha umetayarishaji `Human Resources Development Plan HRDP' ambayo inaonesha idadi ya watumishi waliopo na kiwango cha elimu yao, idadi ya watumishi watakaostafu katika miaka mitatu ijayo, na idadi ya watumishi wanaohitajika. Mpango huu unatumiwa katika ajira na mafunzo. iii. Mkoa unaendelea kutenga fedha kila mwaka katika bajeti yake kwa ajili ya ununuzi wa vitendea kazi.

7.2; Kilimo; Changamoto; i. Dhana ya Kilimo Kwanza bado haijaeleweka na wadau wote katika Mkoa. ii. Mahitaji ya pembejeo ya ruzuku ni makubwa kuliko upatikanaji wake. iii. Bado kuna mahitaji makubwa ya maafisa ugani. iv. Upatikanaji wa fedha za kutosha katika miundombinu mikubwa ya kilimo. Mikakati; i. Kuhakikisha dhana ya Kilimo Kwanza inaeleweka na wadau wote na inatekelezwa ipasavyo katika Mkoa. Vikao mbalimbali vya kuelimisha wadau vilikwishaanza kufanyika ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari. ii. Mkoa utaendelea kuiomba Serikali kuongeza ruzuku ya pembejeo, kwani wakulima hawamudu kununua pembejeo zisizo za ruzuku kutokana na bei kubwa. iii. iv. Mkoa utaendelea kuiomba Serikali kujaza nafasi wazi za maafisa ugani. Mkoa kuiomba Serikali iendelee kuongeza fedha za kuimarisha miundombinu ya kilimo hasa umwagiliaji.

- 50 -

7.3; Mifugo; Changamoto; i. ii. Mwitiko mdogo wa wafugaji wa ngombe wa asili kuhusu uhamilishaji. Upungufu wa wataalamu wenye ujuzi wa uhamilishaji.

Mikakati; i. ii. Kuhamasisha wakulima ili kuongeza mwitiko wa wafugaji kutumia teknolojia ya uhamilishaji. Halmashauri zinasimamiwa ili ziwezeshe kupatikana watalaamu wenye ujuzi wa uhamilishaji. 7.4; Maliasili na Utalii; Changamoto; i. ii. iii. Uvunaji haramu wa mazao ya misitu ya asili hasa Chunya. Uelewa wa wananchi kuhusu vivutio vya Utalii vilivyopo Mkoani Mbeya. Idara ina upungufu wa wataalamu wa Maliasili na mazingira.

Mkakati; i. ii. iii. Kufanya doria za mara kwa mara kwenye maeneo ya misitu. Mkoa unaendelea kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo. Mkoa utaendelea kuiomba Serikali kujaza nafasi wazi za maafisa katika sekta ya maliasili na mazingira.

7.5; Viwanda; Changamoto; i. ii. Uhaba wa viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ya chakula. Viwanda vilivyo vingi kuzalisha chini ya malengo kutokana na · · Upatikanaji wa umeme usio wa uhakika; Gharama kubwa za nishati na mitambo (Viwanda vyote);

- 51 -

·

Miundo mbinu duni ya usafirishaji wa mizigo hivyo kuwepo kwa gharama kubwa ya kusafirisha malighafi na bidhaa zinazozalishwa na viwanda hivyo (Viwanda vyote);

· · ·

Kuwepo kwa bidhaa za nje zinazouzwa rahisi kuliko za ndani (Mbeya Cement); Uhaba wa mali ghafi (Mbozi coffee Curring na New Mbeya Textile); Mitaji midogo kutokana na kushindwa kumudu masharti ya mikopo (viwanda vidogo).

Mkakati; i. ii. Kuandaa Kongamano la Wawekezaji kuhusu fursa zilizopo katika sekta mbalimbali za Mkoa ikiwemo viwanda vya kusindika mazao ya kilimo. Kuwasilisha mahitaji ya viwanda vyetu katika taasisi husika ili kupatiwa ufumbuzi kama vile TANESCO, TANROADS, n.k.

7.6; Maendeleo ya Ushirika; Changamoto; i. Vyama vingi ni vidogo vidogo visivyo na mitaji ya kutosha. Aidha, vyama vya ushirika vya mazao ni dhaifu kutokana na ushindani katika soko. ii. iii. iv. Uhaba wa Maafisa Ushirika wa kusimamia ipasavyo vyama vya ushirika Wilayani. Uhaba wa mitaji ya ndani unaoleta utegemezi wa mitaji toka nje. Imani ndogo ya kuendelea kuwepo kwa vyama vya ushirika hasa vya mazao. Mikakati; i. Vyama vidogo vidogo vinashauriwa kuungana ili kuwa na vyama vichache vikubwa vyenye wanachama na hisa za kutosha.

