Read JIPENDE text version

VITUO VYA WANAWAKE VYA JIPENDE!

MTAALA KWA AJILI YA WAHUDUMU WA SALUNI ZA UREMBO

KITABU CHA KIADA KWA AJILI YA MWEZESHAJI

Muongozo wa Kujifunza Wanarika

Shukrani Muongozo huu wa elimu rika umeandaliwa kwa kuzingatia miongozo mingine iliyokwishaandaliwa na mashirika mengine, vilevile kutoka kwenye kituo cha kudhibiti magonjwa na kuzuia maambukizi ya VVU (CDC) miongoni mwa wanawake watu wazima. Muongozo huu umetoholewa na kufanyiwa marekebisho ili kukidhi mazingira ya mradi wa T-MARC, kituo cha JIPENDE kwa ajili ya Afya ya Wanawake, mkakati huu wa kufanya kazi na wahudumu wa saluni za urembo, ambao watapatiwa mafunzo ili kukuza stadi zao za mawasiliano ya ana kwa ana katika kujadilia masuala ya afya ya uzazi na wateja wao na pia kuboresha stadi za mauzo na namna ya kuhudumia wateja ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha afya ya wanawake na kupunguza VVU Tanzania. Tunapenda kutoa shukrani zetu kwa Raisi wa Marekani kupitia Mpango wa dharura wa

kuleta nafuu kwenye UKIMWI ( PEPFAR) kwa ajili ya msaada wake wa kifedha na michango yake kupitia Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

2

YALIYOMO

Utangulizi ........................................................................................4 MAFUNZO YA 1 Mada ya kwanza: Kuja Pamoja kwa Kusudi .................................................7 Mada ya Pili Stadi za msingi za kufanya ......................................................20 MAFUNZO YA 2 Mada ya Tatu Wakati Maradhi yanaposhambulia: Changamoto kuhusiana na ujinsia na afya ya uzazi .......................................................................................29 Mada ya Nne Taarifa za VVU na UKIMWI ....................................................38 Mada ya Tano Kondom..............................................................................52 MAFUNZO YA 3 Mada ya Sita Saratani ya Matiti na Shingo ya kizazi .......................................64 Mada ya Saba Mawasiliano ya ana kwa ana ................................................72 MAFUNZO YA 4 Mada ya Nane Uzazi wa Mpango ..............................................................93 Mada Tisa Kufunga Mafunzo .................................................................120

3

Utangulizi Kampuni ya mawasiliano na kujitegemea iliyosajiliwa Tanzania kama kampuni isiyofanya biashara ya kupata faida na inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Iliyojitoa kwa ajili ya kuboresha hali ya afya za familia za kitanzania/ T-MARC hutumia utaratibu wa kuwaleta pamoja wadau wa sekta binafsi na sekta rasmi ili kuenedelza na kupanua soko la walaji kwa ajili ya biadhaa z aina mbalimbali za kiafya na kuhamasisha kuhusu mabadiliko ya tabia ambayo yataboresha afya ya jamii' bidhaa hizi na kampeni zinachangia kuleta mabadiliko ya afya kwneye maeneo ya VVU/UKIMWI, afya ya uzazi, uhai wa mtoto, magonjwa ya kumbukiza na malaria na huwalenga umma wenye kipato cha chini ulio katika hali hatarishi Kampuni ya T-MARC itasambaza taarifa za kiafya kwa wanawake kupitia saluni za urembo za Jipende, Kituo cha mpango wa afya za wanawake. Muongozo huu unalenga kutumika kama kiongozi cha waelimisha rika, stadi za kijamii mafunzo ya kijamii kwa madhumuni ya kuongeza uelewa kuhusu masula ya afya ya uzazi miongoni mwa wanawake walioko katika umri wa kuzaa. Saluni za urembo zilizochaguliwa zitapewa jina la kibiashara na kujulikana kama "Jipende, Kituo cha Afya ya wanawake". Madhumuni ni kuwapatia mafunzo wahudumu na wamiliki wa saluni za urembo kama viongozi wa rika ili kuanzisha majadiliano na wateja wanapokuja kwenye Saluni za urembo. Viongozi wa rika watapatiwa mafunzo ya masaa 3-4 kwa wiki kwa mfululizo wa wiki nne, kuhusu masuala kama vile kujivunia ujinsia, afya ya uzazi, taarifa kuhusu namna ya kuzuia magonjwa ya ngono/VVU/UKIMWI,pamoja na masuala ya matumizi ya kondom. Nyongeza ya hayo, wahudumu wa saluni watapatiwa mafunzo kuhusu stadi za mawasiliano ya ana kwa ana ili kuweza kuongeza ubora wa huduma na kukuza stadi za ubora wa huduma kwa wateja ikiwa ni miongoni mwa jitihada za kuongeza mauzo ya kondom za kike kwa wateja wa saluni za urembo. Muongozo huu unalenga kutumiwa kwa utayari wa mabadiliko makubwa na viongozi rika ambao huwa wanaongea na wanawake watu wazima mmoja mmoja au kwenye makundi ya ukubwa tofauti.

4

Kupanga Mikusanyiko ya Rika Kiongozi wa rika ataamua lini na kwa namna gani majadiliano haya yatafanyilka. Wanaweza kuuliza maswali na kuanzisha majadiliano kwa kuwashirikisha wateja wao wachache ama kuwashirikisha kwenye majadiliano ya muda mrefu zaidi kwa kuzungumza na mtu mmoja mmoja. Ni matarajio yetu kwamba waelimishaji watatumia muongozo huu katika siku mbalimbali za wiki kwa masaa tofauti tofauti. Sio kila kitakachowezekana kufanyika kwa ufanisi kwenye saluni moja kikawezekana kufanyika kwa ufanisi huo huo kwenye saluni nyingine. Lengo ni utayari na kuwa na mwitikio kuhusiana na mahitaji ya wateja wao kwenye saluni za urembo. Mabadiliko tunayotarajia kuona baada ya masomo Masomo ya muongozo wa waelimisha rika yanalenga kufanikisha mambo yafuatayo miongoni mwa wanawake watakaoshirikishwa: Wanawake wataelezea changamoto na furaha za kuwa Mwanamke wa Kitanzania kwenye karne hii ya 21. Wanawake watapata stadi muhimu zitakazowasaidia kuboresha afya zao na kufanya maamuzi sahihi ya njia za uzazi wa mpango, kuhudhuria kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kupima afya zao mara kwa mara na kuzingatia matumizi ya kondom mara kwa mara na kwa usahihi wao na wenzi wao. Wanawake watapata taarifa sahihi kuhusu njia za kisasa za uzazi wa mpango zilizopo hapa Tanzania na namna sahihi ya kutumia njia hizo. Wanawake wataanza kuwa na mitazamo chanya kuhusiana na matumizi ya kondom za kike na za kiume kila mara. Wanawake wataepuka mazingira hatarishi na kutafuta njia za kuishi maisha salama kwa ajili ya yao wenyewe. Wanawake watatambua umuhimu wa kuhudhuria klinik kwa ajili ya kuchunguza saratani ya matiti pamoja na maambukizi ya magonjwa ya ngono. Wanawake ambao watakuwa wamefanya mabadiliko kuhusiana na jinsi ya kujilinda wao wenyewe vema, watakuwa na uwezo wa kuwafikia wanarika wenzao kwa njia iliyo chanya zaidi kuhusu suala la njia ya kujilinda wao wenyewe vilevile. Muongozo huu unadhamiria kuwezesha viongozi wa rika kuanzisha majadiliano na shughuli zitakazosaidia kuwa na mtandao mkubwa wa wanawake wenye kujali afya zao na kuweza kuafikiana kuhusu tabia salama zaidi.

5

MAFUNZO 1

ZOEZI LA AWALI LA WARSHA (DAKIKA 20 )

Hatua ya Kwanza Wagawie washirki zoezi la awali ili wajaze. Wajulishe kwamba sio muhimu kama watakuwa hawafahamu majibu yote, wajaze kwa kadri ya ufahamu wao kama wanavyoweza. Hatua ya Pili Waelekeze washiriki kuwa wana dakika 20 za kukamilisha zoezi hili la awali. Baada ya dakika 20 kumalizika kusanya karatasi za zoezi.

Hatua ya Tatu Waambie washiriki kwamba zoezi la awali walilofanya nia yake ni kukupatia mwezeshaji uelewa kuhusu kile wanachokifahamu na itakusaidia kuandaa mada amabzo watakuwa wakizihitaji kwenye kushiriki kwenye mpango wa JIPENDE. Waambie washiriki wafahamu kwamba wakati huu wa mafunzo watapata taarifa sahihi kuhusiana na taarifa za masuala ya afya ya wanawake. Baada ya mafunzo haya wataweza kuwapatia taarifa na huduma nyingine za ziada kwa wateja wanaowahudumia kwenye saluni za urembo ili kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya wateja wao.

6

JIPENDE! VITUO VYA AFYA YA WANAWAKE

ZOEZI LA AWALI

1.

NINI SABABU YA VIFO VYA WANAWAKE KATI YA MIAKA 18-49 HAPA TANZANIA?

VVU, Mimba /matatizo wakati wa kujifungua Magonjwa ya Ngono , Malaria . 2. Je VVU ni tatizo zaidi kwa wanaume au wanawake? Wanaume Wanawake 3. Je upo uwezekano wa kupata magonjwa ya ngono na mtu usifahamu kama umeambukizwa? NDIO HAPANA 4. Je kupata magonjwa ya ngono kunaweza kusababisha kuwa na haya yafuatayo: Kupata Saratani , Kupata VVU Kupata Mimba kupata Malaria 5. Orodhesha njia tatu za kuzuia VVU : a. ____________________ c.______________________ b. ____________________ 6. Ipi njia peke ya kufahamu kama umepata VVU? _______________________ 7. Orodhesha masuala mawili ambayo yanasababishwa na unyanyapaa katika kuzuia VVU na jitihada za matibabu hapa Taznania: a. ____________________________________________________ b. ____________________________________________________ 8. Je wanawake wafanye uchunguzi kuhusu saratani ya matiti kila baada ya muda gani? Kila siku mara moja kwa wiki mara moja kwa mwezi mara moja kwa mwaka 9. Ipi ni njia ya mawasiliano yenye kufikia watu wengi kwa ajili ya kusaidia kufanya mabadiliko ya tabia? Redio Mawasiliano ya ana kwa ana Luninga Vipeperushi

7

10. Orodhesha njia sita za uzazi wa mpango zinazopatikana Tanzania : a. ___________________ d.____________________ b. ___________________ e._____________________ c. ___________________ f.______________________

MADA YA KWANZA: KUJA PAMOJA KWA KUSUDI

Mada ndogo: 1.1 Kufahamiana 1.2 Wanawake wa karne ya 21 1.3 Ukweli kuhusu masuala na changamoto za Ujinsia na Afya ya Uzazi hapa Tanzania 1.4 Maadili yetu 1.5 Fursa yetu na Wengine Madhumuni: Mwisho wa somo tutakuwa: Tumejadili kile kinachomaanisha kuwa mwanamke wa karne ya 21 hapa Tanzania ; Kukamilisha zoezi la awali la mafunzo : Kupitia ukweli kuhusu ujinsia na afya ya uzazi Tanzania; Kutambua mitazamo chanya ya kuwa mwanamke wa sasa Tanzania ; Kutambua wanawake wa Tanzania ambao ni mfano wa kuigwa; Kujadili maadili na jinsi ya ambavyo kuwa na maadiili na kupanga kipaumbele cha maadili kutakavyoweza kuwa na athari chanya kwa maisha ya mtu ; Zana: Bango na kalamu Kitini cha Ukweli kuhusu ujinsia na afya ya uzazi hapa Tanzania Kitini cha Mifano ya Maadili Kitini cha kupanag vipaumbele vya maadili binafsi Kitini cha Kuja pamoja kwa ajili madhumuni Muda Saa na dakika 40

8

1.1 Kufahamiana

Hatua ya kwanza Waambie washiriki kwamba tutaanza na zoezi dogo kujitambulisha na kufahamiana vema zaidi. Wawiliwawili washirikishane taarifa binafsi zifuatazo: 1. Jina lako 2. Jambo moja linalokufanya unakuwa na furaha 3. Jambo moja ambalo watu wanweza kusema wanapokuelezea Hatua ya Pili Waaambie washiriki wajipange wawiliwawili na waanze majadiliano. Ruhusu dakika kadhaa kwa ajili ya washiriki wote kumaliza kazi. Hatua ya Tatu Walete wanakikundi pamoja na wakae kwenye mduara ili kila mmoja aweze kumuona mwenzake. Waambie washiriki kutambulishana mbele ya kikundi kwa kutumia vipande vitatu vya karatasi kuhusu taarifa waliyojifunza. Maelekezo kwa Kiongozi wa Rika: Ingawaje baadhi ya washiriki wanafahamiana, itawasaidia kufanya somo kuwa la kuvutia endapo watatambulishwa tena. Washiriki wanaweza kujifunza jambo kuhusu marafiki wao wa zamani. Hakikisha kila mmoja anapata fursa ya kutambulisha, zoezi hili litachukua dakika 20.

1.2 Kuwa Mwanamke wa Karne ya 21 Tanzania

Hatua ya Kwanza Washiriki wote waketi kwenye mduara ili iwe rahisis kila mmoja kumuona mwenzake. Hatua ya Pili Waulize washiriki: Kuwa mwanamke mtanzania kwenye Karne ya 21 ina maana gani? Nini unacho JIVUNIA kwa kuwa mwanmke wa Tazania wa leo?

9

Hatua ya Tatu Waambie washiriki wajitolee kuelezea mawazo yao na andika baadhi ya mawazo hayo kwenye bango. Maelekezo kwa kiongozi rika: Pokea kila wazo kutoka kwa washiriki na waambie wachangie zaidi. Hizi hapa ni baadhi ya maana ambazo ungehitaji kuzitumia: Kabila: inahusiana na kikundi cha watu wanaoshirikiana mambo ya kufanana kama rangi, utaifa, sayansi ya lugha au urithi wa kitamaduni Ujinsia: Inahusiana na jinsi ya mtu na tabia, utamaduni au tabia za kisaikolojia zinazohusiana na ujinsia wa mhusika Kujivuna: Inahusiana na utu wa mtu, umuhimu wake, anavyojiheshimu na thamani yake. Hatua ya Nne Sasa, Waambie washiriki wataje wanawake wanaowaona ni mfano wa kuigwa katika maisha yao kwa vile ni wanawake majasiri. Waambie washiriki wajitolee kushirikishana mawazo yao kuhusiana na wanawake ambao ni mfano mzuri na wa kwa kuigwa. Washukuru kwa kuchangia. Hatua ya Tano Waambie washiriki kwamba tayari wameshajifahamu wao ni kina nani, kwamba kuwa mwanamke wa karne ya 21 maana yake ni nini na kwamba wameshatambua wanawake ambao huwa tukiwatazama wanatupa moyo wa kusonga mbele. Utamaduni wetu ni wa aina mbalimbali na una utajiri mwingi kama walivyo wanawake wa Tanzania tunajivunia thamani yetu na utu wetu. Kwamba tuko sote hapa kwajili ya kusaidiana na kujifunza kutoka kwa kila mmoja wetu. Elezea kwamba wakati wa kutekeleza mpango wa Jipende tutamwezesha kila mwanamke aliyeko hapa leo kwa kumpatia taarifa za kufaa kuhusiana na afya biashara na stadi za kimawasiliano za kuweza kuleta mabadiliko chanya kwa maisha ya wanawake wengine.

10

1.3 Ukweli kuhusiana na Masuala ya Kiafya ya wanawake hapa Tanzania

Hatua ya Kwanza Waambie washiriki: Wanawake kote dunia hawako sawa, wanawake kila mmoja ni wa kipekee- kama wanawake, wamama, mabinti na marafiki ­. Jambo moja tu ambalo tunafanana ni kwamba sote tunakutana na hatari na mazingira yenye changamoto ambayo huwa yanaathiri afya zetu kama wanawake. Waulize washiriki, Je changamoto hizo au hali hatarishi hizo ni zipi? Wabungue bongo kwa pamoja na waandike majibu hao kwenye bango. Baadhi ya hali hatarishi au changamoto zitakazopaswa kutajwa endapo kikundi hakitakuwa kimezitaja ni: UKIMWI na magonjwa mengine ya kuambukiza kwa njia ya ngono Mimba zisizotarajiwa Utoaji Mimba usio salama Wanawake wengi hufa wakati wa ujauzito, wakati wa kuumwa uchungu na wakati wa kujifungua. Hatua ya Pili Wapatie washiriki kipeperushi cha Ukweli kuhusu Afya ya Uzazi na Ujinsia hapa Tanzania. Waambie washiriki kwamba sasa tutasoma kuhusu ukweli wa hali ya kiafya ya wanawake wa Tanzania kwa pamoja kama kikundi. 1. Ukweli kuhusu Afya ya Uzazi na Ujinsia hapa Tanzania Kufanya ngono zisizo salama kunaweza kusababisha kupata mimba zisizotarajiwa, UKIMWI na Magonjwa ya ngono. 2. Matatizo wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua ni mambo ya kwanza kabisa yanayosababisha vifo vya wanawake hapa Tanzania . 3. Kila mtu anaweza kupata VVU ­ Wanaume wanwake vijana wazee, matajiri, masikini, wliosoma au wasiosoma. Mara ukipat VVU huwezi kuviondoa. 4. Maambukizi ya VVU ni makubwa zaidi kwa wanawake wa Tanzania waishio mijini na mashambani. 5. Kupata magonjwa yatokanayo na ngono kunaongeza uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya VVU.

