Read Microsoft Word - Taarifa ya Miaka 50 ya Uhuru _Afrika Mashariki_ text version

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI (50) YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

S.L.P 9280 DAR ES SALAAM MEI 2011

Miaka 50 ya uhuru.indd 1 7/23/11 10:02 PM

Page 2

Miaka 50 ya uhuru.indd 2 7/23/11 10:02 PM

Page 3

DIBAJI KUTOKA KWA WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI 6 MANENO YA UTANGULIZI KUTOKA KWA KATIBU MKUU 7 1.0 UTANGULIZI 7 1.1 Historia Fupi ya Ushirikiano katika Afrika Mashariki 8 1.2 Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwanzo 1967 8 1.3 Madhumuni ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 1967 8 1.4 Mafanikio Katika Ushirikiano wa Mwanzo Katika Afrika Mashariki 8 1.4.1 Shirika la Reli 8 1.4.2 Shirika la Posta 8 1.4.3 Shirika la Bandari 8 1.4.4 Shirika la Ndege 9 1.4.5 Benki ya Maendeleo 9 1.5 Kuvunjika kwa Jumuiya ya Mwanzo ya Afrika Mashariki 1977 9

1.6 Athari za Kuvunjika kwa Iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki 9 2.0 JUMUIYA MPYA YA AFRIKA MASHARIKI 10 2.1 Hatua Zilizochukuliwa Baada ya Kuvunjika kwa Jumuiya ya Mwanzo 10 2.2 Kuundwa Upya kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, 1999 10 2.3 Hatua Zilizochukuliwa Kuepuka Kuvunjika Tena kwa Jumuiya 10 2.4 Malengo ya Jumuiya mpya 10 2.5 Maeneo ya Ushirikiano 10 2.6 Faida za kuanzishwa kwa Jumuiya 11 2.6.1 Faida za Kiuchumi 11 2.6.2 Faida za Kijamii 11 3.0 KUANZISHWA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI 12 3.1 Miundo ya Wizara na Jumuiya na Jinsi Ilivyobadilika 12 3.1.1 Muundo wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki 12 3.1.2 Muundo Uliopitishwa na Rais Tarehe18 Aprili, 2006 13 3.1.3 Muundo ulivyorekebishwa tarehe 26 Januari, 2009 13 3.1.4 Muundo Ulivyorekebishwa Tarehe 26 Februari, 2010 13 3.2 Muundo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 15 3.2.1 Mkutano wa Kilele (Summit) 15 3.2.2 Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki 15 3.2.3 Kamati ya Makatibu Wakuu 15 3.2.4 Kamati za Kisekta 15 3.2.5 Mahakama ya Jumuiya 15 3.2.6 Bunge la Afrika Mashariki 16 3.2.7 Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 16 3.3 Taratibu za Utendaji na Maamuzi 18 3.3.1 Utaratibu wa Utendaji

18 3.3.2 Taratibu za Maamuzi 18 3.3.3 Taratibu za Uenyekiti katika Jumuiya 18 4.0 MAJUKUMU NA MALENGO YA WIZARA NA JUMUIYA 18 4.1 Majukumu na Malengo ya Wizara 18 4.2 Madhumuni ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 18 5.0 HALI YA UTAWALA NA UONGOZI 19 5.1 Hali ya Utawala na Uongozi katika Wizara 19 5.1.1 Mawaziri 19 5.1.2 Manaibu Mawaziri 19 5.1.3 Makatibu Wakuu 19 5.1.4 Naibu Katibu Mkuu 20 5.1.5 Wakurugenzi 20 5.1.6 Wakurugenzi Wasaidizi 21 5.1.7 Wakuu wa Vitengo 22 5.1.8 Mgawanyo wa Jinsia Katika Ngazi za Uongozi 2010/11 23 5.1.9 Idadi ya Watumishi 23 5.2 Hali ya Utawala na Uongozi Katika Jumuiya 24

YALIYOMO

Miaka 50 ya uhuru.indd 3 7/23/11 10:02 PM

Page 4

6.0 SERA, MIKAKATI NA SHERIA 26 6.1 Sera, Mikakati na Sheria Katika Wizara 26 6.2 Sera na Sheria 26 6.3 Sera, Mikakati, Sheria na Itifaki Katika Jumuiya 26

6.3.1 Sera na Mikakati Katika Jumuiya 26 6.3.2 Sheria na Itifaki Katika Jumuiya 26 7.0 MABADILIKO NA MATUKIO MAKUU 27 7.1 Matukio Makuu katika Jumuiya 27 8.0 MAFANIKIO KATIKA MTANGAMANO WA AFRIKA MASHARIKI 31 8.1 Kuanzisha Taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki 31 8.1.1 Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC) 31 8.1.2 Oganaizesheni ya Uvuvi Katika Ziwa29 Victoria (LVFO) 32 8.1.3 Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) 32 8.1.4 Wakala wa Usalama wa Anga Afrika Mashariki (CASSOA) 32 8.1.5 Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) 32 8.2 Mafanikio Katika Utekelezaji wa Hatua za Mtangamano 32 8.2.1 Umoja wa Forodha 32 8.2.1.1 Utekelezaji wa Vipengele Muhimu vya Umoja wa Forodha 32 8.2.1.2 Mafanikio ya Utekelezaji wa Umoja wa Forodha 34 8.2.2 Utekelezaji wa Soko la Pamoja 35 8.2.2.1 Maeneo ya msingi katika Soko la Pamoja 35 8.2.3 Umoja wa Fedha 36 8.2.4 Shirikisho la Kisiasa 36 8.2.5 Uimarishaji wa Sekta Binafsi 36 8.2.6 Ushirikiano baina ya Jumuiya (EAC) na Kanda Nyingine 37 8.2.6.1 Utatu wa EAC-COMESA-SADC (EAC-COMESA-SADC Tripate Arrangement) 37 8.3 Mafanikio Katika Utekelezaji wa Miradi na Programu za Kikanda 38 8.3.1 Uendelezaji wa Miundombinu 38 8.3.2 Uendelezaji wa Barabara 38 8.3.3 Uendelezaji wa Sekta ya Reli

38 8.3.4 Uendelezaji wa Sekta ya Nishati 39 8.3.4 Sekta ya Usafiri wa Anga 39 8.3.5 Sekta ya Usafiri wa Majini 39 8.3.6 Kuanzisha Vituo vya Pamoja vya Utoaji Huduma Mipakani 40 8.3.7 Miradi ya Zanzibar 40 8.3.8 Uendelezaji wa Sekta ya Kilimo 40 8.3.9 Uendelezaji wa Miradi na Programu za Huduma za Jamii 40 8.3.10 Mafanikio Katika Sekta ya Siasa, Ulinzi na Usalama 41 8.3.11 Utekelezaji wa Mradi wa Utunzaji Mazingira ya Ziwa Victoria 41 8.3.12 Ujenzi wa Makao Makuu ya Jumuiya 42 8.3.14 Upanuzi wa Jumuiya 43 9.0 CHANGAMOTO 43 9.1 Changamoto Katika Ngazi ya Jumuiya 43 9.1.1 Uhaba wa Raslimali Fedha 43 9.1.2 Kuendelea Kuwepo kwa Vikwazo Visivyo vya Kiforodha 43 9.2 Changamoto za Kiundeshaji Katika Ngazi ya Wizara 43 9.2.1 Kuhuishwa kwa Masuala ya Mtangamano 43 9.2.2 Mwamko na Uelewa Mdogo Juu ya Masuala ya Mtangamano 43 9.2.3 Majukumu Kutoendana na Raslimali 43 10.0 MATARAJIO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 50 IJAYO 43

Miaka 50 ya uhuru.indd 4 7/23/11 10:02 PM

Page 5

TAARIFA MUHIMU KUHUSU JUMUIYA

Jumuiya:

· Inajumuisha nchi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri za Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda. · Ina jumla ya eneo la kilomita za mraba milioni 1.82; · Ina idadi ya watu wanaokadiriwa kuwa milioni 133.5 (hadi Juni, 2010)

· Ina pato la ndani la Dola za Kimarekani bilioni 74.5 (hadi Mei, 2010) · Ina wastani wa pato la taifa kwa kila mtu la Dola za Kimarekani 558 (Hadi Mei, 2010)

Dira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki:

· Kuwa na Jumuiya iliyositawi na kuimarika kiushindani, kiusalama, na iliyoungana kisiasa.

Dhima ya Jumuiya:

· Kupanua na kuimarisha ushirikiano kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni ili kuboresha maisha ya watu wa Afrika ya Mashariki kwa kuongeza ushindani, thamani katika uzalishaji, biashara na uwekezaji.

ALAMA ZA UTAMBULISHO ZA JUMUIYA ZINAJUMUISHA: Bendera Nembo Maana ya Rangi za Bendera:

Bluu ikimaanisha Ziwa Viktoria ambayo ni alama ya umoja wa Nchi Wanachama; Nyeupe, Nyeusi, Kijani, Manjano na Nyekundu zinawakilisha rangi mbalimbali za bendera za Nchi Wanachama.Mikono iliyoshikana ikimaanisha Umoja wa Jumuiya na alama ya katikati ni Nembo ya Jumuiya.

Kauli mbiu ya Jumuiya:

Watu wamoja lengo moja. Huu ni wito wa umoja na ukumbusho wa dira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Lugha ya Jumuiya:

Lugha rasmi ya Jumuiya ni Kiingereza, na Kiswahili ni lugha ya mawasiliano.

Vigezo vya kujiunga Nchi: Muombaji anatakiwa:· Kuikubali Jumuiya kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya · Kuzingatia misingi ya utawala bora, demokrasia, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na haki za kiraia · Kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mtangamano ndani ya eneo la Afrika Mashariki · Nchi iwe na nafasi kijiografia kupakana na nchi mojawapo mwanachama · Nchi iwe yenye kujenga na kuendeleza uchumi wa soko; na · Nchi iwe yenye sera za kiuchumi na kijamii zinazowiana na zile za Jumuiya · Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama ndiyo wenye maamuzi ya kuiruhusu nchi kujiunga na Jumuiya.

WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Jumuiya Yetu sote tuilinde; Tuwajibike tuimarike; Umoja wetu ni nguzo yetu; Idumu Jumuiya yetu. 1. Ee Mungu twakuomba uilinde Jumuiya Afrika Mashariki Tuwezeshe kuishi kwa amani Tutimize na malengo yetu. 2. Uzalendo pia mshikamano Viwe msingi wa Umoja wetu Natulinde Uhuru na Amani Mila zetu na desturi zetu. 3. Viwandani na hata mashambani Tufanye kazi sote kwa makini Tujitoe kwa hali na mali Tuijenge Jumuiya bora.

Miaka 50 ya uhuru.indd 5 7/23/11 10:02 PM

Page 6

Ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki; Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, katika kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, imeonelea hakuna budi jamii ya kitanzania ikafahamishwa kuhusu mafanikio na hatua mbalimbali ambazo Jumuiya ya Afrika Mashariki imefikia tangu kuvunjika kwa Jumuiya ya awali mwaka 1977, na kuanzishwa kwa Jumuiya mpya hapo mwaka 1999. Maadhimisho ya Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara yameikuta Nchi

yetu katika uchumi wa sasa unao lazimisha ushindani katika mfumo wa utandawazi ulioshamiri na wenye changamoto nyingi. Mtangamano wa kikanda ni hatua muhimu sana kuelekea katika mtangamano wa kiuchumi wa dunia/kimataifa. Kwa kipindi cha miongo miwili mpaka miaka ya 2000, Uchumi wa nchi za Afrika ulikuwa ni wa kusuasua sana kutokana na changamoto nyingi za kisera, usimamizi, na kubwa zaidi ikiwa ni uwezo wa bidhaa za nchi hizi zinazoendelea kupenya katika soko la dunia. Katika hali hii, pamoja na jitihada mahsusi zilizochukuliwa za kurekebisha sera za kiuchumi, Nchi hizi ziliona bado kuna umuhimu wa kuungana kikanda ili kujipa sauti ya pamoja katika kupambana na changamoto za uchumi wa dunia/kimataifa (global economic integration) na hatimaye kunufaika na fursa zinazotokana na mfumo mzima wa utandawazi. Nchi za Afrika Mashariki zilikwisha litambua hili tangu miaka ya 1960 pale wakuu wa Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania walipoamua kuunda Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pamoja na changamoto zilizopelekea Jumuiya ya awali kuvunjika, bado miaka ishirini baadaye viongozi wetu waliona umuhimu wa kuunganisha tena nguvu zao kwa manufaa ya watu wao. Lengo kuu likiwa ni kuanzisha ushirikano wa kikanda utakaoziunganisha Sekta za Umma na Sekta Binafsi, ili kuwawezesha Wanaafrika Mashariki kupanua fursa za kiuchumi na kijamii na kuwaletea wananchi wao maendeleo. Hivyo, kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulilenga kupanua na kuimarisha ushirikiano wa watu wa Afrika mashariki ambao umedumu kwa muda mrefu tangu hata kabla nchi hizi hazijapata uhuru. Ushirikiano huu umekusudia kuharakisha ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi wake kiuchumi, kisiasa na kijamii. Jumuiya ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa Jumuiya chache za kikanda katika dunia zinazokua na kuimarika kwa kasi na hata kuweza kurekodi mafanikio makubwa sana kwa kipindi cha miaka kumi tu tangu kuanzishwa kwake upya. Chapisho hili limeandaliwa mahsusi, kwa ajili ya kuelezea mafanikio yaliyofikiwa tangu Jumuiya ya awali mpaka sasa. Chapisho hili linatoa fursa ya kuelewa nafasi na malengo ya Tanzania kama mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, pia nafasi na umuhimu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kuhakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo na ushirikiano huu ikiongozwa na dira na dhamira ya taifa ya Tanzania, ya kuiwezesha Tanzania kuwa Taifa la Uchumi wa kati unaongozwa na ongezeko la mauzo nje (kikanda na kimataifa) kama ajenda yake namba moja. Afrika Mashariki tumethubutu, tumeweza, tunazidi kusonga mbele, kila mmoja atimize wajibu wake inawezekana! _____________________ Samuel J. Sitta (Mb), WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI JUNI, 2011

DIBAJI

kutoka kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Miaka 50 ya uhuru.indd 6 7/23/11 10:02 PM

Page 7

MANENO YA UTANGULIZI

kutoka kwa Katibu Mkuu, EAMC

Serikali ya Tanzania inasherehekea miaka 50 ya Uhuru wake huku ikishuhudia mafanikio ya kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Maendeleo hayo yanatokana na sera na mikakati mbalimbali ikiwemo matumizi ya ushirikiano wa kikanda kama majowapo ya nyenzo za kukuza uchumi na kujiletea maendeleo. Ushirikiano za Afrika Mashariki una historia ndefu tangu kabla ya Uhuru. Mwaka 1905 Uganda na Kenya zilianzisha Bodi ya Sarafu Moja ya Afrika Mashariki mwaka 1905, na iliyokuwa Tanganyika ilijiunga na Bodi hiyo mwaka 1922. Mwaka, 1917 Kenya na Uganda zilianzisha Umoja wa Forodha, na Tanganyika ilijiunga mwaka 1922. Aidha, mwaka 1948 Kamisheni ya Ushirikiano ilianzishwa. Mwaka 1961 Mashirika ya Pamoja ya Huduma (Common Services Oraganizations) yalianzishwa ikiwa ni pamoja na Shirika la Posta na Mawasiliano (Post and Telecommunication); Shirika la Reli na Bandari (East African Railways and Harbours); Shirika la Ndege la Afrika Mashariki (East African Airways); Taasisi ya Usafiri wa Anga (East African Aviation Services); Taasisi ya Uchunguzi ya ugonjwa wa malale; na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East African Development Bank). Hatua zilizoonyeshwa hapo juu zilifuatiwa na kuimarikai zaidi kwa mtangamano wa nchi hizi tatu baada ya Tanzania kupata uhuru wake, ambapo Jumuiya ya Afrika Mashariki iliundwa mwaka 1967. Shabaha ya Jumuiya ilikuwa kuimarisha na kuongeza uhusiano uliopo baina ya Nchi Wanachama katika masuala ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na shughuli nyingine ili kuleta maendeleo ya haraka ambayo matunda yake yaligawanywa kwa usawa baina ya Nchi Wanachama. Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya, Nchi Wanachama zilitiliana saini Makubaliano ya Kugawana Mali na Madeni (Mediation Agreement for the Division of Assets and Liabilities) hapo mwaka 1984. Katika makubaliano hayo, kulikuwa na kipengele kilichotoa fursa kwa nchi hizi kutafuta maeneo ya ushirikiano na kuandaa mpango thabiti wa jinsi ya kushirikiana. Kipengele hiki kiliwawezesha Wakuu wa Nchi mnamo mwaka 1993 kusaini makubaliano ya kuanzisha Kamisheni ya Kudumu ya Utatu (The Permanent Tripartite Commission). Kufuatia makubaliano haya, Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulianza tena rasmi mwaka 1996 kwa kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Kudumu ya Utatu wa Afrika Mashariki (The East African Community Secretariat of the Permanent Tripartite Commission), iliyozinduliwa rasmi tarehe 14 Machi, 1996 katika Makao Makuu ya Jumuiya Mjini Arusha, Tanzania. Baada ya hapo majadiliano ya kuianzisha upya Jumuiya ya Afrika Mashariki yalianza na kuwezesha kuundwa upya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Jumuiya hii ilianzishwa mwaka 1999 kwa Wakuu wa Nchi kusaini Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 30 Novemba 1999, ambao ulianza kutumika rasmi tarehe 7 Julai, 2000. Kulingana na makubaliano hayo, Jumuiya ya Afrika Mashariki ni Taasisi ya Kiserikali (inter-Governmental Organization), iliyoanzishwa na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Nchi za Rwanda na Burundi zilijiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2007.

Tangu kufufuliwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Nchi Wanachama zimeendelea na utekelezaji wa hatua za mtangamano na miradi na programu/miradi ya pamoja ikiwa ni pamoja na kuanzisha mipango kabambe mbalimbali katika sekta mbalimbali zinazolenga kukuza uchumi wa nchi za Afrika Mashariki. Kitabu hiki kimelenga kutoa taarifa kuhusu Ushirikiano katika kanda ya Afrika Mashariki hususan, mafanikio yaliyopatikana katika Jumuiya ya Afrika Mashariki toka Tanzania ipate uhuru hapo tarehe 9 Desemba, 1961 hadi sasa, na matarajio ya Wizara katika kipindi cha miaka 50 ijayo. TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE _________________________ Dkt. Stergomena L. Tax KATIBU MKUU WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

Miaka 50 ya uhuru.indd 7 7/23/11 10:02 PM

Page 8

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

8

1.0 UTANGULIZI 1.1 Historia Fupi ya Ushirikiano katika Afrika Mashariki

Ushirikiano wa Nchi za Afrika Mashariki una historia ndefu tangu kabla ya Uhuru. Mwanzoni mwa Karne ya 19 ilijengwa reli kati ya nchi za Kenya na Uganda. Aidha, ili kujenga ushirikiano wa kina na mpana Uganda na Kenya zilianzisha Bodi ya Sarafu Moja ya Afrika Mashariki mwaka 1905, na iliyokuwa Tanganyika, ilijiunga na Bodi hiyo mwaka 1922. Mwaka, 1917 Kenya na Uganda zilianzisha Umoja wa Forodha, na Tanganyika ilijiunga mwaka 1922. Mwaka 1948 Kamisheni ya ushirikiano ilianzishwa.Mwaka 1961 Mashirika ya Pamoja (Common Services Organizations) yalianzishwa ikiwa ni pamoja na: a.) Shirika la Posta na Mawasiliano (Post and Telecommunication); b.) Shirika la Reli na Bandari (East African Railways and Harbours); c.) Shirika la Ndege la Afrika Mashariki (East African Airways); d.) Taasisi ya Usafiri wa Anga (East African Aviation Services); e.) Taasisi ya Uchunguzi ya Ugonjwa wa Malale; na f.) Benki ya Maendeleo ya Jumuiya (East African Development Bank).

1.2 Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwanzo 1967

Hatua zilizoonyeshwa hapo juu zilifikiwa na uimarishaji zaidi wa mtangamano wa nchi hizi tatu baada ya Tanzania kupata uhuru mwaka 1961, ambapo Jumuiya ya Afrika Mashariki iliundwa mwaka 1967.

1.3 Madhumuni ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 1967

Shabaha ya Jumuiya ilikuwa kuimarisha na kuongeza uhusiano uliopo kati ya Nchi Wanachama katika masuala ya Biashara, Uchumi na shughuli nyingine ili kuleta maendeleo ya haraka ambayo matunda yake yatagawanywa kwa usawa kati ya Nchi Wanachama. Mpango huu wa Ushirikiano wa Nchi hizi tatu uligawanyika katika sehemu mbili kama ifuatavyo: a.) Sehemu ya Kwanza ikiwa ni Soko la Pamoja, lililolenga kuhakikisha kwamba hakutakuwa na kizuizi chochote katika

biashara baina ya Nchi Wanachama. b.) Sehemu ya pili ilikuwa uendeshaji wa huduma mbalimbali ambazo usimamizi wake ilikuwa na mamlaka kutoka katika Nchi Wanachama. Misingi kadhaa ilikubalika ili kuhakikisha biashara zinaendelezwa na maendeleo ya Nchi Wanachama yanapatikana. Baadhi ya mambo yaliyokubalika ni pamoja na: a.) Kuwa na sheria ya namna moja inayoongoza bidhaa zote zinazoingia au zinazotengenezwa na Nchi Wanachama. b.) Kuondoa vikwazo vyote vya biashara baina Nchi Wanachama. c.) Kurahisisha malipo ya bidhaa baina ya Nchi Wanachama. na d.) Kurahisisha malipo ya bidhaa zinazouzwa na nchi moja kwenda nchi nyingine. Nchi Wanachama zilikubaliana pia kuwa na sheria maalum za kusimamia uendeshaji wa biashara zote ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Sheria hizo zilianisha kuwa: a.) Hakuna Nchi inayoruhusiwa kujadiliana na nchi yoyote ya nje kwa madhumuni ya kupata fursa za kibiashara bila ya kuhakikisha kuwa fursa hizo zitawanufaisha wanachama wote wa Jumuiya. b.) Bidhaa za nje zinapoingia bandari yoyote ya Afrika Mashariki hutozwa ushuru mmoja, na ushuru huo utalipwa kwenye hazina ya nchi iliyoagiza vifaa hivyo hata kama nchi hiyo haina bandari.

1.4 Mafanikio Katika Ushirikiano wa Mwanzo Katika Afrika Mashariki

Jumuiya ya Afrika Mashariki ya wakati huo iliunda mashirika ya pamoja. Lengo la mashirika haya ilikuwa ni kutoa huduma mbalimbali ndani ya Jumuiya. Huduma hizo ziligawanywa katika makundi mawili: a.) Kundi la kwanza liliwakilisha huduma ambazo uendeshaji wake uligharamiwa kutokana na hazina ya Jumuiya, b.) Kundi la pili ni huduma ambazo zinajilipia zenyewe kutokana na kazi zake za kibiashara. Huduma hizi zilitolewa na Mashirika ya Jumuiya yaliyoainishwa hapo chini:

1.4.1 Shirika la Reli

Shirika hili lilitokana na kuunganishwa kwa Reli na Bandari za Tanganyika, Uganda na Kenya na kuunda Shirika la Reli la Afrika Mashariki mwaka 1948. Mwaka 1956 ujenzi wa Reli mpya yenye Kilomita 330 magharibi toka Kampala hadi Kasese uliwezesha uchimbaji wa shaba huko Kilembe. Mwaka 1960 bandari mpya ilifunguliwa Mwanza, na Mwaka 1961 Reli mpya ilijengwa kutoka Jinja hadi Kampala na Meli mpya ilianzisha safari za kasi ndani ya Ziwa Victoria. Mwaka 1963 Reli kuu ya Tanganyika iliunganishwa na Reli ya Tanga kati ya Ruvu na Mnyusi. Mwaka 1964 Reli ya Pakwach ilikamilika na mwaka 1966, Kisumu na Mwanza ziliunganishwa na Meli za Mabogi ambazo zilikuwa kubwa kuliko zote zilizokuwa zikitumika Afrika. Mwaka 1965 reli ya kilombero ilikamilika na vilindi vipya vikajengwa Mombasa na Dar es Salaam.

1.4.2 Shirika la Posta

Shughuli za Posta katika Afrika Mashariki zilianza mwaka 1878, shughuli hizi za posta na simu ziliunganishwa mwaka 1933. Mnano mwaka 1951 Idara ya posta na simu ya nchi tatu iliunganishwa na kuwa Shilika la Posta na simu la Afrika Mashariki. Ulipofika mwaka 1969 Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki lilikuwa likiendesha Posta 970 na Vituo vya Simu 350 kote Afrika Mashariki.

1.4.3 Shirika la Bandari

Shirika la Bandari lilihusika na uangalizi pamoja na uendeshaji wa

bandari zote zilizo pwani ya Afrika Mashariki.

Miaka 50 ya uhuru.indd 8 7/23/11 10:02 PM

Page 9

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

9

1.4.4 Shirika la Ndege

Shirika la Ndege la Afrika Mashariki liliundwa mwaka 1946 likiwa ni shirika kati ya Nchi za Kenya, Uganda na Tanganyika. Mpaka kufikia mwaka 1970 shirika lilikuwa na ndege zilizokuwa zikifanya safari hadi uingereza Pakistan, India, Aden na Rhodesia.

1.4.5 Benki ya Maendeleo

Jumuiya ilianzisha Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki mwaka 1967, katika Mkataba wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilibuniwa njia kadhaa ambazo zingetumiwa kuleta maendeleo katika ujengaji wa viwanda. Njia mojawapo ilikuwa ni kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Afrika Maashariki Makao Makuu ya benki hiyo yalikuwa Kampala,Uganda. Benki hii ilipata mafanikio kadhaa ikiwa ni pamoja na: a.) iliweza kutoa misaada ya kifedha na kiufundi ili kuwezesha maendeleo ya viwanda na kuendesha kazi ambazo matokeo yake ni kuleta ushirikiano baina ya nchi tatu za Afrika Mashariki. b.) Ilisaidia nchi zile ambazo maendeleo yake ya viwanda yalikuwa nyuma kwa kuzipa misaaada zaidi ya fedha na kushirikiana na mashirika na makampuni ya maendeleo katika nchi zote tatu ili kutimiza malengo ambayo mashirika hayo hayakufanikisha bila msaada wa kifedha. c.) Benki hiyo iliweza kuongeza ajira kwa wannchi wa Afrika Mashariki kwa kuajiri wafanyakazi katika nyanja mabalimbali. Menejimenti ya mashirika haya ilikuwa chini ya Bodi za Wakurugenzi ambazo ziliteuliwa na wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki. Shughuli za Mashirika yote ziliendeshwa kwa misingi ya kibiashara ili kuhakikisha kwamba gharama zote za uendeshaji zinatokana na faida inayopatikana katika uendeshaji. Kila mwaka mashirika haya yalitakiwa kutoa taarifa ya kazi zake mbele ya Baraza la Kutunga Sheria la Afrika Mashariki.