- 52 -

ii.

Soko holela la mazao ya kahawa, kokoa, korosho kudhibitiwa ili kutoa fursa kwa vyama vya ushirika kushindana kwa manufaa ya wakulima. Vile vile, vyama vikuu vya KYECU, RUCU MBOCU, MICU na ISAYULA kuhamasishwa kuungana ili kuwa na Unions chache zenye nguvu.

iii.

Kuzishauri mahitaji.

Halmashauri

kuajiri

Maafisa

Ushirika

wa

kukidhi

7.7; Nishati; Changamoto; Uharibifu na hujuma ya miundombinu ya umeme hasa wizi wa mafuta ya transformer, nyaya za umeme, vyuma kwenye nguzo kubwa za umeme pamoja na vifaa vingine kama vile mita. Wizi huu unachochewa na biashara ya vyuma chakavu. Mikakati; Kuiomba Serikali kuongeza udhibiti wa biashara ya vyuma chakavu.

7.8; Elimu; Changamoto; i. ii. iii. Idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza Kidato cha nne na kufaulu. Uhaba wa walimu hasa wa masomo ya Sayansi. Tatizo la mimba mashuleni.

Mikakati; i. Mkoa unahamasisha ujenzi wa shule za kidato cha tano na sita lengo ni kuwa na angalau sekondari 2 za kidato cha Tano na sita katika kila Tarafa ifikapo mwaka 2015 lengo ni kuwa na Sekondari 50. ii. Kuiomba Serikali kuongeza idadi ya wanaojiunga na mafunzo ya ualimu hasa wa masomo ya sayansi.

- 53 -

iii.

Mkoa unahimiza ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi wa kike na kuhakikisha wanaosababisha mimba kwa wanafunzi wanachukuliwa hatua za kisheria.

7.9; Afya; Changamoto; i. ii. iii. Uhaba wa majengo ya kutolea huduma na eneo dogo lililoko ambalo ni ekari 14 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Mkoa. Uhaba wa watumishi wenye sifa katika vituo vya tiba. Baadhi ya zahanati na vituo vya afya vimejengwa kwa kutumia ramani za zamani baada ya ramani mpya kuchelewa. Mikakati; i. Mkoa utaendelea kuiomba Serikali kuongeza fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo na kufidia wananchi waliojenga karibu ili kupanua eneo la Hospitali ya Mkoa. Ujenzi wa majengo kwa mtindo wa ghorofa pia utazingatiwa ili kutumia kwa ukamilifu eneo la Hospitali. ii. iii. Mkoa utaendelea kuiomba Serikali kujaza nafasi wazi za maafisa katika sekta ya Afya. Halmashauri zinasisitizwa kutumia ramani mpya na kufanya ufuatiliaji wa karibú katika ujenzi wa vituo vya tiba vinavyojengwa kupitia MMAM na kushirikisha jamii katika ujenzi wa vituo vya tiba katika hatua za awali. 7.10; Sekta ya Maji; Changamoto; i. ii. iii. Ongezeko kubwa la watu na mahitaji makubwa ya maji katika jamii. Ugumu wa jamii wa kutambua na kuchangia ujenzi na ulipiaji huduma ya maji katika Kamati na Mamlaka za Maji. Kupungua kwa maji kutokana na athari za mazingira.

- 54 -

Mikakati; i. Kushirikisha na kuhamasisha jamii katika kubuni, kupanga, kujenga na kusimamia miradi na kuimarisha Mamlaka za uendeshaji wa miradi ya maji. ii. iii. Kuendelea na kuhamasisha jamii kulipia huduma ya maji na kuchangia ujenzi wa miradi ya maji. Kushirikisha jamii kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji kulingana na sheria na kanuni za utunzaji mazingira. 7.11; Maendeleo ya Jamii; Changamoto; i. ii. Kusuasua kwa uundwaji wa vikundi vya wanawake na vijana. Kusuasua kwa uanzishaji wa mifuko maalum ya kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika baadhi vijiji. Mikakati; i. ii. iii. iv. Kuhamasisha na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa uundwaji wa vikundi vya wanawake na vijana. Kuhamasisha uundaji wa mifuko maalum ya kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi. Kutoa elimu ya ujasiliamali katika jamii kupitia vikundi vya uzalishaji mali. Kuelimisha jamii juu ya sera ya watoto na jinsia kwa ujumla

7.12; Barabara; Changamoto; Kuchelewa kukamilika kwa miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara. Mikakati; Kuimarisha usimamizi wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara na kuiomba Serikali kutoa fedha zilizotengwa kwa kuzingatia msimu unayofaa kwa ujenzi na ukarabati wa barabara. - 55 -