11

6. Wanawake na wanaume wa Tanzania wailoko kwenye ndoa wanapswa kupimwa kama wana maambukizi ya VVU. 7. Wanawake wanaweza kujikinga wasipate VVU magonjwa ya ngono ama mimba zisizotarajiwa kwa kutumia kondom kila wakati na kwa usahihi wao na wenzi wao wa kimapenzi. Maelekezo kwa Kiongozi wa Waelimsha Rika: : Uwe huru kutumia maneno yako mwenyewe kwenye kuelezea ukweli ulioainishwa hapo juu ila usiwajengee hofu, waeleze ukweli kwa faida ya wanwake ambao wanaweza wasiwe wanafahamu kinachoendelea. Hatua ya Tatu Ongoza majadiliano na kikundi kuhusiana na mambo ya ukweli saba mliyosoma pamoja. Unaweza kudodosa kwa ajili ya kupata majibu zaidi kwa akuuliza maswali yafuatayo au kuuliza mswali uliyotunga mwenyewe: Kwanini unafikiri wanawake wameathirika zaidi kuliko wanaume? Kuna yeyote miongoni mwenu angependa kutushirikisha wanawake wenzake kuhusu matatizo aliyowahi kukumbana nayo wakati akiwa mjamzito au au wakati wa kujifungua? Kwa nini unafikiri watu walio kwenye mahusiano ya ndoa wanawake kwa wanume wanahitaji kupima VVU? Hatua ya Nne Waambie washiriki kwamba mpango wa Jipende unafanya kazi ya kubadilisha ukweli wa mambo saba kwa ajili ya kuleta ubora zaidi. Mpango wa JIPENDE unao uwezo wa kufanya mabadiliko kwenye maisha ya mwanamke kwa kuwapatia taarifa, usaidizi na kuwatia moyo ili waweze kulinda afya zao. Rejea dondoo hizi pamoja na washiriki: Mpango wa JIPENDE unatuwezesha kupata fursa ya kusaidia kufanya mabadiliko ya hali iliyopo! Wakati wa kufanya mafunzo ya JIPENDE tutapokea taarifa, na kupata stadi mpya na kujadiliana njia za kuboresha hali ya wanawake wa Tanzania Kwa pamoja tunao uwezo wa kupunguza hatari miongoni mwa mmoja wetu kupata maambukizi ya VVU au wengine kupata magonjwa ya

12

ngono, kusambaza VVU na magonjwa ya ngono kwa wengine au kupata mimba zisizotarajiwa.

1.4 Maadili yetu

Hatua ya Kwanza Waambie washiriki kwamba tumeshajadiliana uzoefu wetu binafsi na kwa vile ni wanawake wa Tanzania na kuweza kutambua wanawake majasiri maisahni mwetu. Sasa tuatajadiliana kuhusu maadili, umuhimu wake na jinsi yanavyotikisa maamuzi tunayoyafanya. Waulize washiriki, Je hapa dumiani ni nini cha umuhimu kwako? Andika majibu ya kikundi kwenye bango. Majibu yanayotarajiwa: Elimu, Uaminifu, Mapenzi, Familia zetu, Kuwa na pesa Kumiliki gari, Baada ya kikundi kutoa majibu yake wasomee kilichoandikwa kwenye bango na waambie washiriki kwamba "Haya ndio Maadili yetu". Hatua ya Pili Waambie washiriki wajaribu kufafanua tunamaanisha nini tunaposema "Maadili" Jumuisha majibu ya kikundi kwa kutumia maana moja au zaidi ya yaliyotajwa hapa: Maadili ni misingi , viwango, au ubora unao kubalika au kutarajiwa Thamani ni imani ya mtu au kikundi cha kijamii ambapo kunakuwa na ushawishi wa kihisia (ama kwa ajili ya kuunga mkono au kupinga jambo fulani) Maadili yanapewa thamani kubwa na maadili ya mtu binafsi huwa ni ngumu kuyabadilisha.

13

Hatua ya Tatu Sasa waulize washiriki, Je ni wapi tunaweza kupata MAADILI yetu? Baada ya kupata majibu kutoka kwenye kikundi washiriki hawana budi kufahamu kuwa mara nyingi huwa tunajifunza maadili yetu kutoka kwenye familia zetu, historia yetu kuhusu imani za dini, au kutokana na uzoefu wa kimaisha. Hatua ya Nne Wagawie washiriki Kitini kinachoitwa Mifano ya maadili binafsi kwa kila mshiriki. Elezea kwamba kitini hiki kina mifano ya baadhi ya maadili ya mtu binafsi. Maadili yao binafsi yanaweza yasiwe yameorodheshwa na hivyo unaweza kuongezea maadili mengine kama yatakuwa yamekosekana, sisi sote ni wa kipekee na kila mmoja anayo maadili yake ingawaje huwa tuna baadhi ya maadili ambayo huwa yanafanana. Waambie washiriki wajitolee kuchagua baadhi ya maadili kwenye orodha ambayo yanataekelezeka kwenye jamii au kwao wenyewe binafsi.

Hatua ya Tano Waambie washiriki kwamba sasa tutafanya zoezi kwa kutumia Maadili. Wagawie washiriki Kitini chenye jina Kupanaga kwa vipaumbele maadili yangu binafsi, zoezi hili ni kwa kila mshiriki. Waambie washiriki kwamba kitini kimegawanyika katika makundi matatu tofauti. : 1. Muhimu sana: kuwa tayari kuachana na maadili mengine yote na kupokea hili 2 Muhimu 3. Sio muhimu Waambie washiriki wajigawe kwenye makundi matano. Kila kikundi kijadiliane na kukubaliana kuhusu maadili matatu kwa kila kundi lililopo hapo juu.

14

Wapatie dakika chache kufanya zoezi hili na baada ya hapo wawe tayari kuwasilisha majibu yao.. Baada ya kila kikundi kimeshawasilisha waambie washiriki waangali namna ambavyo maadili ya kikundi kimoja yanavyotofautiana ama kufanana na kikundi kingine. Hatua ya Sita Sasa waambie washiriki: Je ilikuwa ni vigumu kuchagua baina ya maaadili mbalimbali? Yapi yalikuwa ni vigumu kuyachagua? Je kwa nini ni muhimu kufahamu maadili yetu kabla ya kufanya maamuzi? Je ni kwenye aina gani ya maamuzi ambapo zoezi hili linaweza kutusaidia? Waambie washiriki kuwa kushikilia maadili yao kunaathiri utaratibu mzima wa kufanya maamuzi. Kuwa na utaratibu wa kutafakari kuhusu maadili yetu kabla ya kufikia maamuzi ya mwisho kunaweza kukuzuia kufanya maamuzi mabaya au kufanya chaguo dhaifu ambalo linaweza kusababisha kuwa na matokeo hasi kwako au kwa wale wapendwa wako. Kwa mfano, kama wahudumu tunaweza kufanya maamuzi yatayosaidia kuweza kuwavutia wateja wasiondoke kwenye saluni zetu, kama tunathamini huduma nzuri kwenye saluni ili kuweza kuwafurahisha wateja wetu na ili warudi tena kwa mara nyingine kufanya biashara zaidi.

1.5 Fursa kwa Ajili yetu na kwa Wengine

Hatua ya Kwanza Waambie washiriki kwamba mpango wa JIPENDE uliandaliwa ili kuwezesha wanawake wa Tanzania kusaidiana wao kwa wao na kuboresha afya zao. Tutakuwa tunakutana kila wiki kujifunza stadi mpya na kujadiliana taarifa muhimu kuhusu kuboresha afya ya wanawake na kukuza biashara za salauni za urembo. Ila kabla ya kubadilsisha au kuwasaidia wengine inabidi sisi wenyewe

15

tubadilike kwanza. Tunaweza kuanza kwa kuwajibika kwenye maamuzi tunayofanya na kujiheshimu wenyewe. Mikutano hii itatusaidia kubadilika sisi wenyewe na wengine pia. Wakati wa mikutano hii ni vema kama tutaweza kujadiliana kwa uaminifu mada na kuwatia moyo wengine: Pamoja, tunaweza:: · Kusikiliza simulizi za wengine · Kusikiliza changamoto walizopitia wengine · Kusherehekea mafanikio ya wengine ya kimaisha na kikazi · Kuhamasishana moyo kuhusu kufanya mabadiliko, hata kama ni vigumu kufany mabadiliko. Hatua ya Pili Waulize washiriki wanavyojisiskia baada ya zoezi lilotangulia na kuhusu mpango mazima wa JIPENDE. Rejea mada zitakazofanyiwa kazi hapa chini. Waambai washiriki kuwa tuanweza kutumia muda mfupi ama nrefu kwa kila mada kwa kuzingatia jinsi watakavyovutiwa na mada zenyewe. Mada zetu Mada ya Kwanza Mada ya Pili Mada ya Tatu na ujinsia Mada ya Nne Mada ya Tano Mada ya Sita Mada ya Saba Mada ya Nane Mada ya Tisa Kuja pamoaj kwa Madhumuni Stadi za msingi za kibiashara Wakati maradhi yanapoingia: changamoto za afya ya uzazi Taarifa kuhusu VVU na UKIMWI Kondomu Saratani ya matiti Mawasiliano ya ana kwa ana Uzazi wa mpango Kufunga

Waambie washiriki kwamba inawezekana kwetu kuwa viongozi wa rika kwenye jitihada hizi zenye nguvu za kuboresha afya na uhai wa wanawake wa Tanzania .

16

Kuongea na wateja wetu kwenye saluni za urembo kuhusu kile tulichojifunza tunaweza kuwasaidia kufanya maamuzi mazuri zaidi na uchaguzi wa kuhusu afya zao. Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu kipi kilicho cha muhimu amabcho kinatuweka sisi na wapendwa wetu kuendelea kuwa na afya kwa wateja wetu. Hatua ya Nne Kupitia ujumbe umuhimu tena kwa kuomba washiriki wajitokeze kusoma kila ujumbe kwa sauti kutoka kwenye Ujumbe muhimu: Kitini cha Kuja pamoja kwa ajili ya nia moja. Ujumbe Muhimu: Kuja pamoja kwa kusudi Tunaanzisha jambo jipya hapa Tanzania kwa kuzingatia uzoefu wa wanawake wengine duniani. Tumejionea ukweli kuhusu mimba zisizotarjiwa, Magonjwa ya ngono, VVU na UKIMWI kwenye nchi yetu ambayo inahitaji tuifanyie kazi. Tunafursa ya kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta mabadiliko kwetu wenyewe na kwa wengine. Tunaweza kuwa viongozi na kusaidia kulinda afya zetu na afya za wanawake wa Tanzania.

17

MADA 1: KITINI

UKWELI KUHUSU UJINSIA NA AFYA YA UZAZI TANZANIA

1. Kufanya ngono zisizo salama inaweza kusababisha kupata mimba zisizotarajiwa, VVU na Magonjwa ya Ngono. 2. Matatizo wakati wa mimba na wakati wa kujifungua ni sababu kubwa inayosababisha vifo vya wanawake Tanzania 3. Kila mtu anaweza kupata VVU ­ wanaume, wanawake, vijana, wazee, matajiri, masikini, wasomi na wasiosoma. Mara utakapopata VVU huwezi kuviondoa. 4. VVU vinaathiri wanawake zaidi iwe ni kwenye maeneo ya mijini au vijijini hapa Tanzania . 5. Kupata magonjwa ya zinaa kunaongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya VVU. . 6. Wanawake na wanaume waliooana wanapaswa kupima VVU. 7. Wanawake wanaweza kujilinda wasipate VVU, magonjwa mengi ya ngono ama mimba zisizotarajiwa kwa kutumia kondom mara kwa mara na kwa usahihi wao na wenzi wao wa kingono.

18

MADA YA KWANZA KITINI

MIFANO YA MAADILI BINAFSI

Kuwa na afya na kuwa na mchangamfu Kuwa na furaha Kuwa na pesa nyingi Kuwa maarufu Kuwa na marafiki wa karibu Kutekeleza imani yangu ya dini Kusaidia jamii yangu Kufanya vyema kwenye masomo shuleni Kuweza kjitegemea mwenyewe Kunywa Pombe Kuwa mwaminifu kwangu mwenyewe

Kuwa na kazi ninayoipenda Kualiikwa kwenye sherehe Kuwatunza na kuwahudumia watoto wangu Kuwa nadhifu Kuwa na rafiki wa kiume Kufanya vyema kwa mambo ninayoyafanya Kupata mtoto Kuapat kibali cha wazazi wangu Kuwa kama wateja wangu Kuweza kuwajibika na kuwa mwaminifu Kudhaniwa kuwa mwenye muonekano wenye mvuto Kuilinda familia yangu

19

KITINI CHA MADA YA 1

KUPANGA KWA KIPAUMBELE MAADILI BINAFSI

Maana ya Maadili: Maadili ni taratibu, sheria, viwango, au ubora unaofikiriwa kama ni wa thamani ama wa kufurahisha. Maadili ni imani ya ya mtu au kikundi cha kijamii ambapo kuna miguso iliyowekezwa (ama kwa ajili ya kuendeleza jambo fulani ama kupinga jambo fulani) Maadili yanaheshimiwa sana, na kwa kawaida maadili binafsi ya mtu ni magumu sana kuyabadilisha.

Kupanga kwa vipaumbile Maadili binafsi : Orodhesha maadili ya binafsi kwa kila kikundi kwa kuzingatia makundi haya chini: KUNDI 1 MAADILI YA MUHIMU:

KUNDI 2

MAADILI MUHIMU :

KUNDI 3

MAADILI YASIYO YA MUHIMU:

20

KITINI MADA YA 1

UJUMBE MUHIMU: KUJA PAMOJA KWA KUSUDI

Tunaazisha kitu kipya Tanzania, kuendeleza kutoka kwenye uzoefu wa wanawake wengine duniani.

Tunakubaliana na ukweli kwamba mimba zisizo tarajiwa, Magonjwa ya Ngono, VVU na UKIMWI kwa nchi yetu ni masuala yanayohitaji sana tuyaangalie kwa makini.

Tunayo fursa ya kufanya kazi pamoja kuleta fanya mabadiliko kwetu sisi wenyewe na kwa wengine.

Tunaweza kuwa viongozi na kusaidia kulinda afya na uhai wa wanawake wa Tanzania.

21

MADA YA PILI: STADI ZA MSINGI ZA BIASHARA NA MPANGO WA JIPENDE

Mada Ndogo : 2.1 Msingi wa Matangazo 2.2 Dondoo za matangazo na mauzo Madhumuni: Mwisho wa somo tutakuwa: Tumejadili masuala muhimu ya masuala ya matangazo Kutambua mbinu za mauzo na matangazo Zana: Mabango na kalamu (maker) Kitini Mahusiano na Mteja Fomu ya Tathmini Muda: Dakika 50

2.1 Misingi ya Matangazo Basic Marketing

Hatua ya kwanza Eleza kwamba wakati wa somo tutajadiliana dhana za msingi za kutangaza biashara. Miongoni mwenu wengine tayari mnafahamu kuhusu habari hizi ila tutarejea tena ikiwa ni sehemu ya jitihada ya kuboresha biashara zetu ili kutangaza bidhaa au kutoa huduma. Wewe tayari ni kongozi miongoni mwa wanawake wa karne ya 21. Umekuwa na biashara yenye mafanikio na tulivutiwa sana siku ile ya kwanza tulipofika kwenye saluni yako. Sasa tutaongea kuhusu mamabo amabyo tayari unayafanya kuendeleza biashara yako pia jinsi ya kuboresha biashara iwe nzuri na kutoa huduma nzuri zaidi kwa wateja. Tutaanza kwa kuangalia kuhusu umuhimu wa wewe kuwafahamu wateja wako na huduma unayotoa. Hatua ya Pili Waambie washiriki kwamba tutajadili baadhi ya njia za namna ya kuwafikia wateja wao au wateja muhimu ili waweze kuwa wazi kuelezea mahitaji yao na

22

waweze kupata bidhaa au huduma ili kukidhi mahitaji yao. Wagawe kwenye makundi ya watu watatu hadi wanne kwa kila kikundi. Wapatie Kitini Kutosheleza Mahitaji ya Wateja. Waambie kila kikundi wapitie maswali kwa pamoja na wajaze majibu. Baada ya kila kikundi kupitia maswali pitia maswali tena kweny kundi kubwa. Waambie washiriki kwamba majibu ya maswali yanaweza kupatikana kwa urahisi kwa kuongea na wateja, waulize watumia bidhaa na huduma na uwaulize maswali kama wanapenda nini na hapendi nini nk.

Kutosheleza Mahitaji ya Wateja 1. Kufahamu kile wateja wanachohitaji (kumbuka: itaweza kuwa ni muhimu kueleza unaposema "mahitaji"( k.m unaposema una njaa unahitaji chakula, kunapokuwa giza unahitaji mwanga n.k) a. Wateja wako ni kina nani? JeKina nani wanaweza kuwa wateja wako wapya? b. Wako wapi? c. Huduma gani/bidhaa zipi wanazozipenda kutoka kwenye saluni yako? d. Nini wanachokifurahia zaidi kwenye huduma au bidhaa unazowapatia? e. Mara ngapi huwa wanakuja kwenye saluni yako kupata huduma? 2. Kuwatia wateja wako bidhaa/huduma wanazozihitaji. a. Ni kwa njia gani bidhaa zinaweza kuwafikia wateja mara watakapozihitaji 3. Unaweza kupata bidhaa na taariafa wateja wako wanazozihitaji kwa mara kwa mara kwa kiasi gani? 4. Unaweza kwa namna gani kuendelea kuwavutia wateja wako kununua bidhaa zako? Kwa namna gani utaweza kuendelea kuimarisha sifa za bidhaa zako kwa wateja na kuelezea vikwazo ili kujihakikishia mauzo ya mara kwa mara ya bidhaa na matumizi yake?