1.5 Kuvunjika kwa Jumuiya ya Mwanzo ya Afrika Mashariki 1977

Kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwanzo hapo mwaka 1977 kulitokana na sababu za kisiasa, kijamii na kimaslahi. Sababu hizo ni pamoja na: a.) Itikadi tofauti za kisiasa zilizokuwa zikifuatwa na Nchi Wanachama; b.) Kutoelewana katika mgao wa mapato kutoka katika mashirika ya huduma za pamoja na kutokuwepo kwa Sera ya kushughulikia tatizo hilo; c.) Athari za vita baridi baina ya Amerika na Urusi kwa wakati huo; d.) Ushiriki mdogo wa sekta binafsi na vyama vya kiraia katika uendeshaji wa Jumuiya; e.) Mtizamo finyu kuhusu mtangamano kwa baadhi ya viongozi na watendaji; na f.) Msukumo toka nje ya Jumuiya.

1.6 Athari za Kuvunjika kwa Iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki hapo mwaka 1977

kulipelekea athari kubwa ikiwa ni pamoja na kurudi nyuma maendeleo na mafanikio yaliyotokana na Mashirika ya iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyoanishwa hapo juu. Athari hizo zilikuwa ni pamoja na: a.) Kukosekana kwa ajira. b.) Kupotea na kukosekana kwa huduma za pamoja. c.) Kusitishwa kwa uhuru wa watu wa Afrika Mashariki kutembea ndani ya Jumuiya, soko huru la bidhaa na huduma ndani ya Jumuiya. d.) Kuibuka kwa mtazamo hasi wa utaifa. e.) Kuibuka kwa ushindani usio na tija. f.) Kuibuka kwa hujuma za kisiasa baina ya Nchi Wanachama kulikosababisha kuondoa utulivu wa kisiasa. g.) Kutokuaminiana baina ya Nchi Wanachama.

Miaka 50 ya uhuru.indd 9 7/23/11 10:02 PM

Page 10

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

10

2.0 JUMUIYA MPYA YA AFRIKA MASHARIKI 2.1 Hatua Zilizochukuliwa Baada ya Kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya, Nchi Wanachama zilitiliana saini makubaliano ya kugawana mali na madeni (mediation agreement for the division of assets and liabilities) hapo mwaka 1984. Katika makubaliano hayo, kulikuwa na kipengele kilichotoa nafasi ya nchi hizi kutafuta maeneo ya ushirikiano na kuandaa mpango thabiti wa jinsi ya kushirikiana. Kipengele hiki kilitoa fursa kwa Wakuu wa Nchi kusaini makubaliano ya kuanzishwa kwa Kamisheni ya Kudumu ya Utatu (The Permanent Tripartite Commission) iliyoanzishwa mwaka 1993. Kufuatia makubaliano haya, ushirikiano wa Afrika Mashariki ulianza tena rasmi mwaka 1996 wakati ambapo Sekretarieti ya Kudumu ya Utatu (The East African Community Secretariat of the Permanent Tripartite Commission).Sekretarieti ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilizinduliwa rasmi tarehe 14 Machi, 1996 katika Makao Makuu ya Jumuiya Mjini Arusha, Tanzania. Baada ya hapo Majadiliano ya kuianzisha upya Jumuiya ya Afrika Mashariki yalianza mwaka 1999 na kuwezesha kuundwa upya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

2.2 Kuundwa Upya kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, 1999

Jumuiya mpya ya Afrika Mashariki ilianzishwa rasmi mwaka 1999 kwa Wakuu wa Nchi kusaini Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 30 Novemba, 1999. Tarehe 7 Julai, 2000 Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianza na ilizinduliwa rasmi na Wakuu wa Nchi (tarehe 15 Januari, 2001). Jumuiya ya Afrika Mashariki ni Taasisi ya Kiserikali (inter-Governmental Organization), iliyoanzishwa na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Nchi za Rwanda na Burundi zilijiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2007.

2.3 Hatua Zilizochukuliwa Kuepuka Kuvunjika Tena kwa Jumuiya

Kutokana na uzoefu uliopatikana kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mkataba wa Kuanzisha upya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliandaliwa kwa kujifunza kutokana na sababu

zilizopelekea Jumuiya ya awali kuvunjika. Kama njia za kuwezesha Jumuiya ya sasa isivunjike tena, Mkataba umezingatia masuala yafuatayo: a.) Uendelezaji wa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hatua kwa hatua. Hatua ya Kwanza ikiwa ni Umoja wa Forodha, ikifuatiwa na Soko la Pamoja, kisha Umoja wa Fedha na hatimaye Shirikisho la Kisiasa. b.) Kupunguza madaraka ya kimaamuzi. c.) Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuongozwa na Wananchi wa Afrika Mashariki, na kuchochewa na Sekta binafsi ndani ya Jumuiya. d.) Ushirikishwaji wa Asasi za Kiraia kwenye mtangamano. e.) Kuainishwa kwa ufasaha taratibu za kujiondoa uanachama. f.) Mtangamano imara utatokana na uchumi imara na endelevu

2.4 Malengo ya Jumuiya mpya

Lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuendeleza ujirani mwema, kupanua na kuimarisha ushirikiano wa watu wa Afrika Mashariki ili kuharakisha ukuaji wa kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki kiuchumi, kisiasa, na kijamii. Ili kufikia malengo haya, Nchi Wanachama hukubaliana kukusanya nguvu kwa pamoja kutekeleza Miradi na Programu mbalimbali za kikanda ili kufikia malengo mahususi yafuatayo: a.) Kuhakikisha kunakuwa na ukuaji na maendeleo endelevu kutokana na uendelezaji na uwiniashaji sawia wa maendeleo baina ya Nchi Wanachama. b.) Kuhakikisha kunakuwa na uwiano sawa wa maendeleo ya kiuchumi unaoweza kuinua hali ya maisha ya jamii. c.) Kuimarisha matumizi endelevu ya maliasili na utunzaji wa mazingira.

Wakuu wa Nchi Wakisaini Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, 30 Novemba, 1999

Miaka 50 ya uhuru.indd 10 7/23/11 10:02 PM

Page 11

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

11

d.) Kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kijamii na kisiasa uliojengeka kwa muda mrefu ili kujenga Jumuiya ya watu. e.) Kuhuisha masuala ya jinsia katika mipango na program za Jumuiya ili kuendeleza ushiriki wa wanawake katika masuala ya kiutamaduni, kijamii, kisiasa, kiuchumi na maendeleo ya kiteknolojia. f.) Kuendeleza amani, usalama na ujirani mwema. g.) Kuendeleza na kuimarisha ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. h.) Kuendeleza shughuli nyingine kwa lengo la kuendeleza Jumuiya.

2.5 Maeneo ya Ushirikiano

Kulingana na mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, maeneo ya Ushirikiano miongoni mwa Nchi Wanachama ni pamoja na: a.) Ufunguaji wa Biashara na Maendeleo. b.) Umoja wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. c.) Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda. d.) Kuendeleza Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda. e.) Kuendeleza Uhusiano wa Kiuzalishaji Baina ya Viwanda.

f.) Uwianishaji wa Viwango, Ubora, na Vipimo. g.) Masuala ya Fedha na Kodi. h.) Uwianishaji wa Sera. i.) Maendeleo ya Soko la Mitaji na Huduma za Benki. j.) Uwekaji wa Mazingira Mazuri ya Maendeleo. k.) Masuala ya Siasa. l.) Ulinzi, Amani na Usalama. m.) Masuala ya Sheria na Mahakama. n.) Ushirikiano wa Kikanda, Mashirika ya Kimataifa na Washirika wa Maendeleo. o.) Maendeleo ya Rasilimali Watu. p.) Ushirikiano Katika Elimu na Mafunzo. q.) Maendeleo ya Sayansi na Teknologia. r.) Ushiriki wa Wanawake Katika Masuala ya Maendeleo, Kijamii na Kiuchumi. s.) Uhuru wa Watu Kutembea, Soko la Ajira, Soko la Huduma, Haki ya Kuanzisha Shughuli za Kiuchumi, na Uhuru wa Makazi. t.) Ushirikiano katika masuala ya afya, utamaduni, michezo, na ustawi wa jamii. u.) Maendeleo ya Vyombo vya Habari na Programu za Uhamasishaji. v.) Maendeleo ya Kilimo na Uendelezaji na Matumizi endelevu ya Maliasili w.) Miundombinu na Huduma. x.) Usalama wa Anga na Usafiri wa Anga. y.) Usafiri wa Majini na Bandari; Usafiri Katika Maziwa na Mito; na Usafiri Mchanganyiko z.) Huduma za Posta na simu aa.) Huduma za Hali ya Hewa na Nishati Ushirikiano katika maeneo haya huendelezwa hatua kwa hatua kulingana na hatua za mtangamano zilizofikiwa na utayari wa Nchi Wanachama.

2.6 Faida za kuanzishwa kwa Jumuiya 2.6.1 Faida za Kiuchumi

a.) Uwezo mkubwa wa matumizi ya fursa za maendeleo. b.) Kuwa na soko kubwa. c.) Uhuru wa watu kutembea, soko huru la bidhaa na soko huru la ajira vitakavyochochea kukua kwa uchumi na ustawi wa wananchi wa Afrika Mashariki. d.) Kuwa na miradi ya miundombinu yenye faida na gharama nafuu kama vile Mpango Kabambe wa Nishati wa Afrika Mashariki, Mtandao wa Barabara wa Afrika Mashariki na Mtandao wa Reli wa Afrika Mashariki. e.) Matumizi bora ya maliasili za pamoja. f.) kutumia raslimali kwa pamoja kunaleta manufaa ya kuzalisha kulingana na uwezo na urahisi kwa kila nchi, kuwa na uwezo mkubwa wa uzalishaji na matumizi bora ya raslimali za umma. g.) Kuepusha gharama zisizokuwa za lazima zinazosababishwa na nchi moja moja kutoa huduma zinazofanana. h.) Kuwa na uwezo wa kiushindani katika biashara kimataifa. i.) Wawekezaji wa ndani na wa kimataifa watavutiwa kuwekeza katika eneo lenye idadi kubwa ya watu na wingi wa raslimali. j.) Wigo wa pamoja wa mapato wa nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utatumika vizuri na kwa ufanisi mkubwa. k.) Matumizi ya sarafu moja yatawanufaisha wananchi wa Afrika

Mashariki kwa kuepuka hasara wanazozipata sasa kutokana na kulazimika kubadilisha fedha wanaposafiri kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine. l.) Usimamizi bora wa rasilimali za pamoja kuitangaza Jumuiya ya Afrika Mashariki kama eneo moja la utalii.

2.6.2 Faida za Kijamii

a.) Ufanisi katka kuendesha masuala ya kisiasa. b.) Utawala bora, demokrasia na utulivu wa kisiasa. c.) Kukuza wigo wa demokrasia, kuepusha upendeleo wa kindugu, kikanda na ukabila. d.) Uhifadhi wa urithi wa asili na utamaduni. e.) Matumizi ya lugha moja ya (Kiswahili). f.) Kuaminiana na utashi wa kisiasa. g.) Kuishi kwa amani na ujirani mwema. h.) Utatuzi wa migogoro kwa njia za amani. i.) Ugawanaji uliosawa wa faida za mtangamano. j.) Ushirikiano kwa faida ya wote.

Miaka 50 ya uhuru.indd 11 7/23/11 10:02 PM

Page 12

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

12

3.0 KUANZISHWA KWA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilianzishwa kwa Tamko la Rais la tarehe 4 Januari, 2006, ikiwa ni azma ya Serikali kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mheshimiwa Andrew Chenge (Mb.) aliteuliwa kuwa Waziri wa Kwanza wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Aidha, ndugu, Omar M.S. Bendera aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Chimbuko la kuanzisha Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo Ibara ya 8(3) inatamka kuwa Nchi Wanachama zitaunda/zitateua Wizara zitakazoratibu masuala ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Itifaki zake. Wizara hizo ndizo kiungo baina ya Nchi Wanachama na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hivyo, mawasiliano yote kati ya Nchi Wanachama na Sekretarieti hutakiwa kufanyika kupitia Wizara hizi. Wizara mahususi zinazoshughulikia mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeundwa katika nchi zote, yaani Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Kama ilivyoelezwa hapo juu ushirikiano wa Afrika Mashariki umekuwepo hata kabla Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, haijaundwa. Kabla ya kuundwa kwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, masuala ya ushirikiano wa Afrika Mashariki yalikuwa chini ya Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Madhumuni ya kuanzishwa kwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni kuwa na chombo kinachosimamia na kuratibu utekelezaji wa Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki, na hivyo chombo kinachoziunganisha sekta za umma na sekta binafsi na kuhakikisha, kuwa Nchi Wanachama, ikiwa ni pamoja na Tanzania zinanufaika kutokana na ushirikiano wa kikanda katika mtangamano wa

Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika kutekeleza dhumuni hili, Wizara inaratibu maeneo ya ushirikiano kwa kuwashirikisha wadau toka sekta za umma na binafsi ili kuiwezesha Tanzania kushiriki kikamilifu na kunufaika na fursa zitokanazo na mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika kufikia lengo hili, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inaongozwa na Dira na kuzingatia Dhima ifuatayo:

Dira ya Wizara

Kuwa na Jumuiya iliyoshamiri na inayoiwezesha Tanzania kunufaika kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Dhima ya Wizara

Kuhakikisha ushiriki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kujenga Jumuiya iliyoshamiri ni wenye tija na unaolinda maslahi ya Taifa.

3.1 Miundo ya Wizara na Jumuiya na Jinsi Ilivyobadilika Katika Nyakati Tofauti 3.1.1 Muundo wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyoanzishwa mwaka 2006, Muundo wake ulipitishwa na Rais tarehe 18 April, 2006 ikiwa na Idara nne (4) na vitengo saba (7) kama inavyoonekana hapa chini: a.) Idara ya Utawala na Utumishi; b.) Idara ya Sera na Mipango; c.) Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji; d.) Kitengo cha Miundombimu ya Kiuchumi na Kijamii; e.) Kitengo cha Siasa, Ulinzi na Usalama; f.) Kitengo cha Fedha na Uhasibu; g.) Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu wa Ndani; h.) Kitengo cha Sheria; na i.) Kitengo cha Manunuzi na Ugavi. Kutokana na kuongezeka kwa majukumu ya Wizara na kupanuka kwa shughuli katika uendelelezaji wa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Muundo wa Wizara ulirekebishwa na kuhusishwa ili kuiwezesha Wizara kutekeleza majukumu yake kikamilifu. Tarehe 26 Januari, 2009 muundo ulirekebishwa kwa kuunda Idara za Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii; na Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama; kila Idara ikiwa na Mkurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wawili. Aidha, Idara ya Uwekezaji, Biashara, na Sekta za Uzalishaji iliimarishwa kwa kuongezewa nafasi za Wakurugenzi Wasaidizi wawili. Kutokana na mabadiliko hayo, Muundo mpya wa Wizara ukawa na Idara tano (5) ambazo ni: a) Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji; b) Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii; c) Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama; d) Idara ya Sera na Mipango na e) Idara ya Utawala na Rasilimali Watu. Aidha, muundo wa Wizara ulijumuisha Vitengo sita ambavyo ni: a.) Kitengo cha Sheria; b.) Kitengo cha Uhasibu na Fedha; c.) Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani; d.) Kitengo cha Ununuzi; e.) Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano; na f.) Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Kompyuta Tarehe 26 Februari, 2010 Muundo ulirekebishwa na kupandisha

hadhi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu kwa kuongezewa nafasi za Wakurugenzi Wasaidizi mbili, katika sehemu ya Utawala na sehemu ya Rasilimali watu. Aidha, Idara ya Sera na Mipango iliongezewa nafasi tatu za Wakurugenzi Wasaidizi katika sehemu ya Sera na Mipango, Bajeti na sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini. Aidha Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Kompyuta kilibadilishwa jina kuwa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Mheshimiwa Andrew Chenge (Mb.) , Waziri wa Kwanza wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashsriki. Bw. Omar S.M Bendera, Katibu Mkuu wa Kwanza wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashsriki.

Miaka 50 ya uhuru.indd 12 7/23/11 10:02 PM

Page 13

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

13

3.1.2 Muundo Uliopitishwa Na Rais Tarehe 18 Aprili, 2006 Wakati Wizara Ikianzishwa ­ Idara Nne (4) Na Vitengo Saba (7) 3.1.3 Muundo ulivyorekebishwa 26 Januari, 2009 - Idara tano (5) na Vitengo sita (6) 3.1.4 Muundo ulivyorekebishwa 26 Februari 2010 -Idara tano (5) na Vitengo sita (6)

IDARA Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Utawala na Rasilimali watu Sera na Mipango KITENGO Siasa, Ulinzi na Usalama Uhasibu na Fedha Ukaguzi Hesabu za Ndani Sheria Habari, Elimu na Mawasiliano Manunuzi na Ugavi Usimamizi wa Mifumo ya Kompyuta S/N 1 2 3 4 S/N 1 2 3 4

5 6 7 IDARA Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Siasa, Ulinzi na Usalama Utawala na Rasilimali Watu Sera na Mipango KITENGO Uhasibu na Fedha Habari, Elimu na Mawasliano Ukaguzi Hesabu wa Ndani Ununuzi na Ugavi Usimamizi wa Mifumo ya Kompyuta Sheria S/N 1 2 3 4 5 S/N 1 2 3 4 5 6 IDARA Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Biashara, uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Siasa, Ulinzi na Usalama Utawala na Rasilimali Watu Sera na Mipango KITENGO Uhasibu na Fedha Habari, Elimu na Mawasliano Ukaguzi Hesabu wa Ndani Ununuzi na Ugavi Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Sheria

S/N 1 2 3 4 5 S/N 1 2 3 4 5 6

Jedwali hapo chini linaonyesha mabaliko ya Muundo katika vipindi mbalimbali:

Miaka 50 ya uhuru.indd 13 7/23/11 10:02 PM

Page 14

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

14

THE APPROVED ORGANISATION STRUCTURE OF THE MINISTRY OF EAST AFRICAN CO-OPERATION (Approved by the President on 26th February, 2010)

MINISTER PERMANENT SECRETARY

FINANCE AND ACCOUNTS UNIT CHIEF ACCOUNTANT INTERNAL AUDIT UNIT CHIEF INTERNAL AUDITOR INFORMATION AND COMMUNICATION TECHNOLOGY UNIT PRINCIPAL COMPUTER SYSTEMS ANALYST LEGAL SERVICES UNIT PRINCIPAL LEGAL OFFICER ECONOMIC INFRASTRUCTURE AND SOCIAL SUPPORT SERVICES DIVISION DIRECTOR ECONOMIC INFRASTRUCTURE SECTION SOCIAL AND SUPPORTIVE SERVICES SECTION POLITICAL, DEFENCE AND SECURITY AFFAIRS DIVISION DIRECTOR POLITICAL AFFAIRS SECTION DEFENCE AND SECURITY AFFAIRS SECTION TRADE, INVESTMENT AND PRODUCTIVE SECTORS DIVISION DIRECTOR TRADE, FINANCE AND INVESTMENT SECTION PRODUCTIVE SECTORS SECTION ADMINISTRATION AND HUMAN RESOURCES MANAGEMENT DIVISION DIRECTOR POLICY AND PLANNING DIVISION DIRECTOR PROCUREMENT MANAGEMENT UNIT PRINCIPAL SUPPLIES OFFICER

INFORMATION, EDUCATION AND COMMUNICATION UNIT PRINCIPAL INFORMATION OFFICER

Miaka 50 ya uhuru.indd 14 7/23/11 10:02 PM

Page 15

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

15

3.2 Muundo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Ibara ya 9 ya Mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki imeainisha Vyombo (Organs) na Taasisi zinazounda Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Vyombo (Organs) na Taasisi za Jumuiya ni kama ifuatavyo: a.) Mkutano wa Kilele (Summit); b.) Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki; c.) Kamati ya Makatibu Wakuu; d.) Kamati za Kisekta; e.) Mahakama ya Jumuiya; f.) Bunge la Afrika Mashariki; na g.) Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

3.2.1 Mkutano wa Kilele (Summit)

Ibara ya 12 ya Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki imeainisha kuwa Mkutano wa Kilele (Summit) utaundwa na Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkutano huu unaongozwa na Mwenyekiti ambaye huchaguliwa miongoni mwa Wakuu wa Nchi kwa utaratibu wa mzunguko kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja. Mkutano wa Kilele hufanyika angalau mara moja kwa mwaka. Maamuzi ya Mkutano wa Kilele hufanyika kwa utaratibu wa maridhiano (consensus). Mkutano wa Kilele ndio chombo kikuu cha maamuzi kinachotoa dira na mwelekeo wa jumla katika kutekeleza na kufikia malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

3.2.2 Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kulingana na Ibara ya 13 ya Mkataba, Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki linaundwa na Mawaziri wenye dhamana na masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Nchi Wanachama na Mawaziri wengine kutoka sekta mbalimbali kama Nchi Mwanachama itakavyoona inafaa. Ibara ya 14 ya Mkataba imeainisha majukumu ya Baraza la Mawaziri. Pamoja na mambo mengine, Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki lina jukumu la kufanya maamuzi ya kisera, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Miradi na Programu za Jumuiya kulingana na Mkataba unaounda Jumuiya ya Afrika Mashariki. Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ni chombo kikuu cha kuwashauri Wakuu wa Nchi. Aidha, Baraza hili pia ni chombo kikuu cha kusimamia uendelezaji wa Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa Kilele. Baraza la Mawaziri hukutana angalau mara mbili kwa mwaka. Baraza la Mawaziri limepewa uwezo wa kuunda Mabaraza ya Mawaziri wa Kisekta kushughulikia masuala yanayojitokeza katika kutekeleza Mkataba wa Kuanzishwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hivyo, Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki hukasimu madaraka yake kwa Mabaraza ya Kisekta na hivyo Maamuzi ya Mabaraza hayo ni sawa na maamuzi ya Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki, isipokuwa kwa masuala ya kisera na yanayohitaji rasilimali.

3.2.3 Kamati ya Makatibu Wakuu

Ibara ya 17 ya Mkataba inaainisha kuwepo kwa Kamati ya Makatibu

Wakuu kama washauri wa Baraza la Mawaziri. Kamati ya Makatibu Wakuu huundwa na Makatibu Wakuu kutoka Wizara zinazoshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Makatibu Wakuu wengine kama itakavyoamuliwa na Nchi Mwanachama. Kamati hii hukutana angalau mara mbili kwa mwaka kabla ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri. Aidha, Makatibu Wakuu wanaweza kukutana kadri itakavyohitajika kulingana na taratibu watakazojiwekea kujadili masuala ya uendelezaji wa mtangamano, au kushughulikia masuala ya dharura kwa ombi la Mwenyekiti wa Makatibu Wakuu. Ibara ya 18 ya Mkataba imeainisha majukumu ya Kamati ya Makatibu Wakuu ambayo ni pamoja na kutekeleza na kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri, na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji, na kutoa mapendekezo kwa Baraza la Mawaziri kuhusu uendelezaji wa Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

3.2.4 Kamati za Kisekta

Kamati za Kisekta zinaundwa na Baraza la Mawaziri kutokana na maombi yaliyowasilishwa na Kamati ya Makatibu Wakuu kama watakavyoona inafaa katika kutekeleza Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kamati hizi zinatambulika katika muundo wa Jumuiya kama ilivyoonyeshwa katika Ibara ya 20 ya Mkataba. Kamati za Kisekta zina jukumu la kuandaa mipango endelevu na kuainisha vipaumbele vya utekelezaji katika Sekta husika. Aidha, ni jukumu la Kamati za Kisekta kuhakikisha kwamba zinatoa taarifa za utekelezaji wa mipango yote na kuishauri Kamati ya Makatibu Wakuu njia bora za kutekeleza mipango hiyo.

3.2.5 Mahakama ya Jumuiya

Kulingana na Ibara ya 23 ya Mkataba, jukumu kuu la Mahakama ya Afrika Mashariki ni kuhakikisha kuwa Mkataba wa Jumuiya unazingatiwa na kutoa tafsiri sahihi ya Mkataba pale inapohitajika. Mahakama hii imegawanyika katika vitengo viwili; Kitengo cha Awali (Court of First Instance) na Kitengo cha Rufaa (Appellate Court). Mahakama hii kwa sasa inaundwa na majaji kumi. Majaji watano wapo katika Kitengo cha Awali na watano wengine wapo katika Kitengo cha Rufaa cha Mahakama hiyo. Majaji wa Mahakama hii hupendekezwa kutoka Nchi Wanachama na kuteuliwa na Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 24 ya Mkataba. Majaji walioteuliwa hutumikia nafasi zao kwa kipindi kisichozidi miaka saba (7). Majaji wa Mahakama ya Afrika Mashsriki wakiwa katika moja ya majukumu yao ya kusikiliza kesi mbalimbali. Kutoka kushoto ni Waheshimiwa Majaji Kassanga Mulwa, Joseph Mulenga, Moijo ole Keiwua, na Augustino Ramadhan. Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja siku ya uzinduzi wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 30 Novemba, 2001 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Mjini Arusha. Kutoka kushoto waliokaa katikati ni Waheshimiwa Marais, Benjamin William Mkapa wa Tanzania, Daniel Arap Moi wa Kenya na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda.

Miaka 50 ya uhuru.indd 15 7/23/11 10:02 PM

Page 16

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

16

3.2.6 Bunge la Afrika Mashariki

Kwa mujibu wa Ibara ya 49 ya Mkataba wa Uanzishaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bunge la Afrika Mashariki ni chombo cha Jumuiya ambacho majukumu yake makuu ni pamoja na; kutunga sheria za

Jumuiya; na kujadili na kupitisha Bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki huchaguliwa na Mabunge ya Nchi Wanachama. Kila Bunge la Nchi Mwanachama huteua Wabunge tisa (9) wanaowakilisha Vyama vya Siasa vyenye uwakilishi ndani ya Bunge kwa kuzingatia jinsia na makundi mengine maalum kwa utaratibu utakaoamuliwa na Bunge la Nchi Mwanachama. Wabunge waliochaguliwa hutumikia Bunge kwa kipindi cha miaka mitano (5) na wanaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Spika wa Bunge hili huchaguliwa kutoka miongoni mwa Wabunge wa Afrika Mashariki kwa utaratibu wa mzunguko na hutumikia kipindi cha miaka mitano.

3.2.7 Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ndio chombo cha utendaji wa shughuli za kila siku za Jumuiya na kinaongozwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya. Kazi kubwa ya Sekretarieti ni kutekeleza maamuzi ya Mkutano wa Kilele, Baraza la Mawaziri, Mkutano wa Makatibu Wakuu na Kamati za Kisekta kwa kushirikiana na Nchi Wanachama na Wadau wengine. Majukumu ya Sekretarieti yameainishwa kwa kina katika Ibara ya 71 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Majukumu haya ni kama ni kama ifuatavyo: a.) Kuanzisha, kupokea na kuwasilisha mapendekezo katika Baraza la Mawaziri, na kuwasilisha Miswada katika Bunge la Afrika Mashariki kupitia Kamati ya Makatibu Wakuu (Coordination Committee); b.) Kuanzisha chambuzi na tafiti zinazohusiana na utekelezaji wa programu kwa muda muafaka na kwa umakini ili kuhakikisha malengo ya Jumuiya yanatimia; c.) Kupanga mikakati na kufuatilia utekelezaji wa programu kwa maendeleo ya Jumuiya; d.) Kufanya uchunguzi na kukusanya taarifa, au kuhakiki masuala yanayoweza kuiathiri Jumuiya; e.) Kuratibu na kuhuisha Sera na Mikakati inayohusu Jumuiya kupitia Kamati ya Makatibu Wakuu; f.) Kuhamasisha na kutoa taarifa za Jumuiya kwa Wadau mbalimbali, Umma, na Jumuiya ya Kimataifa; g.) Kuwasilisha ripoti za shughuli mbalimbali za Jumuiya kwa Baraza la Mawaziri kupitia Kamati ya Makatibu Wakuu; h.) Kushughulikia shughuli za kiutawala na Menejimenti ya fedha za Jumuiya; i.) Kutafuta fedha kutoka kwa Wahisani wa Maendeleo na vyanzo vingine kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya Jumuiya; j.) Kuwasilisha Bajeti ya Jumuiya kwa Baraza la Mawaziri kama inavyoelekezwa katika Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya (Treaty); k.) Kutoa mapendekezo ya ajenda za mikutano ya Vyombo vya Jumuiya isipokuwa za Mahakama na Bunge; l.) Kutekeleza Maamuzi ya Wakuu wa Nchi (Summit) na ya Baraza la Mawaziri; m.) Kupangilia na kutunza kumbukumbu za mikutano

ya Vyombo na Taasisi za Jumuiya isipokuwa za Mahakama na Bunge; n.) Kutunza ipasavyo mali za Jumuiya; o.) Kutengeneza mazingira na mahusiano mazuri ya utendaji kazi na Mahakama na Bunge; na p.) Kutekeleza masuala mengine ambayo yamebainishwa katika Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya.