7.13; Ardhi na Maendeleo ya Makazi; Changamoto; Eneo kubwa la miji kutopimwa na vijiji kukosa hati miliki. Mkakati; Kuihimiza Mkoa. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Halmashauri kutekeleza kazi ya Upimaji miji na vijiji katika

8. MATARAJIO YA MKOA WA MBEYA KATIKA MIAKA 50 IJAYO Mkoa unatarajia kuwa na mabadiliko makubwa katika Sekta za Elimu, Maji, Barabara, Afya, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda Biashara na Masoko, Ushirika, Miundombinu, Umeme, Ardhi, Maliasili na Mazingira. Matarajio haya yanategemea miongozo, mipango, sera, sheria, ilani za uchaguzi, hali ya ukuaji wa uchumi na idadi ya watu kama inavyoainishwa katika sekta mbalimbali; 8.1 Sekta ya Elimu;

Matarajio ya mkoa katika sekta ya elimu yataenda sambamba na mfumo wa elimu kwa nchi nzima kwa kuzingatia mabadiliko ya sayansi na teknolojia na mfumo wa elimu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Elimu ya Awali; Mkoa unatarajia kuwa baada ya miaka 50 ijayo utakuwa umepiga hatua kubwa katika elimu ya awali kwa kuhakikisha kuwa watoto wote waliofikia umri wa kuanza elimu ya awali wanapata nafasi ya kujiunga na shule, katika kutekeleza hili mkoa umepanga kuweka utaratibu wa kuongeza vyumba vya madarasa katika shule za msingi zilizopo kwa kila kijiji ilikuwapa nafasi wanafunzi wa elimu ya awali kupata nafasi ya kujifunza, pia mkoa unatarajia

- 56 -

kuboresha mfumo wa utoaji wa elimu ya awali kwa kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya awali. Elimu ya Msingi; Mkoa unatarajia kuwa baada ya miaka 50 ijayo utakuwa umepiga hatua kubwa katika elimu ya msingi kwa kutekeleza sera ya elimu ya taifa inayoelekeza kuwa kila mtoto aliefikia umri wa kwenda shule aweze kupata nafasi kwa kuwa na vyumba ya madarasa vya kutosha,katika kutekeleza hili mkoa uanatarajia kuongeza shule z msingi kwa kila kijiji kuwa na angalau shule mbili ili kuwawezesha watoto wote kupata elimu, vilevile mkoa unatarajia kuboresha upatikanaji wa elimu ya shule ya msingi kwa miaka 50 ijayo kwa kuweka miundombinu stahiki kama umeme, maji, kompyuta, mtandao wa mawasiliano wa kielekroniki, ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu inayoendana na mahitaji ya jamii na kuwapa nafasi ya kuweza kujitegemea baada ya masomo. Mkoa unatarajia kuwa wanafunzi wote wanaomaliza elimu ya msingi wanapata nafasi za kuendelea na masomo ya elimu ya sekondari kwa asilimia moja.Ili kutekeleza malengo hayo mkoa umepanga kuongeza idadi ya ujenzi wa sekondari katika ngazi ya kata kwa kuwa na shule mbili kwa kila kata na pia kuendelea kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya elimu mkoa wa Mbeya kwa kujenga shule nyingi kadiri itavyowezekana ili kukidhi ongezeko la wanafunzi. Elimu ya Sekondari; Mkoa wa Mbeya unatarajia kuwa baada ya miaka 50 ijayo wanafunzi wote wanaohitimu elimu ya msingi wanajiunga na sekondari kwa asilimia mia moja,pia wanafunzi wote wanaojiunga na elimu wa sekondari wanapata nafasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita.ili kuweza kutekeleza mpango huu mkoa umepanga kuboresha miundombinu ya elimu kwa kuweka mazingira mazuri yanayokidhi matakwa ya walimu na wanafunziikiwa ni

- 57 -

pamoja na kujenga maabara,maktaba,nyumba za walimu na madarasa ya kutosha kwa kila shule Upande wa elimu ya kidato cha tano na sita mkoa unatarajia kuwa ili kukabiliana na ongezeko la idadi ya wanafunzi mkoa umepanga kuongeza idadi ya shule za sekondari kwa kujenga shule za kidato cha tano na sita kwa kila kata baada ya miaka 50 ijayo. Elimu ya Juu; Mkoa unatarajia kuwa baada ya miaka miaka 50 asilimia 70 ya wanafunzi wote wanaomaliza kidato cha sita wanapata nafasi ya kuendelea na elimu ya juu,ili kutekeleza mipango hii mkoa umeendelea kuhamasisha wadau mbalimbali kuwekeza katika sekta ya elimu ya juu ili kuongeza idadi ya vyuo vya elimu ya juu ili angalau kuwa na chuo kikuu kimoja kwa kila wilaya. 8.2 Afya;