23

2.2 Dondoo za Mauzo na Matangazo

Hatua ya Kwanza Kuwasilisha kuhusu bidhaa zako Waambie washiriki kwamba tutajadili bidhaa wanazouza kwenye saluni zao na bidhaa watakazokuwa wanaziuza, kama vile kondom za kike. Kwa ujumla huwa unawapatia wateja: Orodha ya huduma zinazotolewa kwenye Saluni Majina ya bidhaa zinazouzwa kwenye Saluni Waambie washiriki jinsi wanavyozielezea bidhaa na huduma zitolewazo ni jambo muhimu na kawaida picha ya awali ndiyo ambayo watu huwa wanakumbuka. Hakikisha unaongea na wateja wako kuhusiana na bidhaa na huduma unazotoa kwa njia ya heshima na kiurafiki. Kama unajali na kuonyesha nia kwa wateja wako itaonyesha mauzo yako yameongezeka. Waambie wanakikundi wabungue bongo kuhusu namna wanaweza kuitangaza bidhaa mpya ya nywele kwa wateja wao. Andika baadhi ya majibu kwenye bango. Hakikisha dondoo zifuatazo zimetajwa. Uliza kuhusu mahitaji ya wateja kwahiyo unaweza kuwaelekeza kwenye bidhaa sahihi. Taja faida za bidhaa iliyotangazwa Taja faida za bidhaa kabla ya kujadili bei. Elezea kwa kina kuhusu viwango vya ubora wa bidhaa Jadili kuhusu mambo mengine yanayoonyesha hali ya kuridhika kuhusu bidhaa ( bila kusaliti usiri wake). Onyesha sampuli na fanya maonyesho ya utumiaji wa bidhaa. USItangaze bidhaa ambayo haikubaliki kiafya kwa ajili ya wateja.

Hatua ya Pili Waambie washiriki watafakari nini wanachofikiri ni jambo muhimu linalowezesha wateja wao kukubali kujaribu bidhaa mpya? Baada ya washiriki

24

kadhaa kutoa majibu yao washiriki waelewe kwamba imani amabyo huwa inasababishwa na kuwa na wateja uhusiano mzuri ni ufunguo wa mafanikio. Waambie kikundi kwamba, je wanawezaje kuanzisha mahusiano mazuri na mteja? Andika majibu kwenye bango. Wapatie kitini cha Mahusiano na Mteja wapitie dondoo za jinsi ya kujenga mahusiano mazuri na wateja kama kikundi.

Mahusiano na Wateja : Kushirikiana na wateja ni jambo muhimu kwa sababu wao ndio sababu ya kuwa na biashara, wateja ni muhimu kama zilivyo bidhaa na huduma unazotoa. Baadhi ya dondoo za kusaidia kujenga kuaminiana na pia kuwa na mahusiano mazuri na wateja: 1. Kila mara hakikisha kwamba wateja wako wanajiona wao ni muhimu kwako 2. Usiwaweke wateja wakusubirie, kila mara unapaswa kuwa makini na uwe mwaminifu. Unapofanya miadi na mteja hakikisha unazingatia muda. 3. Kila wakati zifahamu bidhaa zako (taarifa za kiufundi za bidhaa, zinatumikaje) usiwe na hofu kusema huna jibu kwa swali utakalokuwa hufahamu jibu lake kuliko kusema uongo kuhusu bidhaa.. 4. Usionee aibu kuhusu mauzo. Wewe unawapatia bidhaa ambazo ni za viwango salama na kwa bei nafuu.. 5. Kila mara hakikisha una pesa za chenji za viwango mbalimbali ili kwamba uwe na uwezo wa kumudu manunuzi ya bidhaa kwa mafanikio 6. Weka ahadi ya kukutana na wateja katika muda ambao watakuwa na uwezekano wa kununua bidhaa za ziada na kwa njia hii utaimarisha tabia hii, elezea hofu zilizojitokeza na kumpatia mteja bidhaa ambazo zilizokwisha. Wapatie wateja wako taarifa za kuweza kuwasiliana nawe mara watapohitaji kuwasiliana nawe endapo watahitaji kununua bidhaa zaidi kabla ya tarehe mliyokubaliana. 7. Wasikilize watu kwa makini. 8. Kuwa muwazi na sikiliza maoni hasi pia. 9. Waheshimu wengine kila mara kuhusu viwango vyao vya uelewa na imani zao.

25

10. Wapatie taarifa sahihi kwa ajili ya kuweza kuwashawishi na kuwezesha wateja kuondokana na hali ya kusitasita katika kutumia bidhaa. 11. Ongea kuhusiana na faida za kutumia bidhaa kwa usahihi. 12. Ongea na wateja wako kuhusiana na kujijikinga na VVU, masuala ya afya za wanawake nchini, masuala ya njia za uzazi wa mpango na jinsi ya kutumia na mada nyinginezo za kiafya ambazo unajifunza kutoka kwa mafunzo ya viongozi rika. 13. Uza bidhaa zenye ubora kama bidhaa za Mpango wa JIPENDE. Hatua ya Tatu Washiriki wafahamishwa kwamba tutapitia njia nne za kukuza mauzo na kuboresha biashara: 1. Kuwavutia wateja 2. Kuonyesha tofauti kati ya saloni zao na zile zilizoko kwanye mapango wa JIPENDE 3. Kutunza vyema mahesabu ya fedha 4. Kuweka malengo ya kibiashara

Kuvutia wateja wapya Waambie washiriki, je ni kwa njia gani wanaweza kuvutia wateja wapya? Andika majibu yao kwenye bango na hakikisha dondoo zilizoko hapa chini zimetajwa. · · Kwa kusikia maneno kutoka kwa wateja waliopo wakiwaelekeza kuja. Kuhakikisha unaendeleza viwango vya hali ya juu na ubora wa huduma na bidhaa kwenye saluni yako.

Kupitia mbinu za kutangaza, kama kutoa punguzo la bei wakati wa siku ambazo za wiki ambazo hazijachangamka sana kama vile Jumanne, Jumatano au kwa kutoa punguzo la bei endapo wateja watanunua huduma mbalimbali Kutofautisha kati ya Saluni nyingine kupitia Mpango wa JIPENDE. Waambie wanakikundi kwamba chini ya mpango wa JIPENDE watakuwa na mengi ya

26

kuwapatia wateja wao. Hali hii itakutofautisha na saluni nyingine kwa sababu tofauti na saluni nyingine kwenye saluni yako wanawake wataweza kupata taarifa na bidhaa za kiafya. Huduma hizi za ziada zinaweza kuwavutia wateja wapya kama njia ya kupata bidhaa na kuweza kuwavutia wateja wa zamani waendelee kuwa wateja wako. Utunzaji mzuri wa Mahesabu Ili biashara yako ifanye vyema na kuleta faida ni muhimu kufahamu kuhusu matumizi yako na uweze kutunza kumbukumbu zake kila siku.Hii itakusaidia kufahamu inakugharimu kiasi gani kuendesha na kiasi gani cha fedha kinatakiwa kuingizwa kwenye biashara kila siku ili uziba gharama hizi na pengine kusaidia kupata faida. Gharama ambazo unaweza kuingia ni pamoja na umeme, maji n.k Gharama ya vifaa vya nywele mishahara na kodi ya pango. Gharama zote hizi zinapaswa zionekane kwenye kitabu cha mahesabu ya fedha vilevile kufuatilia kutunza kumbukumbu kutakusaidia kupanga bei vyema, Tambua ni bidhaa ama huduma gani inayoingiza faida zaidi ili uweze kuzitangaza zaidi na kuweza kufahamu wapi pa kupunguza matumizi ili kuokoa gharama endapo biashara haiongezeki kama ulivyotarajia. Kuweka malengo ya biashara yako Kuweka malengo kwa ajili ya biashara yako utaweza kufuatilia vema jinsi ambavyo biashara ya saluni yako inavyoendelea kinyume na matarajio yako na maeneo gani yanayohitaji kuboreshwa. Dondoo chache za namna ya kuweka malengo ni pamoja na: 1. Hakikisha kuwa kila mmoja kwenye saluni anafahamu vyema malengo hayo ili kufahamu wanafanya kazi kukamilisha malengo na kwa ajili ya nini. 2. Mfano wa malengo yanakuwa ni pamoja na: 1. Idadi ya wateja waliohudumiwa kwa wiki (wapya na wale waliorudi kwa mara nyingine tena ) 2. Malengo ya mauzo ya bidhaa/huduma kwa juma (mf idadi ya waliofika kuosha, na kutengeneza nywele , idadi ya waliofanya huduma kwa mvuke) 3. Kiasi cah fedha kilichopatikana kwa wiki

27

3. Ili kufikia malengo ni muhimu kuwa na mpango kazi wako kwa wiki pamoja na ratiba kwa kila shughuli zako. 4. Mwisho wa kila wiki tathmini uone kama umefikia malengo yako. 5. Tengeneza mkakati kwa kila lengo uliloweka. Mf kuongeza idadi ya wateja wiki hii nitatoa punguzo ya asilimia 10 kwa wateja kutoka jamii yangu ya kanisa la kibaptisti. Hatua ya Nne Waeleze washiriki kwamba sasa tumesha maliza mada zote zilizopangwa kwa ajili ya siku ya kwanza ya mafunzo.Tunawashukuru sana kwa kuwa pamoja nasi. Waambie washiriki kuwa tungependa kupata mrejesho kuhusiana na mada zilizomaliza leo. Wapatie fomu ya tathmini ya kupata mrejesho kutoka kwa kila mshiriki hakikisha zinajazwa kabla washiriki hawajaondoka. Wakumbushe washiriki kuhusu tarehe za mafunzo yanayofuata na uwashukuru mara nyingine kwa kuja.

28

KITINI MADA YA PILI

MAHUSIANO NA WATEJA

Mahusiano na wateja: Kufanya kazi na wateja ni muhimu kwa sababu wao ni sababu ya kuwepo kwa biashara yako, wao ni muhimu kama zilivyo kwa bidhaa na huduma unazotoa. Baadhi ya dondoo za kusaidia kujenga kuaminiana na kuwa na mahusiano mazuri na wateja: 1. Hakikisha wateja wako wanajisikia kupewa kipaumbele na wamepewa umuhimu. 2. Wateja wako wasikae wanakusubiri, kila mara uwe makini na uwe mwaminifu. Kila unapopanga kukutana na mteja wako kila wakati hakikisha unazingatia muda. 3. Kila mara unapswa kufahamu bidhaa zako (Taarifa za kitaalamu za bidhaa, na jinsi ya kutumia). Usiogope kukiri hufahamu jibu la swali kama ukiulizwa. 4. Usionee aibu kuhusu kuuza. Kwa vile unawapatia bidhaa zenye ubora salama na za bei wanayoimudu. 5. Kila mara hakikisha unakuwa na pesa za chenji kwa viwango mbalimbali ili kwamba uwe na uwezo wa kumudu manunuzi ya bidhaa kwa mafanikio 6. Andaa mikutano na wateja katika wakati ambao upo uwezekano wa kununua bidhaa za ziada ili kuweza kujenga tabia ya kufanya hivyo kila wakati , wakati wa kukutana jadili mambo yoyote yaliyowakwaza na wapatie wateja wako bidhaa hasa kwa wale ambao walishawahi kununua tena. Wapatie taarifa kwa ajili ya mawasiliano zaidi ili wafahamu jinsi ya kukupata kama watahitaji kununua bidhaa zaidi kabla ya kukutana kwa mikutano inayofuata. 7. Wasilikize watu kwa makini. 8. Uwe muwazi na usikilize maoni hasi. 9. Kila mara heshimu viwango vya uelewa na imani za wengine. 10. Toa taarifa sahihi kwa nja ya ushawishi na kwa njia ambayo wateja wako wataweza kushinda hali ya mashaka kuhusiana na matumizi ya bidhaa.

29

11. Ongelea suala la kutumia bidhaa kwa usahihi. 12. Ongea na wateja wako kuhusiana na suala la kujikinga na VVU, afya za wanawake hapa nchini, njia za uzazi wa mpango na masuala yake na mada nyingine za kiafya ambazo umejifunza wakati wa mafunzo ya viongozi wa rika . 13. Uza bidhaa zenye ubora kama bidhaa za Mpango wa JIPENDE.

30

MAFUNZO YA 1: FOMU YA TAHMINI

Fomu hii ni ya siri. Usiandike jina lak. Asante . 1. Je matarajio yako kwa ajili ya mafunzo haya yamefikiwa? (weka mduara kwenye jibu) NDIO HAPANA Kama hapana, kwanini?

2. Je ni mada gani umeipenda zaidi? Kwanini ?

3. Mada gani huajipenda? Kwanini?

4. Ni mada ipi tulihitaji kuipa muda zaidi?

5. Unaweza kupima namna gani mtindo wa uwezeshaji? ( zungushia duara jibu moja) a. Nzuri sana b. Wastani c. Nzuri d. Dhaifu Maoni: 6. Je tunweza kufanya nini tofauti ili kuboresha yaliyomo kwenye mafunzo haya? 7. Tunaweza kufanya nini touti ili kuboresha utaratibu mzima wa mafunzo haya? (muda, mapumziko ya chai/ kahawa, n.k)

31

8. Kwa ujimla, unaweza kuyapa mafunzo haya kiwango gani cha ufanisi ? (Weka duara kwenye jibu moja) a. Nzuri sana b. Nzuri c. wastani d. Dhaifu 9. Tumia nyuma ya ukurasa huu kama unayo maoni zaidi.

32

MAFUNZO YA PILI

Wakaribishe tena washiriki. Wakumbushe kwamba tuliongea kuhusu changamoto za masuala ya afya ambazo wanawake wote duniani wanakutana nazo kama vile VVU, vifo wakati wa ujauzito, utoaji mimba usio salama na saratani ya matiti na shingo ya kizazi. Pia tulijadiliana kwamba tunaweza kubadilisha hali hii kwa kufanya kazi na kujadiliana na wanawake wengine ili kupunguza maabukizi ya VVU, mimba zisizo tarajiwa, saratani ya matiti na vifo wakati wa kujifungua. Hii itawezekan kwa kushirikishana na kutoa taarifa kwa wengine, tunaweza kuboresha afya za wengine. Mada ya leo inahusisha taarifa za kina zaidi kuhusu changamoto za kiafya zilizotajwa wakati wa mkutano wa mafunzo ya kwanza. Tutaongelea Magonjwa ya ngono, VVU/UKIMWI na njia za kuzuia magonjwa ya ngono na VVU. Pia tutaongelea kuhusu kondom za Dume na Lady Pepeta.

33

MADA YA TATU: WAKATI MARADHI YANAPOSHAMBULIA: MAGONJWA YA NGONO

Mada ndogo 3.1 Kuchukua hatua 3.2 Dalili za magonjwa ya ngono 3.3 Kupata majibu ya maswali yetu na kupata Matibabu ya Magonjwa ya Ngono Madhumuni: Mwisho wa somo tutakuwa tumefanya yafuatayo: Kufanya kwa vitendo igizo dhima kuhusu hatari za Magonjwa ya ngono Changanua dalili zinazoweza kuonekana za Magonjwa ya ngono Kutambua maeneo ya kwenda kupata tiba ya magonjwa ya ngono. Zana Mabango na kalamu kubwa (markers) Kitini cha Igizo dhima la Visa mkasa kuhusu Magonjwa ya ngono Kitini cha Dalili za Magonjwa ya Ngono Kitini cha Kliniki za Magonjwa ya ngono Kitini cha Ujumbe mahususi: wakati maradhi yanaposhambulia Wageni Waalikwa Mwakilishi wa kituo cha kutolea huduma kuongelea Magonjwa ya ngono Local clinic representative to talk about STIs (Dakika 30) Muda Dakika 90

3.1 Kuchukua Hatua

Hatua ya Kwanza Waambie washiriki kwamba sasa tutaongea kuhusu changamoto mbalimbali zinazoathiri afya za wanawake kupitia igizo dogo. Waambie washiriki wajipange wawiliwawili.