Mheshimiwa Abdulrahman Kinana, Spika wa Kwanza wa Bunge la Afirka Mashariki Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja siku ya uzinduzi wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 30 Novemba, 2001 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Mjini Arusha, Tanzania. Kutoka kulia waliokaa ni Waheshimiwa Maraisi Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Daniel Arap Moi wa Kenya, Benjamini William Mkapa wa Tanzania, na Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki Mheshimiwa Ablahaman Kinana

Miaka 50 ya uhuru.indd 16 7/23/11 10:02 PM

Page 17

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

17

Muundo wa Secretariet ya Jumuiya kwa kutumia mchoro ni kama inavyoonyeshwa hapa chini:

SUMMIT

COUNCIL

C-ORDINATION COMMITEE SECRETARY GENERAL SECTORAL COMMITEES DSG Finance & Administration DG Customs & Trade DSG Productive & Social Sectors DSG Planning & Infrastructure DSG Political Federation

EA DEVELOPMENT BANK

Chef de Cabinet Internal Audit Corporate Communication and Public Affairs Resource Mobilization Coordinator Director of Planning and Investment Director of Productive Sectors Director of Social Sectors Education, Culture & Sports, Science & Technology Department Agriculture, Food Security and Rural Development Department

Transport and Works Department Meteorology Department Civil Aviation and Airports Department Communications Department Investment & Private Sector Promotion Department Planning, Research, Monitoring and Evaluation Department Political Affairs Department International Relations Department Peace and Security Department Fiscal and Monetary Affairs Department Statistics Department

Gender, Community Development and Civil Society Department Energy, Environment and Natural Resources Department Tourism and Wildlife Development Department Health Department

Labour and Immigration Department Industrial Development Department Director of Finance Director of Human Resources and Administration Director of Customs Director of Trade Internal Trade Department International Trade Department Procedures Department Prevention and Enforcement Department SQMT Department Tariff and Valuation Department Information Technology

Department Management Information Division Library and Documentation Division Information and Communications Division Administration Department Human Resources Management Department Budget Department Finance Department Funding Division Expenditure Division Accounts Division Payroll Division Training Division Human Resources Management Division Protocol Division Procurement Division Conferences Division Stores Management Division Security Division Estates Management Division Director of Infrastructure Counsel to the Community Defense Liaison EAC LEGISLATIVE ASSEMBLY EAC COURT OF JUSTICE

LAKE VICTORIA FISHERIES ORGANISATION INTER-UNIVERSITY COUNCIL OF EAST AFRICA LAKE VICTORIA BASIN COMMISSION CIVIL AVIATIO SAFETY & SECURITY OVERSIGHT AGENCY

Miaka 50 ya uhuru.indd 17 7/23/11 10:02 PM

Page 18

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

18

3. 3 Taratibu za Utendaji na Maamuzi 3.3.1 Utaratibu wa Utendaji

Ibara ya 6 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki imeainisha Kanuni za Msingi zitakazoongoza utendaji na maamuzi ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwa Jumuiya. Kanuni hizo ni kama zifuatazo:

a.) Kuaminiana, utashi wa kisiasa na usawa wa utaifa; b.) Amani na ujirani mwema; c.) Kutatua migogoro kwa njia za amani; d.) Utawala bora na kufuata misingi ya demokrasia, utawala wa sheria, uwajibikaji, uwazi, kuheshimu haki za kijamii, fursa sawa, usawa wa jinsia na kutambua, kuendeleza na kulinda haki za binadamu; e.) Mgawanyo sawa wa faida zitokanazo na Jumuiya; na f.) Ushirikiano kwa manufaa ya wote.

3.3.2 Taratibu za Maamuzi

Ibara ya 12(3) na Ibara ya 15(4) ya Mkataba, zinaelekeza kuwa maamuzi ya Mikutano ya Jumuiya katika ngazi zote yatafanywa kwa njia ya maridhiano (consensus). Aidha, katika Mikutano hiyo idadi ya Wajumbe wanaohitajika katika Mkutano hutimia endapo Nchi zote Wanachama zitakuwa zimewakilishwa katika ngazi husika. Maamuzi yanayofanywa katika Mkutano bila ya kuwa na uwakilishi wa Nchi zote Wanachama huchukuliwa kuwa ni Mkutano wa Mashauriano (Consultative Meeting). Maamuzi ya Mkutano huo huwa ni maamuzi ya Jumuiya pale Nchi Mwanachama asiyehudhuria atakaporidhia na kuweka saini taarifa ya Mkutano husika. Utaratibu huu hutoa fursa kwa Nchi Wanachama kuendeleza mtangamano, bila kuathiri maslahi ya kitaifa. Aidha hutoa mwanya wa kushauriana hadi kuweza kupata uelewa na uamuzi wa pamoja, hivyo kujenga Mtangamano endelevu.

3.3.3 Taratibu za Uenyekiti katika Jumuiya

Ibara ya 12(2) imeainisha kuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Jumuiya atachaguliwa miongoni mwao kwa utaratibu wa mzunguko kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja. Nchi X inapochukua nafasi ya uenyekiti katika ngazi ya Marais (Mkutano wa Kilele ­ Summit) basi huwa mwenyekiti katika ngazi zingine zote ikiwemo Baraza la Mawaziri, Kamati ya Makatibu Wakuu, Kamati za Kisekta, Vikosi Kazi na Watalaamu.

4.0 Majukumu Na Malengo Ya Wizara Na Jumuiya 4.1 Majukumu na Malengo ya Wizara

Ili kuiwezesha Tanzania kunufaika kikamilifu katika mtangamano wa Afrika Mashariki, Wizara ina dhamana ifuatayo: a.) Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Itifaki zake; b.) Kuratibu, kushiriki na kusimamia majadiliano na utekelezaji wa hatua za mtangamano wa ushirikiano wa Afrika Mashariki hususan, Umoja wa Forodha, Soko la Pamoja, Umoja wa Fedha na Shirikisho la Kisiasa; c.) Kusimamia na kuratibu shughuli za Idara zinazojitegemea na miradi itakayokuwa chini ya Wizara; d.) Kusimamia na kuratibu shughuli za Wakala za serikali zitakazokuwa chini ya Wizara; na e.) Kuimarisha utendaji na kujenga uwezo wa wafanyakazi wa Wizara. Katika kutekeleza dhamana hii, Wizara inayo majukumu makuu yafuatayo: a.) Kufanya tafiti na tathmini mbalimbali ili kujipanga vema katika majadiliano katika Jumuiya na kuiwezesha nchi kunufaika na ushiriki wake katika Jumuiya; b.) Kushiriki, kusimamia, na kuratibu ushirki wa Tanzania katika majadiliano mbalimbali, na shughuli mbalimbali za uendelezaji wa

mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki; c.) Kufuatilia utekelezaji wa mradi ya kikanda na shughuli za uendelezaji wa mtangamano wa Jumuiya; na d.) Kutoa elimu kwa umma ili kuwawezesha Watanzania kuzifahamu na kuzitumia ipasavyo fursa zitokanazo na mtangamano wa Afrika Mashariki. Hivyo, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatarajiwa kuwa chachu na kitovu cha fikra (Think Tank) za kuendeleza mtangamano wa Afrika Mashariki kwa manufaa ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

4.2. Madhumuni ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Ibara ya 5(1) ya Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki imeainisha madhumuni ya kuanzisha Jumuiya kuwa ni kupanua na kuimarisha ushirikiano baina ya Nchi Wanachama katika nyanja za kisiasa; kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, pamoja na masuala ya kiutafiti, sayansi na teknolojia, ulinzi na usalama, sheria na mahakama kwa manufaa ya Wanaafrika ya Mashariki (manufaa ya pamoja). Kwa hiyo, jukumu kuu la Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kukusanya nguvu za Nchi Wanachama pamoja ili kutekeleza maeneo ya ushirikiano kupitia Miradi na Programu mbalimbali za Jumuiya kulingana na mikakati ya maendeleo ya Jumuiya. Katika kufikia lengo hilo kuu, Ibara ya 5(1) ya Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki imeainisha kuwa uendelezaji wa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika hatua kwa hatua. Hatua hizo zikiwa ni; Umoja wa Forodha, ikifuatiwa na Soko la Pamoja, kisha Umoja wa Fedha na hatimaye Shirikisho la Kisiasa.

Miaka 50 ya uhuru.indd 18 7/23/11 10:02 PM

Page 19

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

19

5.0 HALI YA UTAWALA NA UONGOZI 5.1 Hali ya Utawala na Uongozi katika Wizara 5.1.1 Mawaziri

Tangu Wizara ianzishwe mwaka 2006 imepata kuongozwa na Mawaziri Wanne kama ifuatavyo:

5.1.2 Manaibu Mawaziri Manaibu Waziri waliowahi kutumika Wizara ni: 5.1.3 Makatibu Wakuu Makatibu Wakuu waliowahi kuongoza Wizara ni:

Mheshimiwa Andrew J. Chenge, (Mb) Januari 2006 - Novemba, 2006 Mheshimiwa Dkt. Ibrahim S. Msabaha Desemba, 2006 - Februari 2008 Mheshimiwa Dkt. Diodorus B. Kamala (Mb) Februari, 2008 - Juni, 2010 Mheshimiwa Samuel J. Sitta (Mb) Novemba, 2010 hadi sasa Mheshimiwa Dkt. Diodorus B. Kamala (Mb) Januari, 2006 ­ Februari, 2008

Mheshimiwa Mohamed Aboud (Mb) Februari, 2008 ­ Oktoba, 2010 Mheshimiwa Dkt. Abdulla J.A. Saadalla (Mb), Novemba, 2010 hadi sasa Bw. Omari Bendera Januari, 2006 ­ Januari, 2007 Bw. Wilfred L. Nyachia Januari, 2007 ­ Machi 2008 Bw. Bakari Mahiza Aprili ­ Oktoba, 2008 Dkt. Stergomena L. Tax Novemba, 2008 hadi sasa

Miaka 50 ya uhuru.indd 19 7/23/11 10:02 PM

Page 20

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

20

5.1.4 Naibu Katibu Mkuu Mwaka 2008 Wizara ilipata Naibu Katibu Mkuu, Bw. Uledi A. Mussa ambaye anashikilia nafasi hiyo hadi sasa. 5.1.5 Wakurugenzi Tangu Wizara ianze mwaka 2006 hadi mwaka 2011 imekuwa na Wakurugenzi wafuatao:

Bw. Uledi Abbas Mussa 25 Juni, 2009 Hadi sasa (Juni, 2011) Bibi Salome Mollel Mkurugenzi 2/2/2006 - 8/6/2007 Bibi Joyce K. Mwakisyala Kaimu Mkurugenzi 3/5/2006 - 30/4/2007 Mkurugenzi 1/5/2007 - Hadi sasa (Juni, 2011) Bw. Aloyce Mlay Mkurugenzi 2/8/2007 - 17/12/2008 Bw. Uledi Abbas Mussa Kaimu Mkurugenzi 1/5/2006 - 30/4/2007 Mkurugenzi 1/5/2007 - 24/6 2009 Bw. Bernard Haule Kaimu Mkurugenzi 25/6/2009 - 16/8/2009 Bw. Amantius Msole Mkurugenzi 17/8/2009 - Hadi sasa (Juni, 2011) Bibi Mary Majula Kaimu Mkurugenzi

19/12/2008 - 4/6/2009 Bibi M.R. Shelukindo Mkurugenzi 5/6/2009 - Hadi sasa (Juni, 2011)

IDARA: UTAWALA NA RASILIMALI WATU IDARA: SERA NA MIPANGO IDARA: BIASHARA, UWEKEZAJI NA SEKTA ZA UZALISHAJI

Miaka 50 ya uhuru.indd 20 7/23/11 10:02 PM

Page 21

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

21

5.1.6 Wakurugenzi Wasaidizi Tangu wizara ianze mwaka 2006 hadi mwaka 2011 imekuwa na Wakurugenzi Wasaidizi wafuatao:

Bw. Eliabi Chodota Kaimu Mkurugenzi 27/11/2007 - 21/10/2009 Dkt. Abdullah H. Makame Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Sekta za Uzalishaji 13/10/2009 - Hadi sasa (Juni, 2011) Bw. Aman Mwatonoka Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Masuala ya Siasa 13/10/2009 - Hadi sasa (Juni, 2011) Bw. Stephen P.Mbundi Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Ulinzi na Usalama 15/5/2011 - Hadi sasa (Juni, 2011) Bw. Bernard Haule Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu Biashara, Uwekezaji 13/10/2009 - Hadi sasa (Juni, 2011) Bw. Eliabi Chodota Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Miundombinu ya Kiuchumi 14/8/2009 - Hadi sasa (Juni, 2011) Bw. Abdillah M. Mataka Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Miundombinu ya Kiuchumi 10/11/2009 - Hadi sasa

(Juni, 2011) Bw.George E. Lauwo Mkurugenzi 22/10/2009 - Hadi sasa (Juni, 2011) Bw. Stephen P. Mbundi Kaimu Mkurugenzi 25/2/2008 - 5/3/2009 Kaimu Mkurugenzi

20/7/2010 - Hadi sasa (Juni, 2011)

Bw. Job D. Masima Mkurugenzi 6/3/2009 - 20/7/2010

IDARA: MIUNDOMBINU YA KIUCHUMI NA HUDUMA ZA KIJAMII IDARA: SIASA, ULINZI NA USALAMA IDARA: BIASHARA, UWEKEZAJI NA SEKTA ZA UZALISHAJI IDARA: MIUNDOMBINU YA KIUCHUMI NA HUDUMA ZA KIJAMII IDARA:ULINZI, SIASA NA USALAMA

Miaka 50 ya uhuru.indd 21 7/23/11 10:02 PM

Page 22

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

22

5.1.7 Wakuu wa Vitengo Tangu wizara ianze mwaka 2006 hadi mwaka 2011 imekuwa na Wakuu Wa Vitengo wafuatao:

Bw. Marcel Cosmas Kaimu Mhasibu Mkuu 3/5/2006 - 30/4/2007 Mhasibu Mkuu 15/9/2006 - 19/4/2009 Vedastina Justinian Kaimu Mkuu Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano 1/4/2010 - 26/7/2010 27/7/2010 - Hadi sasa (Juni, 2011) Richard Francis Ngoda Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani 8/2/2006 - 17/9/2006 18/9/2006 - 18/6/2008 Bibi Teresia Mihayo Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani 19/6/2008 - Sept.2009 Bw. Celestin Nyaluchi, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani Mkaguzi Mkuu wa Ndani 1/11/2010 - Hadi sasa

(Juni 2011) Bw. Fredy M. G.Issa, Kaimu Mkuu Kitengo cha Manunuzi

Bibi Asina Kisinzah, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi

- 14/3/2011

Mkuu Kitengo cha Ununuzi na Ugavi

15/3/2011 - Hadi sasa (Juni 2011)

Bw. Erasto Raphael Kaimu Mkuui wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Bibi Achentalika Mahunda Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Julai, 2009 - Hadi sasa (Juni 2011)

Bw. Mugisha Kyamani Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Mawasiliano

Februari 2006 - 14/3/2011

Mkuu wa Kitengo cha Sheria

15/3/2011 - Hadi sasa (Juni, 2011) Bibi Neema Lemunge Kaimu Mhasibu Mkuu 20/4/2009 - Hadi sasa (Juni, 2010) Bw Ahadi Msangi Mhasibu Mkuu Juni 2010 - Hadi sasa (Juni, 2011) Flora P. Bilauri Kaimu Mkuu Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano 26/3/2008 - 2/4/2009 (Juni, 2011) Othman M. Othman Kaimu Mkuu Kitengo cha Habari, Elimu na

Mawasiliano 12/6/2009 - 30/3/2010 (Juni, 2011)

IDARA: UHASIBU NA FEDHA IDARA: HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO IDARA: TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO IDARA: SHERIA IDARA: TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO IDARA: UKAGUZI HESABU WA NDANI IDARA: UNUNUZI NA UGAVI

Miaka 50 ya uhuru.indd 22 7/23/11 10:02 PM

Page 23

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

23

5.1.8 MGAWANYO WA JINSIA KATIKA NGAZI ZA UONGOZI 2010/11 5.1.9 IDADI YA WATUMISHI Tangu kuanzishwa kwa wizara mwaka 2006 wizara imepanuka na watumishi wamekuwa wakiongezeka kama ifuatavyo:

MAWAZIRI NAIBU WAZIRI KATIBU MKUU NAIBU KATIBU MKUU WAKURUGENZI WAKURUGENZI WASAIDIZI WAKUU WA VITENGO JUMLA 1 1 0 1 2 6 3 14 1 1 1 1 5 11 6 26 CHEO IDADI WA WANAUME 0 0 1

0 2 0 2 6 0 0 0 0 1 5 1 6 IDADI WA WANAWAKE JUMLA YA NAFASI ZILIZO WAZI JUMLA YA NAFASI ZILIZOPO 1 2 3 4 5 6 7 S/N

2006/2007 2007/2008 2008/2009 2009/2010 Januari 2011 Watumishi 69 Watumishi 77 Watumishi 85 Watumishi 101 Watumishi 109 MWAKA IDADI YA WATUMISHI 1 2 3 4

5 NA

Miaka 50 ya uhuru.indd 23 7/23/11 10:02 PM

Page 24

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

24

5.2 Hali ya Utawala na Uongozi Katika Jumuiya

Kulingana na Ibara ya 67 ya Mkataba wa Uanzishaji wa Jumuiya, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huteuliwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi kutumikia nafasi hiyo kwa kipindi kisichozidi miaka mitano (5). Mapendekezo ya jina la Katibu Mkuu huwasilishwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Nchi Wanachama kwa utaratibu wa mzunguko. Tangu Jumuiya ianzishwe mwaka 1999, imepata kuongozwa na Makatibu Wakuu wanne kama ifuatavyo: Muundo wa awali ulikuwa na Manaibu Katibu Wakuu watatu. Mwaka 2008 muundo huo ulirekebishwa na kuwa na Manaibu Katibu Wakuu wanne. Manaibu Katibu Wakuu waliowahi kushika wadhifa huo ni kama ifuatavyo: Mheshimiwa Balozi Francis Muthaura kutoka Kenya 1999 ­ 2001 Dkt. Kipyego Cheluget Kenya 2004 - 2007 Balozi Julius Onen Uganda 2006 - 2009 Mheshimiwa Nuwe Amanya Mushega kutoka Uganda 2001 ­ 2006 Balozi Fulgence Kazaura Tanzania 2001 - 2002 Bw. Aloys Mutabingwa Rwanda 2009 ­ 2011 Mheshimiwa Balozi Juma Volter Mwapachu kutoka Tanzania 2006 ­ 2011 Balozi Ali Mchumo Tanzania 2002 - 2004 Mheshimiwa Dkt. Richard Sezibera kutoka Rwanda 2011 hadi sasa, Dkt. Richard Sezibera ameshika wadhifa huu tangu tarehe 19 Aprili, 2011 kufuatia kumalizika kwa muda wa Balozi Juma Mwapachu. Balozi Ahmada Ngemera Tanzania

2004 - 2006

Miaka 50 ya uhuru.indd 24 7/23/11 10:02 PM

Page 25

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

25

Manaibu Katibu Wakuu waliopo kwa hivi sasa ni kama ifuatavyo: Manaibu Katibu Wakuu huteuliwa kutoka kila Nchi Wanachama ambayo haijatoa Katibu Mkuu. Kulinga na Ibara ya 71 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Manaibu Makatibu Wakuu wana jukumu la kumsaidia Katibu Mkuu wa Jumuiya katika kazi zake. Aidha, Mshauri wa Sheria wa Jumuiya (Counsel to the Community) ndiye Mshauri Mkuu wa masuala ya kisheria, masuala yaliyomo katika Mkataba wa Uanzishaji wa Jumuiya na anayo haki ya kuhudhuria katika Mahakama za Nchi Wanachama iwapo kuna masuala yanayohusu Jumuiya na Mkataba wa Uanzishaji wa Jumuiya. Mpaka sasa Jumuiya imekuwa na Mshauri (Counsel to the Community) mmoja ambaye ni Mheshimiwa Wilbert T. Kaahwa kutoka Uganda toka mwaka 2001 hadi sasa.

Dkt. Julius Rotich Kenya 2007 hadi leo Mhe. Beatrice Kiraso Uganda 2006 hadi leo Bw. Jean Claude Nsengyumva, Burundi 2009 hadi leo Dkt. Enos Bukuku Tanzania 2011 hadi leo

Miaka 50 ya uhuru.indd 25 7/23/11 10:02 PM

Page 26

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

26

6.0. SERA, MIKAKATI NA SHERIA 6.1. Sera, Mikakati na Sheria Katika Wizara

Wizara katika utekelezaji wa majukumu yake inaongozwa na Sera ya Taifa ya Mambo ya Nje; Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010; Mkakati wa Taifa wa Kupambana na Umaskini (MKUKUTA); na sheria na kanuni mbalimbali za utumishi wa umma, matumizi ya fedha za umma, na ununuzi. Aidha, Wizara inazingatia Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Itifaki zake; maagizo ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki; Maamuzi ya Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki; na Mikakati ya Maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wizara tangu iundwe mwaka 2006, imeandaa Mipango Mikakati miwili Mkakati wa kwanza ni wa mwaka 2007/2008 ­ 2009/2010; Mpango mkakati wa kwanza ulilenga katika kuwezesha utekelezaji wa Umoja wa

Forodha, Maandalizi ya Itifaki ya Soko la Pamoja, na ushirikishwaji wa Wananchi katika Mtangamano ikiwemo kukusanya maoni na kufuatilia Utekelezaji wa Programu na Miradi ya Jumuiya. Mpango Mkakati wa Pili 2010/11 ­ 2012/2013 umezingatia upanukaji wa majukumu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Muundo wa Wizara pamoja na utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja na maandalizi ya majadiliano ya Umoja wa Fedha wa Afrika Mashariki.

6.2. Sera na Sheria

Utekelezaji wa hatua za Mtangamano wa Afrika Mashariki unagusa sekta mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Katika hali hii, utekelezaji wa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umeendelea kuongozwa na sera na mikakati ya kisekta husika. Kwa kuzingatia kuwa suala la mtangamano ni mtambuka linahitajika mwongozo wa kisera na kisiasa ili kulinda maslahi ya Taifa, na kwa kuzingatia umuhimu wa mtangamano kiuchumi na kijamii, Wizara iko katika mchakato wa kuandaa Sera ya Mtangamano wa Afrika Mashariki. Sera hii itaiwezesha Tanzania kujipanga kimkakati na kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kujiendeleza kiuchumi, kijamii, na katika kuimarisha ujirani mwema.

6.3. Sera, Mikakati, Sheria na Itifaki katika Jumuiya 6.3.1 Sera na Mikakati katika Jumuiya

Tangu Jumuiya ianzishwe, kumekuwepo awamu tatu za Mikakati ya Maendeleo (East African Development Strategies). Mpango Mkakati wa Kwanza ulikuwa kati ya mwaka 1997-2000. Mkakati huu ulilenga katika kuwezesha kuanzishwa upya kwa ushirikiano wa Afrika Mashariki na hivyo kupelekea kusainiwa kwa Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1999. Mkakati wa pili wa Maendeleo wa mwaka 2001-2005 ulilenga kujenga misingi ya utekelezaji wa mtangamano wa Afrika Mashariki, hususan maandalizi na utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Forodha ulioanza tarehe 01 Januari, 2005. Mkakati wa Tatu wa Maendeleo wa mwaka 2006-2010 ulihusu utekelezaji wa maeneo ya msingi ya kisekta katika kupambana na umaskini. Sekta zilizopewa kipaumbele ni kilimo na uhakika wa chakula; viwanda; utalii na wanyamapori; miundombinu; afya; elimu; nishati; mawasiliano; utamaduni na lugha; mazingira na maliasili; na sheria na Mambo ya Mahakama. Uteuzi wa sekta hizi ulinzingatia haja ya kuleta maendeleo yaliyo sawa baina ya Nchi Wanachama, na pia kukuza uchumi na kupunguza umaskini na hivyo kuboresha maisha ya watu walio wengi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha, Mkakati huu ulizingatia kuwepo kwa uwiano kati ya mipango na programu za kikanda na kitaifa. Mkakati wa Nne wa mwaka 2011-2015 unakusudia kusaidia mipango ya ndani ya maendeleo ya Nchi Wanachama ambayo nchi moja moja zisingeweza kutekeleza au utekelezaji wake ungechukua muda mrefu kutokana na ufinyu wa Bajeti. Kwa hiyo, Mkakati huu unakusudia kuziwesha Nchi Wanachama kuweka nguvu zao pamoja na hivyo kufanikisha malengo ya msingi ya maendeleo ya kuichumi na kijamii kwa haraka zaidi.

6.3.2 Sheria na Itifaki Katika Jumuiya

Tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1999, Nchi Wanachama zimefanikiwa kuhuisha sera na sheria kadhaa na kukamilisha Itifaki mbalimbali. Katika kipindi cha kuanzia mwaka 1999 hadi Disemba, 2010 Itifaki zilizopitishwa ni pamoja na: a.) Itifaki ya kuanzisha Umoja wa Forodho wa Afrika Mashariki;

b.) Itifaki ya Kuzuia Usafirishaji na Usambazaji wa Madawa ya kulevya katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; c.) Itifaki ya uhakiki wa Ubora, vipimo na uthibiti katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; d.) Itifaki ya kuanzisha Baraza la Vyuo Vikuu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; e.) Itifaki ya Maendeleo Endelevu katika Bonde la Ziwa Victoria; f.) Itifaki ya kuanzisha Ushuru wa Forodha katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; g.) Itifaki ya Mazingira na Maliasili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; h.) Itifaki ya Kuanzisha Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; i.) Itifaki ya kuanzisha Wakala wa Kusimamia Usalama wa Anga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; j.) Itifaki ya kuanzisha Kamisheni ya Utafiti wa Magonjwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; k.) Itifaki ya Kuanzisha Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; l.) Itifaki ya Soko la Pamoja ya Afrika Mashariki; na m.) Itifaki ya Uratibu wa Sera ya Nje ya Afrika Mashariki; Aidha, Nchi Wanachama zimekamilisha majadiliano ya Miswada mbalimbali inayohusu masuala ya Jumuiya. Miswada hiyo kupitishwa na Bunge la Afrika Mashariki na hatimaye kuidhinishwa na Wakuu wa Nchi ili kuwa Sheria za Jumuiya. Katika kipindi cha kuanzia mwaka 1999 sheria zilizopitishwa ni pamoja na: a.) Sheria ya Tafsiri ya Sheria za Jumuiya ya Afrika Mashariki (The East African Community Interpretation Act); b.) Sheria ya Nembo ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (The East African Community Emblem Act); c.) Sheria ya Mamlaka na Kinga kwa Wabunge wa Afrika Mashariki (The East African Legislative Assembly Powers and Privileges Act); d.) Sheria ya kutunga Sheria za Jumuiya (The Acts of the Community Act); e.) Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (The East African Community Customs Management Act 2004); f.) Sheria ya Kusimamia Usafiri katika Ziwa Victoria (The Lake Victoria Transport Management Act 2007); g.) Sheria ya Wakuu wa Nchi kutoa Mamlaka kwa Vyombo vingine vya Jumuiya (The Summit ­ Delegation of Powers and Functions Act 2007); h.) Sheria ya Mapato na Matumizi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2002, 2003, 2004, 2005, 2006, 2007,2009 na 2009; i.) Sheria ya Uhakiki wa Ubora, Vipimo na Udhibiti katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2006; j.) Sheria ya Ushindani ya Afrika Mashariki, 2006; k.) Marekebisho ya Sheria ya Kutunga Sheria za Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2008; l.) Sheria ya Baraza la Vyuo Vikuu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2008; m.) Marekebisho ya Sheria ya Nembo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2008; na n.) Marekebisho ya sheria ya Kusimamia Ushuru wa Forodha katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2008.