Mkoa wa Mbeya unatarajia kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na vituo vya kutolea huduma kwa miaka 50 ijayo kwa kuongeza ubora wa huduma na vifaa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa urahisi zaidi katika maeneo yao. 8.3 Hali ya Ulinzi na Usalama;

Katika miaka 50 ijayo, mkoa umejipanga kuhakikisha kwamba hali ya ulinzi na usalama kwa wananchi wake kupitia dhana ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi itakuwa imeimarika na kuwawezesha wananchi kutekeleza shughuli zao za maendeleo kwa amani na utulivu. 8.4 Ushirika;

Mkoa umejipanga kuhakikisha kuwa unakuwa na vyama vya ushirika vya akiba na mikopo vilivyo imara na vyenye nguvu, katika maeneo ya kata ili kuwawezesha kupata mitaji kwa urahisi kwa njia ya mikopo yenye riba nafuu. Hii ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kuunda Benki za wananchi (Community

- 58 -

Bank) katika ngazi za Wilaya. Hii inafanyika kwa kuendelea kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuunda vyama vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) na vyama vya ushirika. Aidha sekta ya ushirika itaendelea kuimarisha vyama vya ushirika wa mazao katika mkoa ili kuwawezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao ikiwamo kuimarisha mfumo wa stakabadhi ghalani kwa lengo la kuongeza thamani ya mazao. 8.5 Biashara na Viwanda;

Mkoa utaendelea kutangaza vitu mbambali vinavyopatika ili kuwavutia wawekezaji mbalimbali waweze kuwekeza na kuanzisha viwanda mbalimbali, ambavyo vitasaidia kukuza wananchi. 8.6 Barabara; hali ya uchumi wa mkoa na kuwapatia ajira

Mkoa utaendelea kuhakikisha unajenga miundombinu ya barabara inayopitika katika kipindi chote cha mwaka. Hii ni pamoja na kuandaa na kusimamia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 2,261.50 katika mkoa. 8.7 Maji;

Mkoa utaendelea kuboresha miiundo mbinu ya maji ili kuhakikisha asilimia 85 ya wakazi wa mkoa wa Mbeya wanapata maji safi na salama, hii ikiwa ni pamoja kusambaza maji katika miji na vijiji/mitaa kutoka vyanzo vikubwa vya maji, sambamba na kutoa elimu juu ya matumizi bora ya maji na Aidha, mkoa umejipanga utunzaji wa mazingira katika vyanzo vya maji.

kuhakikisha kwamba unakuwa na visima vifupi na virefu kwa kila kijiji ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama vijijini. 8.8 Maliasili na Utalii;

Mkoa utaendelea kuelimisha na kuhamasisha wanachi kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira, ikiwa ni pamoja na kusimamia sheria na sera ya - 59 -

mazingira, hii ikiwa ni sambamba na kuandaa vitalu vya miti katika wilaya zote 7 yenye miche isiyopungua 10,000 kwa kila kitalu kwa mwaka na kusambaza katika kila Wilaya husika. Aidha, mkoa utaendelea kuweka mkazo katika uhifadhi wa vyanzo vya maji, hii ikiwa ni sambamba na kuongeza hifadhi ndogo ndogo za vijiji chini ya program ya usimamizi shirikishi wa misitu (Perticipartory Forest Management PFM). Hii ni pamoja na uboreshaji wa matumizi ya mizinga ya kisasa. 8.9 Umeme;

Mkoa unatarajia kuongeza miundombinu ya umeme kwa asilimia 75 vijijini, hii ikiwa ni pamoja na kuelimisha na kuwahamasisha wananchi kujenga nyumba bora vijijini na matumizi bora ya nishati mpango huu utaenda sambamba na mipango ya serikali katika kuboresha sekta ya umeme kupitia mpango wa umeme vijijini chini ya usimamizi wa wakala wa umeme vijijini (REA)

Kauli Mbiu ya Miaka 50 ya Uhuru ni; "Tumethubutu, Tumeweza, Tunazidi Kusonga Mbele"

- 60 -

Information

Microsoft Word - K-HISTORIA YA MKOA WA MBEYA - MIAKA 50 YA UHURU_FINAL DRAFT

63 pages

Find more like this

Report File (DMCA)

Our content is added by our users. We aim to remove reported files within 1 working day. Please use this link to notify us:

Report this file as copyright or inappropriate

798162


You might also be interested in

BETA
Microsoft Word - K-HISTORIA YA MKOA WA MBEYA - MIAKA 50 YA UHURU_FINAL DRAFT
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
23juni03.doc