34

Kila washiriki wawili wachukue hadithi moja ambayo wanaweza kuigiza. Igizo linapaswa kwa kina kuonyesha jinsi ambavyo rafiki anaelezea kwa mwenzake tatizo alilonalo na namna ambavyo rafiki yake atakavyojibu na kile atakachomwambia afanye. Wapatie igizo dhima na uwapatie washiriki muda wa kufanyia majaribio ya kuigiza. Waambie washiriki kwamba huenda wakachaguliwa kuonyesha igizo lao kwenye kundi kubwa. Hadithi tano amabzo wanweza kuchagua kwa ajili ya igizo 1. Pili anamwambia rafiki yake "nimekuwa nikitokwa na uchafu sehemu za siri na mwezi huu nilitokwa na damu baada ya kumaliza hedhi. Dada yangu ameniambia niende hospitali lakini sijaona kama ni tatizo kubwa na sitaki kupoteza fedha au muda wangu" 2. Tunu anafanya kazi kwenye saluni moja mdogo ya urembo. Anamwambia rafki ya Pendo, "Nafikiri nina maambukizo. Nasiki kama kuungu wakati wa kukojoa na inauma haswa.sina fedha za kutosha kununua dawa.Je unafikiri unaweza kuniazima kiasi cha dawa ulizonunua mara ya mwisho?" 3. Upendo ananunua kadi ya simu kwa ajili ya simu yake mpya wakati unamkimbili alipokuwa kwenye duka.Anaonekana asiye na furaha. Unamuuliza ku nini kibaya anaanza kulia.anasema amegundua kuwa ni mjamzito na ana maambukizi ya magojnjwa ya ngono. Anakuuliza, "nifanye nini sasa?" 4, Mwajuma amekuwa akiishi na raki yake wa kiume kwa miezi mitatu sasa. Anamwambia rafki yake, "Tumekuwa tukilala pamoja sasa kwa majuma kadhaa bila kutumia kondom. Mara moja tulipokuwa tunataka mapenzi ghafla alikataa akisema na matatizo kwenye uume wake. Ila anasema kwamba tatizo litakwisha. Kwahiyo hadi sasa tunasubiri hadi tatizo liishe na awe kwenye hali njema ya Rafiki yake atafanya nini au atamwambia nini ...

35

kufanya mapenzi." 5. Imma anafanya kazi kwenye kibanda cha kuuza chai, anae mtoto wake mdogo wa kiume. Anawaambia wenzake," sijisikii vyema siku hizi. Naona aibu na kudhalilika kwenda kwenye kliniki jirani na ninapoishi kwa baadhi ya wahudumu pale ni majirani zangu. Sitaweza kwenda kwenye klinik ya jirani na ninapoishi kwa sababu nafahamu ni mbali na hakika siafamu mahali ilipo." Hatua ya Pili Alika kikundi kimojawapo kijitolee kuigiza moja ya kisa mkasa. Wakishamaliza waulize maswali yafuatayo: Unawaza nini kuhusu kile rafiki yako alichofanya/alichokisema? Sasa mwambie mmoja wapo ajitolee kusoma visa mkasa vyote kwa ajili ya igizo. Je visa hivi vina uhalisia kiasi gani? Kiambie kikundi kwamba wanawake wote kwenye hadithi wanapaswa kwenda kwenye kituo cha kutolea huduma ya afya kwa sababu huenda wakawa na maambukizi amabyo ni ya hatari sana. Sasa tutaongea kuhusu dalili zilizo zoeleka za Magonjwa ya ngono kwa wanawake na wanaume.

3.2 Dalili za Maambukizi ya Magonjwa ya Ngono

Hatua ya kwanza Wapatie kitini cha Dalili za hatari za maambukizi ya Magonjwa ya ngono. Pamoja kama kikundi someni dalili za hatari za Magonjwa ya ngono kwa wanaume na kwa wanawake. Baadhi ya dalili za hatari za zilizozoeleka za Maabukizi ya Magonjwa ya ngono Wanawake Wanaume Kutokwa majimaji yasiyokuwa ya Kutokwa maji maji ya rangi ya kawaida ukeni njano isvyo kawaida kwenye kiasi cha damu kuendelea kutoka uume.

36

baada ya siku za hedhi kupita Maumivu yasiyokuwa ya kawaida mabli na maumivu wakati wa siku za hedhi maumivu wakati wa kufanya tendo la ngono Muwasho na maumivu makali kwenye sehemu za via vya uzazi Upele mdogo ambao hauwashi vidonda kando kando mwa via vya uzazi

Maumivu wakati wa kukojoa Upele mdogo ambao hauwashi Vidonda kando kando mwa uume na njia ya haja kubwa vinaweza kuwa na maumivu au bila maumivu Malengelenge yanayokuja na kuondoka ( pengine ni uambukizo hata kama hakuna malengelenge) Kuvimba mitoki

Waambie wana kikundi kwamba endapo utaona unazo dalili miongoni mwa zilizotajwa sio lazima iwe ni maambukizi, itabidi ufanye kipimo kwenye kliniki ili kuwa na uhakika kabisa. MUHIMU: Maambukizi huweza kutokea bila kuonyesha dalili iwe ni kwa wanaume au kwa wanawake. Hatua ya Pili Waulize washiriki baadhi ya majina ya Magonjwa ya Ngono wanayoyafahamu? Zipo aina nyingi za Magonjwa ya Ngono. Baadhi ya majina uanyowez kusikia ni pamoja na kaswnde kisonono, pangusa klamidia, viotea sehemu za siri na mengine mengi.. Waeleze washiriki kwamba hatuhitaji kufahamu aina maalumu ya uambikizi ili kuweza kujilinda sisi wenyewe na familia zetu. Ila ni muhimu kufahamu dalili zilizo za kawaida ili kuweza kutafuta tiba. Maambukizi haya huweza kuwa ya hatari endapo hayatitibiwa mapema na pia husababisha mwili kuwa katika hatari ziadi ya kuambukizwa VVU. Hatua ya Tatu Watambulishe wageni uliowaalika kutoka kwenye klinik ili waweze kuongelea kwa ufupi kuhusu magonjwa ya ngono. La umuhimu zaidi waweze kuwa na wasaa wa kujibu maswali ambayo huenda kikundi kinaweza kuwa nayo kuhusiana na magonjwa ya ngono na jinsi ya kupata tiba.

37

Angalizo kwa Kiongozi Rika : Kama inawezekan jaribu kumpata mwakilishi kutoka klinik au mtaalamu wa afya" kwa ajili ya sehemu hii ya somo. Itakuwa ni fursa njema kwa washiriki kuuliza maswali kuhusiana na magonjwa ya ngono na kuweza kupata majibu sahihi kutoka kwa wataalamu wa afya. Hatua ya Nne Waambie washiriki kwamba ni muhimu kwenye saluni kuwa na orodha ya mahali ziliko klinik na aina ya huduma zinazotolewa na gharama zao ili kuweza kuwapatia wateja wao ambao wangependelea kufahamu. Wahimize kuongea na kituo cha kutolea huduma kilichoko jirani wawasidie kutengeneza orodha hii kwa ajili ya jamii yao. Hatua ya Tano Waeleze washiriki kwamba ni muhimu kuchunguza miili yetu endapo tutagundua dalili za Magonjwa ya Ngono tutapaswa kwenda klinik kwa ajili ya matibabu. Wape kitini chenye Ujumbe Muhimu: wakati maradhi yanapotupata na pitia kitini hicho kwa kikundi. Ujumbe Muhimu: Wakati maradhi yanapovamia Ngono hatarishi ni kufanya ngono bila kutumia kondom unapokuw ahuna uhakika kama mwenzi wako ameathirika na VVU au Ugonjwa mwingine wa ngono AU kutokuwa na hakika kama mwenzi wako anafanya ngono na wewe peke yake. Unaweza kupata Magonjwa ya Ngono ambayo unayadharau au yale ambayo huyafahamu kabisa. Kama umewahi kufany ngono hatarishi ni muhimu kwenda klinik kupima na kupatiwa matibabu. Kuwa na Mgonjwa ya Ngono kunaongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya VVU. Kutumia kondom kila mara wakati na kwa usahihi wakati kufanya Ngono kunaweza kutusaidia kujilinda na magonjwa karibu yote yatokanayo na ngono.

38

Tunaweza kuelimisha wanawake wengine kuhusu kile tulichojifunza kuhusiana na maambukizi ya mgonjwa ya ngono, kupima na kupatiwa tiba.

39

KITINI CHA MADA YA 3 KITINI

IGIZO DHIMA MAGONJWA YA NGONO VISA MKASA

Hadithi tano za kuchagua Rafiki yake atapaswa kufanya nini au atamwambia nini ...

1. Pili anamwambia rafiki yake, "nimekuwa nikitokwa na majimaji yasiyokuwa ya kawaida kwa muda sasa na mwezi huu nilipata damu kidogo kabla ya tarehe zangu za siku za hedhi. Dada yangu ameniambia eti niende klinik lakini kwa kweli bado sijaona kama ni tatizo sana. Sitaki nipoteze pesa na muda wangu." 2. Tunu anafanya kazi kwenye saluni ndogo ya urembo. Huwa namwambia rafiki yake Upendo, "Nafikiri nina maambukizi. Nahisi kuungua wakati wa kupii na inauma sana. Sian fedha za kutosha za kununua dawa. Je waweza kuniazima kiasi cha dawa ulizonunua mara ya mwisho?" 3. Upendo ananunua kadi ya simu kwa ajili ya simu yake mpya wakati unapomkimbilia hapo dukani. Anaonekana mwenye majonzi. Unamuuliza amepatwa na nini ghafla anaanza kulia. Amegundua kuwa ni mjamzito na amepatwa na maambukizi ya VVU. Anakuuliza je wewe utafanya nini? 4, Mwajuma amekuwa akiishi na rafiki yake wa kuime kwa miezi mitatu sasa. Anamwambia rafiki yake, "Tumekuwa tukilala pamoja kwa majuma kadhaa sasa na hatukuwa tunatumia kondom. Mara moja tu tulikuwa karibia tufanya ngono ghafla akakataa kwa sababu alisema kuna wakati anakuwa na matatizo kwenye uume wake. Ila nakasema tatizo litakwisha. Kwa hiyo sasa tunasubiri tatizo liishe na atajisikia nafuu kufanya ngono." 5. Imma anafanya kazi kwenye kibanda cha chai na ana mtoto mdogo wa kiume. Anamwambia rafiki yake, siku hizi huwa sijisikii vizuri. Najisikia kama nimedahlilika na aibu kwenda kwenye klinik jirani na eneo ninaloishi kwa sababu baadhi ya watumishi wanaishi jirani na mimi. Pia siwezi kwenda kweny klinik iliyo jirani na kwako kwa sababu ni mbali na zaidi ya hayo sifahamu ni sehemu gani."

40

KITINI CHA MADA YA 3 MAGONJWA YA NGONO: DALILI ZA HATARI ZILIZOZOELEKA

Baadhi ya dalili za hatari za magonjwa ya Ngono Wanawake Wanaume Kutokwa majimaji ukeni kwa Kutokwa majimaji ya rangi njano kiasi kisicho cha kawaida isiyo ya kawaida kwenye uume Wengine hutokwa na damu baada Maumivu au hali ya kuungua ya kumaliza siku za hedhi wakati wa kukojoa Maumivu yasiyokuwa ya kwaida Upele kweny ngozi ambao mabli na yaliyozoeleka wakati unaweza usiwe unawasha mzunguko wa hedhi Vidonda ambavyo haviumi ­ Maumivu wakati wa tendo la kando ya uume na kwenye njia ya ngono haja kubwa Muwasho na hali ya kuungua Malenglenge yanayokuja na kandokando ya via vya uzazi kuondoka (inaweza kuwa ni Upele amabo unaweza kuwa uambukizi hata kama hauwashi malengelenge hayaonekani ) Vidonda ndani na pemebeni mwa Kuvimba mitoki via vya uzazi

41

KITINI CHA MADA YA 3 UJUMBE MUHIMU: WAKATI MARADHI YANAPOINGIA

Ngono hatarishi ni kufanya ngono bila kutumia kondom kama huna hakika kama mwenzi wako ameambukizwa VVU au magonjwa mengine ya ngono AMA kama huna uhakika kama mwenzi wako huwa anafanya ngono na wewe peke yako tu. Una Magonjwa ya Ngono ambayo umeyadharau au ambayo hujui kama unayo. Kama umefanya ngono hatarishi ni muhimu sana kwenda klinik kupimwa na kutibiwa. Kuwa na ugonjwa wowote wa ngono kunaongeza hatari ya kupata maambukizi ya VVU. Matumizi ya kondomu kila wakati na kwa usahihi kunaweza kutusaidia kujilinda na maambukizi ya magonjwa mengi ya ngono. Tunaweza kuelimisha wanawake wengine kuhusu kile tulichojifunza kuhusiana na maambukizi ya Magonjwa ya Ngono kuhusu kupima na kutibiwa.

42

MADA YA NNE: VVU NA UKIMWI

Mada Ndogo 4.1 VVU: Maambukizi yaliyofichika 4.2 Tofauti baina ya VVU na UKIMWI 4.3 Njia za kuzuia VVU 4.4 Umuhimu wa kupima VVU 4.5 VVU/UKIMWI na unyanyapaa Madhumuni: Mwisho wa somo hili tutakuwa tumeweza: Kutofautisha kati ya VVU na UKIMWI Kueleza jinsi ya kuzuia VVU Kuelezea umuhimu wa kupima VVU Kujadili kuhusu unyanyapaa na jinsi ya kuzuia Zana Bango na kalamu (markers) Kitini cha Jinsi ya Kuzuia VVU Kitini cha Kupima VVU Ujumbe muhimu: Kitini cha Taarifa kuhusu VVU na UKIMWI Key Messages: HIV and AIDS Information Handout Muda Saa 1 na dk 30

4.1 VVU: Maambukizi yaliyofichika

Hatua ya Kwanza Waeleze washiriki kwamba mada yetu sasa ni "VVU na UKIMWI"Kama tulivyojadili hapo awali, VVU ni maambukizi yatokanayo na ngono, hadi hivi leo tiba haijapatikana. . Waulize washiriki kwanini wanafikiri tunaita VVU maambukizi yaliyofichika? Baada ya kupata majibu, hitimisha majadiliano kwa kusema kwamba: VVU sio kitu unachoweza kukiona au kuhisi. Huwezi kuelezea kwa kumtazama mtu au kwa kuwa unamfahamu, kama ameambukizwa au hajaambukizwa na

43

VVU. VVU vinawapata watu wote vijana na wazee, masikini na matajiri, wasomi na wasiosoma. Hatua ya Pili Wapatie washiriki Kitini cha Mambo Saba ya ukweli kuhusu VVU. Soma kila ukweli kwa pamoja. Baada ya kusoma kila ukweli elezea kwa maneno yako mwenyewe kilichoko kwenye kila ukweli na washiriki wachangie taarifa yoyote ya nyongeza kuhusiana na ukweli waliousoma punde. Tumia taarifa za ukweli kuelezea au kuhakisha kile wanachofahamu washiriki. Mambo saba tuanyofahamu kuhus VVU 1. Virusi vinasambazwa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine wakati ambapo maji maji ya mwilini yanapogusana, hususani damu, mbegu za kiume, majimaji ya ukeni au maziwa ya mama. Njia ya kwanza ambayo VVU vinasamabzwa ni kwa njia ya vitendo vya ngono. 2. VVU vinasambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa mimba, wakati wa kujifungua au wakati wa kunyonyesha.. 3. Hakuna chanjo ya VVU. Njia pekee ya mtu kujikinga ni kutumia kondom ya kiume au ya kike kila wakati na kwa usahihi wakati wote wa tendo la ngono. 4. VVU haviwezi kusambazwa kwa njia ya machozi, mate, kinyesi, mkojo, matapishi na jasho. 5. Ni salama kabisa kuchangia chakula, vyombo, choo, ama nguo na mtu mwenye VVU. Pia ni salama kushikana mikono, kukumbatiana kuoga na kufanya kazi na mtu mwenye VVU. 6. VVU hudhoofisha mwili taratibu. Mtu anaweza kuishi na virusi na asionyeshe dalili kwa kipindi kirefu. Kipimo cha VVU ni njia pekee ya kufahamu kama umeambukizwa virusi hivyo ama la. 7. Kwa akutumia vidonge vya kupunguza makali ya VVU na kurefusha maisha (ARV) Waathirika wa VVU wanaweza kuishi maisha marefu zaidi, kwa utoshelevu na kuishi maisha chanya. Watu wanaoishi na VVU (WAVIU) wanapaswa kutumia kondom kujilinda wasipate maambukizi mapya na kuzuia wasiambukize wengine virusi.

44

4.2 Tofauti kati ya VVU na UKIMWI

Hatua ya kwanza Rejea kwa pamoja na wanakikundi kwamba VVU ni maambukizi na huweza kuchukua muda mrefu kuonyesha dalili. UKIMWI ni hali inayotokea wakati ambapo maambukizi ya VVU yanakuwa yamedhoofisha uwezo wa mwili kupambana na magonjwa au uwezo wa kupona kutokana magonjwa.. Tutafanya mchezo mfupi kukusaidia kuelewa hili vema zaidi. Kwa kutumia chaki na kamba tengeneza mduara wenye upana wa mita tatu wanakikundi waelewe kwamba mduara huu unawakilisha mwili wa binadamu. Waalike watu wajitolee kutoka kwenye kikundi na kutenheneza timu ya waigizaji 5 wakusaidie kutengeneza mchoro mfupi. Mpe kila mshiriki kazi ya kufanya: majukumu matano ni: Chembechembe hai Nyeupe za Damu" "VVU", "Maambukizi" , Maambukizi mengine" na "Dawa za kupunguza makali ya VVU na kurefusha maisha- ARV" Andika vibandiko vya majina kabla ya kuanza zoezi kuhusu tabia ya kila kimojawapo ili ubandike kwenye shati la kila mmoja. Ikiwezekana mshiriki anayeonekana kuwa ndiye mrefu zaidi, mwenye nguvu zaidi ndio awe "Chembe Hai Nyeupe za Damu". Soma andiko kutoka kwenye jedwali hapa chini au wasimulie simulizi uliyoibuni mwenyewe, Unapokuwa unafanya hivyo hakikisha waigizaji wanafanya kwa vitendoo yale unayoyasema na kufanya yaliyoandikwa upande wa kulia wa jedwali. Kila baada ya hatua moja weka kituo kwa muda ili kuhakikisha kila hatua imeeleweka.