Miaka 50 ya uhuru.indd 26

7/23/11 10:02 PM

Page 27

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

27

1967:

Jumuiya ya Afrika Mashariki yaundwa na hivyo kuashiria mwanzo wa kutumia kwa azma ya Marehemu Mwalimu Julius Kambarage ya kuunda muungano wa Afrika Mashariki;

7.0 MABADILIKO NA MATUKIO MAKUU 7.1 Matukio Makuu katika Jumuiya

Mabadiliko na matukio makuu kuhusiana na mtangamano wa Afrika ya mashariki tangu Tanzania ipate uhuru ni kama ifuatavyo:

1991: Mkutano wa Viongozi wa Nchi za Afrika Mashariki ulifanyika Harare, Zimbabwe ambapo Viongozi Wakuu walikubalina kuanzisha tena ushirikiano wa Afrika Mashariki. 30 Novemba, 1993: Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki walitia Sahihi ya kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu Utatu ya Ushikiano wa Afrika Mashariki. Machi, 1996: Katibu Mkuu wa Kwanza wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Francis Mathaura kutoka nchi ya Kenya ateuliwa. 1977: Iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yavunjika na kusababisa mtikisiko mkubwa wa kiuchumi katika Afrika Mashariki na hususan, katika Nchi zilizotegemea huduma kadhaa za kikanda katika kuendesha uchumi wake. Huduma zilizoathirika sana zilihusu uchukuzi na usafirishaji (nchi kavu, majini na angani), mawasiliano (simu na posta).

Kutoka kushoto ni Waheshimiwa Marais Hayati Milton Obote wa Uganda, Hayati Jomo Kenyatta wa Kenya na Hayati Julius Nyerere wa Tanzania. Kutoka kushoto ni Waheshimiwa Marais Daniel Arap Moi wa Kenya, Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na Viongozi wengine wa Serikali. Katibu Mkuu wa kwanza wa Jumuiya, Mheshimiwa Balozi Francis Mathaura kutoka Kenya. Moja ya ndege za lililokuwa Shirika la Ndege la Afrika Mashariki.

Miaka 50 ya uhuru.indd 27 7/23/11 10:02 PM

Page 28

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

28

14 Machi, 1996:

Maandalizi Kamili ya utekelezaji wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki yaanza baada ya Sekretarieti ya Tume ya Kudumu ya Utatu kuzinduliwa katika Makao Makuu ya Jamuiya Mjini Arusha, Tanzania.

14 Machi, 1996:

Tume ya Sekretariati ya Afrika Mashariki yazinduliwa Arusha,

Tanzania.

19 Aprili, 1996:

Makubaliano ya kuanzisha Baraza la Biashara la Afrika Mashariki yatiwa saini Nairobi, Kenya.

28 Aprili, 1997:

Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watia sahihi Makubaliano ya Utatu ya Uepukaji Ushuru Marambili (Avoidance of Double Taxation).

20 Novemba, 1997:

Wakuu wa Majeshi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya wakutana Arusha kukubaliano rasimu ya Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya ulinzi.

26 Mei, 1998:

Kitengo cha Mahusiano ya Ulinzi (Defence Liaison Unit) cha Jumuiya chaanzishwa katika Sekretarieti ya Jumuiya.

30 Novemba 1999:

Kuwekwa saini kwa Mkataba wa kuanzisha upya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha, Tanzania. Tukio hilo lililohushuhudiwa na Viongozi Wakuu wa Afrika Masharika ambao walihudhuria.

1 Januari, 2000: Utekelezaji wa Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki waanza rasmi na hivyo kuashiria mwanzo wa safari ya kuimarisha mtangamano wa Afrika Mashariki ikiwa ni hatua ya kwanza ya mtangamano wa Afrika Mashariki. Novemba, 2001: Bunge la Afrika Mashsriki (East Afriacan Legislative Assembly ­ EALA) laanza kazi rasmi ambapo Spika wa kwanza alitokea Tanzania, Mheshimiwa Abdilrahman Kinana. 30 Novemba, 1999: Mahakama ya Afrika Mashariki (East African Court of Justice ­ EACJ) yaundwa. Januari, 2006: Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki yaanzishwa rasmi ili kutoa msukumo zaidi katika ushiriki wa Tanzania katika mtangamano wa Afrika Mashariki ambapo Mheshimiwa Andrew Chenge aliteuliwa kuwa Waziri wa Kwanza wa Wizara hii. 2007: Wizara yakusanya maoni ya wananchi nchi nzima, Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, kuhusu hoja ya kuharakisha Shirikisho la Kisiasa, ambayo ni hatua ya nne na mwiso katika ushirikiano wa Afrika Mashariki. Hatua hii ni miongoni mwa hatua kadhaa zilizochukuliwa na Wizara ili kushirikisha na kupata maoni ya wananchi katika uendelezaji wa mtangamano wa Afrika Mashariki. 18 Aprili, 2007: Itifaki ya kuanzisha Wakala wa Kusimamia Usalama wa Anga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yasainiwa. 18 Juni 2007: Rwanda na Burundi zajiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na hivyo kupelekea uundwaji wa soko kubwa zaidi kwa bidhaa za Tanzania na Nchi zingine Wanachama.

11 Julai, 2007: Tume ya Bonde la Ziwa Victoria yazinduliwa rasmi ili kufanyia kazi miradi ya maendeleo ya ziwa Victoria ikiwemo, matumizi endelevu ya rasilimali za Ziwa Victoria, usalama wa usafiri majini, ulinzi na utunzaji wa mazingira, na miradi endelevu katika bonde la ziwa Victoria. 13 Septemba, 2008: Itifaki ya kuanzisha Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yasainiwa.

Kutoka kulia ni Waheshimiwa Marais Benjamini Mkapa wa Tanzania, Daniel Arap Moi wa Kenya na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakisaini Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Spika wa sasa (2011) wa Bunge la Afrika Mashariki, Mheshimiwa Abdirahin Haithar-Abdi pamoja na Viongozi wa Serikali

Miaka 50 ya uhuru.indd 28 7/23/11 10:02 PM

Page 29

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

29

28 Aprili, 2009: Wakuu wa Nchi Wanachama wazindua rasmi ujenzi wa barabara ya Arusha ­ Namanga ­ Athi River ikiwa ni moja ya miradi ya pamoja ya Jumuiya. Sherehe hii ya uzindizi ilifanyika Arusha, Tanzania. 8 Septemba, 2009: Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alizindua mazoezi ya Kijeshi kwa majeshi ya Nchi Wanachama katika Chuo cha Kijeshi, Monduli, Arusha. 20 Novemba, 2009: Wakuu wa Nchi Wanachama wasaini Itifaki ya kuanzishwa kwa Soko la Pamoja, ambapo utekelezaji wake ulianza rasmi tarehe 1 Julai, 2010; ambayo ni hatua ya pili ya mtangamano. Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Stergomena L. Tax akipokea cheti cha ungozi mahiri katika majadiliano ya Itifaki ya Soko la Pamoja, katika ngazi ya Makatibu Wakuu. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Bw. Uledi Abbas Mussa akipokea cheti cha ungozi mahiri katika majadiliano ya Itifaki ya Soko la Pamoja, katika ngazi ya Wataalaam.

Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua ujenzi wa barabara ya Arusha ­ Namanga ­ Athi River, akiwa pamoja na Waheshimiwa Marais, Paul Kagame wa Rwanda, na Mwai Kibaki wa Kenya. Wakuu wa Nchi wakisaini Itifaki ya Soko la Pamoja jijini Arusha. Mstari wa mbele kutoka kushoto ni Rais Museveni, Rais Kagame, Rais Kikwete, Rais Kibaki na Rais Nkurunziza.

Rais Paul Kagame wa Rwanda akimkabidhi uenyekeiti wa Jumuiya Rais Dkt. Jakaya Kiwkete wa Tanzania.

Miaka 50 ya uhuru.indd 29 7/23/11 10:02 PM

Page 30

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

30

20 Novemba, 2009: Wakuu wa Nchi Wanachama waweka jiwe la msingi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha. 26 Januari, 2010: Wizara yazindua Mkataba wa Huduma Bora kwa wateja ili kuimarisha huduma kwa wananchama. 26 Janurai, 2010: Wizara yazindua rasmi tovuti yake, www.meac.go.tz Januari, 2011: Majadiliano ya Umoja wa Fedha yaanza, ambayo ni hatua ya tatu ya mtangamano wa Afrika Mashariki. Rais Paul Kagame wa Rwanda akimkabidhi uenyekeiti wa Jumuiya Rais Dkt. Jakaya Kiwkete wa Tanzania.

Mhe. Dkt. Diodorus B. Kamala Waziri wa Ushirikiano wa Afika Mashariki akizindua Mkataba wa huduma kwa wateja, kushoto kwake ni Mhe Aboud Mohamed Aboud, Naibu wa Waziri wa Ushirikiano wa Afika Mashariki, na kulia kwake ni Dkt. Stergomena L. Tax Mhe. Dkt. Diodorus B. Kamala Waziri wa Ushirikiano wa Afika Mashariki akizindua Tovuti wa Wizara ya wa Ushirikiano wa Afika Mashariki

Miaka 50 ya uhuru.indd 30 7/23/11 10:02 PM

Page 31

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

31

8.0 MAFANIKIO KATIKA MTANGAMANO WA AFRIKA MASHARIKI

Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1967 na kuianzisha upya Jumuiya iliyovunjika mwaka 1977 ni miongoni mwa mafanikio ya Miaka Hamsini ya Uhuru. Miongoni mwa Mafanikio makubwa yaliyopatikana hadi sasa ni kujenga moyo wa kuaminiana ambao umeongeza nguvu kwa Nchi Wanachama katika kuendeleza mtangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nchi Wanachama zimeongeza moyo wa ushirikiano na kuimarisha Jumuiya na kukubaliana kuendeleza mtangamano hatua kwa hatua, kwa kuanza na hatua zinazojenga misingi ya kiuchumi na kijamii (hususani Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja) ili kuwawezesha wananchi kunufaika na ushirikiano katika Jumuiya kwa kuendeleza biashara, shughuli za kiuchumi na uzalishaji, uwekezaji na ajira na hivyo kujiongezea kipato.Hatua hizo za mwanzo zitawawezesha wananchi kuelewa na kuyashuhudia mafanikio na faida za mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na hatimaye kufikia hatua ya kuwa na Shirikisho la Kisiasa. Mafanikio yaliyopatikana kwa ujumla ni kama yafuatayo:

Mafanikio ya Kiuchumi

a.) Kuanzishwa kwa Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki. na hivyo kuongeza biashara, uwekezaji na ajira miongoni mwa Nchi Wanachama; b.) Kuanzishwa kwa Soko la Pamoja; c.) Kupunguza vikwazo vya kibiashara katika nchi; d.) Kutekeleza uondoaji wa ushuru wa forodha; e.) Kuwianisha viwango vya ubora wa bidhaa zilizozalishwa katika Afrika Mashariki;

f.) Utambuzi wa vyeti vya afya vinavyotolewa na Bodi za Kitaifa kwa bidhaa zinazouzwa katika Afrika Mashariki; g.) Utekelezaji wa mkakati wa kuendeleza uratibu wa uwezo wa utafiti wa kisayansi katika Afrika Mashariki; h.) Kuanzishwa kwa Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika Mashariki (East African Community Science and Technology Commission - EASTEC); i.) Kuanzishwa kwa Wakala wa Usalama wa Anga wa Afrika Mashariki (Civil Aviation Safety and Security Oversight Agency CASSOA); j.) Kuanzishwa kwa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (East African Kiswahili Commssion - EAKC); k.) Kuanzishwa kwa Kamisheni ya Utafiti wa Afya ya Afrika Mashariki (East African Health Research Commission EAHRC); l.) Kukua kwa uhuru wa soko la hisa na uendelezaji wa soko mitaji m.) Uhuru wa soko la mitaji; n.) Uwianishaji wa shughuli za Wizara za Fedha na Benki Kuu wakati wa maandalizi ya kusomwa kwa Bajeti; o.) Kuwa na Wimbo wa Jumuiya; p.) Kuanzisha programu na miradi ya pamoja ya kuendeleza miundombinu ya kiuchumi (Barabara, reli, nishati, udsafiri wa anga); q.) Kuimarisha uwezo wa kujadiliana Katika masuala ya uchumi na biashara kwa pamoja; na r.) Kuwepo kwa utaratibu unaowezesha kubadilisha fedha za Nchi Wanachama.

Mafanikio Kisiasa na Kijamii

a.) Kusainiwa kwa Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1999; b.) Kuridhia Itifaki mbalimbali; c.) Kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika masuala ya ulinzi mwaka 2000; d.) Kuendelea kurahisisha uhuru wa watu na bidhaa kuvuka mipaka ya nchi; e.) Utekelezaji wa siku saba za ziada kwa magari binafsi kuvuka mipaka ya Nchi Wanachama; f.) Kuanza kutumika kwa Hati ya Kusafiria ya Afrika Mashariki; g.) Kuanzisha Dirisha la Afrika Mashariki kwenye viwanja vya ndege; h.) Kutolewa kwa hati za muda za kusafiria kwa wananchi wa Afrika Mashariki; i.) Kuwianisha fomu za uhamiaji katika vituo vya mipakani; j.) Kuhuisha Baraza la Vyuo Vikuu la Afrika Mashariki; k.) Kuondoa visa za wanafunzi wa Afrika Mashariki; l.) Kuwianisha ada za vyuo vikuu; m.) Utekelezaji wa program za kuelimisha na kuhamasisha; n.) Utekelezaji wa program ya kubadilishana wanafunzi na wahadhiri katika ngazi ya Vyuo Vikuu; o.) Utekelezaji wa Programu ya kudhibiti kuenea kwa magonjwa mipakani (EAIDSnet); p.) Kuwepo kwa jukwaa la kila mwaka kuhusu masuala ya afya ya Afrika Mashariki; q.) Kuhuisha masuala ya jinsia katika miradi na program za Jumuiya ya Afrika Mashariki; r.) Kuwianisha taratibu za kutoa vibali vya kufanya kazi; s.) Kuanzishwa kwa jukwaa la Wakuu wa Polisi, Wakurugenzi wa

Upelelezi, Wakuu wa Operesheni, Wakuu wa Usalama kuratibu masuala ya amani na usalama ikiwemo ukaguzi na ufuatiliaji wa pamoja, kudhibiti uhalifu kupeana taarifa za uhalifu na kutekeleza Itifaki ya Kupambana na Usafirishaji Madawa Haramu ya kulevya; t.) Kuwa na Mkakati wa Maendeleo ya sekta binafsi; u.) Kuendesha maonyesho ya kila mwaka ya Juakali/Nguvu Kazi; v.) Kudhibiti hali ya ukosefu wa usalama katika Ziwa Viktoria; w.) Kudhibiti kusambaa kwa silaha ndogo ndogo haramu na nyepesi; x.) Kuendesha mashindano ya Insha kwa wanafunzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; y.) Kuandaa Mkakati wa Kupambana na Majanga na Tahadhari wa Afrika Mashariki; na z.) Kuendesha mazoezi ya pamoja ya kijeshi, utamaduni na michezo.

8.1 Kuanzisha Taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (Institutions of the Community)

Tangu Jumuiya ianishwe hapo 1999 hadi sasa imeweza kuunda Taasisi zinazosimamia utendaji katika maeneo mbalimbali ya mtangamano kulingana na sheria zinazoanzisha Taasisi hizo. Pamoja na majukumu mengine, Taasisi hizi zina jukumu la kuibua na kutekeleza miradi na programu mbalimbali. Taasisi hizo ni: a.) Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria (Lake Victoria Basin Commission - LVBC); b.) Oganaizesheni ya Uvuvi Katika Ziwa Victoria (Lake Victoria Fisheries Organisation - LVFO); c.) Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (Inter-University Council for East Africa - IUCEA); d.) Wakala wa Usalama wa Anga ya Afrika Mashariki (Civil Aviation Safety and Security Ovesight Agency - CASSOA); na e.) Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East African Development Bank - EADB). Maelezo mafupi kwa kila Taasisi ni kama ifuatavyo hapo chini. Aidha, maelezo ya kina kuhusu shughuli zinazofanywa na Taasisi hizi yametolewa katika Itifaki na sheria zinazoanzisha Taasisi hizi.

8.1.1 Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC)

Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC) ni Taasisi maalum ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye dhamana ya kuratibu na kusimamia maendeleo endelevu ya Bonde la Ziwa Victoria. Taasisi hii inaongozwa kulingana na Itifaki ya Kuanzishwa Taasisi iliyotiwa saini tarehe 29

Miaka 50 ya uhuru.indd 31 7/23/11 10:02 PM

Page 32

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

32

Novemba, 2003 na kuridhiwa mwaka 2004. Mkuu wa Taasisi hii ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ambaye huajiriwa kwa vigezo vya ushindani na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa utaratibu wa Mzunguko wa miaka mitano (5).

8.1.2 Oganaizesheni ya Uvuvi Katika Ziwa Victoria (LVFO)

Oganaizesheni ya Uvuvi Katika Ziwa Victoria (LVFO) ni Taasisi ya Kikanda chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye Jukumu la kuratibu na kusimamia rasilimali za uvuvi katika Ziwa Victoria. Taasisi hii

ilianzishwa kwa mujibu wa Makubaliano (Convention) yaliyosainiwa na Nchi tatu waanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1994. Lengo la Taasisi hii ni kukuza ushirikiano kati ya Nchi Wanachama kwa kuwianisha juhudi za kitaifa, kuendeleza hatua za uhifadhi na taratibu za usimamizi katika kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali hai za Ziwa Victoria.

8.1.3 Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA)

Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) ni Taasisi ya Kikanda iliyoanzishwa mwaka 1980 na Nchi tatu waanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika kuimarisha zaidi Taasisi hii Nchi Wanachama ziliunda Itifaki iliyosainiwa na kuridhiwa na Nchi Wanachama mwaka 2002. Lengo la kuanzishwa kwa Baraza la Vyuo Vikuu ni kuwezesha mawasiliano baina ya Vyuo Vikuu ndani ya Jumuiya, na kutoa nafasi ya majadiliano yenye lengo la kuboresha masuala ya taaluma ya elimu ya juu.

8.1.4 Wakala wa Usalama wa Anga Afrika Mashariki (CASSOA)

Wakala wa Usalama wa Anga ya Afrika Mashariki (CASSOA) ni Taasisi ya Kikanda yenye jukumu la kusimamia usalama wa usafiri wa Anga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Chombo hiki kilianzishwa mwaka 2007 na kuongozwa na sheria ya kuanzisha chombo hiki. Makao Makuu ya CASSOA yapo mjini Entebbe, Uganda.

8.1.5 Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB)

Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) ni Taasisi kongwe iliyoanzishwa mwaka 1967 na iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977. Benki hiyo ilijiunda upya na kujiendesha kwa kufuata kanuni na taratibu zake. Kwa sasa Benki hii inamilikiwa na Nchi nne Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda. Aidha, baadhi ya wamiliki wengine wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo la Uholanzi (FMO), Shirika la Uwekezaji na Maendeleo la Ujerumani (DEG), na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA). Aidha, Taasisi zifuatazo zimeidhinishwa na Baraza la Mawaziri wa Jumuiya na mchakato wa kuanzisha Taasisi hizi unaendelea: a.) Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika Mashariki (East African Science and Technology Commission- EASTECO); b.) Kamisheni ya Utafiti wa Afya ya Afrika Mashariki (East African Health Research Commission-EAHRC); c.) Kamisheni ya Kiswahili; na d.) Kamisheni ya Afya ya Afrika Mashariki.

8.2 Mafanikio Katika Utekelezaji wa Hatua za Mtangamano

Ibara ya 2 (1) ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, imeainisha kuwa Nchi Wanachama zitaanzisha Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja kama hatua mahsusi za mtangamano. Aidha, Ibara ya 5(2) ya Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki imeainisha hatua za mtangamano wa Jumuiya kuwa ni Umoja wa Forodha, ukifuatiwa na Soko la Pamoja, kisha Sarafu Moja, na hatimaye Shirikisho la Kisiasa. Hatua hizi hutekelezwa hatua kwa hatua zikiongozwa na utayari Nchi Wanachama, na ukamilishwaji wa hatua za awali.

Hatua za Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

8.2.1 Umoja wa Forodha

Utekelezaji wa Umoja wa Forodha ambayo ni hatua ya kwanza ya mtangamano wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa mafanikio ya Tanzania katika miaka hamsini ya Uhuru. Katika utekelezaji wa hatua hii, Itifaki ya Umoja wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilisainiwa mwaka 2004 na utekelezaji wake kuanza tarehe 1 Januari 2005. Malengo makuu ya kuunda Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki yameainishwa katika Ibara ya 3 ya Itifaki ya Umoja wa Forodha. Malengo hayo ni: a.) Kukuza biashara; b.) Kuongeza ufanisi katika uzalishaji; c.) Kukuza uwekezaji wa ndani baina ya Nchi Wanachama; na d.) Kuendeleza viwanda. Katika kufikia malengo haya, Ibara ya 2(4-5) ya Itifaki ya Umoja wa Forodha inaainisha vipengele muhimu katika Umoja wa Forodha. Vipengele hivyo ni kama ifuatavyo: a.) Kuondoleana Ushuru wa Forodha Katika Biashara ya Bidhaa Miongoni mwa Nchi Wanachama (Internal Tariff Elimination); b.) Kuweka Wigo wa Pamoja wa Ushuru wa Forodha kwa Bidhaa Zinazotoka Nje ya Jumuiya (Common External Tariff); c.) Kuondoa Vikwazo Visivyo vya Kiforodha (Elimination of Non Tariff Barriers); d.) Kuwa na Vigezo vya Afrika Mashariki vya Kutambua Uasili wa Bidhaa (EAC Rules of Origin); na e.) Kuwa na Sheria Moja ya Usimamizi wa Forodha Ndani ya Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004).

8.2.1.1 Utekelezaji wa Vipengele Muhimu vya Umoja wa Forodha A: Uondoaji wa Ushuru wa Forodha

Kwa kuzingatia tofauti za kiuchumi baina ya Nchi Wanachama, Nchi Wanachama zilikubaliana kuanzisha Umoja wa Forodha kwa kuwa kipindi cha mpito cha miaka mitano cha kuondoa ushuru wa forodha ni kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2010. Hivyo ushuru wa forodha

Umoja wa Forodha 2005 Soko la Pamoja 2010 Sarafu moja 2012 Shirikisho la kisiasa

Miaka 50 ya uhuru.indd 32 7/23/11 10:02 PM

Page 33

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

33

uliondolewa hatua kwa hatua ili kutoleta athari kubwa katika maendeleo ya viwanda, ajira na mapato ya Serikali. Katika kipindi cha mpito, bidhaa zilizozalishwa Tanzania na Uganda ziliingia katika Soko la Kenya bila kutozwa ushuru wa forodha. Aidha, katika kipindi hicho, bidhaa zilizozalishwa Kenya na kuingia Tanzania

ziligawanywa katika makundi mawili kundi A, na kundi B. Bidhaa katika kundi A ambazo ni pamoja na malighafi ziliingizwa toka Kenya pasipo kutozwa ushuru. Bidhaa katika Kundi B ambazo ni zile zilizosindikwa kwa kiwango cha kati (semi-finished) na bidhaa zilizokamilika (finished goods) zilipoingia Tanzania na Uganda toka Kenya zilitozwa ushuru ambao viwango vyake vimekuwa vikipungua mwaka hadi mwaka na kufikia Sifuri tarehe 31 Desemba, 2009. Kufuatia kipindi hiki cha mpito kuisha, biashara ya bidhaa miongoni mwa Nchi Wanachama sasa hazitozwi ushuru wa forodha tangu mwezi Januari 2010. Bidhaa hizi ni zile zinazozalishwa katika Nchi Wanachama na kutambuliwa kulingana na Vigezo vya Afrika Mashariki vya Kutambua Uasili wa Bidhaa (EAC Rules of Origin).

Jedwali Na. 1: Mpango wa Kuondoa Ushuru wa Forodha kwa Bidhaa Toka Kenya Chanzo: Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki B: Wigo wa Pamoja wa Ushuru wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Bidhaa Kutoka Nje ya Jumuiya.

Katika kutekeleza wigo wa pamoja wa ushuru wa forodha, Nchi Wanachama zilikubaliana kuwa na ushuru wa forodha wa viwango vitatu kwa bidhaa kutoka nje ya Jumuiya. Viwango hivyo ni: a.) Asilimia sifuri (0%) kwa malighafi, mitambo na bidhaa za mitaji; b.) Asilimia kumi (10%) kwa bidhaa zilizosindikwa kwa kiwango cha kati na bidhaa zinazotumika kwa uzalishaji viwandani; na c.) Kiwango cha 25% kwa bidhaa za mwisho za mlaji zilizokamilika usindikaji wake. Aidha, ili kulinda uchumi na kusaidia maendeleo ya viwanda na ajira ndani ya Jumuiya, Nchi wanachama zilikubaliana orodha ya bidhaa nyeti ambazo zinatozwa ushuru wa forodha wa zaidi ya 25% kama ifuatavyo:

Jedwali Na. 2: Orodha ya Bidhaa Nyeti Ambazo Zinatozwa Ushuru wa Forodha wa Zaidi ya 25% C: Kuondoa Vikwazo Visivyo vya Kiforodha Katika Biashara ya Bidhaa Baina ya Nchi Wanachama.

Itifaki ya Umoja wa Forodha katika Ibara ya 13 inazitaka Nchi Wanachama kuondoa vikwazo vyote zisivyo vya kiforodha katika biashara ya bidhaa miongoni mwa Nchi Wanachama na kutoanzisha vikwazo vipya. Vikwazo hivyo ni pamoja na vizuizi vya barabarani visivyo vya lazima, vikwazo vya kiufundi kwenye viwango vya bidhaa, na vikwazo vya mahitaji ya kiafya kwa wanyama na mimea Sanitary and Photosanitary Standards (SPS). Katika kutekeleza kipengele hiki cha Itifaki, Jumuiya imeandaa mpango mahsusi unaoainisha vikwazo visivyo vya kiforodha na muda wa kuondoa vikwazo hivyo. Aidha kila Nchi imeunda Kamati ya Kitaifa ya kushughulikia uondoaji wa vikwazo hivi. Vilevile, Jumuiya imeunda Kamati ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kushughulikia uondoaji wa vikwazo hivyo. Nchi Wanachama zimepiga hatua katika uondoaji wa vikwazo visivyo vya kiforodha, hasa kwa kuweka muundo wa kimfumo wa kutambua na kushughulikia vikwazo.