Hatua ya 1: Bado kuathirika na VVU Stage 1: Not yet infected with HIV Mwezeshaji anasema Ndani ya eneo hili inawakilisha mwili wa mtu ulio na afya "kwenye mwili huu kuna mamilioni ya chembe hai nyeupe za damu kwa kawaida ni kati ya chembe 600 na 1000 kwa kila ujazo wa mililita ya damu . Kazi za chembe hizi nyeupe ni kama askari, kulinda na kupambana na maabukizi yoyote yanayouingilia mwili. Ni sehemu ya kinga ya mwili. Tumkaribishe na kumpa Chembe nyeupe za damu Je waigizaji wanafanya nini Chembe nyeupe ya damul anaingia kwenye eneo akiwakilisha mwili wa binadamu, anaonekana mwenye nguvu , anatunisha misuli,anachukua umbo la mtu mwenye maguvu/ watunisha misuli, na anakaa katika mkao wa kupigana.

45

makofi mengimengi ya pongezi.."

"kwa kawaida chembe nyeupe za damu zina nguvu na zinao uwezo wa kupigana na kila aina ya maambukizi. Hapa anakuja maambukizi kama vile yanayosababisha kuharisha au magonjwa kama ya ngozi."

Maambukizi yanaingia ,,mwilini . Chembe hai nyeupe za damu l ,,anashambulia maambukizi, na kuyatupa nje ya mwili.

"Hapa yanakuja maambukizi mengine ­ pengine ni nimomia ama kifua kikuu

Maambukizi mengine yanauingilia mwili. Chembe hai nyeupe "zinavamia" Maambukizi mengine, na baada mapambano mafupi, na baadae inaulazimisha kuutupa nje.

"Kinga ya mwili inaweza kupambana na maambukizi na magonjwa ya kawaida na kuweza kuyaondoa kwa upesi."

Chembe nyeupe za damu anatunisha misuli,anaonyesha nguvu zake

Hatua ya 2: Kuishi na VVU, Hakuna dalili Mwezeshaji anasema "Siku moja VVU akaingia mwilini. Mara kadhaa hufanya hivi kwa kupitia ngono isiyo salama na mwili mwingine amabo tayari VVU ameshaingia na anaishi. Chembe hai nyeupe anapigana na VVU na kumsukuma VVU kwenye eneo fulani la mwili, lakini Chembe hai nyeupe inashindwa kumto VVU nje kabisa ya mwili Waigizaji wanafanya nini VVU wanaingia mwilini, anaanza kwa utaratibu tu kushambulia chembe hai nyeupe. Chembe hai nyeupe anamsukuma pembeni VVU au kwenye kona ya mwili, na kumlazimisha VVU kupungua nguvu.

"Ikiwa ni pamoja na kumweka VVU pembeni, chembe hai nyeupe anabakia kuwa mwenye nguvu na akiweza kuendelea kuafanikisha mapambano dhidi ya maambukizi mengine. Inawezekana

Maambukizi yanaingia tena na chembe hai nyeupe kwa mara nyingine anamsukuma maambukizi nje ya mwili. Maambukizi mengine yanaingia na hali

46

kwa chembe hai nyeupe zikawa bado zenye nguvu na kuendelea kupambana na maabukizi mengine kwa miaka mingi. Kwa kawaida kati ya miaka 5 hadi 10 na wakati mwingine muda mwingi zaidi hadi miaka 20 hata zaidi.kupata lishe nzuri mtazamo chanya kuhusu maisha yake, kuwa na muono wa mbele kupata dawa za kupunguza makali ya VVU ambapo muda wa kuishi unaongezeka. Watu wachache wenye VVU huwa wanakuwa na VVU lakini hawafikii hatu ya UKIMWI."

kama hiyohiyo inatokea.

Hatua ya 3: Kuishi na UKIMWI / Tiba-Kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI Mwezeshaji anasema "Mara nyingi VVU vinaanza kupata nguvu na unaweza kushambulia na kumshinda Chembe hai nyeupe za Damu kwa hiyo mfumo wa kinga ya mwili unauwa dahifu kabisa.". Mwigizaji anafanya nini VVU inasimama na kuvamia chembe hai nyeupe na kushika mikono yote miwili ya chembe hai nyeupe na kuifunga nyuma yake ili kwamba chembe nyeupe za damu hawezi tena kupambana na maambukizi.

"wakati maambukizi mengine yanaingia mwilini sasa, chembe hai nyeupe zinakuwa haziwezi kupamabana tena.kinga ya mwili sasa ni dhaifu sana unaweza kushambuliwa na magonjwa nyemelezi yoyote. Maambukizi yanakuwa huru kukimbia na kucheza kila kwenye kona ya mwili, chembe hai nyeupe zinakuwa hazina nguvu ya kuzuia. Mwili sasa unakuwa umepata UKIMWI ­ "Ukosefu wa Kinga Mwilini "

Maambukizi na maambukizi mengine yote yanauingilia mwili kucheza kila mahali. VVU inaendelea kushikilia Chembe hai nyeupe. Chembe Hai Nyeupe za Damu

47

Wakati mtu anahesabu chembe za CD 4 za chembe hai nyeupe zinashuka na kufikia kati ya chembe 200 kwa maikro lita moja ya damu au wanakuwa na UKIMWI Kuelezea maradhi, wnaweza kuanza kutumia mchanyiko wa dawa za kurefusha maisha ARVs kwa kipindi Fulani. ARV zinauwezo wa kuzuia VVU kuongezeka kama vinavyoka kuwa, ingawaje ARV haiwezi kuondoa VVU moja kwa moja. Zinaruhusu chembe hai nyeupe kujijenga tena, ili ziweze kwa mara nyingine kupambana na maambukizi mengine.

Dawa za kupunguza makali ya VVU (ARV) inaingia mwilini na kushambulia VVU. Kunasua chembe hai nyeupe zilizokamatwa na VVU na kumsukuma VVU kwenye kona. Chembe hai nyeupe zinakusanya nguvu tena kupambana na maambukizi na kutatupa mabali kwenye nje ya mwili.

Hatua ya Pili Mara baada ya kumaliza mchoro wape pongezi waigizaji na kuuliza maswali yaliyoko hapa chini kuhakikisha kwamba kikundi kina elewa dondoo za muhimu kutokana na mchezo.

1. Kuna toafauti gani kati ya VVU na UKIMWI?

Jibu:: VVU ni virusi vinavyosababisha UKIMWI. Mtu anaweza akawa na virusi ila asiwe na UKIMW.

2. Ni kwa muda gani VVU inaweza kupambana na maambukizi bila kuhitaji

msaada wa dawa za kupunguza makali ya VVU? Jibu: inategemea na mtu binafsi ila inaweza kuwa kama miaka 20 au zaidi. Kudumisha mtindo wa maisha wenye afya njema ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi na kupata lishe vinasaidia mwili kupambana na VVU kwa kipindi kirefu zaidi.

3. Ni wakati gani tunaweza kusema mtu ana UKIMWI"?

Ji.bu: wakati mtu anapokuwa na magonjwa nyemelezi na kinga ya mwili haina uwezo wa kupambana na maambukizi. Jibu: dawa hizi huvamia VVU vilivyoko kwenye mwaili na kwamba VVU havitaweza kuongezeka nah ii inawezesha chembe hai nyeupe kujijenga tena ili kuweza kupambana na maambukizi. .

4. Je dawa za kurefusha maisha huwa zinafanya nini mwilini?

48

4.3 Kuenea Na Kuzuia VVU

Hatua ya Kwanza Wakumbushe washiriki kwamba VVU ili viweze kusambaa lazima kuwepo na kiasi cha kikubwa cha virusi vilivyoingia mwilini kupitia njia zinazokuwa hatarishi zaidi kupata maambukizi. Hatua ya Pili Juu ya bango andika "Maji ya mwilini ambayo yanaweza kusambaza VVU". Waulize washiriki ni aina gani ya majimaji ya mwilini wanafikiri yanaweza kusambaza VVU? Andika majibu yote. Baada kikundi kutaja aina zote za majimaji yanayoweza kuwa njia ya kusambaza VVU, angalia orodha hiyo pamoja na washiriki. Pitia kila aina ya majimaji kama ambavyo washiriki watakubaliana kama ni njia ya kusambaza VVU, kama hawataelewana kuhusu njia mojawapo ikate. Endapo kirusi hakitaweza kupita, Kama kuna maji maji mengine ambayo kwenye orodha hayakutajwa andika kwenye bango. Maji maji ya mwilini ambayo yanaweza kusambaza VVU: Majimaji ya ukeni, mbegu za kiume, damu, maziwa ya mama Hatua ya Tatu Sasa juu ya bango jingine andika "VVU vinaweza kuingia mwini kwa njia gani." Waambie wanakikundi je ni njia kuu zipi ambazo VVU vinaweza kuingia mwilini? Andika majibu yote. Baada ya kikundi kumaliza kutaja njia zote amabzo VVU vinaweza kuingia mwilini, angalia orodha hiyo pamoja na wanakikundi. Pitia kila njia na kwa jinsi ambavyo wanakikundi watakavyoa amua kama VVU vinaweza kuingia kwenye mwili. Endapo watashindwa kukubaliana basi iondoe njia hiyo.Kama zipo njia ambazo hawakuzitaja basi ziandike kwenye bango. Hakikisha wanakikundi wanaelewa kwamba Uke, Uume, na Njia ya haja kubwa ni njia kuu za kueneza maambukizi Ni kwa njia gani VVU vinaweza kuingia kwenye mwili: Uke, Uume, Njia ya haja kubwa, kudunga mwili, ameneo ya mwili yaliyo na vVdonda na Uwazi, kupitia Mdomoni Hatua ya Nne Waambie washiriki watafakari kuhusu majimaji ya mwini yaliyotajwa moja baada ya nyingine, kwa kujiuliza "ni kwa njia gani majimaji haya yanaweza

49

kuingia mwilini kupitia njia zilizotajwa" waache wanakikundi wajadiliane na kufanya masahihisho kadri watakavyoona ni muhimu. Kwa mfano maji ya uume, maji ya ukeni na damu vinaweza kusambaza VVU wakati wa vitendo vya ngono kupitia ukeni au kupitia uume au kupitia njia ya haja kubwa. (Ngono kwa njia ya haja kubwa) Angalizo kwa kiongozi Rika: Kikundi kinaweza kujikuta kwenye malumbano kuhusu baadhi ya mambo madogo madogo ya hatari za kinadharia na mengineyo yatakayochokonolewa " "Itakuwaje endapo ......kisa mkasa" . Mwezeshaji anapaswa kuhakiksha kwamba wanakikundi wanaweza kutofautisha baina ya yale yanatowezekana kinadharia na yale tunayofahamu kuwa ni njia za maambukizi ya VVU. Njia kuu za maambukizi ya VVU hapa Tanzania ni ngono. Hatari kubwa ni uume kuingiliana na uke na uume kuingiliana na njia ya haja kubwa. Wakati wa kufanya ngono ya kuingiliana VVU huweza usafirishwa kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume au kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke. Huwa kuna hatari kidogo ya kusambaza VVU kutoka kwenye uume kupitia kinywani. Hakuna kumbukumbu ya matukio ya maambukizi kutoka kwenye kinywa kwenda kwenye uke au kutoka kwenye kinywa kwenda kwenye uume. Mfano wa njia Nadharia za Maambukizi Kuchangia miswaki: hakuna kumbukumbu za matukio duniani pote ila upo uwezekano kwa sababu ya damu kukutana na damu hatuwezi kudharau kabisa Ngono baina ya wanawake ambapo maji maji ya ukeni yanasafirishwa kutoka uke kwenda uke mwingine kwa matumizi ya vifaa vya mfano (toys) vya kufanyia ngono ama vidole (kuna mikasa michache sana ulimwengu mzima kuhusiana na hali kama hii na mijadala bado inaendelea). Ajali kazini: Endapo watu wameumia na wakati huo damu na damu kugusana. Hali hizi si za kawaida na huweza kutokea mara chache sana. Hatua ya Tano Tunaweza kuzuia VVU. Wapatie kitini cha Kuzuia VVU wapitie mikakati mitatu ya kuzuia VVU:

50

Kuacha kabisa mahusiano ya kingono . Chagua kutokujishirikisha na vitendo vya ngono na yeyote. Kuwa mwaminifu kwa mwenzi mmoja mwaminifu . Mfahamu mwenzi wako vizuri na muongee kwa kina kuhusu historia zenu za mahusiano ya kingono. Nendeni mkapime pengine mnaweza kuwa hatarini mmoja wenu ameathirika. Ili makati huu ufanikiwe, mwenzi wako anapaswa kuwa mwaminifu kwako. Kama huna hakika asilimia 100 kwamba mwenzi wako hashiriki vitendo vya ngono na watu wengine, tumia kondom pamoja na kuendelea kuwa waaminifu. Tumia kondom kila wakati unapofanya ngono kupitia ukeni au kwa njia ya mdomo endapo....... · Unampenzi zaidi ya mmoja · Wewe au / mwenzi wako hajapima kama ana maambukizi ya VVU; · Huna hakika 100% kwamba mwenzi wako hajishirkishi na ngono na watu wengine e Kwenye saluni yako msichangie sindano nyembe au vitu vingine vya kutogea. Kama umelazimishwa kuchangia vitu kama hivyo kila mara visafishe kwa maji na vitakasio kama blichi. Uwe na hakika kwamba maji masafi peke yake havitoshi kutakasa. Tumia maji na blichi ingawaje huwa inaharibu makali ya nyembe .

4.4 Kupima VVU

Hatua ya Kwanza Waulize washiriki maswali yafuatayo: Ni kwa namna gani mtu anaweza kufahamu kuwa ana VVU au la? Kipimo cha VVU huwa kinapima nini? Hatua ya Pili Wapatie washiriki kipimo cha VVU na alika mtu ajitolee kusoma taarifa ifuatayo: Kipimo cha VVU Kinaelezea endapo mwili wa mtu umezalisha antibodi za VVU za kupambana na virusi Majimaji ya mwilini ambayo huwa yana VVU wengi ambao wanaweza kusababisha uambukizi ni pamoja na damu, maji ya uume, maji ya ukeni, na maziwa ya mama. Kipimo cha VVU hakina uwezo wa kutoa maelezo kama:

51

Endapo mtu ana UKIMWI (Ni daktari peke yake ndie mwenye uwezo wa kufanya vipimo hivi) Ni kwa njia gani huyu mtu alipata maambukizi ya VVU Kwa muda gani huyu mtu ameishi na VVU. Nani alimwambukiza

Mtu anaweza kupima VVU hospitalini au klinik. Yapo mashirika yanayofanya kazi kuhusu UKIMWI ambao huwa wanatoa huduma za kupima VVU.

Waambie washiriki kwamba ni muhimu kuwa na orodha ya maeneo ambayo huduma ya ushauri nasaha na kupima hutolewa na kuwa nayo kwenye saluni yako ili kuwapatia wateja wa saluni yako ambao wataonyesha nia ya kuhitaji huduma hizo. Wahamasid=she waweze kuongea na vituo vya kutolea huduma vilivyoko jirani katika kuweza kutengeneza orodha hii kwa ajili ya jamii. Hatua ya Tatu Waulize washiriki: kwanini ni muhimu kupima VVU? Pata majibu mengi na uyaandike kweny bango. Hakikisha majibu yaliyoorodheswa hapa chini yametajwa. Tarajia majibu yafuatayo: Njia pekee ya kufahamu kama wewe au mwenzi wako ana VVU ni kupima. . Watu wenye VVU walio wengi huwa hawana dalili na wanaweza wasiiwe na dalili zozote na hawana maradhi yoyote ya muda mrefu hata baada ya kuambikizwa. Hata wakati ambapo watu wenye VVU hawana dalili zozote lakini bado wanaweza kuambukiza wengine. Watu wengi waliopimwa wamekutwa hana maambukizi. Kama umepima na ukawa hauna maambukizi unaweza kukaa na mshauri nasaha na kuchanganua tabia hatarishi maishani mwako na kujifunza namna ya kuendelea kuishi bila maambukizi. Kama utapima na kukutwa una maambukizi unaweza kukaa na mshauri nasaha kujifunza jinsi ya kuishi maisha chanya yenye afya na ya

52

utoshelevu ukiwa na VVU. Unaweza kutambua tabia hatarishi maishani mwako na kujifunza jinsi ya kuzizuia na kuzuia kuambukiza wengine.

4.3 Unyanyapaa na VVU/ UKIMWI

Hatua ya Kwanza Waulize washiriki nini maana ya Unyanyapaa? Andika majibu kwenye bango na uyatumie majibu yaliyoorodheshwa hapa chini kuhitimisha. Pia waulize wakupatie mifano yakuonyesha unyanyapaa. Majibu yanayotarajiwa: Unyanyapaa unaweza kuelezewa kama "alama ya aibu au kudharauliwa mtu au kikundi cha watu". Unyanyapaa msingi wake ni hofu na ukosefu wa ufahamu. Mifano ya unyanaypaa unaowaathri watu wanaoishi na VVU/UKIMWI na familia zao: Wakati ambapo wanafamilia wanapomfukuza mwanafamilia wao nyumbani kwa sababu anapima na kugundulika ana VVU; Wakati ambapo mtu anapofukuzwa kazini kwa sababu amepatwa na VVU; Wakati ambapo mume anampiga mkewe kwa vile amegundua kwamba amepima na akakutwa ana maambukizi ya VVU. Waambie washirki kwamba kwa bahati mbaya mara nyingi watu wanaoishi na VVU wananynyapaliwa na watu wa jamii wanamoishi. Hii ina maana kwamba wanatendewa kinyume au kubaguliwa, kwa vile wanaishi na VVU/AIDS, au kwa sababu wanafahamu fulani anaishi na VVU/UKIMWI. Wanawake na wasichana mara nyingi wanaaandamwa na unayanaypa kwenye jamii wanapolaumiwa kuwa wanasambaza VVU. Hatua ya Pili Waulize washiriki, ni kwa namna gani unyanyapaa unaathiri kuzuia VVU? Baada ya kupat majibu weleze washiriki kwamba unyanyapaa ni hatari kwa sababu inawawia watu vigumu kutafuat huduma za taarifa na msaada, kama vile wapi kipimo cha VVIU kianapatikana, jinsi ya kuizuia na VVU au wapi pa kupata tiba. Unyanyapaa unawasababisha watu kuvunjiak moyo kutumia

53

kondom kwa hofu ya "kujulika" au kutuhumiwa kuwa na VVU kama watakuwakuwa wanasisitiza kutumia kondom. Hatua ya Tatu Waulize washiriki: Tunaweza kwa namna gani kupunguza unyanyapaa? Waeleze washiriki kwamba unyanyapaa msingi wake ni hofu na kutokuwa na ufahamu kwa hiyo njia nzuri ya kupambana na unyanyapaa ni kupitia kupatiwa taarifa na kuzipokea. Waambie washiriki wabunge bongo kuhus ni njia zipi ambazo wanaweza kuzitumia kupambana na unyanyapaa kwenye jamii yao na hasa kweny saluni zao. Pitia majibu yaliyoko hapa chini endapo washiriki hawakuyataja. Majibu tarajiwa: Kushirikisha taarifa sahihi kuhusu VVU na UKIMWI na kuongelea kuhusu hayo wazi wazi. Bila kificho wakubali wanajamii wateja na ndugu au marafiki wanaoishi na VVU. Kama kiongozi kwenye jamii njia hii ianweza ikaleta mabadiliko makubwa kuhusu namna watu wengine wanavyowatendea watu wanaoishi na VVU (WAVIU). Hatua ya Nne Hitimisha ujumbe muhimu. Ujumbe muhimu: Taarifa kuhusu VVU na UKIMWI VVU ni maambukizi kama yalivyo maambukizi mengine ya magonjwa mengine ya Ngono hayawezai kuonekana. Watu wengi huwa hawafahamu kama wana VVU.Njia pekee ya kufahamu ni kupima tu. VVU ni maambukizi amabyo yanaweza kusababisha UKIMWI wakati ambapo mtu anapoumwa mara kwa mara. Hakuna tiba ya VVU au UKIMWI. Kuna mikakati mitatu ya kuzuia VVU: Kuacha mahusiano ya kingono, kuwa mwaminifu kwa mwenzi mmoja na kutumia kondom kila wakati na kwa usahihi ni baadhi ya mikakati hiyo.

54

Njia pekee ya kufahamu kama una VVU ni kuafanya kipimo cha VVU. Unyanyapaa kichocheo chake kikubwa ni hofu. Unyanyapaa huumiza kisaikolojia, kiakili na hata wakati mwingine kimwili. Unyanyapaa unafanya iwe vigumu kutafuta taarifa au msaada kama vile wapi wakapime VVU au wapi wakapate tiba. Kama viongozi kwenye jamii yetu tunaweza kuwasaidia wanajamii kupambana na unyanyapaa kwa kufanya yafuatayo. 1) Kushirikishana taarifa sahihi kuhusu VVU na UKIMWI na kuyaongelea wazi wazi. 2) Bila kificho kuwakubali wanajamii wateja na ndugu au marafiki wanaoishi na VVU. Kama kiongozi kwenye jamii njia hii inaweza ikaleta mabadiliko makubwa kuhusu namna watu wengine wanavyowatendea watu wanaoishi na VVU (WAVIU).

55

KITINI CHA MADA YA 4

KUZUIA VVU

1. Kuacha kabisa mahusiano ya kingono: Chagua kutokujishirikisha na vitendo vya ngono na yeyote. 2. Kuwa Mwaminifu kwa mwenzi mmoja mwaminifu: Mfahamu mwenzi wako vizuri na muongee kwa kina kuhusu historia zenu za mhusiano ya kingono. Nendeni mkapime pengine mnaweza kuwa hatarini mmoja wenu ameathirika. Ili mkakati huu ufanikiwe, mwenzi wako anapaswa kuwa mwaminifu kwako. Kama huna uhakika asilimia 100 kwamba mwenzi wako hashiriki vitendo vya ngono na watu wengine, tumia kondom pamoja na kuendelea kuwa mwaminifu. 3. Kutumia Kondom kila wakati unapofanya ngono kwa njia ya uke, njia ya haja kubwa au kwa njia ya kinywa endapo......... o Unakuwa na zaidi ya mwezi mmoja wa kingono ; o Wewe/au mwenzi wako hamjapima VVU; o Huna uhakika asilimia 100 kama mwenzi wako anajihusisha kingono na watu wengine.

56

KITINI CHA MADA YA 4

KUPIMA VVU

Kipimo cha VVU ndicho huonyesha endapo mtu amezalisha antibodi za kupambana na virusi. Kipimo cha VVU hakiwezi kuonyesha endapo: Mtu ana UKIMWI (ni daktari peke yake anaweza kupima na kuelezea) Ni kwa njia gani mtu alipata maambukizi ya VVU Kwa muda gani mtu amekuwa akiishi na VVU Nani aliyemwambukiza Mtu anaweza kupata kipimo cha VVU hospitalini au kliniki. Yapo pia mashirika ya misaada ambayo hutoa huduma ya upimaji VVU.

57

KITINI CHA MADA YA 4

UJUMBE MUHIMU KEY MESSAGES: TAARIFA KUHUSU VVU NA

UKIMWI

VVU ni maambukizi kama yalivyo maambukizi mengine ya magonjwa mengine ya Ngono hayawezi kuonekana. Watu wengi huwa hawafahamu kama wana VVU.Njia pekee ya kufahamu ni kupima tu. VVU ni maambukizi ambayo yanaweza kusababisha UKIMWI wakati ambapo mtu anapoumwa mara kwa mara. Hakuna tiba ya VVU au UKIMWI. Kuna mikakati mitatu ya kuzuia VVU: Kuacha mahusiano ya kingono, Kuwa mwaminifu kwa mwenzi mmoja na kutumia kondom kila wakati na kwa usahihi ni baadhi ya mikakati hiyo. Njia pekee ya kufahamu kama una VVU ni kufanya kipimo cha VVU. Unyanyapaa kichocheo chake kikubwa ni hofu. Unyanyapaa huumiza kisaikolojia, kiakili na hata wakati mwingine kimwili. Unyanyapaa unafanya iwe vigumu kutafuta taarifa au msaada kama vile wapi wakapime VVU au wapi wakapate tiba. Kama viongozi kwenye jamii yetu tunaweza kuwasidia wanajamii kupambana na unyanyapaa kwa kufanya yafuatayo. 1) Kushirikisha taarifa sahihi kuhusu VVU na UKIMWI na kuongelea kuhusu hayo wazi wazi. 2) Bila kificho kuwakubali wanajamii wateja na ndugu au marafiki wanaoishi na VVU. Kama kiongozi kwenye jamii njia hii inaweza ikaleta mabadiliko makubwa kuhusu namna watu wengine wanavyowatendea watu wanaoishi na VVU (WAVIU).

58

MADA YA TANO: KONDOM

Mada Ndogo 5.1 Mambo ya msingi kuhusu kondom 5.2 Maonyesho ya naman ya kutumia bidhaa: Dume na Lady Pepeta Madhumuni: Mwisho wa somo tutakuwa tumefanya yafuatayo: Tambu taarifa muhimu kuhusu kondom Shiriki kwenye mazoezi ya matumizi ya kondom za Lady Pepeta na Dume Zana Karatsi za bango na kalamu (markers) Kondomu za Lady Pepeta na Dume Mfano wa umbo la uume na uke Kitini cha Hatua za kutumia kondom ya kiume Kitini cha Hatua za kutumia kondom ya kike Kitini cha Ujumbe muhimu: Kondom Muda Dk 30

5.1 Msingi wa kondom

Angalizo kwa Kiongozi wa Rika: Kabla ya kuanza zoezi hili na ili liwe la kuvutia ficha kondomu ya kike na ya kiume mahali fulani kwenye chumba kabla ya kuanza somo. Hatua ya kwanza Waambie washiriki kuangalia kila mahali kenye chumba na wapate kondomu ya DUME na Lady Pepeta zilizofichwa kwenye kona mbalimbali za chumba. Baada ya dakika chache waulize kama wameziona bidhaa hizo. Baada ya hapo washiriki wote warudi kwenye somo kwa ajili ya majadiliano. Hakikisha washiriki wamepata kondom ya kike nay a kiume: Dume na Lady Pepeta. Waulize washiriki:

59

Je wanafahamu kondom gani? Watu huwa wanasema nini kuhusu kondom? Hatua ya Pili Pitia aina mbalimbali za bidhaa ya kondom ambazo zinapatikan kwa urahisi na mahali ambapo wanaweza kununua. Hakikisha kwamba Dume na Lady Pepeta ni miongoni mwa hizo. Taja kondom nyingine zaidi kama unazifahamu. Jina la Kondom Kondomu ya Dume Gharama yake na mahali pa kuipata - Tshs 100 -Maduka ya dawa, dukaa kuu la kujihudumia bidhaa, maduka madogo bar na nyumab za kulala wageni -Tshs100 - Maduka ya dawa, dukaa kuu la kujihudumia bidhaa, maduka madogo, bar na nyumba za kulala wageni

Kondom ya Lady Pepeta

Kabla ya kwenda kwenye jambo lingine kuna mambo mawili muhimu ya kuzingatia. Kondom zote hizi zimehakikiwa kwa ubora na viwango vya usalama zote zinauwezo wa kuhimili kutulinda na maambukizi. Ila lazima zitumike kwa usahihi. Kondom zote hizi zimewekewa maufta maalum ya kuwezesah kutumika kwa urahisi. Hatua ya Tatu Angalizo kwa kiongozi wa Rika: Hii ni fursa ya kujadiliana kwa uwazi na ukweli sababu za kwanini watu huwa hawatumii kondom. Wawili wawili washiriki wajadiliane maswali yafuatayo:. Zipi ni sababu ambazo umewahi kuzikia watu wakitoa kuhusu kutotumia kondom? Wapatie dakika chache ndipo ualike watakaojitolea kutoa sababu walizowahi

60

kuzisikia Give them a few minutes and then ask for volunteers share the reasons they have heard. Eleza kwamba hivi ni vikwazo au vizuizi kwa watu amabo wanataka kuafnya ngono salama. Vizuizi au vikwazo hivi lazima tuvishinde enedpao tunataka watu watumie kondom. Sas baada ya kutambua vikwazo vya kwanini watu hatumii Kondom , hebu tuajadiliane faida: waulize washiriki zipi ni faida za kutumia kondom ? Majibu Tarajiwa: Kondom zinatulinda na mimba zisizotarajiwa Kondom zinatulinda na magonjwa ya ngoNo ukiwemo UKIMWI Wakati ukifanya Ngono Salama huna haja ya kuwa na hofu ya kupata mimba magonjwa ya ngono au VVU unakuwa huru kufurahia. Ni safi haileti karaha ya kufanyia usafi

5.2 Maonyesho ya Bidhaa Za Dume na Lady Pepeta

Hatua ya Kwanza Mwambie mashiriki mmoaj ajitolee kuwaonyesha wengine jinsi ya kutumia kondom ya kiume. Kama hakuna aliye tayari kuonyesha unaweza wewe kuwa wa kwanza kuonyesha. Wahimize wote washiriki kufanya zoezi hili hata kama wanafahamu jinsi ya kufanya. Usiwaeleze hatua 5 za kuvaa na kuvua kondom ya DUME. Baada ya kuwasikiliza wakiongea unaweza kutaka kuongezea wazo lako ­ onyesha kile walichofanya kwamba kilikuwa salama na kile ambacho huenda walisahau kilikuwa ni cha umuhimu. Hatua ya Pili Sasa kila mmoja amepata fursa ya kujaribu, rejea njia sahihi za matumizi ya kondom pamoja na kundi lote. Wapatie kitini cha JInsi ya Kutumia Kondom ya Kiume wasome kwa utaratibu maelekezo yote ya jinsi ya kuvaa na kuvua kondom. Mtu mmoja ajitolee aonyeshe kila hatua kama unavyosoma.

61

Hatua TANO za kutumia kondom: MOJA : Angali tarehe ya kumalizika muda wake wa matumizi au hakisha pakiti haijapasuka kabla ya kufungua. Kwa utaratibu fungua pakiti. Hakikisha kondom haichaniki wakati wa kufua pakiti.

MBILI: Valisha kondomu kwenye uume uliosimama. Shikilia kwenye chuchu ya kondom.

TATU : Endelea kuminya chuchu ya kondom na anza kuviringisha taratibu kulekea sehemu ya chini ya uume uliosimama. Endapo kondom itateleza na kutoka wakati wa zoezi hili tumia kondom nyingine. ..

62

NNE: Baada kitendo cha ngono, shikilia chini kwenye shina la uume wakati uume ukiwa umesimama viringisha kondom kuivua. Hakiksha uume na kondomu iliyotumika havijakaribiana na uke au sehemu yoyote ya mwili.

TANO: Ifunge fundo kondom iliyotumika na uitupe kwenye chombo cha takataka. Usiitupe kondom chooni.

Waulize washiriki: Kwenye jaribio la awali, ni hatua ipi tuliyoifanya tuliifanya kwa ufanisi zaidi ? Je tumesahau nini? Kwanini uanhiatji kuminya chuchu ya juu ya kondom wakati wa kuivaa? Hatua Tatu Waambie washiriki kwamba sasa tunaangalia kuhusu kondom ya kike. Waeleze kwamba kondom ya kike ni utando mwembamba ambao huvaliwa na wanawake wakati wa tendo la ngono. Hufunika eneo lote la uke na huzuia mimba na maambukizi ya magonjwa ya ngono, ikiwa ni pamoja na VVU. Hapa Tanzania aina hii ya kondom hujulikana kama Kondom ya Lady Pepeta.Hakikisha unazo sampuli za kutosha za Lady Peptea kwa ajili ya wanawake wote kuzifahamu Lady Pepeta. Waambie kwamba watapatiwa kondom za bure wakati wa mwisho wa somo.

63

Waulizea wshiriki wote: Umewahi kuiona kondom ya Lady Pepeta? Je unafamu nini kuhusiana na kondom hii?

Angalizo kwa Kiongozi wa rika: Hii ni bidhaa mpya na watu wengi wanaweza wasiwe wanaifahamu Lady Pepeta. Hii ni fursa nzuri ya kuelezea na kuwapatia baadhi ya kondom za kike kila mmoja aweze kuiona na kuigusa. Unapaswa uonyeshe kwa ufasaha jinsi ya kuitumia kondom ya kike ya lady Pepeta kwa kutumia mfano wa umbo la uke kama itapatikana. Hakikisha kila mmoja ana shiriki kufanya mazoezi haya.Ili ujihakikishie kuwa wanajiamini kutumia kondom ya kike. Kama huwezi kupata mfano wa umbo la uke unaweza kutumia viganja vyako au unaweza kukata kitako cha chupa ya plastiki ili uweze kuona pete ya kondom kwa nje na sehemu nyingine iliyosalia ikiwa inaningiania kwa ndani. ya chupa. Hatua ya Nne Waambie washiriki wakuangalie wakati unaonyesha kwa vitendo jinsi ya kutumia kondom ya kike. Wapatie kitini Jinsi ya kutumia kondom ya kike na washiriki wafuate hatuya zilizoainishwa (kama utaamua kuwapatia)

64

Jinsi ya kutumia kondom ya kike Jinsi ya Kuanza Hatua ya Kwanza: Fungua pakiti ya kondom kwa makini kwa kukata sehemu iliyowekewa alamasehemu ya juu ya pakiti. Usitumie mkasi au kisu unaweza kuitoboa kondom. Hatua ya 2: Kondom ya kike inaonekana kama kondom ya kiume iliyo kubwa sana inakuwa na pete mbili: pete iliyoko kwa nje inafumika njia ya uke na pite ya ndani inatumika kuiingiza kondom nani ya uke. Pia inasaidia kuizuia kondom isitoke wakati wa tendo la ngono. Hatua ya 3: Ukiwa umeishikilia kondom kwa karibu, ishike kwenye pete ya ndani na uiminye kwa kutumia kidole gumba na kidole cha pili cha shahada kwa hiyo inakuwa kama umbo la nane ndefu na nyembamba. Hatua ya 4: Chagua mkao ambao unaona ni wa kufaa ili uweze kuingiza kondom kwenye uke - chuchumaa,inua mguu mmoja, keti au lala chali. Hatua ya 5: Taratibu sana ingiza pete ya ndani kwenye uke. Isikilizie pete ya ndani imeingia nadani na kukaa mahala pake. Hatua ya 6: Ingiza kidole cha kati ndani ya kondom na usukume pete ya ndani ya kondom ndani kadri inavyoweza kuingiza. Hakikisha mfuniko wake haujakaa vibaya. Pete ya nje inatakiwa iendlee kuwa kwa nje ya uke Hatua ya 7: Kondom ya kike sasa iko mahali pake na sasa uko tayari kwa ajili ya tendo la ngono. Hatua ya 8: Baada ya kumaliza kuweka kondom yako ya kike, kwa uratibu elekeza uume wa mwenzi wako kwenye eneo la wazi kwa kutumia mkono wako kuhakikisha kwamba inaingia sawasawa ­ hakikisha kwamba uume hauingii pembeni yaani kati ya kondom na kuta za uke. Jinsi ya Kumaliza Hatua ya 9: Kutoa kondom ya kike, zungusha pete ya nje na taratibu ivute kondom nje.. Hatua ya 10: Ifunge kondom kwenye kimfuko au karatasi na uitupe kwenye chombo

65

cha takataka. Usiitumbukize chooni.