D: Vigezo vya Kutambua Uasili wa Bidhaa

Ibara ya 14 ya Itifaki ya Umoja wa Forodha inazitaka bidhaa ambazo hazitalipiwa ushuru wa Forodha kukidhi vigezo vya Utambuzi wa Uasili wa Afrika Mashariki kama ilivyoainishwa katika Kiambatanisho cha tatu cha Itifaki cha Uasili wa Bidhaa. Ibara ya 4(1) ya Kiambatanisho cha

Uasili wa Bidhaa (rules of origin) kimeainisha vigezo vinne ili bidhaa ikubalike kuwa ina uasili wa Afrika Mashariki.Vigezo hivyo ni: a.) Bidhaa zilizozalishwa ndani ya Nchi Mwanachama kwa 100%; b.) Bidhaa zilizozalishwa ndani ya Nchi Mwanachama kwa kutumia malighafi toka ndani ya Jumuiya kwa kiwango kisichopungua 40%; c.) Kiwango cha ongezeko la thamani ya uzalishaji kisichopungua 35%; na d.) Bidhaa ambazo zimebadilika (tarrif heading) ukilinganisha na bidhaa hizo zilipokuwa zinaingia ndani ya Jumuiya kama ilivyoonyeshwa katika jedwali la pili la uasili wa bidhaa.

2005 2006 2007 2008 2009 2010 146 25 20 15 10 5 0 15 15 12 9 6 3 0 20 10 8 6 4 2 0 516 5 4 3 2 1 0 112 3 2 1 0 0 0 54 2 1 0 0 0 0 Year/No. of tariff lines TANZANIA

Na. 1 2 3 4 5 6 7 8

9 10 11 12 13 14 15 Bidhaa Bidhaa za Maziwa (Milk and Cream) Ngano (Wheat and Meslin grain) Unga wa Ngano (Wheat and Meslin Flour) Mahindi Mchele (Rice) Sukari (Cane and Beet sugar) Khanga, Kikoi na Kitenge Mitumba (Worn Clothes) Tumbaku (Cigars/Tobacco) Saruji Viberiti (Matches) Magunia ya Jute (Jute bags) Crown corks Betri (Primary Cells and Primary Batteries) Mashuka ya Pamba Ushuru wa Forodha (%) 60 35 60 50 75 au USD 200 MT 100 or USD 200 MT 50 45 or USD 0.3 per Kg 35 55 (currently removed) 50 45 or USD 45 Cts per bag 40 35 50

Miaka 50 ya uhuru.indd 33 7/23/11 10:02 PM

Page 34

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

34

Ili bidhaa iweze kunufaika na punguzo la ushuru wa forodha cheti cha uasili wa bidhaa huhitajika kama uthibitisho wa kufikia vigezo vilivyokubaliwa vya uasili wa bidhaa. Vyeti hivi hutolewa na Idara za forodha kwa upande wa nchi nne za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Kwa upande wa Tanzania vyeti hivi hutolewa na TCCIA. Aidha, Nchi Wanachama zimeandaa vyeti rahisi vya uasili wa bidhaa (simplified certificates of origin) kwa biashara ndogo ndogo zisizozidi thamani ya kiasi cha Dola za Kimarekani 500. Ili Wafanyabiashara wadogo wasilipe ushuru wa forodha kwa bidhaa zisizozidi kiasi hicho na hivyo kunufaika na fursa za soko huru la bidhaa, wanapaswa kujaza vyeti hivi katika ofisi za TRA mpakani kabla ya kuvuka mpaka. Vyeti hivi rahisi vya uasili hupatikana katika kila ofisi za TRA zilizopo mipakani bila malipo yoyote.

E: Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act 2004)

Tangu mwaka 2005 Mamlaka za usimamizi wa forodha za Nchi Wanachama zimekuwa zikiendesha shughuli za kiforodha katika nchi zao kwa kutumia Sheria moja ya Usimamizi wa Forodha ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004. Aidha sheria hiyo imekuwa ikifanyiwa marekebisho na maboresho kulingana na mahitaji. Faida ya kuwa na sheria moja ya usimamizi wa forodha ni kutoa fursa sawa kwa wafanyabiashara katika kufuata taratibu za kuagiza, kuuza nje bidhaa na ukadiriaji wa viwango vya ushuru kwa bidhaa zote toka ndani na nje ya Jumuiya.

8.2.1.2 Mafanikio ya Utekelezaji wa Umoja wa Forodha A: Uondoaji wa Ushuru wa Forodha

Nchi Wanachama zimeweza kutekeleza ratiba ya uondoaji wa ushuru wa forodha kama ilivyokubaliwa. Kuanzia Januari 2010 bidhaa zote zinazokidhi vigezo vya uasili wa bidhaa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupewa cheti cha uasili wa bidhaa hazitozwi ushuru wa forodha zinapouzwa ndani ya Jumuiya.

B: Kuongezeka kwa Biashara

Kuanzishwa kwa Umoja wa Forodha kumeongeza uhai katika sekta za biashara, uwekezaji na ajira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mwitikio chanya wa Umoja wa Forodha umepelekea utekelezaji wa Umoja wa Forodha wenye mafanikio makubwa katika kuendeleza biashara miongoni mwa Nchi Wanachama. Mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Afrika Mashariki yameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka. Mauzo ya Tanzania katika soko la Jumuiya yaliongezeka kutoka Dola za Kimarekani Milioni 96.4 mwaka 2005 hadi kufikia Dola za Kimarekani milioni 117.7 mwaka 2006, sawa na ongezeko la asilimia 22.1, na kuongezeka tena hadi kufikia Dola za Kimarekani milioni 173.1 mwaka 2007, sawa na ongezeko la asilimia 47.1. Mwaka 2008 mauzo yaliongezeka na kufikia Dola za Kimarekani milioni 315.5, sawa na ongezeko la asilimia 82.2. Katika mwaka 2009, mauzo yaliongezeka na kufikia dola za kimarekani milioni 316.85, sawa na ongezeko la asilimia 0.43 na kuongezeka tena hadi kufikia Dola za Kimarekani milioni 454.29, sawa na ongezeko la asilimia 43.38 (Kiambatanisho Na. 1). Bidhaa ambazo Tanzania inauza kwa wingi katika nchi za Afrika Mashariki ni pamoja na chumvi, vifaa vya umeme, mafuta ya kupikia, nafaka, magunia, sabuni, vifaa vya plastiki,nyama, chuma, nondo na kahawa iliyosindikwa.

C: Kuongezeka kwa Uwekezaji

Utekelezaji wa Umoja wa Forodha unalenga pia kutoa fursa za kuongeza uwekezaji na hivyo ajira kwa watanzania. Miradi iliyowekezwa hapa nchini kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2005 ilikuwa 35 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 39.65. Katika mwaka 2006 kulikuweko na ongezeko la miradi 38 yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 41.06 ambapo mwaka 2007 miradi mipya ilikuwa ni 27 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 50.88. Mwaka 2008 uwekezaji uliongezeka kwa miradi mipya 77 yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 310.35 na uliongezeka tena kwa miradi mipya 42 yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 83.77 katika mwaka 2009. Katika mwaka 2010 kulikuwa na miradi mipya 33 yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 73.66. Sekta zilizoongoza katika uwekezaji ni pamoja na Uzalishaji, Ujenzi, Kilimo, Usafirishaji na Utalii (Kiambatanisho Na. 2).

D: Kuongezeka kwa Ajira

Ongezeko la uwekezaji kutoka katika Nchi Wanachama kulifuatiwa na ongezeko la ajira mpya ambapo mwaka 2006 kulikuwa na ajira mpya 2,643, mwaka 2006 zilikuwa 5,379, mwaka 2007 zilikuwa 2,605, na mwaka 2008 zilikuwa ni 1,424 na ajira mpya mwaka 2009 zilikuwa 1,515 na katika mwaka 2010 ajira ziliongezeka hadi kufikia 4,328. Sekta zilizoongoza katika kuongeza nafasi za ajira ni pamoja na uzalishaji, ujenzi, kilimo, usafirishaji, na utalii (Kiambatanisho Na. 3).

E: Kuwianisha Viwango vya Ubora

Ili kujenga mazingira yaliyo sawa na kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha, Nchi Wanachama zimeandaa Sheria ya Ubora na Viwango ya mwaka 2006. Sheria hii imewianisha taratibu za ukaguzi, viwango, vifaa vya upimaji na ugezi baina ya Nchi Wanachama ili kuwezesha watumiaji

wa sheria hii kutekeleza mfumo unaofanana. Idadi ya bidhaa ambazo viwango vyake vimewianishwa hadi sasa kutokana na sheria hii ni 1500. Hatua hii inaziwezesha pia Nchi Wanachama kuondoa uwezekano wa kutumia viwango kama kikwazo cha kiufundi katika biashaara (Technical Barriers to Trade- TBT).

F: Uondoaji wa Vikwazo Visivyo vya Kiforodha

Eneo jingine ambalo Nchi Wanachama zimeendelea kushirikiana katika Umoja wa Forodha na kupata mafanikio ni Uondoaji wa Vikwazo Visivyo vya Kiforodha. Nchi Wanachama zimekubaliana programu maalum ya kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha katika biashara ya bidhaa. Ili kusimamia programu hii, kila Nchi imeunda kamati ya kitaifa ya kusimamia uondoaji wa vikwazo visivyo vya kiforodha (Elimination of Non-Tariff Barriers). Kamati hizi ni muhimu sana katika kutatua matatizo yatokanayo na Vikwazo Visivyokuwa vya Kiforodha. Kwa upande wa Tanzania fomu maalum zimeandaliwa zinazowezesha kubaini vikwazo katika shughuli za kibiashara. Fomu hizo zinapatikana Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, TCCIA, CTI, TRA na katika vituo vya Forodha vya mipakani. Aidha, wananchi wanaweza kupata fomu hizo katika Tovuti ya Wizara ya Afrika Mashariki. Baada ya kuzijaza wanatakiwa kuziwasilisha Wizarani moja kwa moja au kwa kutumia Tovuti yetu, yaani www.meac.go.tz na pia kwa njia ya posta. Kuwapo kwa chombo hiki kumewawezesha wafanyabiashara na wasafirishaji mizigo nchini kuwasilisha kero wanazokabiliana nazo katika kufanya shughuli zao za kibiashara. Kero zilizowasilishwa zimefuatiliwa, zimejadiliwa na kupatiwa ufumbuzi. Kero hizo ni pamoja na malalamiko ya Ms. Konyagi Tanzania Ltd aliyenyimwa haki ya kupeleka konyagi nchini Kenya, na Kenya kutumia Certificates of Origin za COMESA badala ya zile za Jumuiya ya Afrika Mashariki; unga wa ngano unaozalishwa na Kampuni ya Mikoani Traders Ltd (Azania) kukataliwa kuingia nchini Rwanda na Kenya kwa madai kwamba haukidhi vigezo vya uasili wa bidhaa; tofauti za sheria ya viwango vya uzito wa mizigo inayobebwa

Miaka 50 ya uhuru.indd 34 7/23/11 10:02 PM

Page 35

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

35

na malori (axle load weights) katika ya Nchi nyingine za Jumuiya na Kenya ambapo Kenya inaruhusu uzito wa juu mwisho tani 48 wakati nchi nyingine ikiwemo Tanzania zinaruhusu uzito hadi kufikia tani 56; Nchi ya Kenya kutoza ushuru wa asilimia mbili (2) kwa bidhaa za maua na mimea kinyume na makubaliano ya Umoja wa Forodha; kukataliwa kuingia nchini Kenya kwa maziwa yanayozalishwa na Kampuni ya Musoma Dairy Ltd; kukataliwa kuingia nchini Kenya kwa nyama ya ng'ombe inayozalishwa na Kampuni ya SAAFI Ltd.

8.2.2. Utekelezaji wa Soko la Pamoja

Uanzishwaji wa Soko la Pamoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa mafaniko ya miaka hamishi ya Uhuru katika sekta ya Mtangamano wa kikanda.Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki zimeanza rasmi kutekeleza makubaliano ya kuanzisha Soko la Pamoja kuanzia tarehe 1 Julai 2010. Tarehe 1 Julai, 2010 itakumbukwa katika historia ya mtangamano wa Afrika Mashariki kama siku ambayo Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianza rasmi utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja ambayo ni hatua ya pili na muhimu katika mtangamano wa Afrika Mashariki. Tofauti na Umoja wa Forodha ambao unalenga

kuondoa vikwazo na kuruhusu uhuru wa biashara ya bidhaa miongoni mwa Nchi Wanachama, Soko la Pamoja linatoa uhuru na kuondoa vikwazo katika maeneo yote ya msingi katika uchumi wa Nchi Wanachama. Kwa kuzingatia unyeti wa hatua hii ya mtangamano, Nchi Wanachama zilikubaliana kuunda Soko la Pamoja hatua kwa hatua kulingana na ratiba ya utekelezaji iliyokubalika. Mfumo huu unalenga kuunda Soko la Pamoja imara, endelevu na lenye manufaa kwa Nchi zote Wanachama.

8.2.2.1 Maeneo ya msingi katika Soko la Pamoja

Soko la Pamoja la Afrika Mashariki linalenga kupanua na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii miongoni wa Nchi Wanachama kwa maslahi ya kila Nchi Mwanachama. Ushiriki wa Tanzania katika Soko la Pamoja la Afrika Mashariki unatarajiwa kuwa na manufaa yafuatayo: a) Kuongezeka kwa uzalishaji na biashara kutokana na kuchochewa na fursa nyingi zaidi za kimasoko; b) Kuwepo kwa uhuru wa ajira ndani ya Jumuiya kutawezesha Watanzania wengi kupata fursa za ajira na kuongeza ujuzi na uzoefu kutokana na maingiliano ya kijamii na kiuchumi; c) Soko la Pamoja litachochea uwekezaji kwa vile litaambatana na uwekaji wa sera, sheria na taratibu zinazolenga kukuza na kuendeleza Sekta Binafsi. d) Kuimarika kwa miundombinu ya kiuchumi na kijamii kutokana na utekelezaji wa miradi ya pamoja ya kikanda. Kwa mujibu wa Ibara ndogo za 76(1) na 104(2) za Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki umeainisha maeneo ya msingi yaliyohusishwa katika Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ifuatavyo: a.) Soko Huru la Bidhaa Ndani ya Jumuiya (Free Movement of Goods) b.) Uhuru wa raia wa Afrika Mashariki kusafiri katika Nchi yoyote ndani ya Jumuiya (Free Movement of Persons) c.) Kufanya kazi katika Nchi yoyote ndani ya Jumuiya (Free Movement of Workers) d.) Uhuru wa kufanya Biashara ya Huduma katika Nchi Yoyote Ndani ya Jumuiya (Free Movement of Services) e.) Uhuru wa raia wa Afrika Mashariki kuwekeza mitaji katika Nchi yoyote ndani ya Jumuiya (Free movement of Capaital) f.) Uhuru wa raia wa Afrika Mashariki kuwekeza mitaji katika Nchi yoyote ndani ya Jumuiya (Free movement of Capaital) g.) Haki ya ukazi kwa raia wa Afrika Mashariki katika nchi yoyote ndani ya Jumuiya (Right of Residence)

A: Soko Huru la Bidhaa Ndani ya Jumuiya (Free Movement of Goods)

Soko huru la bidhaa linasimamiwa na Itifaki ya Umoja ya Forodha na Sheria ya Afrika Mashariki ya Usimamizi wa shughuli za Forodha ya mwaka 2004. Utekelezaji wa Umoja wa Forodha ulianza rasmi mwezi January 2005 na kipindi cha mpito cha miaka mitano cha kuondoa Ushuru wa Forodha katika biashara ya bidhaa kwa nchi wanachama kiliisha rasmi tarehe 31 Disemba 2009. Kuanzia tarehe moja January, 2010 biashara ya bidhaa zote zinazozalishwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kukidhi vigezo vya utambuzi wa uasili wa bidhaa zinaweza kusafirishwa kutoka nchi moja hadi nyingine bila kutozwa ushuru wa forodha. Aidha wigo wa pamoja wa ushuru wa forodha hutumika kwa bidhaa kutoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

B: Uhuru wa raia wa Afrika Mashariki kusafiri katika

Nchi yoyote ndani ya Jumuiya (Free Movement of Persons)

Ibara ya 7 ya Itifaki ya Soko la Pamoja la Afrika Mashariki inawahakikishia raia wa Nchi Wanachama uhuru wa kuingia, kutembea na kupata ulinzi na usalama bila kubaguliwa kwa misingi ya utaifa wao. Uhuru huu utawanufaisha raia wa Nchi Wanachama wanaotaka kuingia katika Nchi kutembelea ndugu na jamaa; kutafuta huduma ya matibabu, masomo au kupita kuelekea nchi nyingine. Ili kunufaika na uhuru huu raia mhusika atawajibika kuwa na Hati halali ya kusafiria; na kupita katika vituo rasmi mipakani ambapo baada ya kukamilisha taratibu za uhamiaji kulingana na sheria za Nchi Mwanachama atapewa hati ya kuingia na kukaa nchini kwa kipindi cha miezi sita. Hati hiyo ya kuingia na kukaa nchini itatolewa bila kulipia ada. Hati halali za kusafiria zilizokubalika katika ngazi ya Jumuiya ni pasipoti za Nchi Wanachama, pasipoti za Afrika Mashariki na hati za Muda za Kusafiria za Nchi Wanachama.Hata hivyo, vifungu vya 9(2) na 9(3) vya Itifaki vinaruhusu nchi zilizo tayari kutumia vitambulisho vya uraia vinavyosomeka kwa mashine kama hati ya kusafiria kufanya hivyo kwa makubaliano maalum baina yao bila kulazimisha Nchi yoyote kutumia utaratibu huo. Wanafunzi watatakiwa kuonyesha uthibitsho wa kukubaliwa katika shule, vyuo au taasisi za elimu zilizosajiliwa rasmi, na uthibitisho wa ufadhili kwa kipindi cha masomo yao. Wanafunzi wanaotimiza masharti hayo watapewa hati ya kuingia na kukaa nchini kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja. Hati hiyo itakuwa ikiongezwa muda kwa kipindi cha mwaka mmoja mmoja hadi kukamilisha kipindi cha masomo. Hati ya mwanafunzi ya kuingia na kukaa nchini itatolewa bila kulipia ada. Uhuru huu wa kuingia, kutembea na kukaa katika Nchi Wanachama unaweza kukataliwa au kusitishwa kwa sababu za Kisera; Kiusalama au Kiafya za Nchi husika. Aidha raia aliyeingia katika Nchi nyingine Wanachama kwa njia hii hataruhusiwa kuajiriwa au kujishughulisha na shughuli za kiuchumi na biashara katika nchi husika.

C: Uhuru wa raia wa Afrika Mashariki kufanya kazi katika Nchi yoyote ndani ya Jumuiya (Free Movement of Workers)

Ibara ya 10 ya Itifaki ya Soko la Pamoja inawahakikishia raia wa Nchi Wanachama uhuru wa kupata ajira katika Nchi yoyote Mwanachama na kutobaguliwa kwa misingi ya utaifa katika masuala ya ajira, maslahi na haki nyingine za wafanyakazi. Mfanyakazi ataruhusiwa kuambatana na mke/mume na watoto ambao pia watanufaika na uhuru wa kuajiriwa au kujiajiri. Uhuru huu unalenga kutoa nafasi za ajira kwa raia wa Nchi Wanachama. Watanzania watanufaika kwa kupata ajira katika Nchi Wanachama na hivyo kupunguza tatizo la ajira. Ili kunufaika na uhuru huu, mfanyakazi atawajibika kuwa na Hati halali ya kusafiria; Mkataba wa ajira, na kupita katika vituo rasmi mipakani

Miaka 50 ya uhuru.indd 35 7/23/11 10:02 PM

Page 36

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

36

ambapo baada ya kukamilisha taratibu za uhamiaji kulingana na sheria za Nchi Mwanachama atapewa hati ya kuingia na kukaa nchini kwa kipindi cha miezi sita wakati akikamilisha taratibu za kupata kibali cha kufanya kazi (Work Permit) kwa kazi inayozidi siku 90 au hati maalum

(Special Pass) kwa kazi isiyozidi siku 90. Aidha mume/mke na watoto wa mfanyakazi watapaswa kukamilisha taratibu za kupata hati ya utegemezi (Dependant Pass). Kwa kuzingatia mfumo uliokubalika wa kuunda Soko la Pamoja hatua kwa hatua kulingana na ratiba zilizokubalika, kila Nchi Mwanachama imeainisha kada zitakazohusishwa na ufunguaji wa Soko la ajira. Raia wa Nchi Wanachama wataruhusiwa kutafuta ajira katika maeneo hayo yaliyofunguliwa.

D: Uhuru wa kufanya Biashara ya Huduma katika Nchi Yoyote Ndani ya Jumuiya (Free Movement of Services)

Ibara ya 16 ya Itifaki ya soko la Pamoja inahakikisha uhuru wa soko la biashara ya huduma ndani ya Jumuiya kwa kuondoa vikwazo hatua kwa hatua na kutoanzisha vikwazo vipya kwa watoa huduma kutoka katika Nchi wanachama. Aidha, Nchi Wanachama zimekubaliana kutowabagua wafanyabiashara ya huduma kwa msingi wa utaifa. Hatua hii inatoa fursa kwa watanzania na raia wengine wa Afrika Mashariki kuanzisha biashara ya huduma katika Nchi yoyote Mwanachama kwenye sekta za biashara za huduma zilizofunguliwa. Kwa kuanzia Nchi wanachama zimekubaliana kuondoa vikwazo katika sekta saba za huduma zilizoanishwa katika jedwali la uhuru wa biashara ya huduma kama ifuatavyo: (i) Sekta ya Huduma za Biashara (ii) Sekta ya Huduma za Mawasiliano; (iii) Sekta ya Huduma za Ugavi; (iv) Sekta ya Huduma za Elimu; (v) Sekta ya Huduma za Fedha; (vi) Sekta ya Huduma za Utalii; (vii) Sekta ya Huduma za Usafiri

E: Uhuru wa raia wa Afrika Mashariki kuwekeza mitaji katika Nchi yoyote ndani ya Jumuiya (Free movement of Capaital)

Nchi Wanachama zimekubaliana kuondoa vikwazo kwa raia wa Afrika Mashariki kuwekeza kwenye soko la mitaji katika nchi nyingine ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hatua kwa hatua kwa mujibu wa ratiba ya utekelezaji inayooneshwa katika Jedwali la kuondoleana vikwazo katika uwekezaji wa mitaji. Katika jedwali husika kila Nchi Mwanachama imeainisha vikwazo vilivyopo katika soko lake la mitaji na ratiba ya kuviondoa vikwazo hivyo ili hatimaye soko la mitaji liwe huru kwa wawekezaji kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

F: Haki ya Raia wa Afrika Mashariki Kuanzisha na Kuendesha Shughuli za Biashara na Uchumi Katika Nchi Yoyote Ndani ya Jumuiya (Right of Establishment)

Ibara ya 13 ya Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki inawahakikishia raia wa Afrika Mashariki haki ya kuanzisha na kuendesha shughuli za biashara na uchumi katika Nchi yoyote Mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuondoa vikwazo vinavyohusiana na utaifa wa Kampuni au mjasiriamali husika. Aidha Nchi Wanachama zimekubaliana kuandaa orodha ya vikwazo katika sheria zao na kuviwasilisha katika Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya Itifaki ya Soko la Pamoja kupata nguvu ya kisheria. Ibara ya 15 ya Itifaki inabainisha wazi kuwa suala la upatikanaji na matumizi ya Ardhi na majengo ndani ya Nchi Mwanachama litasimamiwa kwa mujibu wa sheria za Nchi husika.

G: Haki ya ukazi kwa raia wa Afrika Mashariki katika nchi yoyote ndani ya Jumuiya (Right of Residence)

Ibara ya 14 ya Itifaki ya Soko la Pamoja inawahakikishia raia wa Nchi Wanachama walioruhusiwa kuingia katika nchi nyingine kwa ajili ya ajira kwa mujibu wa ibara ya 10 ya Itifaki hii au kwa ajili ya kuanzisha shughuli za biashara na uchumi kwa mujibu wa ibara ya 13 ya itifaki hii, haki ya ukazi katika nchi husika. Raia anayetaka kukaa nchini anatakiwa kuomba kwa mamlaka husika kibali cha ukazi (Residence Permit) ndani ya siku 30 tangu tarehe ya kuingia nchini akiambatanisha hati halali ya kusafiria, kibali cha kufanya kazi nchini na nyaraka nyingine zitakazihitajika na ofisi za uhamiaji. Aidha, Nchi wanachama zimekubaliana kuwa suala la ukazi wa kudumu (Permanent Residence) litaendelea kusimamiwa kwa mujibu wa sheria husika za Nchi Wanachama. Baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki zina sheria hiyo ya ukazi wa kudumu. Kwa hivi sasa Tanzania haina sheria ya ukazi wa kudumu. Utekelezaji wa maeneo ya msingi yaliyoainishwa katika taarifa hii hauzuii Nchi Mwanachama kuchukua hatua za kujihami pale itakapotokea athari katika utekelezaji kijamii, kiusalama na kiafya. Aidha Nchi Mwanachama inaweza ikachukua hatua za kujihami kudhibiti matokeo yoyote hasi katika utekelezaji. (Kifungu cha 78 na 88). Maeneo yaliyofunguliwa na Nchi Wanachama katika utekelezaji wa Soko la Pamoja yanafungua fursa kwa Watanzania katika soko la bidhaa, soko la biashara ya huduma, fursa za kuanzisha shughuli za kiuchumi, fursa za ajira na fursa katika soko la mtaji. Maelezo ya kina kuhusu maeneo yaliyofunguliwa mpaka sasa ni kama yanavyoonekana katika Kiambatanisho Na. 2.

8.2.3 Umoja wa Fedha

Umoja wa Fedha ni hatua ya tatu katika Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Madhumuni makuu ya hatua hii ni kujenga ukanda tulivu wa kifedha katika Jumuiya (Monetary and Financial Stability Zone) utakaochangia katika ukuaji wa biashara na shughuli nyingine za kiuchumi. Nchi Wanachama zimeanza majadiliano ya kuanzisha Umoja wa Fedha, ambapo hatua madhubuti zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na chambuzi/tathmini za kupima utayari wa Tanzania kuingia katika Umoja wa Fedha ili kuhakikisha kuwa Umoja wa Fedha wa Jumuiya utakaoundwa unazingatia maslahi ya Tanzania na Jumuiya. Katika hatua hii Nchi Wanachama hukubaliana: a.) Kuwa na sera moja ya fedha (single monetary policy); b.) Kuwa na sera moja ya viwango vya ubadilishanaji fedha za kigeni (exchange rate policy); c.) Kuunda Benki Kuu moja ya Jumuiya; d.) Kuanzisha sarafu moja ya Jumuiya; e.) Kuongeza kiwango na kasi ya kiwango cha mtangamano wa masoko ya fedha na mitaji (deepen financial market integration); f.) Kuwa na kanuni moja/zinazoshabihiana za kusimamia sekta ya fedha; na g.) Kuweka utaratibu wa kuendesha shughuli za uchumi bila kukinzana na malengo ya Umoja wa Fedha.

8.2.4 Shirikisho la Kisiasa

Shirikisho la Kisiasa ni hatua ya nne katika mtangamano ambayo inategemea sana misingi imara itokanayo na utekelezaji wa hatua za mwanzo za mtangamano. Mwaka 2006 Nchi Wanachama zilikusanya maoni kutoka kwa wananchi juu ya kuharakisha au kutoharakisha uundwaji wa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki. Matokeo ya

mchakato huo yaliwasilishwa katika mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama (Summit) uliofanyika Agosti 2007. Nchi za Uganda na

Miaka 50 ya uhuru.indd 36 7/23/11 10:02 PM

Page 37

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

37

Kenya ziliunga mkono uharakishaji wakati wananchi wa Tanzania walipinga hoja ya kuharakisha uanzishwaji wa Shirikisho la Kisiasa, na kuunga mkono utekelezaji wa mtangamano hatua kwa hatua. Asilimia 75.9 ya Watanzania walipinga uharakishwaji wa kuanzishwa Shirikisho la Kisiasa, wakati asilimia 64.9 ya wananchi wa Kenya waliunga mkono, na asilimia 56.3 ya wananchi wa Uganda waliounga mkono uharakishwaji wa Shirikisho la Kisiasa. Kwa kuwa Nchi za Rwanda na Burundi zilikuwa ngeni katika Jumuiya na hivyo hazikushiriki katika mchakato huo, Wakuu wa Nchi Wanachama waliziagiza kufanya mchakato huo. Nchi hizo zilikamilisha mchakato na kuwasilisha ripoti katika Mkutano wa 11 wa Wakuu wa Nchi uliofanyika Novemba, 2009. Nchi hizo mbili ziliunga mkono uharakishwaji wa uundwaji wa shirikisho la kisiasa. Ili kuhakikisha kuwa mawazo ya wananchi, hususan wananchi wa Tanzania waliopinga uharakishwaji wa shirikisho la kisiasa yanazingatiwa, Wakuu wa Nchi Wanachama wameliagiza Baraza la Mawaziri la Jumuiya kuunda timu ya wataalamu kufanya uchambuzi wa kero na hofu zilizoainishwa na wananchi wakati wa mchakato wa kukusanya maoni na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana nazo. Kukubaliana kufanya uchambuzi wa kero, hofu na changamoto na kupendekeza jinsi ya kukubaliana nazo ni miongoni mwa mafanikio ya ushirikiano katika Jumuiya, kwani ni ishara ya dhamira ya kweli miongoni mwa Nchi Wanachama kuendeleza mtangamano na kwa kuwasikiliza wananchi wake.

8.2.5 Uimarishaji wa Sekta Binafsi

Katika miaka hamsini tangu Tanzania ipate uhuru, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki imechangia katika uendelezaji wa Sekta Binafsi kwa lengo kuiwezesha kutumia fursa zitokanazo na mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wizara imekuwa ikiandaa ziara za wafanyabiashara wa Tanzania kutembelea na kukutana na wafanyabiashara wa Afrika Mashariki na pia kuwashirikisha katika maonesho ya kibiashara ya Jua Kali/ Nguvu Kazi. Lengo la ziara hizo ni kuwapa fursa wafanyabiashara kupata masoko ya bidhaa wanazozalisha katika Nchi Wanachama na kukutana na wafanyabiashara wa nchi hizo ili kukuza ushirikiano wa kibiashara miongoni mwao. Ziara hizo zimepata mafanikio ikiwa ni pamoja na kupata Soko la Bidahaa na fursa nyingine za kibiashara zilizopo katika Nchi za Afrika Mashariki. Aidha wafanyabiashara wameunda umoja wao wa kibiashara unaoitwa Friends of East Africa. Umoja huo una lengo la kubadilishana taarifa za kibiashara, uzoefu na mbinu za kufanya biashara katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika ziara hizo, Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) ikiwa mwakilishi wa vyama vya sekta binafsi nchini ilifanikiwa kusaini hati za makubaliano (Memorandum of Understanding) na vyama vya sekta binafsi vya nchi zilizotembelewa na ujumbe wa Tanzania. Makubaliano hayo yalilenga zaidi kuboresha ushirikiano katika shughuli mbalimbali za kuendeleza biashara na uwekezaji miongoni wa wanachama wao.

Wafanyabiashara wa Tanzania walipata fursa ya kukutana ana kwa ana na wafanyabiashara wa nchi zilizotembelewa na kufanikiwa kujenga uhusiano wa kibiashara; ambapo wanaendelea kuwasiliana na kufanya biashara. Wizara inaandaa utaratibu wa kupata mrejesho kutoka kwa wafanyabishara waliohudhuria ziara ili kupina mafanikio yanayopatikana kutokana na ziara hizo katika biashara na kubuni utaratibu wa kuboresha ziara hizo. Aidha, Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umeainisha kuwa sekta binafsi ni miongoni mwa mihimili mikuu ya kuendeleza ushirikiano katika Jumuiya. Kwa kuwa sekta binafsi bado ni changa, Nchi Wanachama zimejiwekea utaratibu wa kuandaa maonyesho ya kikanda ya sekta isiyo rasmi kila mwaka, maarufu kama Maonyesho ya Jua Kali/ Nguvu Kazi. Madhumuni ya maonyesho haya ni kujenga sekta isiyo rasmi ili hatimaye ikue na kufikia ngazi ya sekta rasmi. Maonyesho ya Jua Kali/Nguvu Kazi yametoa fursa kwa wajasiriamali wa Tanzania kukutana na kubadilishana mawazo na uzoefu juu ya kukuza na kuendeleza biashara zao, kujifunza teknolojia mpya na kuanzisha uhusiano wa kibiashara.

8.2.6 Ushirikiano baina ya Jumuiya (EAC) na Kanda nyingine 8.2.6.1 Utatu wa EAC-COMESA-SADC (EAC-COMESASADC Tripate Arrangement)

Katika jitihada za kupanua wigo wa kikanda, hususan, baina ya kanda za kiuchumi za Afrika Mashariki (East African Community - EAC), Kusini mwa Afrika (Southern Africa Development Community -SADC) na Mashariki na Kati (Common Market for Eastern and Southern Africa - COMESA) Viongozi Wakuu wa Jumuiya hizo katika Mkutano wao wa tarehe 20 Oktoba, 2008 uliofanyika Kampala, Uganda walikubaliana kuanza mchakato wa kuanzisha Eneo Huru la Biashara, na hatimaye Umoja wa Forodha wa Nchi Wanachama za EAC-COMESA-SADC. Nchi Wanachama wa EAC-COMESA-SADC zinakamilisha maandalizi ya ratiba ya utekelezaji (roadmap) wa Eneo hilo Huru la Biashara, na mfumo wa kitasisi. Kuundwa kwa Eneo huru la Kibiashara la Nchi Wanachama wa EACCOMESA-SADC kutasaidia kupunguza gharama za kufanya biashara kwa kuwianisha taratibu za kiforodha, viwango vya ushuru wa forodha na kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTB). Aidha Utatu huu utaongeza soko la Bidhaa za Kilimo na Viwanda, ajira na kuinua kipato cha wananchi na pato la Taifa kwa ujumla. Soko la COMESA-EAC-SADC likajumuisha Nchi mbazo ni: Angola, Botswana, Burundi, Comoros, Democratic Republic of Congo, Djibouti, Egypt, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Libya, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Rwanda, Seychelles, South Africa, Sudan, Swaziland, Tanzania, Uganda, Zambia, na Zimbabwe.

8.2.6.2 Ubia wa Kiuchumi kati ya Jumuiya ya Afrika Mashairiki na Jumuiya ya Ulaya

Katika miaka Hamsini ya Uhuru, Nchi Wanachama ikiwa ni pamoja na Tanzania, zimefanikiwa kuendeleza unafuu wa kodi uliyokuwa ukitolewa na Jumuiya ya Ulaya kupitia makubaliano mbalimbali ya ushirikiano wa kibiashara. Kwa sasa Nchi Wanachama zinaendelea na majadiliano ya Mkataba wa Ubia wa kiuchumi (Economic Partnership Agreement - EPA) kati ya nchi za kundi la Afrika, Caribean na Pasifiki (ACP) na Jumuiya ya Ulaya (EC). Majadiliano yalianza mwaka 2002 ikiwa ni majadiliano ya jumla. Majadiliano haya yaliingia sehemu ya pili mwaka 2003 ambapo nchi za ACP zilijigawa kwenye makundi ambayo ziliona yanafaa.

Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuzingatia maagizo ya Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2002 kwamba zimefanikiwa kuendelea na majadiliano kama kundi moja katika masuala ya WTO na EU/ACP, na kuweka alama ya awali ya makubaliano (initialing) ya Mkataba wa Mpito wa Ubia wa Uchumi (Framework for Economic Partnership Agreement ­ FEPA) tarehe 27 Novemba 2007. Katika mkataba wa mpito nchi za EAC ziliainisha kufungua masoko yake kwa bidhaa za Jumuiya ya Ulaya kwa asilimia 82.6 kuanzia mwaka 2010 hadi 2032, na kuweka asilimia 17.4 kwenye orodha ya bidhaa nyeti. Jumuiya ya Ulaya kwa upande wake ilifungua soko lake kwa bidhaa kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa asilimia 100 (Duty Free Quota Free ­ DFQF). Aidha mkataba huu wa mpito uliainisha katika ibara ya 37 maeneo ya kuendelea na majadiliano ili kufikia mkataba kamili. Majadilino ya Ubia wa Kiuchumi baina ya EAC na EC yameendelea na kukamilika katika maeneo mengi kama Ushuru wa Forodha, Viwango vya Afya ya Binadamu, Wanyama na Mimea, Vikwazo vya Kiufundi vya Biashara, Ushirikiano wa Forodha na Uwezeshaji wa Biashara. Majadiliano yanaendelea katika maeneo yaliyosalia.

Miaka 50 ya uhuru.indd 37 7/23/11 10:02 PM

Page 38

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

38

8.3 Mafanikio Katika Utekelezaji wa Miradi na Programu za Kikanda 8.3.1 Uendelezaji wa Miundombinu

Uendelezaji wa miundombinu ni miongoni mwa mafanikio ya miaka hamsini ya uhuru kutokana na ushiriki wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kubuniwa mipango kabambe na mikakati ya uendelezaji miundombinu, hususan barabara, reli, usafirishaji na umeme. Jumuiya imebuni na inaendelea kutekeleza mipango kabambe ifuatavyo: a) Mpango Kabambe wa kuendeleza Mtandao wa Barabara katika Jumuiya (The East African Road Network Project); b) Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Reli ya Afrika Mashariki (The EAC Railways Development Masterplan); c) Mpango Kabambe wa Upatikanaji wa Nishati ya Umeme katika Jumuiya (EAC Power Master Plan); na d) Usafirishaji wa Mawasiliano. Maelezo mafupi na mafanikio ya utekelezaji wa miradi na mipango hii ni kama ilivyoainishwa katika aya zifuatazo:

8.3.2 Uendelezaji wa Barabara

Mpango Kabambe wa kuendeleza Mtandao wa Barabara katika Jumuiya (The East African Road Network Project) unaojumuisha kanda (corridor) tano. Kanda hizo ni: a.) Kanda ya kwanza (Corridor 1): Mombasa - Malaba - Katuna - Kigali-Kanyaru Haut-Bujumbura-Gatumba ikijumuisha Marangu ­Tarakea, Chalinze ­ Segera na Segera ­ Himo; b.) Kanda ya pili (Corridor 2): Dar-es-salaam-IsakaLusahunga-Mutukula-Masaka, na Lusahunga-Nyakasanza-Rusumo -Kigali-Gisenyi; c.) Kanda ya tatu (Corridor 3): Biharamulo - Mwanza Musoma - Sirari - Lodwar ­ Lokichogio ambayo pia ni sehemu ya mtandao wa barabara katika ukanda wa Ziwa Victoria (Lake

Victoria Road Circuit); d.) Kanda ya Nne (Corridor 4): Tunduma - Sumbawanga - Kigoma ­ Manyovu (Mugina) ­ Rumonge ­ Bujumbura ­ Ruhwa (Bugarama) ­ Karongi ­ Gisenyi; na e.) Kanda ya Tano (Corridor 5): Tunduma - Iringa ­ Dodoma - Arusha - Namanga ­ Moyale. Utekelezaji wa ujenzi wa mtandao wa barabara wa Jumuiya katika kanda hizo tano umefikia hatua mbali mbali kama ifuatavyo:

Arusha ­ Namanga ­ Athi River

Ujenzi wa barabara ya Arusha ­ Namanga ­ Arthi River yenye urefu wa Kilomita 104.4 kwa upande wa Tanzania na kilomita 136 upande wa Kenya unaendelea vizuri. Kasi ya ujenzi wa barabara hii iliongezeka ambapo hadi kufikia Desemba 2010, Kilometa 87 zilikuwa zimewekwa lami. Aidha, ujenzi ulifikia asilimia 63 ya kazi zote za ujenzi wa mradi.

Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina (Feasibility Studies and Detailed Design) wa Barabara ya Arusha ­ Holili/Taveta - Voi

Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Arusha ­ Holili ­ Voi yenye urefu wa kilomita 118 upande wa Tanzania unaendelea ambapo Mshauri Mwelekezi alianza kazi mwezi Septemba 2009 na anatarajiwa kumaliza kazi hiyo mwezi Aprili, 2011. Mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kilomita 110 upande wa Kenya yanaendelea sambamba na upande wa Tanzania.

Barabara ya Malindi ­ Lunga Lunga na Tanga ­ Bagamoyo

Kampuni ya M/s Aurecon ya Afrika Kusini ilisaini Mkataba wa kufanya kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara hii mapema Mwezi Desemba 2010. Kazi hii imeanza kutekelezwa mwezi Februari, 2011.

Barabara ya Tanga ­ Horohoro

Kufikia mwezi Desemba, 2010 Mkandarasi ameendelea na kazi ya ujenzi wa barabara hii yenye urefu wa kilomita 66 kutoka Horohoro mpaka wa Tanzania na Kenya hadi Tanga mjini ambayo imepata ufadhili kupitia mradi wa Millenium Challenge Corporation. Ujenzi huo bado upo katika hatua za awali za uchimbaji na usawazishaji eneo la ujenzi ambapo kilomita 15 zimekamilika.

Mtandao wa Barabara wa Afrika Mashariki 8.3.3 Uendelezaji wa Reli Sekta ya Reli

Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekamilisha maandalizi ya Mpango kabambe wa Maendeleo ya Reli wa Afrika Mashariki (The EAC Railways Development Masterplan) uliodhinihwa mwaka 2009. Mtandao huu kwa upande wa Tanzania umeainisha njia zifuatazo: a.) Liganga - Mchuchuma - Mtwara; b.) Mchuchuma - Mbambabay; c.) Liganga - Mlimba; Dar es Salaam - Mtwara; d.) Isaka - Kigali - Kabanga; e.) Keza ­ Ruvubu ­ Gitega ­ Musongati; f.) Isaka - Kigali - Biharamulo - Bukoba - Masaka; g.) Tunduma- Sumbawanga- Mpanda - Kigoma; h.) Uvinza ­ Bujumbura; i.) Mbegani (Bagamoyo) Port ­ Kidomole; na j.) Tanga - Arusha ­ Musoma.

Miaka 50 ya uhuru.indd 38 7/23/11 10:02 PM

Page 39

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

39

Katika kutekeleza Mpango Kabambe wa reli, majadiliano kuhusu kuunganisha reli kati ya Dar es Salaam na Isaka, na ujenzi wa reli ya Isaka-Kigali/Keza ­ Gitega ­ Musongati unaolenga kuziunganisha nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi na DRC na kuendeleza matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam yamekamilika. Aidha, kazi ya upembuzi yakinifu ilikamilika mwaka 2009 kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika iliogharimu kiasi cha Dola za Marekani 12 milioni. Ujenzi wa reli hiyo yenye jumla ya Kilometa 1,651 unaokisiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 5.1, utahusisha ujenzi wa reli mpya na ya kisasa kuanzia Isaka- Kigali/Keza hadi Musongati yenye urefu wa Kilometa 681 na ujenzi wa reli kutoka Isaka hadi Dar es Salaam yenye urefu wa Kilometa 970. Reli ya Isaka- Kigali/Keza hadi Musongati inakisiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 2.63 na ujenzi wa reli kutoka Isaka hadi Dar es Salaam kupitia Bandari ya Bagamoyo utagharimu Dola za Marekani bilioni 2.47. Aidha, Serikali za Tanzania na Uganda zimekubaliana kushirikiana kujenga reli ya Tanga ­ Arusha- Musoma ­ Port Bell/New Kampala. Hati ya makubaliano (Memorandum of Understanding - MOU) ya ushirikiano wa ujenzi wa reli hiyo kati ya Tanzania na Uganda umekamilika. Serikali hizi mbili zinashirikiana katika kutafuta fedha za kutekeleza mradi huu.

8.3.4 Uendelezaji wa Sekta ya Nishati

Mpango kamambe wa upatikanaji wa Nishati ya Umeme katika Jumuiya (EAC Power Master Plan) unalenga kuimarisha uwezo wa Nchi wanachama kuzalisha na kusambaza umeme kwenye Kanda ya Afrika Mashariki. Pamoja na mambo mengine, mpango huu nakusudia kuipatia umeme miji ya mipakani kupitia umeme unaozalishwa katika Nchi Wanachama (crossborder electrification). Utekelezaji wa mpango huu umeanza kwa kuipatia umeme miji ya Lungalunga nchini Kenya kutoka mji wa Horohoro nchini Tanzania, na mji wa Namanga nchini Tanzania umepatiwa umeme kutoka mji wa Namanga (Kenya). Aidha, Mkoa wa Kagera unapata umeme kutoka Uganda na upembuzi yakinifu kwa ajili ya mradi wa kuupatia umeme mji wa Mutukula nchini Tanzania kutoka mji wa Mutukula nchini Uganda umekamilika. Aidha, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki inaendelea na mazungumzo kati yake na Serikali ya Uganda kuhusu mradi wa kuzalisha umeme wa Murongo/Kikagati (mpakani mwa Uganda na Tanzania) kwa lengo la kuwezesha uwekezaji unaotarajiwa kuzalisha umeme wenye msongo wa 16MW. Mradi huu utakapokamika utawezesha kuipatia umeme miji ya Murongo na maeneo mengine Wilayani Karagwe. Ili kukabiliana na upungufu wa nishati ya umeme, Nchi za EAC na SADC zimekubaliana kuanzisha mpango wa kuunganisha umeme ambao unalenga kuunganisha mifumo ya kitaifa ya umeme ujulikanao kwa jina la Southern Africa Power Pool. Kwa kuanzia mpango huu utaunganisha nchi za Zambia, Tanzania, na Kenya ambapo Tanzania itapokea umeme wenye msongo wa 400 KV kutoka mji wa Pensulo nchini Zambia. Umeme utapita katika miji ya Mbeya, Iringa, Dodoma, Singida, Arusha na hatimaye mji wa Nairobi nchini Kenya. Mradi huu ni wa miaka saba (2010/2011 ­ 2016/2017) ambapo Tanzania itachangia Dola za Marekani Milioni 309.1 kati ya Dola za Marekani Milioni 860 zinazohitajika kutekeleza mradi huu.

8.3.5 Sekta ya Usafiri wa Anga

Nchi Wanachama zimeendelea kujipanga katika kuimarisha usafiri wa anga. Miongoni mwa mafanikio yaliypatikana ni kuanzishwa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Anga katika Jumuiya (East Africa Civil Aviation Safety and Security Oversight Agency - CASSOA) ambao umeimarisha hali ya usalama wa usafiri wa anga hivyo kujenga misingi imara ya kuvutia uwekezaji katika sekta ya anga. Tangu kuanzishwa kwa chombo hiki mwaka 2007 masuala yafuatayo yametekelezwa: d.) Uboreshaji wa usalama wa anga kulingana na viwango vilivyowekwa na Shirika la Kimataifa linalosimamia usafiri na usalama wa anga (ICAO); e.) Kuandaa na kutumia Kanuni zilizowianishwa na Kanuni za usalama wa anga za Kimataifa (East Africa Harmonized Safety and Security Aviation Regulations) ambazo zinatambulika na ICAO; a.) Kuanzishwa kwa mpango wa mafunzo ya pamoja ya marubani na waongoza ndege katika nchi wanachama ili kuendana na mabadiliko yanayotokea katika sekta ya usafiri wa anga duniani na hivyo kutoa leseni ya urubani ya Afrika Mashariki; b.) Kupitia CASSOA Jumuiya imefanya utafiti unaolenga kubainisha mfumo wa kuratibu na kusimamia masuala ya usalama wa Anga ya Juu kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Upper Flight Information Regional Project); na

Miaka 50 ya uhuru.indd 39 7/23/11 10:02 PM

Page 40

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

40

c.) Kupitia CASSOA Jumuiya imeanzisha mfumo rahisi wa mawasiliano ya Anga (Cheaper Navigation System) utakaotumia mfumo wa Global Navigation Satellite System (GNSS). Mfumo huu utapunguza gharama za mawasiliano ya anga. Aidha, Nchi Wanachama zimeanzisha mpango kabambe wa miaka kumi wa kuendeleza viwanja vya ndege vilivyopewa kipaumbele katika Jumuiya ili viwe vituo vya Kimataifa na Kikanda vya kuingilia na kutokea kwenye vivutio vya utalii kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa mtandao wa utalii katika Jumuiya. Viwanja vya ndege vitakavyohusika katika mpango huu ni Arusha, Ziwa Manyara, Kigoma, Mafia, Kilwa Masoko na Loliondo.

8.3.6 Sekta ya Usafiri wa Majini

Ushirikiano wa kikanda katika Jumuiya ya Afika Mashariki umechangia katika uimarishaji wa usalama na uokoji wa wavuvi na wasafiri katika maeneo ya Maziwa. Katika eneo hili, Tanzania imenufaika kwa Makao Makuu ya Taasisi ya Uratibu wa Usalama na Uokozi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Inland Waterways Maritime Search and Rescue Coordination Centre ­ MRCC) kuwa mjini Mwanza.

8.3.7 Kuanzisha Vituo vya Pamoja vya Utoaji Huduma Mipakani (One Stop Border Posts - OSBPs)

Nchi Wanachama zimekubaliana kuanzisha vituo vya pamoja vya mipakani (One Stop Boarder Posts OSBP). Uanzishaji wa vituo hivi unalenga kurahisisha taratibu za uhamiaji na forodha kwa kutoa huduma hizi upande mmoja wa mpaka bila kulazimika kupitia taratibu kama hizi upande wa pili wa mpaka. Hatua hii inawezesha biashara na usafirishaji shehena kufanyika kwa urahisi na gharama nafuu baina ya Nchi

Wanachama. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda zimekubaliana kuanzisha Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani Rusumo (Billateral Agreement on Establishment of One Stop Border Post-Rusumo). Uanzishwaji wa kituo hicho unakwenda sambamba na ujenzi wa daraja la Rusumo ambalo ni kiungo muhimu kati ya Tanzania na Rwanda. Serikali ya Japan kwa kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan ­ JICA litagharamia ujenzi wa kituo na Daraja la Rusumo. Maandalizi ya uanzishwaji wa vituo vingine vya pamoja vya mpakani yanaendelea ili kuanzisha vituo Namanga, Horohoro/ Lungalunga, Sirali/Isebania, Mutukula na Holili/Taveta.

8.3.8 Miradi ya Zanzibar

Mkakati wa Maendeleo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa mwaka 2006 ­ 2010 unajumuisha miradi ifuatayo toka Tanzania Zanzibar: a) Uwanja wa Ndege wa Karume; b) Ujenzi wa Bandari ya Maruhubi; na c) Ujenzi wa Cherezo (Dry dock construction na Roll On ­ Roll Off (RORO) kati ya Bandari za Zanzibar, Dar es Salaam na Mombasa. Baraza la Mawaziri wa Kisekta ya Usafirishaji, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) limekwishaidhinisha miradi hii kuwa miongoni mwa miradi inayotafutiwa fedha katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Jumuiya inaendelea na majadiliano na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu ufadhili wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Karume. Aidha, mradi wa Bandari ya Maruhubi ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele katika Mikakati ya usafiri wa Jumuiya (EAC Trasport Strategy). Mradi wa Ujenzi wa Cherezo (Dry dock construction na Roll on ­ Roll Off (RORO) kati ya Bandari za Zanzibar, Dar es Salaam na Mombasa ni miongoni mwa vipaumbele katika Ushirikiano wa Utatu wa Kikanda (Tripartite COMESA-EAC-SADC).

8.3.9 Uendelezaji wa Sekta ya Kilimo

Katika kuhimiza maendeleo ya Sekta ya Kilimo kwa lengo la kukuza biashara ya bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Tanzania ilifanikiwa kuzishawishi nchi nyingine wanachama kuiweka sekta ya kilimo katika vipaumbele vya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tayari Nchi Wanachama zimeandaa Mpango Maalum wa Kilimo na Usalama wa Chakula. Aidha majadiliano ya uanzishaji wa Itifaki ya Afya ya Wanyama na Mimea (SPS Protocol) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanaendelea vizuri. Itifaki hiyo itakapokamilika itawezesha kuhuisha viwango na kurahisisha biashara miongoni mwa Nchi Wanachama na nje ya Jumuiya kwa vile bidhaa kutoka Afrika Mashariki zikuwa na viwango vya kimataifa na ushindani katika soko la kimataifa. Vile vile, Jumuiya ya Afrika Mashariki imejiwekea utaratibu wa pamajo wa kupambana na maradhi ya mimea na mifugo na hivyo kuongeza ubora wa bidhaa za kilimo kutoka katika Jumuiya.

8.3.10 Uendelezaji wa Miradi na Programu za Huduma za Jamii 8.3.10.1 Sekta ya Elimu

Katika Sekta ya Elimu, Tanzania imeendelea kushirikiana na Nchi Wanachama na kupata mafanikio katika maeneo yafuatayo: a.) Uwianishaji wa Mifumo ya Elimu na Mitaala katika Nchi Wanachama (Harmonization of Education System and Training Curricula). Uwianishaji wa Mifumo na mitaala ya elimu utasaidia katika utekelezaji wa hatua ya mtangamano katika Soko la Pamoja kwa maana ya kuwawezesha Watanzania na Wanaafrika Mashariki kupata ajira katika Nchi Wanachama kwa urahisi;

b.) Mchakato wa kutambua Taasisi za Elimu zilizobobea (Centres of Exellence) kwa lengo la kuzifanya kuwa Taasisi za Utoaji Elimu/ Utafiti katika Jumuiya kwenye maeneo husika; Tanzania hadi sasa imewasilisha taasisi 17 zitakazoshirikishwa katika utambuzi wa Taasisi za Elimu zilizobobea katika Jumuiya. Utambuzi wa Taasisi zilizobobea unasaidia kuokoa raslimali za kanda kwa Taasisi zilizotambuliwa kutumika katika kutoa elimu na kufanya utafiti na Wanajumuiya wote badala ya kila Nchi Mwanachama kujenga yake au kupeleka watu wake Nje ya Jumuiya; c.) Kuhakikisha kuwa wanafunzi wa Sekondari katika Jumuiya wanaielewa Jumuiya yao kwa kuwashirikisha katika mashindano ya Insha ya Jumuiya (Essay Writing Competition) ambayo hufanyika kila mwaka yakilenga kuwafanya wawe na uelewa mzuri wa masuala ya Jumuiya. Mashindano katika Insha yamekuwa na maudhui tofauti kwa mwaka kuhusu mambo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa mfano mwaka 2011 mada ya shindano ni `Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Wanaelekea Kuanza Matumizi ya Sarafu Moja. Jadili Faida na Hasara ya Kuwa Na Sarafu Moja' Utaratibu huu unawezesha wanajumuiya tangu ngazi za chini kuwa na uelewa zaidi juu ya Jumuiya yao na fursa zilizopo katika Jumuiya.