Waulize washiriki: Je mna maswali au hofu yoyote? Nini kilichokushangaza kutoka na kondom hii?

Hatua ya tano Waeleze washiriki kwamba tutajadiliana kuhusu maswali mawili ambayo huulizwa mara kwa mara kuhusiana na kondom ya kike. Uliza maswali na pata majibu kutoka kwa kikundi .Hakiksha wamekupatia majibu sahihi. Maswali Majibu Naweza kuiweka kondom ya Kondom ya kike inaweza kuwekwa hadi kwa kike masaa mangapi kabla masaa nane kabla ya tendo la ngono ili isije ya kufanya kitendo cha ikaingiliana na wakati. ngono? Je naweza kuitumia kondom ya kike zaidi ya mara moja? Inashauriwa kondom ya kike itumike mara moja tu.

Hatua ya Sita Wapatie Ujumbe Muhimu: Pitia Kitini cha kondom pamoja na kikundi. Ujumbe Muhumu: Kondom Wanawake wanaweza kujilinda wao wenyewe kutokana na magonjwa ya ngono ikiwa ni pamoja na UKIMWI na mimba zisizotarajiwa kwa kutumia kondom na wenzi wao kila wakati na kwa usahihi. Kondom ya Dume na Lady Pepeta ni rahisi na zinapatikana kwenye maeneo mengi ya kuuzia kondom..

66

Ili kondom iweze kufanikisha ni lazima itumike kwa usahihi, kufanya mazoezi ya jinsi ya kutumia yanasaidia kutumia vizuri. Ni muhimu kushirikishana taarifa kuhusiana na umuhimu wa kutumia kondom kila wakati na kwa usahihi ili kuzuia mimmab zisizotarajiwa magonjwa ya ngono, na kuzuia maambukizi ya VVU kwa wateja wa saluni yako. Hatua ya Saba Waambie washiriki kwamba kwa sasa tumemaliza sehemu ya pili ya mafunzo yetu ya Mpango wa Jipende kwa ajili ya Saluni. Tunapenda kuwashukuru kwa kuja leo na tutakutana wiki ijayo kumalizia mada za kusisimua zilizobakia. Kabla hamjaondoka tafadhali jaza dodoso la maswali ya kutathmini masomo haya. Wapatie fomu ya tathmini washiriki wote na uzikusanye watakapokuwa wanaondoka.

67

KITINI CHA MADA YA 5

HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA KUTUMIA KONDOM YA

KIUME

MOJA: Angali tarehe ya kumalizika muda wake wa matumizi au hakisha pakiti haijapasuka kabla ya kufungua. Kwa utartibeu fungua pakiti. Hakikisha kondom haichaniki wakati wa kufua pakiti.

MBILI: Weka kondomu kwenye uume uliosimama. Shikilia kwenye chuchu ya kondom.

TATU: Endelea kuminya chuchu ya kondom na anza kuviringisha taratibu kuelekea sehemu ya chini ya uume uliosimama. Endapo kondom itateleza na kutoka wakati wa zoezi hili tumia kondom nyingine. NNE: Baada kitendo cha ngono, shikilia chini kwenye shina la uume wakati uume ukiwa umesimama. Hakiksha uume na kondomu iliyotumika havijakaribiana na uke au sehemu yoyote ya mwili .

TANO: ifunge fundo kondom iliyotumika na uitupe kwenye chombo cha takataka. Usiitupe kondom chooni.

68

KITINI CHA MADA YA 5

HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA KUTUMIA KONDOM YA KIKE

Hatua ya 1: Fungua pakiti ya kondom kwa makini kwa kukata sehemu iliyowekewa alama kwenye sehemu ya juu ya pakiti. Usitumie mkasi au kisu unaweza kuitoboa kondom.. Hatua ya 2: kondom inaonekana kama kondom ya kiume kubwa sana iliwa na pete mbili: pete iliyoko kwa nje inafumika njia ya uke na pite ya ndani inatumika kuiingiza kondom nani ya uke. Pia inasaidia kuizuia kondom isitoke wakati wa tendo la ngono. Hatua ya 3: Ukiwa umeishikilia kondom kwa karibu, ishike kwenye pete ya ndani na uiminye kwa kutumia kidole gumba na kidole cha shahada kwa hiyo inaonekana kama umbo la namba nane ndefu na nyembamba. Hatua ya 4: Chagua mkao ambao unaona ni wa kufaa ili uweze kuingiza kondomchuchumaa,inua mguu mmoja, keti au lala chali . Hatua ya 5: Taratibu sana ingiza pete ya ndani kwenye uke. Isikilizie pete ya ndani imeingia ndani na kukaa mahala pake. Hatua ya 6: Ingiza kidole cha kati ndani ya kondom na usukume pete ya ndani ya kondom ndani kadri inavyoweza kuingia. Hakikisha mfuniko wake haujakaa vibaya. Pete ya nje inatakiwa iendlee kuwa kwa nje ya uke. Hatua ya 7: Kondom ya kike sasa iko mahali pake na sasa uko tayari kwa ajili ya tendo la ngono. Hatua ya 8: baada ya kumaliza kuweka kondom yako ya kike , kwa uratibu elekeza uume wa mwenzi wako kwenye eneo la wazi kwa kutumia mkono wako kuhakikisha kwamba inaingia sawasawa ­ hakiksha kwamba uume hauingii pembeni kati ya kondom na kuta za uke. Jinsi ya Kumaliza Hatua ya 9: Jinsi ya kuvua kondom ya kike, zungusha pete ya nje na taray=tibu ivute kondom nje. Hatua ya 10: Ifunge kondom kwenye kimfuko au karatsi na uitupe kwe chombo cha takataka. Usiitumbukize chooni.

69

KITINI CHA MADA 5

UJUMBE MUHIMI: KONDOM

Wanawake wanaweza kujilinda wao wenyewe kutokana na magonjwa ya ngono ikiwa ni pamoja na UKIMWI na mimba zisizotarajiwa kwa kutumia kondom na wenzi wao kila wakati na kwa usahihi. Kondom ya Dume na Lady Pepeta ni rahisi na zinapatikana kwenye maeneo mengi ya kuuzia kondom.. Ili kondom iweze kufanikisha ni lazima itumike kwa usahihi, kufanya mazoezi ya jinsi ya kutumia yanasaidia kutumia vizuri. Ni muhimu kushirikishana taarifa kuhusiana na umuhimu wa kutumia kondom kila wakati na kwa usahihi ili kuzuia mimmab zisizotarajiwa magonjwa ya ngono, na kuzuia maambukizi ya VVU kwa wateja wa saluni yako.

70

MAFUNZO YA PILI : FOMU YA TATHMINI

Fomu hii ni ya siri.Usiandike jina lako. Asante. 1. Je matarajio yako kwa ajili ya mafunzo haya yamefikiwa? (Weka mduara kwenye jibu) NDIO HAPANA Kama hapana, kwanini ni hapana? 2 Je ni mada gani umeipenda zaidi? Kwanini ?

3 Mada gani hujaipenda? Kwanini?

4.

Ni mada ipi tulihitaji kuipa muda zaidi?

Unaweza kupima namna gani mtindo wa uwezeshaji? ( zungushia duara jibu moja) ? e. Nzuri sana f. Wastani g. Nzuri h. Dhaifu Maoni: 5. Je tunweza kufanya nini tofauti ili kuboresha yaliyomo kwenye mafunzo haya? Tunaweza kufanya nini touti ili kuboresha utaratibu mzima wa mafunzo haya? (muda, mapumziko ya chai/ kahawa, n.k) Kwa ujimla, unaweza kuyapa mafunzo haya kiwango gani cha ufanisi? (Weka duara kwenye jibu moja) b. Nzuri sana b. Nzuri c. wastani d. Dhaifu Tumia nyuma ya ukurasa huu kama unayo maoni zaidi.

71

MAFUNZO YA 3 MADA YA SITA: SARATANI YA MATITI NA SHINGO YA

KIZAZI

Mada ndogo 6.1 Saratani ya matiti na ya shingo ya uzazi uelewa kuhusu dalili (dk 45) 6.2 Umuhimu wa kujichunguza mwenyewe saratani ya matiti (dk 15) Madhumuni: Mwisho wa somo tutaweza kufanya yafuatayo: Kuelezea faida za uelewa kuhusu dalili za saratani ya shingo ya kizazi na matiti. Kutambua hatua za kufuata wakati wa kujichunguza-mwenyewe matiti Zana: Bango na kalamu (markers) Kitini cha Jinsi ya kujichunguza saratani ya matiti Kitini cha Saratani ya shingo ya kizazi Wageni waalikwa: Wataalamu wa masuala ya saratani kutoka MEWATA ( dakika 60 ) Muda Time: Dakika 40

6.1 Uelewa kuhusu Saratani ya Matiti

Hatua ya kwanza Waambie washiriki kwamba tutaongelea kuhusu maradhi yanayowathiri afya za wanawake, na jinsi ya kuyazuia. Waambie washiriki ajitolee yeyote na aeleze anaelewa nini kuhusu Saratani ya Matiti na ya Shingo ya Kizazi, mathalani, kama inaweza kutibika na kupona, zipi ni taratibu za matibabu yake, na uzoefu wake binafsi kuhusu saratani hizi nk. Swali lolote litakaloulizwa wakati wa majadiliano haya linaweza kuelezewa baadae na mwakilishi kutoka MEWATA. .

72

HATUA YA PILI Kama uliweza kualika mwakilishi kutoka MEWATA (Chama cha wanawake Madaktari Tanzania) mtambulishe mgeni wako maalumu na muombe aanze kuelezea kuhusiana na dalili za saratani ya matiti na shingo ya kizazi na umuhimu wa kujichunguza mwenyewe (SBE) na pia aonyeshe kwa vitendo hatua za kuchujinguza mwenyewe saratani ya matiti. Kama hukuweza kumpata mwakilishi kutoka MEWATA kuongelea mada hii, hizi hapa ni badhi ya mambo ya ukweli kuhusu saratani ya matiti ambayo unaweza kuwashirikisha washiriki wako. Waambie washiriki kwamba: 1. Kuna mambo mengi tunayoweza kufanya ili kujilinda afya zetu, sasa tutaongea kuhusu saratani ya matiti. MEWATA (Chama cha wanawake Madaktari Tanzania) wamefanya kampeni za kitaifa kuhusiana na ksaratni ya matiti ili kujenga uelewa na pia kupima. 2. Mpango huu wa elimu kuhusiana na saratani ya matiti inafanyika kwa ushirikiano kati ya kituo cha kurusha matangazo ya luninga cha binafsi ITV/Radio One, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wadau wengine ambao wamekuwa wakijitolea michango yao ya fedha na vifaa kwa ajili ya kufanikisha kampeni hii. Kampeni hii imesababisha kuwa na ongezeko la ujumla la uelewa kuhusiana na saratani ya matiti hapa nchini na kuwa na ongezeko la wanawake kuhudhuria hospitali wakiulizia huduma za kuchunguzwa matiti. 3. Kwa kuyachunguza matiti mwenyewe kwa utaratibu wa kila mwezi, wanawake wanaweza kutambua kama wana saratani ya matiti mapema. Kadri saratani itakavyogundulika mapema ndivyo inaongeza uwezekano wa matibabu kuwa ya mafanikio pia wanawake wanashauriwa kuwa na tabia ya kujichunguza kila mwezi (BSE) na ikiwezekana siku 3-5 baada ya kuona hedhi ya mwezi husika na wanawake ambao wameshakoma kuona hedhi wanapaswa kuwa na siku maalumu kila mwezi ya kujichunguza (BSE). 4. Wakati wa kujichunguza matiti wanawake wanashauriwa kuwa wanapaswa kuwa makini kugundua hali yoyote isiyokuwa ya kawaida kama vile kubadilika kwa kwa ngozi ya matiti, kuwa na uvimbe, kama chuchu zinatoa majimaji, na endapo dalili moja wapo kama hizo itaonekana unashaurriwa kureport kwenye kituo cha afya kilicho karibu.

73

5. Wanawake walio na umri zaidi ya miaka 40 wanashauriwa kuwa mabli na kujichunguza matiti na kuchunguzwa kliniki kila mwezi (BCE) wanapaswa kufanyiwa kipimo cha mammography kila mwaka au kila mwaka mara mbili kwa maeneo ambayo kipimo hicho kinapatikana hapa Tanzania ).

6.2 Kujichunguza mwenyewe Matiti

Hatua ya Kwanza Waambie washiriki kwamba ni muhimu kwa wanawake kufahamu namna ya kujichunguza kila mwezi (BSE) kugundua dalili za saratni ya matiti. Wapatie kitini cha jinsi ya kujichunguza saratani ya matitii. Soma na kujadiliana hatua za kujichunguza mwenyewe (BSE) pamoja na washiriki. . Hatua ya Pili Wapatie washiriki kitini cha saratani ya shingo ya uzazi na kupitia taarifa zilizomo kuhusiana na saratani hiyo pamoja na kikundi. Maana · · · · Ni aina ya vivimbe vinanvyotokea katika titi ambavyo vinaweza kuwa saratani Si vivimbe vyote vinavyotokea ni saratani Wanaume pia wanaweza kupata saratani ya matiti(1% ya wagonjwa ya saratani ya matiti ni wanaume) Mfano: jipu, vivimbe visivyo saratani Vitu gani husababisha · · Hakuna kitu cha moja kwa moja kinachosababisha ugonjwa huu Mara nyingi huwakuta watu wazima Nani yuko kwenye hatari ya kupata saratani ya matiti? · · · · · Mwanamke Mtu mwenye historia ya magonjwa ya saratani kwenye familia yao hasa ya matiti Mtu aliyewahi kupata saratani Wanawake wasiozaa au waliochelewa kuzaa Utumiaji wa vidonge vya majira vyenye vichocheo vya istrogeni kwa kiwango cha juu sana(zamani)

74

· · ·

Uvutaji wa sigara Unywaji wa pombe wa kupitiliza(ulevi) Mtu aliyewahi kupigwa "mionzi" Dalili

·

Uvimbe usiouma, ambao · Si wa kawaida katika titi · Mara nyingi una tabia ya kuhama kuhama unapoguswa · Unakua kwa taratibu sana · Unafanana na kibuja Kubadilika ngozi ya titi ­ganda la chungwa Chuchu kuzama ndani Kutokwa na majimaji ,damu kwenye chuchu Kidonda kisichopona Titi kukua zaidi ya lingine kusiko kawaida Matibabu

· · · · ·

· · ·

Upasuaji Mionzi Madawa Kujichunguza matiti

· · ·

Kwa kila mwanamke Ndani ya siku tano baada ya kumaliza hedhi au tarehe maalumu kwa wanawake waliokoma hedhi Ni muhimu kujichunguza kila mwezi Vifaa vinavyohitajika

· ·

Kiganja cha mkono Kioo

75

Namna ya kujichunguza · · · · Kwa kutumia kiganja papasa titi kwa mwendo wa saa mpaka umalize titi lote Nenda kwa kupapasa mpaka kwenye kwapa Malizia kwa kukamua chuchu Jiangalie kwenye kioo kama matiti yanalingana(ukubwa na urefu) Ukweli kuhusu saratani ya matiti · · · · Si ugonjwa wa kuambukiza (mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine, kunyonyesha n.k) Ukiwahi mapema kwenda hospitali unapona kabisa Hakuna dawa za kienyeji zilizothibitishwa kuwa zinatibu saratani Tiba ya mionzi haiui Kwanini wagonjwa hawaponi · · Wengi huja katika hatua za mwisho za ugonjwa Baadhi hukataa matibabu wanaposhauriwa na kwenda kujaribu tiba mbadala

76

KITINI CHA MADA YA 6 KUJICHUNGUZA MATITI MWENYEWE

Lala chini na uweke mkono wako wa kuume nyuma ya kichwa chako. Uchunguzi huu hufanyika mtu ukiwa umealala chali na sio ukiwa umesimama. Hii ni kwa vile ukiwa umelala chini ......za matiti zinakuwa zimeatawanyika kwa uwiano mzuri kweny kuta za kifua.na zinakuwa ndogo kadri inavyowezekana na inakuwa ni rahisi kuzisikiliza .....zote za matiti. Tumia sehemu ya vidole vyako 3 vya mkono wa kushoto kwa pamoja (finger pad) kugusa na kusikiliza kama kuna uvimbe wowote kwenye titi la kulia. Tumia vidole kufanya nzunguko kwenye eneo lote la titi kwa ili kuona kama kuna uvimbe wowote.