8.3.10.2 Sekta ya Afya

Katika Sekta ya Afya Nchi Wanachama zimefanikiwa kutekeleza Miradi na Programu za kikanda. Miradi na Programu hizo ni pamoja na: a.) Programu ya kudhibiti maambukizi ya UKIMWI katika sekta ya usafirishaji na vyuo vikuu; b.) Mipango ya pamoja ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza kwa binadamu na wanyama mipakani; c.) Mipango ya pamoja ya ununuzi wa madawa kwa jumla ili kurahisisha udhibiti wake na kupata bei mafuu kutokana na ununuzi wa jumla;

Miaka 50 ya uhuru.indd 40 7/23/11 10:02 PM

Page 41

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

41

d.) Kuwianisha na kutambua wataalam wa meno na madawa katika vyuo vya tiba vilivyo katika Jumuiya; na e.) Mpango wa matibabu kwa njia ya mtandao ambapo majaribio yake yameanza katika Mkoa wa Mwanza. Mafanikio yaliyopatikana kutokana na Miradi na Programu hizo ni pamoja na: a.) Kuwawezesha wadau katika sekta ya usafirishaji na elimu (madereva na wanafunzi) kuwa na uelewa wa vyanzo vikuu vya maambukizi ya UKIMWI; a.) Kuwa na mikakati ya ufuatiliaji wa karibu wa magonjwa ya mlipuko na kuzipatia Nchi Wanachama vifaa (kama magari) vya kuziwezesha kudhibiti magonjwa ya maambukizi kwa binadamu na wanyama ; b.) Kuwa na wataalamu wenye viwango katika tiba ya meno na magonjwa mengine katika Jumuiya; c.) Kurahisisha upatikanaji wa tiba katika Jumuiya kwa kuweza kuwasiliana na madaktari kupitia mtandao.

8.3.10.3 Sekta ya Kazi na Ajira

Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya ajira ni pamoja na kuandaa mpango wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa utekelezaji wa programu ya masuala ya kazi, ujulikanao kama Decent Work Program. Lengo kuu la programu hii ni kuhakikisha upatikanaji wa ajira ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unakua sanjari na kukua na kupanuka kwa Mtangamano. Programu hii inalenga hasa Vijana. Takwimu zinaonyesha kwamba ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, watu wenye umri wa kati ya miaka 25 ­ 35 ni wengi kuliko wenye umri wa kati ya miaka 35 ­ 50. Programu hii itawezesha Jumuiya kukua katika njia endelevu ya kuendeleza ajira kwa rika la vijana. Aidha Jumuiya inaendelea na utafiti wa Nguvu Kazi (manpower survey). Utafiti huu utasaidia kuunda na kuimarisha takwimu na kumbukumbu za rasilimali watu nchini. Dhumuni kuu la kuunda na kuimarisha kumbukumbu za rasilimali watu ni kurahisisha upatikanaji wa Takwimu sahihi na taarifa muhimu za rasilimali watu. Takwimu hizi zitatoa mwongozo kwa Serikali, Taasisi za utafiti, Sekta Binafsi na wadau wengine kwa kutoa taarifa muhimu za rasilimali watu katika nyanja mbalimbali katika sekta rasmi na sekta zisizo rasmi.

8.3.10.4 Sekta ya Utamaduni na Michezo

Mafanikio yaliyopatikana katika Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Sekta ya Utamaduni na Michezo ni pamoja na kuwa na: a.) Itifaki ya Kiswahili ya Jumuiya; na b.) Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Anthem). Itifaki ya Kiswahili ya Jumuiya inaweza kutambuliwa kwa umuhimu wa Kiswahili katika Ukanda wa Afrika Mashariki. Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulizinduliwa na Marais wa Nchi Wanachama mwezi Desemba, 2010 unatoa fursa ya kuendeleza umoja na mshikamano katika Jumuiya.

8.3.10.5 Jinsia na Maendeleo ya Jamii

Yamekuwapo mafanikio katika kuwashirikisha watu wenye mahitaji maalum katika shughuli mbalimbali za Jumuiya ikiwa ni pamoja na kutoa maamuzi juu ya Jumuiya. Nchi Wanachama zimekubaliana kuwa masuala ya watu wenye mahitaji maalum (People with Disabilities) yapewe kipaumbele katika Mtangamano wa Afrika Mashariki. Katika kufanikisha maamuzi hayo, Jumuiya imekubaliana kuwa na Sera ya Afrika Mashariki ya Watu wenye mahitaji maalum (EAC Policy on Persons with Disabilities). Rasimu ya Sera hiyo imekwisha kuandaliwa na kusambazwa kwa Nchi Wanachama kwa lengo la kupata maoni yao. Aidha kumeanzishwa Baraza la Mawaziri wanaohusika na masuala ya jamii ambalo litatoa mwongozo wa utekelezaji wa maamuzi juu ya masuala ya jamii katika Jumuiya.

8.3.11 Mafanikio Katika Sekta ya Siasa, Ulinzi na Usalama 8.3.11.1 Sekta ya Ulinzi

Nchi Wanachama katika kuzingatia umuhimu wa sekta ya Ulinzi na pia kujenga hali ya kuaminiana, zilisaini makubaliano Maalum ya Ushirikiano katika Nyanja za Ulinzi (Memorandum of Understanding on Cooperation in Defence) mwezi Novemba, 2001. Maeneo ya ushirikiano yaliyoainishwa katika makubaliano hayo ni: Mazoezi ya Kijeshi na Operesheni za Pamoja; Kushirikiana katika masuala ya kiufundi; kubadilishana habari za kiusalama; kubadilishana wakufunzi katika vyuo vya kijeshi; kutengeana nafasi za wanafunzi katika vyo; na kutembeleana. Aidha, Jumuiya ya Afrika Mashariki ipo katika hatua za awali za kuanza majadiliano yenye lengo la kupandisha hadhi ya Makubaliano haya kuwa Itifaki.

Kufuatia Makubaliano haya ya Ushirikiano katika Sekta ya Ulinzi katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006-2010 majeshi ya nchi hizi yameendesha mazoezi manne ya pamoja kama ifuatavyo: a.) Exercise Hot Springs, ya Kukabiliana na Maafa/majanga (Disaster and Crisis Management) yaliyofanyika Jinja, Uganda Septemba 2006; b.) Exercise Mlima Kilimanjaro (Combined Joint Field Training Exercise), mazoezi yaliyojumulisha dhima zote tatu (kurejesha amani, kupambana na ugaidi na na kukabiliana na majanga). Mazoezi yalifanyika mwezi Septemba 2009 katika mikoa ya Arusha, Tanga na Kilimanjaro; c.) Exercise Natural Fire lililofanyika Mombasa, Kenya mwezi Juni 2007; na d.) Exercise Natural Fire 10 yaliyofanyika Kitgum Uganda Oktoba 2009. Dhima za mazoezi hayo zilikuwa za: huduma za kibinadamu (humanitarian Mission); majanga (natural disasters); shughuli za misafara (convoy operations); udhibiti wa halaiki (crowd control); kuhifadhi silaha (weapon handling); na vizuizi vya magari (vehicle checkpoints). Mazoezi ya majeshi ya Nchi Wanachama yamelenga kujenga utayari wa kukabiliana na changamoto yoyote ya kiulinzi, kiusalama pamoja majanga mbali mbali. Aidha, mafanikio mengine katika sekta ya ulinzi ni utambuzi wa taasisi za kiufundi katika kila nchi ambazo zitatumiwa kwa pamoja. Kwa upande wa Tanzania taasisi ambazo zimetambuliwa ni Mazao Ordinance Factory (Mzinga) iliyopo Morogoro na Tanzania Automobile Technolgical Centre (Nyumbu) iliyopo Kibaha. Ili kuwa na sera itakayoratibu utumiaji wa taasisi hizi, Nchi Wanachama zimeandaa Sera ya Utafiti na Maendeleo ya Jumuiya katika Sekta ya Ulinzi (EAC Defence Research and Development Policy).

8.3.11.2 Sekta ya Usalama

Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya usalama ni maandalizi ya Mkakati wa Kikanda wa Kusimamia Amani na Usalama (The Strategy for Regional Peace and Security). Katika Mkakati huo yameainishwa maeneo 10 ya ushirikiano amabyo ni: a.) Ubadilishanaji wa taarifa za uhalifu na usalama, b.) Kubadilishana programu za mafunzo ya usalama, c.) Kuanzisha mfumo wa kuimarisha operesheni za pamoja, d.) Mawasiliano,

Miaka 50 ya uhuru.indd 41 7/23/11 10:02 PM

Page 42

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

42

e.) Kupambana na madawa haramu ya kulevya, f.) Viongozi wa vyombo vya usalama kutembeleana, g.) Kuanzisha mfumo wa kudhibiti wakimbizi, kupambana na ugaidi, h.) Kupambana na wizi wa mifugo hususan ng`ombe, kutekeleza mradi wa kudhibiti kusambaa kwa silaha haramu ndogo ndogo na nyepesi, i.) Kusimamia mpango wa kuimarisha usalama katika Ziwa Victoria, na j.) Kuandaa mfumo wa kushughulikia migogoro katika kanda. Jumuiya ipo katika hatua za awali za majadiliano kuhusu kuwa na

Itifaki ya Amani na Usalama. Aidha, Nchi Wanachama wa Jumuiya zimekamilisha uundaji wa Sera ya Kupambana na Silaha Haramu Ndogo Ndogo na Nyepesi katika Jumuiya. Vile vile, Nchi Wanachama zipo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha uundwaji wa Rasimu ya Mfumo wa Kujihadhari na Majanga wa Jumuiya (EAC Conflict Early Warning Mechanism) na Mpango wa Kuzuia na Kusuluhisha Migogoro kwa njia ya Amani wa Jumuiya (Conflict Prevention, Resolution and Management).

8.3.11.3 Masuala ya Siasa

Katika kuimarisha demokrasia na kuhakikisha utawala bora miongoni mwa Nchi Wanachama, Nchi Wanachama zimekamilisha majadiliano ya uundwaji wa Itifaki ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha, Nchi Wanachama zimekubaliana kutekeleza Mpango wa Jumuiya wa Kulinda na Kuimarisha Haki za Binadamu katika Jumuiya. Mafanikio mengine yaliyopatikana ni Nchi Wanachama kusaini Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Uratibu wa Sera za Nje (EAC Foreign Policy Coordination) ambayo ipo katika hatua za kuridhiwa na Nchi Wanachama. Aidha, majadiliano kwa ajili ya Itifaki ya Hadhi na Kinga za Kibalozi (EAC Protocol in Immunities and Privileges) yanaendelea.

8.3.11.4 Utawala Bora na Haki za Binadamu

Katika kuimarisha demokrasia miongoni mwa Nchi Wanachama, Jumuiya inaendeleza demokrasia miongoni mwa Nchi Wanachama. Katika kuhakikisha utawala bora unazingatiwa, Wakuu wa vyombo vya kupambana na rushwa hukutana mara kwa mara kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuwa na mikakati ya pamoja. Aidha, Nchi Wanachama zimekamilisha majadiliano ya uundwaji wa Itifaki ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ili kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa na kuzingatiwa Jumuiya inaratibu vikao vya wakuu wa Tume za Haki za Binadamu kutoka Nchi Wanachama na kwa pamoja wamekubaliana kutekeleza mpango wa kulinda na kuimarisha haki za binadamu katika Jumuiya. Vilevile, Itifaki ya Jumuiya ya Uratibu wa Sera za Nje (EAC Foreign Policy Coordination) imesainiwa na Wakuu wa Nchi sasa ipo kati hatua za kuridhiwa na Nchi Wanachama. Aidha, majadiliano kwa ajili Itifaki ya Hadhi na Kinga za Kibalozi (EAC Protocol in Immunities and Privileges) yanaendelea.

8.3.12 Utekelezaji wa Mradi wa Utunzaji wa Mazingira na Matumizi Endelevu ya Ziwa Victoria (LVEMP II)

Kumekuwepo na mafanikio katika utunzaji wa mazingira na matumizi endelevu ya raslimali kikanda, hususan kupitia katika mradi wa utunzaji na usimamizi wa mazingira katika Bonde la Ziwa Victoria, (Lake Victoria Environment Management Programme ­ LEVEMP) na Sera ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (EAC Climate Change Policy). Awamu ya Kwanza ya Mradi huo ilitekelezwa katika Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania kwa Kipindi cha Mwaka 1997 hadi 2005, kwa kufanya utafiti kwa lengo la kubaini hali halisi ya uharibifu wa mazingira na hali ya maisha ya jamii inayozunguka Ziwa Victoria ili kuweza kuandaa Mpango Kamambe wa Utunzaji na Usimamizi wa Mazingira katika Bonde la Ziwa Victoria. Matokeo ya utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Mradi ambayo yalikuwa ni katika utafiti yalioonyesha kuwa kuna uharibifu mkubwa katika Ziwa Victoria ambao unahitaji kudhibitiwa. Uharibifu huo ulikuwa ni pamoja na ongezeko la magugu maji na uharibifu wa baionuwai yakiwemo maeneo oevu (Wetlands) ambapo udhibiti ulihitajika

kupitia utekelezaji wa mradi wa muda mrefu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hususan jamii inayolizunguka Ziwa Victoria. Kutokana na matokeo ya utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Mradi, Jumuiya ya Afrika Mashariki inatekeleza Awamu ya Pili ya Mradi huu (LVEMP II) ambayo ina vipengele vikuu vinne ambavyo ni: a.) Kuimarisha mfumo wa Utendaji kwa kujenga uwezo wa usimamizi wa Programu (Strengthening Institutional capacity for managing the program); b.) Mpango wa Kuthibiti uchafuzi wa udongo; c.) Uratibu wa Mpango wa Usimamizi wa maji water shed; d.) Uhifadhi na Usimamizi wa vyanzo vya maji na kuboresha maisha ya Jamii inayolizunguka eneo la Mradi. Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Utunzaji na Usimamizi wa Mazingira katika Bonde la Ziwa Victoria (LVEMP II) ulianza Mwezi Agosti, 2009 na utakamilika Mwaka 2013. Makao Makuu ya Mradi huu yako Mkoani Mwanza. Kwa Tanzania miji ya Geita, Nansio na Sengerema itanufaika kupitia vipengele vya mradi huo, ambavyo ni pamoja na: a.) Kuthibiti uchafuzi wa udongo; b.) Mpango wa Usimamizi wa maji (water shed); c.) Uhifadhi na usimamizi wa vyanzo vya maji na kuboresha maisha ya jamii inayolizunguka eneo la mradi.

8.3.13 Ujenzi wa Makao Makuu ya Jumuiya

Arusha imekuwa Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki tangu mwaka 1967. Kwa sasa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yapo katika jengo la Makao Makuu ya Jumuiya iliyovunjika, lililojengwa miaka ya 1970, jengo ambalo kwa sasa linamilikiwa na Tanzania kufuatia mgawanyo wa mali za iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Jengo hilo ni Kituo cha Mikutano ya Kimataifa (Arusha International Conference Centre- AICC). Uamuzi wa kuendelea kuwa na Jumuiya, mara Sekretariet ya Tume ya Kudumu ya Utatu ilipoanzishwa mwaka 1996, ulifuatiwa na wazo la kujenga Makao Makuu ya Jumuiya. Ujenzi huo haukuweza kuanza mara moja kutokana na Sekretariet hiyo kutokuwa na ardhi ya kujenga Makao Makuu hayo na kukosekana kwa fedha za ujenzi huo. Kutokana na kupanuka kwa shughuli za Jumuiya, Nchi Wanachama zilikubaliana kujenga Jengo la kisasa linalokidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye kadiri Mtangamano unavyokuwa. Mchakato wa ujenzi wa Makao Makuu ulianza mara baada ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa ekari 9.85 za ujenzi wa Makao Makuu mwaka 2001. Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianza kutafuta fedha za ujenzi wa Makao Makuu hayo. Serikali ya Shirikisho la Ujerumani ilikubali kutekeleza Mradi huo kwa kutoa Euro 8 milioni. Gharama za ujenzi ziliongezeka kutokana na kupanuka kwa mahitaji hasa baada ya nchi ya Burundi na Rwanda kujiunga na Jumuiya, hadi kufikia Euro 14 milioni. Serikali ya Shirikisho la Ujerumani ilikubali kuongeza kiasi kilichopungua cha Euro 6 milioni. Ujenzi ulianza kwa Wakuu wa Nchi Wanachama kuweka jiwe la msingi tarehe 20 Novemba 2009. Ujenzi huu unaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwa gharama ya TShs. 20,741,505,735.22 (14 Mil. Euros)

Miaka 50 ya uhuru.indd 42 7/23/11 10:02 PM

Page 43

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

43

ulianza rasmi tarehe 28 Januari, 2010 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2011. Ujenzi unaendelea vizuri ambapo hadi kufikia katikati ya mwezi Mei, 2011 asilimia sitini na mbili (62%) ya ujenzi ilikuwa imekamilika. Serikali ya Tanzania imetoa ekari nyingine 126 eneo la Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na upanuzi wa Makao Makuu ya Jumuiya hiyo kulingana na mahitaji. Kuwepo kwa Makao Makuu ya Jumuiya Nchini kuna manufaa mengi kiuchumi, kisiasa na kijamii ambapo ni pamoja na Baadhi ya manufaa hayo ni kutoa ajira kwa Watanzania na Watanzania kunufaika kutokana na mauzo ya bidhaa za kilimo na viwanda kwa wageni wanaofanyakazi katika Makao Makuu ya Jumuiya. Aidha, utalii wa mikutano (conference tourism) utasaidia sana kuitangaza na kukuza Tanzania.

8.3.14 Upanuzi wa Jumuiya

Mwaka 2007 Jumuiya ya Afrika Mashariki ilipanuka kutoka nchi tatu wanachama hadi nchi tano, baada ya nchi za Rwanda na Burundi kujiunga na Jumuiya. Upanuzi huu ni mafanikio kwa Jumuiya ya Tanzania kwa kuwa kujiunga na Rwanda na Burundi kumepanua soko na fursa za kuichumi, (ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji na ajira), na wigo wa ushirikiano katika nyanja za kijamii, kisiasa, kiulinzi na usalama, na hivyo kuendeleza ujirani mwema na amani katika Jumuiya. Aidha Jumuiya inayo sauti zaidi katika masuala/majadiliano kikanda na kimataifa.

9.0 CHANGAMOTO 9.1 Changamoto Katika Ngazi ya Jumuiya 9.1.1 Uhaba wa Raslimali Fedha

Pamoja na kwamba Jumuiya imeendelea kutekeleza Miradi na Programu mbalimbali za Jumuiya, na imeendeleza Mipango Kabambe (Master Plans) mbalimbali changamoto kubwa ni upatikanaji wa fedha za utekelezaji. Ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa rasilimali, Jumuiya ya Afrika Mashariki ipo katika mchakato wa kuanzisha Mfuko wa Maendeleo wa Afrika Mashariki (East African Delopment Fund) utakaowezesha Nchi Wanachama kupata fedha za kutekeleza Miradi na Programu mbalimbali za kikanda ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya Jumuiya, na hivyo ya Nchi Wanachama.

9.1.2 Kuendelea Kuwepo kwa Vikwazo Visivyo vya Kiforodha

Pamoja na kuondolowe kwa ushuru wa forodha katika biashara ya bidhaa, wafanyabiashara wameendelea kukabiliana na vikwazo visivyo vya kiforodha katika masoko ya biashara ya bidhaa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mshariki. Ili kupambana na changamoto hii, Nchi Wanachama wameanzisha mpango mahususi unaoainisha vikwazo visivyo vya kiforodha na kuweka ratiba ya kuviondoa. Aidha, kila Nchi Mwanachama imeunda Kamati ya Kitaifa ya kushughulikia vikwazo hivi sambamba na Kamati ya Kikanda ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoundwa kwa madhumuni hayo. Eneo hili bado lina changamoto na linahitaji mikakati zaidi katika ngazi ya Jumuiya, lakini pia ngazi ya Taifa, linahitaji ushirikiano wa karibu wa wadau toka sekta ya umma na sekta binafsi.

9.2 Changamoto za Kiundeshaji Katika Ngazi ya Wizara 9.2.1 Kuhusishwa kwa Masuala ya Mtangamano Katika Mipango na Bajeti za Kisekta

Kutohuishwa kwa Shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika

mipango na bajeti za Wizara na Kisekta kunasababisha ushiriki na utekelezaji wa shughuli za mtangamano kutotekelezwa kwa ukamilifu na kwa wakati. Ili kukabiliana na changamoto hii Wizara za Kisekta zinaendelea na taratibu za kuhuisha shughuli za Mtangamano katika mipango yao, na hivyo kuweza kushiriki na kukasimia shughuli za Mtangamano katika sekta husika kwa ubora zaidi.

9.2.2 Mwamko na Uelewa Mdogo wa Juu ya Masuala ya Mtangamano

Chambuzi mbalimbali zimebaini kuwa mwamko na uelewa wa masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki bado ni mdogo. Ili kukabiliana na changamoto hii, Wizara imeandaa Mpango wa Elimu kwa Umma unaolenga kutekelezwa kwa kushirikiana na Halimashauri zote nchini na wawakilishi wa sekta binafsi ili kupandisha kiwango cha ufahamu wa Watanzania kuhusu Mtangamano na fursa zitokanao na Mtangamano huu.

9.2.3 Majukumu Kutoendana na Rasilimali

Kupanuka kwa haraka kwa majukumu ya Wizara, kutokana na uendelezaji wa haraka wa hatua za mtangamano ikiwemo uundwaji na utekelezaji wa Umoja wa Forodha tangu 2005, Soko la Pamoja tangu mwaka 2010, na wakati majadiliano ya Umoja wa Forodha yanaendelea sasa, kumepelekea ongezeko kubwa la majukumu na mahitaji ya raslimali kwa Taifa. Hivyo kuleta changamoto kubwa kwa Tanzania katika kujiandaa na kusimamia utekelezaji wa Mtangamano kwa manufaa ya Taifa, na Watanzania kwa umahiri unaotakiwa.

10.0. MATARAJIO YA WIZARA NA JUMUIYA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 50 IJAYO

Ushiriki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jumuiya za Maendeleo za Kikanda, ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni miongoni mwa mikakati inayotumiwa katika kukuza uchumi na kujiimarisha kiushindani katika dunia ya sasa yenye ushindani mkubwa inayoongzwa na utandawazi. Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki ni soko dogo tu, ndani ya soko kubwa litokanalo na ushirikiano wa kikanda na kimataifa. Hivyo matarajio ya miaka hamsini ijayo ni kuitumia Jumuiya ya Afrika Mashariki kujiimarisha kiushindani na hivyo kulitumia vema Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki kukuza biashara, uwekezaji, viwanda, kilimo, na kujiletea maendeleo kiuchumi na kijamii. Ushirikiano wa kikanda ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mwanzo tu wa ushirikiano mpana na wa kina utakaoziunganisha Jumuiya za maendeleo za kikanda barani Afrika na kuzaa Jumuiya kubwa zaidi ya Afrika. Kwa hiyo, matarajio ya Wizara katika kipindi cha miaka 50 ijayo ni kuona juhudi za sasa za Tanzania zinazoendelea kisera, kimikakati za kukabiliana na mfumo wa biashara na uchumi wa dunia zinakuwa kichecheo cha kukuza uwekezaji, uzalishaji, tija na kuwezesha Tanzania kujenga uchumi imara na mahiri na kunufaika na fursa za kikanda na kimataifa na maendeleo ya watanzania. Kwa kutumia ushirikiano wa kikanda Tanzania itajiimarisha kiuchumi na kuligeuza taifa kuwa miongoni mwa nchi zilizoendelea duniani. Kama hatua za mwanzo, inatarajiwa Tanzania itaweza kuitumia fursa ya kipekee ya kujiografia (kama nchi inayopakana na nchi 10) kuwa lango na kitovu cha biashara katika Afrika ya Mashariki, Afrika ya kati na kusini mwa Afrika. Uendelezaji wa miundombinu kitaifa na kikanda utawezesha Tanzania kuendeleza bandari, barabara, reli viwanja vya ndege katika viwango vinavyokubalika kimataifa na hivyo kuwa lango kuu na kitovu cha biashara. Tanzania inapakana na nchi za Msumbiji, Malawi, Zambia,

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya. Mwelekeo wa kuwa na Jumuiya iliyopanuka zaidi si wa kufikirika, kwani tayari Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, SADC, COMESA wanaendelea na maandalizi ya kuanzisha ushirikiano baina ya kanda hizi tatu (COMESA-EAC-SADC Tiripartite Arrangement). Hivyo upo uwezekano mkubwa katika miaka hamsini ijayo Nchi za Afrika kujiunga na kuwa na Jumuiya ya Afrika ambayo itaunganisha Jumuiya ndogo ndogo za kikanda zilizopo sasa Afrika. Bara la Afrika litakuwa limejigeuza kuwa Jumuiya moja kubwa ya kiuchumi inayolingana na mabara mengine ikiwemo Jumuiya ya Ulaya. Kwa maana hiyo, Jumuiya ndogo kama Afrika Mashariki zitatoweka, kwanza kwa kuziunganisha Jumuiya za EAC, SADC na COMESA na kisha Jumuiya zote barani Afrika kuunganishwa na kuunda Jumuiya moja kwa bara lote la Afrika itakayokuwa na Soko la Pamoja na Sarafu Moja.

Miaka 50 ya uhuru.indd 43 7/23/11 10:02 PM

Page 44

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

44

IMETOLEWA NA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI MEI, 2011

Miaka 50 ya uhuru.indd 44 7/23/11 10:02 PM

Page 45

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

45

Kiambatanisho Na. 1: MAUZO YA TANZANIA KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI 2005 -2010 (KATIKA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI) Chanzo: Shirika la Takwimu la Taifa (NBS) Kiambatanisho Na. 2: MANUNUZI YA TANZANIA KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI 2004-2008 (KATIKA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI) Chanzo: Shirika la Takwimu la Taifa (NBS) Kiambatanisho Na. 3: URARI WA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (KATIKA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI) Chanzo: Shirika la Takwimu la Taifa (NBS)

Nchi Kenya Uganda Rwanda Burundi Jumla 2004 83.70

11.70 94.40 2005 76.30 20.10 96.40 2006 97.20 20.50 117.70 2007 101.10 19.30 11.20 41.50 173.10 2008 235.00 40.50 20.60 19.50 315.60 2009 188.96 87.26 16.06 24.57 316.85 2010 255.47 59.28 84.82 54.72 454.29 Nchi Kenya Uganda Rwanda Burundi Jumla

2004 127.82 8.88 136.70 2005 153.94 6.46 160.40 2006 169.10 5.3 174.40 2007 100.1 6.40 0.01 0.02 106.53 2008 197.9 6.40 0.10 0.40 204.80 2009 302.06 11.89 0.02 0.31 314.28 2010 270.55 17.56 1.39 0.60 290.10 MAELEZO Mauzo Manunuzi JUMLA YA URARI

2005 96.4 160.4 (64.0) 2006 117.7 174.4 (56.7) 2007 173.1 106.53 66.57 2008 315.6 204.8 110.8 2009 316.85 314.28 2.57 2010 454.29 290.10 164.19

Miaka 50 ya uhuru.indd 45 7/23/11 10:02 PM

Page 46

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

46

Kiambatanisho Na. 4: MIRADI ILIYOWEKEZWA HAPA NCHINI NA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (IDADI NA THAMANI KATIKA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI) Chanzo: Shirika la Takwimu la Taifa (NBS) Kiambatanisho Na. 5: MIRADI ILIYOWEKEZWA NA TANZANIA KATIKA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (IDADI NA THAMANI KATIKA DOLA ZA KIMAREKANI) Chanzo: Shirika la Takwimu la Taifa (NBS)

NCHI Kenya Uganda Rwanda Burundi JUMLA 2005 IDADI THAMANI 34 37.54 1

2.11 3-5 39.65 2006 IDADI THAMANI 36 38.76 2 2.3 38 41.06 2007 IDADI THAMANI 23 44.08 4 6.80 27 50.88 2008 IDADI THAMANI 72 308.08 5 2.27 77 310.35 2009 IDADI THAMANI 35 49.49 5 33.73 2 0.48 42 83.7 2010 IDADI THAMANI 27 67.23 1 0.17 1 1.64 4 4.62 33 73.66 NCHI

Kenya Uganda Rwanda JUMLA 2005 IDADI THAMANI 3 0.31 4 12.02 7 12.33 2006 IDADI THAMANI 0 0.00 2 2.17 2 2.17 2007 IDADI THAMANI 0 0.00 2 4.34 2 4.34 2008 IDADI THAMANI 2 2.01 3 4.20 5 6.21 2009 IDADI THAMANI 4 3.78 2 1.08 2 1.32 8 6.18 2010 IDADI THAMANI 3 2.84 5 4.07 4 3.76 12 10.67

Miaka 50 ya uhuru.indd 46 7/23/11 10:02 PM

Page 47

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

47

Kiambatanisho Na.6: MIRADI ILIYOONGOZA KATIKA UWEKEZAJI KUTOKA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (IDADI, THAMANI KATIKA DOLA ZA KIMAREKANI, NA AJIRA)

MWAKA 2005 2006 2007 2008 2009 2010 JUMLA MIRADI 5 12 15 23 21 10 86 THAMANI 8.01 15.07 7.64 231.22 30.70 16.55 395.19 AJIRA 127 2,163 255 429 1,143 1,761 5,878 UZALISHAJI MWAKA 2005 2006 2007 2008 2009 2010 JUMLA MIRADI 3 9 4

13 3 11 43 THAMANI 3.06 7.85 2.78 19.16 3.83 17.34 54.02 AJIRA 17 53 21 67 29 395 582 UJENZI MWAKA 2005 2006 2007 2008 2009 2010 JUMLA MIRADI 1 1 2 3 2 3 12 THAMANI 3.25 6.67 7.82 9.28 0.65 11.90 39.57 AJIRA 107 206 1524 12 21 1,382 3,252 KILIMO MWAKA 2005

2006 2007 2008 2009 2010 JUMLA MIRADI 2 3 4 9 3 4 25 THAMANI 2.34 4.62 2.16 11.20 8.07 23.72 52.11 AJIRA 87 363 106 226 141 722 1,645 USAFIRISHAJI MWAKA 2005 2006 2007 2008 2009 2010 JUMLA MIRADI 3 5 4 11 5 3 31 THAMANI 2.30 2.71 2.82 11.56 3.98 1.96 25.33 AJIRA

40 213 29 164 181 68 695 UTALII

Miaka 50 ya uhuru.indd 47 7/23/11 10:02 PM

Page 48

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

48

KIAMBATANISHO A: MAENEO YALIYOFUNGULIWA KATIKA SOKO LA PAMOJA I. Uhuru wa raia wa Afrika Mashariki kufanya kazi katika Nchi yoyote ndani ya Jumuiya (Free Movement of Workers)

Kada zitakazohusishwa na ufunguaji wa soko la ajira ambazo zimefunguliwa kwa raia toka Nchi Wanachama ni kama ifuatavyo:

A. TANZANIA

(i) Walimu wa vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu wenye shahada ya uzamivu kuanzia 2010; (ii) Walimu wa shule za sekondari katika fani ya hisabati, fizikia, bailojia kuanzia 2011) (iii) Walimu wa shule za sekondari katika fani ya lugha za kigeni kuanzia 2015; (iv) Walimu wa shule za msingi zinazofundisha kwa lugha ya kiingereza wenye angalau shahada ya kwanza kuanzia 2010 isipokuwa kwa upande wa Tanzania Visiwani; (v) Walimu wa vyuo vya Kilimo, Ufundi Stadi wenye kiwango cha elimu cha angalau shahada ya pili katika fani husika kuanzia (2010); (vi) Wahandisi wa madini kuanzia 2011; (vii) Wahandisi wa majengo kuanzia na wahandisi wengine 2012; (viii) Maafisa ugani katika sekta ya kilimo kuanzia 2015; (ix) Wauguzi na wakunga kuanzia 2010; (x) Wahudumu wengine wa sekta ya afya kuanzia 2015; (xi) Kada ya waongoza ndege kuanzia 2012; na (xii) Kada ya upimaji ramani kuanzia 2015.

B. KENYA

(i) Wakurugenzi na watendaji wakuu wa makampuni (2010); (ii) Wakuu wa vyuo Vikuu na taasisi nyingine za elimu (2010); (iii) Mameneja wa makampuni (2010); (iv) Wanasayansi na wahandisi (2010); (v) Wataalam wa hisabati, takwimu na kopyuta (2010); (vi) Madaktari, wauguzi na wakunga (2010); (vii) Walimu wa sekondari na vyuo (2010); (viii) Wanasheria (2010); (ix) Wahasibu (2010); (x) Wataalam wa Makataba, watunzi, wasanii (2010); na (xi) Madaktari wa wanyama (2010).

C. UGANDA

(i) Mameneja wa makampuni (2010); (ii) Wakuu wa vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu (2010);

(iii) Wataalam wa Kompyuta (2010); (iv) Wasanii (2010); (v) Mafundi mchundo, mafundi magari na umeme (2010); (vi) Wanasheria (2010); (vii) Wataalam wa anga na marubani (2010); (viii) Wahandisi wa ujenzi na umeme (2010).

D. RWANDA

(i) Wataalam katika fani ya sayansi (2010); (ii) Wataalam wa hisabati, takwimu na utafiti (2010); (iii) Wataalam wa afya (2010); (iv) Wataalam wa Bailojia, mimea, wanyama na mazingira (20100; (v) Wahandisi wa ujenzi, wasanifu majengo na mipango miji (2010); (vi) Walimu wa Sekondari na vyuo vya ufundi (2010); (vii) Walimu wa elimu maalum (vipofu, viziwi, mtindio wa ubongo), (2010); (viii) Wahandisi (2010); (ix) Mafundi sanifu (2010); (x) Wataalam wa Kompyuta, utafiti na mipango (2010)

E. BURUNDI

(i) Wataalam wa Sayansi (hesabu, fizikia, wahandisi wa sayansi, kemia, takwimu, kopyuta, wasanifu majengo na wahandisi (2010); (ii) Wataalam wa afya, madaktari, wauguzi na wakunga (2010); (iii) Wataalam wa Kopyuta (2010); (iv) Wahandisi (2010); (v) Mafundi sanifu (2010); (vi) Wataalam wa Biashara, maktaba, sayansi jamii, waandishi wa vitabu, wabunifu na wasanii (2010); (vii) Wahubiri wa dini (2010). Kada nyingine zitaendelea kufunguliwa hatua kwa hatua kwa kuzingatia mahitaji na utayari wa Nchi wanachama.

II: Uhuru wa kufanya Biashara ya Huduma katika Nchi Yoyote Ndani ya Jumuiya (Free Movement of Services)

Kwa kuanzia Nchi wanachama zimekubaliana kuondoa vikwazo katika sekta saba za huduma zilizoanishwa katika jedwali la uhuru wa biashara ya huduma kama ifuatavyo: (viii) Sekta ya Huduma za Biashara (ix) Sekta ya Huduma za Mawasiliano; (x) Sekta ya Huduma za Ugavi; (xi) Sekta ya Huduma za Elimu; (xii) Sekta ya Huduma za Fedha; (xiii) Sekta ya Huduma za Utalii; (xiv) Sekta ya Huduma za Usafiri Mchanganuo wa sekta na aina za huduma zilizokubalika kufunguliwa na Nchi Wanachama na vipindi vya kuanza utekelezaji ni kama ifuatavyo:

A. TANZANIA SEKTA YA HUDUMA ZA BIASHARA (Business Services) (i) Huduma za Utaalam (Professional Services)

a) Biashara ya Huduma za Uhasibu na Ukaguzi (2010) b) Biashara ya Huduma ya Uhandisi (2010) c) Biashara ya Huduma ya Ukunga na Wahudumu wa Hospitali (2011) d) Biashara ya Huduma ya Utabibu na Huduma za Meno (2010)

(ii) Huduma za ukodishaji na upangishaji

Biashara ya huduma za kukodisha Meli, Ndege, na Mitambo ya kisasa ya

Usafirishaji (2010)

(iii) Huduma nyingine za Kibiashara

a) Biashara ya huduma za utafiti wa masoko na ukusanyaji wa kura za maoni (Market Research an Public Opinion Polling Services) (2010) b) Biashara ya huduma ya ajira ya watumishi (Placement and Supply Services of Personnel) (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA UGAVI (Distribution Services) (i) Huduma ya Uwakala (2010) (ii) Huduma ya Haki Maalum ya Uendeshaji (Franchising)

Miaka 50 ya uhuru.indd 48 7/23/11 10:02 PM

Page 49

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

49

SEKTA YA HUDUMA ZA ELIMU (Education Services)

(i)Huduma za Elimu ya Msingi (2010) (ii) Huduma za Elimu ya Sekondari (2010) (iii) Huduma Nyingine za Elimu a) Biashara ya Huduma za Elimu ya Ufundi (2010) b) Biashara ya Huduma za Elimu ya Chuo Kikuu (2010) c) Biashara ya Huduma za Elimu ya Watu Wazima (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA USAFIRI (Transport Services)

(i) Huduma za Usafiri wa Anga (2015) (ii) Huduma za Usafiri wa Majini (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA MAWASILIANO (Communication Services)

(i) Huduma za Kutuma Barua na Vifurushi (2015) (ii) Huduma za Mawasiliano ya Simu (2015) (iii) Huduma za Haki Maalum ya Uendeshaji (Franchising) (2010) (iv) Huduma za Sauti Picha (Audial Visual) (2015)

SEKTA YA HUDUMA ZA BENKI NA FEDHA

(i) Biashara ya Huduma za Benki na Fedha (2010) (ii) Biashara ya Huduma za Bima (2010) (iii) Biashara ya Huduma nyingine za Fedha (2015)

SEKTA YA HUDUMA ZA UTALII (Tourism Services)

(i) Biashara ya Huduma za Hoteli na Migahawa (2013) Biashara ya Huduma za Hoteli na Migahawa ya hadhi ya angalau nyota tatu (angalau nyota nne kwa visiwani na kwenye Hifadhi za Taifa, na Hifadhi za uwindaji) (ii) Huduma za Uwakala wa Usafiri na Uongozaji Watalii a) Biashara ya Huduma za Kuongoza Watalii (isipokuwa kwa Zanzibar) (2010) b) Biashara ya Huduma za Uwindaji wa Kitalii (2010) c) Biashara ya Huduma za Uvuvi wa Kitalii (2010)

B. BURUNDI SEKTA YA HUDUMA ZA BIASHARA (Business Services)

(i) Huduma za Utaalam (Professional Services) a) Biashara ya Huduma za Sheria(2015); b) Biashara ya Huduma za Uhasibu, Ukaguzi na Utunzaji wa Vitabu vya fedha (2015); c) Biashara ya Huduma za Kodi (2010);

d) Biashara ya Huduma za Uhandisi (2010); e) Biashara ya Huduma za Usanifu wa Majengo(2010); f) Biashara ya Huduma ya Takwimu, Uchapishaji na Utafiti (2010); g) Biashara ya Huduma za Ushauri wa Masoko, Uzalishaji (2010); (ii) Huduma za Kompyuta (2010) (iii) Huduma za Maendeleo ya Utafiti a) Biashara ya Huduma za Maendeleo ya Utafiti katika sayansi ya asili (2010) b) Biashara ya Huduma za Maendeleo ya utafiti katika sayansi ya Jamii (2010) c) Biashara ya Huduma za utafiti katika maeneo mtambuka (2010) (iv) Huduma Nyingine za Kibiashara a) Biashara ya Huduma za Utangazaji (2010) b) Biashara ya Huduma za Utafiti wa Masoko (2010) c) Biashara ya Huduma za Ushauri wa Utawala (2010) d) Biashara ya Huduma za Majaribio ya Ufundi na Uchambuzi (2010) e) Biashara ya Huduma zinazohusiana na Ushauri katika Uzalishaji (2010) f) Biashara ya Huduma za Uvuvi (2010) g) Biashara ya Hudumaza Kilimo, Uwindaji na Misitu (2010) h) Biashara ya Huduma za Usafi wa Majengo (2010) i) Biashara ya Huduma za Ukarabati wa Vifaa (2010) j) Biashara ya Huduma zinazohusiana na Ushauri wa Sayansi na Ufundi (2010) k) Biashara ya Huduma za Upigaji Picha (2010) l) Biashara ya Huduma za Ufungaji wa Vifurushi (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA UGAVI (2010)

(i) Huduma za Uwakala (2010) (ii) Huduma za Biashara ya Jumla (2010) (iii) Huduma za Biashara ya Rejareja (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA ELIMU

(i) Huduma za Elimu ya Msingi (2010) (ii) Huduma za Elimu ya Sekondari (2010) (iii) Huduma za Elimu ya Juu (2010) (iv) Huduma za Elimu ya Watu Wazima (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA BENKI NA FEDHA

(i) Biashara ya Huduma za Bima (2015) (ii) Biashara ya Huduma za Benki (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA UTALII

(i) Huduma za Hoteli na Migahawa Biashara ya Huduma ya Hoteli na Migahawa (2010) (ii) Huduma za Uwakala wa Utalii (2010) (iii) Huduma za Kuongoza Watalii (2010) (iv) Huduma Nyingine za Utalii (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI

(i) Huduma za Usafiri wa Majini (2010) (ii) Huduma za Usafiri wa Anga (2010) (iii) Huduma za Usafri wa Barabara (2010)

C. KENYA SEKTA YA HUDUMA ZA BIASHARA

(i) Huduma za Utaalam a) Biashara ya Huduma za Ushauri wa Sheria, Uwakili na Fani Nyingine za Sheira(2010) b) Biashara ya Huduma za Uhasibu na Ukaguzi (2010)

c) Biashara ya Huduma za Usanifu Majengo (2010) d) Biashara ya Huduma za Ushauri katika uhandisi (2010) (ii) Huduma zinazohusiana na Kompyuta Biashara ya Huduma za Ushauri wa Masuala ya Kompyuta (2010) (iii) Huduma ya Maendeleo na Utafiti Biashara ya Huduma za Utafiti na Maendeleo katika Sayansi ya Asili (2010) (iv) Huduma za Upangishaji na Ukodishaji a) Biashara ya Huduma za kodisha Ndege (2015) b) Biashara ya Huduma za Kodisha Vyombo vya Usafiri wa Nchi Kavu (2015) c) Biashara ya Huduma za Kukodisha Vifaa na Mitambo ya Kilimo (2015) d) Biashara ya Huduma za Kukodisha Mitambo na Vifaa vya Ujenzi (2015) e) Biashara ya Huduma za kodisha mashine na vifaa vingine (2015) (v) Huduma za Mawasiliano a) Biashara ya Huduma ya Kutuma Barua na Vifurushi(2015) b) Biashara ya Huduma za Mawasiliano ya Simu (2015) c) Biashara ya Huduma za Mitambo ya Simu (2015)) d) Biashara ya Huduma za Usambazaji na Ukarabati wa Vifaa vya Simu (2015)

Miaka 50 ya uhuru.indd 49 7/23/11 10:02 PM

Page 50

TUMETHUBUTU,TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

50

(vi) Huduma za Picha na Sauti a) Biashara ya Huduma za Picha za mwendo (2015) b) Biashara ya Huduma za upigaji wa picha za mwendo(2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA UGAVI

(i) Huduma za Uwakala (2010) (ii) Huduma za Biashara ya Jumla (2010) (iii) Huduma za Haki Maalum ya Uendeshaji (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA ELIMU

(i) Huduma za Elimu ya Msingi (2015) (ii) Huduma za Elimu ya Sekondari (2015) (iii) Huduma za Elimu ya Juu (2015) (iv) Huduma za Elimu ya Watu Wazima (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA BENKI NA FEDHA

(i) Huduma za Bima a) Biashara ya Huduma za Bima za Afya (2010) b) Biashara ya Huduma za Bima zisizokuwa za maisha (isipokuwa anga, majini na uhandisi) (2010) c) Biashara ya Huduma za uwakala wa Bima (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA KITALII

(i) Huduma za Hotel na Migahawa Biashara ya Huduma za Hoteli na Migahawa (2010) (ii) Huduma za Uwakala wa Usafiri na Uongozaji Watalii a) Biashara ya Huduma za Waongozaji Watalii b) Biashara ya Huduma za Usafiri wa Majini (iii) Huduma za Usafiri wa Anga a) Biashara ya Huduma ya Ukarabati na Matengenezo ya Ndege (2015)

b) Biashara ya Huduma saidizi za Usafiri wa Anga (2015) c) Biashara ya Huduma za Masoko kwa Huduma za Ndege (2015) d) Biashara ya Huduma za Tiketi za Usafiri wa Ndege (2015) (iv) Huduma za Usafiri wa Barabara (2010) a) Biashara ya Huduma za Usafiri wa Abiria (2010) b) Biashara ya Huduma za Usafiri wa Mizigo (2010) c) Biashara ya Huduma za Matengenezo na Ukarabati wa Vyombo vya Usafiri wa Barabara (2010) d) Biashara ya Huduma saidizi za Usafiri wa Barabara (2010) (v) Huduma Nyingine za Usafiri Biashara ya Huduma za Taarifa za Hali ya hewa

D. RWANDA SEKTA YA HUDUMA ZA KIBIASHARA

(i) Huduma za Utaalam a) Biashara ya Huduma za Sheria (2010) b) Biashara ya Huduma za Uhasibu, Ukaguzi na Utunzaji wa Vitabu vya Hesabu (2010) c) Biashara ya Huduma za Kodi (2010) d) Biashara ya Huduma za Usanifu wa Majengo (2010) e) Biashara ya Huduma za Uhandisi (2010) f) Biashara ya Huduma za Mipango na Usanifu wa Ardhi (2010) g) Biashara ya Huduma za Matibabu ya Meno (2010) h) Biashara ya Huduma za Utabibu wa Mifugo (2010) i) Biashara ya Huduma Nyingine za Matibabu (2010) (ii) Huduma zinazohusiana na Kompyuta (2010) (iii) Huduma za Utafiti na Maendeleo a) Biashara ya Huduma za utafiti na Maendeleo katika Sayansi ya asili (2010) b) Biashara ya Huduma za Utafiti na Maendeleo katika sayansi ya Jamii (2010) c) Biashara ya Huduma za Utafiti na Maendeleo katika masuala mtambuka (2010) (iv) Huduma Nyingine za Kibiashara (2010) a) Biashara ya Huduma za Utangazaji (2010) b) Biashara ya Huduma za tafiti za masoko na ukusanyaji kura za maoni (2010) c) Biashara ya Huduma za Ushauri wa Utawala (2010) d) Biashara ya Huduma zinazohusiana na ushauri wa Uzalishaji (2010) e) Biashara ya Huduma za Majaribio ya Ufundi na Uchambuzi (2010) f) Biashara ya Huduma zinazohusiana na Ushauri wa Sayansi na Ufundi (2010) g) Biashara ya Huduma za ukarabati na matengenezo ya vifaa (2010) h) Biashara ya Huduma za Usafi wa Majengo (2010) i) Biashara ya Huduma za Upigaji Picha (2010) j) Biashara ya Huduma za Ufungaji wa vifurushi (2010) k) Biashara ya Huduma za Uchapaji (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA MAWASILIANO (2010)

(i) Huduma za Posta (2010) (ii) Huduma za Courier (2010) (iii) Huduma za simu (2010) (iv) Huduma za sauti picha (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA UGAVI

(i) Huduma za Uwakala (2013) (ii) Huduma za haki maalum ya uendeshaji (2013) (iii) Huduma za Biashara ya Jumla (2013) (iv) Huduma za Biashara ya Rejereja (2013)

SEKTA YA HUDUMA ZA ELIMU (2010)

(i) Huduma za Elimu ya Msingi (2010) (ii) Huduma za Elimu ya Sekondari (2010) (iii) Huduma za Elimu ya Watu Wazima (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA BENKI NA FEDHA (2015)

(i) Huduma za Benki na Fedha (2015) (ii) Huduma za Bima (2015)

SEKTA YA HUDUMA ZA KITALII (2010)

(i) Huduma za Hoteli na Migahawa (2010) (ii) Huduma za Uwakala wa Usafirishaji na Uongozaji Watalii (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI

(i) Huduma za Usafiri wa Majini (2010) (ii) Huduma za Usafiri wa Anga (2010) (iii) Huduma za Usafiri wa Reli (2013) (iv) Huduma za Usafiri wa Barabara (2010) (v) Huduma za Usafri kwa njia ya Bomba (2013)

E. UGANDA SEKTA YA HUDUMA ZA KIBIASHARA

(i) Huduma za Utaalam a) Biashara ya Huduma za Sheria (2015) b) Biashara ya Huduma za Uhasibu, Ukaguzi na Utunzaji wa Vitabu vya Hesabu (2010) c) Biashara ya Huduma za Kodi(2010) d) Biashara ya Huduma za Usanifu Majengo(2010) e) Biashara ya Huduma za Uhandisi (2010) f) Biashara ya Huduma za Mipango Miji na Upimaji wa Ardhi (2010) g) Biashara ya Huduma za Utabibu na Meno (2010) h) Biashara ya Huduma za Utabibu wa Mifugo (2010) i) Biashara ya Huduma nyingine za utabibu (2010)

Miaka 50 ya uhuru.indd 50 7/23/11 10:02 PM

Page 51

MAFANIKIO YA MIAKA HAMSINI YA UHURU KATIKA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

51

(ii) Huduma zinazohusiana na Kompyuta (2015) (iii) Huduma za Utafiti na Maendeleo a) Biashara ya Huduma za utafiti na Maendeleo katika Sayansi ya asili (2012) b) Biashara ya Huduma za Utafiti na Maendeleo katika sayansi ya Jamii (2012) c) Biashara ya Huduma za Utafiti na Maendeleo katika masuala mtambuka (2012) (iv) Huduma za Upangishaji wa Majengo na Makazi (2015) (v) Huduma Nyingine za Biashara a) Biashara ya Huduma za Utangazaji (2010)

b) Biashara ya Huduma za tafiti wa Masoko na ukusanyaji wa kura za maoni (2010) c) Biashara ya Huduma za Ushauri wa Utawala (2010) d) Biashara ya Huduma zinazohusiana na ushauri wa Uzalishaji (2010) e) Biashara ya Huduma za Majaribio ya Ufundi na Uchambuzi (2010) f) Biashara ya Huduma zinazohusiana na Ushauri wa Sayansi na Ufundi (2010) g) Biashara ya Huduma za Ukarabati na Matengenezo ya Vifaa (2010) h) Biashara ya Huduma za Usafi wa Majengo (2010) i) Biashara ya Huduma za Upigaji Picha (2010) j) Biashara ya Huduma za Ufungaji Vifurushi (2010) k) Biashara ya Huduma za Uchapaji (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA MAWASILIANO

(i) Huduma za Kutuma Barua na Vifurushi (2010) (ii) Huduma za Mawasiliano ya Simu (2010) (iii) Huduma za Sauti Picha (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA UGAVI

(i) Huduma za Uwakala (2010) (ii) Huduma za Biashara ya Jumla (2015) (iii) Huduma za Biashara ya Rejareja (2015)

SEKTA YA HUDUMA ZA ELIMU (2010)

(i) Huduma za Elimu ya Msingi (2010) (ii) Huduma za Elimu ya Sekondari (2010) (iii) Huduma za Elimu ya Juu (2010) (iv) Huduma za Elimu ya watu wazima (2010) (v) Huduma nyingine za Elimu (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA BENKI NA FEDHA (2010)

(i) Huduma za Benki na Fedha (2010) (ii) Huduma za Bima (2010)

SEKTA YA HUDUMA ZA UTALII

(i) Huduma za Hoteli na Migahawa (2010) (ii) Huduma za Uwakala wa Usafiri na Uongozaji Watalii (2013) (iii) Huduma za Uongozaji Watalii (2015)

SEKTA YA HUDUMA ZA USAFIRI

(i) Huduma za Usafiri wa Majini (2012) (ii) Huduma za Usafiri wa Anga (2010) (iii) Huduma za Usafiri wa Reli (2010) (iv) Huduma za Usafiri wa Barabara (2010) (v) Huduma za Usafiri kwa njia ya Bomba (2010) Sekta nyingine zitaendelea kufunguliwa hatua kwa hatua kwa kuzingatia mahitaji na utayari wa Nchi wanachama. III: Uhuru wa raia wa Afrika Mashariki kuwekeza mitaji katika Nchi yoyote ndani ya Jumuiya (Free movement of Capital) Vikwazo katika soko la mitaji la Tanzania na ratiba ya kuviondoa ni kama ifuatvyo: (i) Raia wa kigeni hawaruhusiwi kununua zaidi ya asilimia 60 ya hisa katika soko la mitaji kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kikwazo hiki kinatarajiwa kuondolewa ifikapo mwaka 2015. Kwa upande wa Jamhuri ya Kenya, Jamhuri ya Uganda na Jamhuri ya Rwanda hakuna kikwazo hiki; (ii) Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania raia wa kigeni hawaruhusiwi kushiriki katika soko la amana na hati fungani sa Serikali;

kikwazo hiki kinatarajiwa kuondolewa ifikapo 2012. Nchi nyingine Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hazina kikwazo hiki; (iii) Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawaruhusiwi kukopesha nje ya nchi ambapo kikwazo hiki kinatarajiwa kuondolewa ifikapo 2015; na (iv) Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawakuruhusiwa kuwekeza nje ya nchi ambapo kikwazo hiki kinatarjiwa kuondolewa ifikapo 2014.

Miaka 50 ya uhuru.indd 51 7/23/11 10:02 PM

Page 52

Miaka 50 ya uhuru.indd 52 7/23/11 10:02 PM

Page 53 www.meac.go.tz

IMETOLEWA NA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI MEI, 2011

Miaka 50 ya uhuru.indd 53 7/23/11 10:02 PM

Information

Microsoft Word - Taarifa ya Miaka 50 ya Uhuru _Afrika Mashariki_

86 pages

Report File (DMCA)

Our content is added by our users. We aim to remove reported files within 1 working day. Please use this link to notify us:

Report this file as copyright or inappropriate

892689


Notice: fwrite(): send of 201 bytes failed with errno=104 Connection reset by peer in /home/readbag.com/web/sphinxapi.php on line 531