Tumia aina kama 3 za mkandamizo ili uweze kuzihis tishu zote za matiti.. Mkandamizo mdogo unafaa kwa ajili ya kusikizia tishu zilizoko karibu na ngozi, mkandamizo wa kati unafaa kwa ajili ya tishu zilizoko ndani zaidi kiasi, na mkandamizo mkubwa ni kwa ajili ya tishu zilizoko karibu kabisa na kifua na mbavu. Ni kawaida kusikia ugumu kwenye mkunjo wa chini wa kila titi, ila itakupasa umweleze daktari wako kama utasikia kitu kisicho cha kawaida. Kama huna uhakika ukandamize kwa nguvu kiasi gani ongea na daktari au muguzi wako. Tumia kila kiwango cha mkandamizo kusikilizia tishu za titi kabla ya kuhamia kwenye eneo jingine la titi. Tembeza kiganja chako kwa mtindo wa kwenda juu na chini ya titi kwa kuanzia kwenye mstari wa kufikirika ulioko kwenye kwapa na kuutembeza mkono wako kati ya titi hadi kati yamfupa wa kifua ( mfupa wa matiti) . Hakikisha unakagua titi lote kwa kueleke sehemu ya chini ya titi hadi uwe unasikilizia mifupa ya mbavu kuelekea juu hadi kufikia mfupa wa shingo (clavicle).

77

Upo ushahidi wa kushauri kwamba mtindo wa juu na chini (mara nyingine huitwa mtindo wa kutoka juu kwenda chini) ni mtindo unaofanikisha zaidi ambao unawezesha kufikia titi lote bila kuruka tishu yoyote ya titi. Rudia kukagua titi lako kushoto, kwa kuweka mkono wako wa kushoto nyuma ya kichwa na kwa kutumia kiganja cha vidole vyako vya mkono wa kulia kujikagua. Ukiwa umesimama kwenye kioo na mikono yako ikiwa umeikandamiza kwa nguvu kando ya hips zako, angalia matiti yako kama kuna mabadiliko yoyote kwa maana ya ukubwa umbo lake, kama kuna miinuko au hali ya kubonyea ndani ua wekundu au ngozi ya matiti. (Kukandamiza mikono chini kwenye hips kunabana kuta za kifua na kuonyesha mabadiliko yoyote kwenye matiti. Chunguza kila kwapa ukiwa umeketi ama umesimama na mkono wako ukiwa umeunyoosha juu ili iwe rahisi kuhisi hali ilivyo kwenye eneo hili. Kuinua mkono juu kunakaza tishu za eneo hili na kuzifanya ziwe ngumu kuchunguzika.

78

KITINI CHA MADA YA 6

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Saratani ya shingo ya kizazi ni nini? Saratani ni ugonjwa ambao unasababisha baadhi ya seli za mwili zisifanya kazi sawasawa, zinagawanyika kwa upesi sana na kuzalisha tishu nyingi ambazo hutengeza uvimbe. Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani, hii ni saratni ya amayo huathiri sehemu ya chini ya mji wa mimba. Saratani ya shingo ya kizazi ni ugonjwa ambao unaweza kuwa hatari sana, ingawaje, ni miongoni mwa magonjwa unayoweza kuyazuia. Kwa kawaida huchukua miaka mingi kwa seli za kawaida za kizazi kubadilika na seli za saratani, ila wakati mwingine huweza kutokea kwa kipindi kifupi tu. Zipi ni dalili za Saratani ya Shingo ya Kizazi? Kabla ya sratani au katika hatua za wali za saratani ya shingo ya kizazi kwa kawaida huwa haionyeshi dalili zozote. Mwanamke huwa anaonyesha dalili wakati ambapo saratani inakuwa imebadilika na kuvamia seli zilizoko jirani na shingo ya kizazi. Wakati hali hii ikitokea dalili ambayo hujitokeza mara nyingi ni kutokwa maji sehemu sehemu za siri yasiyokuwa ya kawaida kutokana na uvimbe mkubwa ambao umeathirika na kusababisha kutokwa na maji yenye harufu (harufu mbaya) ambayo hutokea kabla ya kuanza kutokwa damu. Mambo ya hatarishi yatokanayo na kuwa na kuwepo kwa Saratani ya shingo ya kizazi? Mambo hatarishi ni pamoja na: Kuathiriwa na kirusi cha kijulikanacho kama "human papillomavirus" (HPV). Madaktari wanaamini kwamba wanawake wanakuwa tayari wamethiriwa na kirusi hiki kabla ya kuonyesha dalili za saratani ya shingo ya kizazi. Tabia za kingono- kufanya ngono katika umri mdogo na historia ya kuwa na wapenzi wengi. Matumizi ya tumbaku ­ wanwake wanovuta sigara wanakuwa kwenye hartari mara mbili ya wale ambao hawavuti kupata saratni ya shingo ya kizazi. Tunaweza kugundua saratani mapema kwa njia gani? Saratani inaweza kugundulika mapaema kwa kufanya kipimo kijulikanacho kama "Pap" mara kwa mara. Wanawake wapime afya zao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na mifupa ya nyonga na kufanya kipimo cha Pap. Mwanamke anatakiwa aanze kufanyiwa kipimo cha hiki kati ya miaka mitatu baada ya kuvunja ungo au kwenye umri wa miaka 21, kimojawapo kati chochote kati ya hayo mawili kitatangulia ni sawa.

79

MADA YA SABA: MAWASILIANO YA ANA KWA ANA

Mada hii inahusisha taarifa kuhusiana na umuhimu wa mawasilianao ya ana kwa ana kwa ajili ya wamiliki wa saluni za urembo. Mada inaendeleza satdi za wahudumu ili waweze kutoa ujumbe wa afya wenye kufanikisha kwa wateja wao wakati wa mikutano ya ana kwa ana kwenye saluni. Kukuza stadi za mawasiliano za ana kwa ana kwa wahudumu wa saluni kutaweza kuleta badiliko katika kutoa ujumbe wa afya na kuleta mabadiliko ya tabia kuhusiana na kuzuia magonjwa ya ngono, VVU na tabia nyingine za afya ya uzazi amabzo zinaweza kuleta tofauti na kuboresha afya za wateja. Mada ndogo 7.1Maana ya Mawasiliano (dakika 15) 7.2 Salamu (dakika 15 ) 7.3 Kusikiliza kwa makini (DK 30) 7.4 Kuuliza maswali 7.5 Taarifa rahisi na sahihi 7.6 Zana saidizi 7.7 kufanyia majaribio stadi za mawasiliano ya ana kwa ana Madhumuni: Mwisho wa somo tutakuwa tumeweza Kuelewa kuwa mawasiliano ya ana kwa ana ni njia ya mawasiliano yenye nguvu katika kuchochea mabdiliko ya tabia Kuelezea stadi za msingi zinazohitajika wakati wa kufanya mawasiliano ya ana kwa ana Kutambua salamu inayofaa na ya heshima ikiwa ni msingi wa kuwezesha kuanza majadiliano Kuajdiliana kuhusu kusikiliza kwa makini ambapo ni msingi wa stadi za mawasiliano ya ana kwa ana. Kutambua na kufanya mazoezi ya kuuliza maswali ikiwa ni njia ya kuhimiza majadiliano. Kutambua umuhimu wa kutumia lugha rahisi wakati wa kutoa taariafa sahihi. Kujadiliana kwa kutumia zana za kusaidia kutoa taarifa sahihi. Kufanyia mazoezi stadi za msingi kwa ajili ya mawasiliano ya ana kwa ana wakati wa kufanya igizo.

80

Zana: Vipeperushi vya ina mbalimbali na zana nyingine zilizoandaliwa kusaidia kufikisha ujumbe kuhusiana na Dume, Lady Pepeta njia za uzazi wa mpango za Flexi P n.k. Kitini cha Mawasiliano ya ana kwa ana Kitini cha Stadi za mawasiliano ya ana kwa ana Kitini cha Matukio ya kufanyia maigizodhima ya mawasiliano ya ana kwa ana Kitini cha Ujumbe Muhimu : Mawasilinao ya ana kwa ana Muda: Saa 1 na dakika 30

7.1 Maana ya Mawasiliano

Hatua ya Kwanza Washiriki wawili wawili, waambie wajibu swali hili , Je mawasiliano ni nini ? Baada ya dakika chache waambie washiriki wasome maana walizoziandika kwenye kundi kubwa. Wapatie kitini cha Mawasilino ya ana kwa ana. Rejea kitini na washiriki na umwambie mmoja wao ajitolee kusoma kwa sauti: Mawasiliano yana maana nyingi na yanaweza kumaanisha kitu tofauti kwa watu tofauti. . Mawasiliano ni kubadilishana mawazo taarifa, hisia maoni au taswira baina ya watu wawili ama zaidi au kikundi cha watu. Mawasiliano ni utaratibu wa kupashana habari na kupokea habari ( kwa njia ya maneno au bila maneno) Kuhusiana na jambo au mada maalumu baina ya watu wawili au zaidi kwa lengo la kufikia muafaka wa jambo. Jambo muhimu kwenye mawasiliano ni uwezo wa kupeleka ujumbe wenye maana ilei le baina ya watu wawili au zaidi walioshirikishwa kwenye kubadilishana habari. Kwa ufupi waambie washiriki kwamba: Madhumuni ya warsha hii ni ili kuwasaidia wamiliki wa saluni na wahudumu

81

wao kuenedeleza stadi za jinsi ya kutoa taarifa za kiafya kwa wateja, wakati wa mikutano ya anakwa ana. Kuboresha stadi za mawasiliano ya ana kwa ana ya wahudumu wa saluni ili waweze kutoa ujumbe wa kuleta mabadiliko ya tabia kuhusiana na kuzuia VVU na tabia nyingine za afya ya uzazi.

7.2 Salamu

Waambie washiriki kwamba sasa tutanagalia jinsi ya kuendeleza satdi zinazohitajika katika kuanzisha majadiliano na wateja na kutoa taarifa zitakazoweza kuleat mabadiliko na kuboresha afya za wateja wao. Hatua ya Kwanza Waulize washiriki, nini hutokea unapokutana na mtu unaemfahamu wakati ukiwa unatembe mitaani? Elezea hali hiyo nini kinachotokea. Waambie waelezee njia zilizo zoeleka za watu kusalimiana kwenye jamii mbalimbali za Tanzania. Andika majibu yao kwenye bango. Zipi ni tabia za kupeana salamu? Tarajia majibu yafuatayo: Wenye umri mdogo wanasimama kuwasalimia watu wazima Wanaume wanavua kofia wakiwasalimia wanawake Watu wanashikana mikono Kila moja kuonyesha heshima kwa mwingine Kuinamisha vichwa vyao chini kuonyesha dalili ya heshima. Ku mkubali mwingine Hatua ya Pili Waambie washiriki kwamba salamu ni jambo la kwanza kwenye mawasiliano ya ana kwa ana na hutengeneza mazingira kwa ajili mazungumzo mengine yote yatakayoendelea. Kwahiyo stadi muhimu wakati wa mawasiliano ya ana kwa ana ni kutoa salamu inayokubalika.

82

Waambie washiriki waeleze ni kwa namna gani waaweza kuwasalimia vyema wateja wao kwa kwenye saluni. Hitimisha maelezo ya kikundi kwa kusema kwamba. Kuazisha mazingira yanayofaa na ya kuvutia tangu mwanzoni ni muhimu ili kuanzisha mahusiano mazuri. Msalimie mtu kwa heshima tumia matendo yanayokubalika na utamaduni wenu kwa maneno au bila maneno kuonyesha heshima na kujali nah ii itakusaidia kuwa na mkutano wenye matokeo chanya. Waalike watu wengi wajitolee na kusimama mbele kuonyesha baadhi ya matendo ya salamu amabyo yanaonyesha mazingira mazuri na yanayoweza kukauribisha watu kwenye saluni yako.

Hatua ya Tatu Stadi nyingine muhimu ni kusikiliza kwa makini kwa kuangalia ujumbe unaotolewa mwa maneno na bila maneno wakati wa mikutano ya ana kwa ana. Waambie washiriki waeleze maana ya mawasiliano ya maneno na yasiyo na maneno. Mawasiliano yasiyo na maneno yanahusisha matumizi ya mwili (bila maneno) Kusikiliza kunahusiana ni zaidi ya kusikia maneno au kile wanchosema wengine. Ukweli ni kwamba tafiti zinaonyesha asilimia 93 ya mawasilino yote ni mawasiliano bila maneno, hii ni pamoja na lugha ya mwili, ladha ya sauti na muonekano wa usoni n.k. mawasilino yasiyo na maneno yanatusaidia kuelewa "yanayopita bila kutakwa" kama vile hisia za mwili na mguso. Ni muhimu kuanagalia mawasiliano yasiyo ya maneno ili kuweza kufungua majadiliano au kuhamasisha majadiliano. Hatua ya Nne Waambie washiriki watoe mfano wa nyakati ambazo mawasiliano ya maneno na yasiyo ya maneno yanahitilafiana. Mfano: Maneno: Sema: ndio ......nina muda ........ Yasiyo ya maneno: Wakati huo huo ukianaglia kwenye saa yako ya mkono, unahema na kutikisa kichwa ......

83

Waambie washiriki kwamba ili kuweza kusema mtu amesikiwa na kueleweka lazima kuwepo na makubaliano kati ya ujumbe wa mawasiliano ya maneno na yasiyo na maneno. Rejea kitini cha Mawasiliano na kupitia dondoo za jinsi ya kutumia mawasiliano ya maneno na yasiyo ya maneno kwa ajili ya kuwa na mawasiliano yenye mafanikio. Y a Maneno: Rudia maneno yale yale uliza maswali, tumia lugha hiyohiyo, tumia sauti zinazochochea majadiliano na utumie sauti ya kirafiki. Yasiyo ya maneno: Angalia lugha ya mwili mwangalie na mtu mwingine, mtazame machoni, tikisa kichwa kama ishara ya kukubali na usikilize ladha ya sauti iko ya aina gani.

7.3 Kusikilza kwa Makini

Hatua ya Kwanza Waambie washiriki kwamba sasa tutafanya zoezi. Wagawe washiriki wawili wawili wape majina mmoja awe A na wa pili awe B. Mwambie A amuulize B (msikilizaji) kuhusiana na kilichotokea mwisho wa Juma . Mwache "A" aelezee hadithi yake kwa dakika tatu. "B" asikilize bila kuongea lolote, katika muda wa hizo dakika tatu. Baada ya dakika tatu watu hao wawili wabadilishane na wafanye kama walivyo fanya hapo awali kwa maana kwamba (B) anakuwa ndio msimulizi na (A) anakuwa msikilizaji.

Hatua ya Pili Baada ya zoezi, kila pea ijadili kuhusu uzoefu walioupata kwenye zoezi na kuelezea kuhusu wakati ambao walijisikia kama mwenzake anasikiliza ama hasikilizi wakati zoezi likiwa linaendelea. Waambie watakaotaka kujitolea kuwashirikisha wengine uzoefu wao wafanye hivyo. Orodhesha mifano ya jinsi walivyojisikia wakati mtu alipokuwa anamsikiliza mwenzake bila kuongea, andika kwenye bango.

84

Changamoto ni kwamab msikilizaji hakuweza kutumia maneno yoyote bali kulikuwa kuna njia nyingi za kuwa alikuwa anamsikiliza mwenzake kwa kutumia mawasilino yasiyokuwa ya maneno. Kusiikiliza kwa makini ni kusikiliza mwitikio wa mawasiliano yaliyo ya maneno nayale yasiyokuwa ya maneno na kutoa mrejesho. Mfano wa mrejesho usiokuwa wa maneno: Kufuatilia kile anachosema mwingine Alitoa sauti za kuniashiria kwamba yeye alielewa Alitumia lugha ya mwili sahihi (alinitazama machoni, alitikisa kichwa kama ishara ya kukubaliana nami, alitabasam, hakunikatiza wakati naongea, aliniapa heshima na kuonyesha urafiki, alikaa huku ameegemea kwa mbele)

Waambie washiriki kwamba wakati wa zoezi la mawasiliano tulibuni taarifa na kuwashirikisha wengine kwa ajili ya kufikia makubaliano ya pamoja. Kwa hali hii lugha isiyokuwa ya maneno ilitumika ili kuwezesha kila mmoja kufanya mazoezi ya kusikiliza kwa makini.. Waulize awashiriki kama kuna aliye na swali .

7.4 Kuuliza Maswali

Waulize washiriki nini ni madhumuni ya kuuliza maswali na kusikiliza? Andika majibu kwenye bango. Baada ya kubunga bongo hitimisha majibu na uhakikishe kwamba madhumuni ya maswali yafutayo yanameongelewa: Kuanzisha majadiliano Kuhimiza mteja kuongea Kuwasilisha matarajio yako kwa mtu mwingine i Kuongeza uelewa wako kuhusiana na hisia za wengine Kuweza kuibua taarifa mpya Kumpa mteja kiwango fulani cha kuweza kuongoza Sasa waulize wanakikundi, tumejifunza nini kwenye zoezi la maswali? Andika majibu kwenye bango. Baada ya kubunga bongo, hitimisha majibu yao kwa

85

kuhakikisha kwamba dondoo zifuatazo tulizojifunza kwenye zoezi la maswali zimeguswa: Hali halisi kwa ujumla "Ungependa kuongea kuhusu nini "? Ukweli "Nini kilichotokea "? Hisia "Ulijisiakiaje "? Sababu "Kwanini ulifanya hivyo "? Mahususi "Unaweza kunipatia mfano ? Sasa waulize washiriki, Je haya ni maswali ya aina gani? Andika majibu kwenye bango. Baada ya kubunga bongo hitimisha majibu yao na wafahamishe kwamba kwa ajili ya madhumuni ya somo hili maswali haya tutayapanga kwa aina tatu, maswali yaliyofungwa, maswali yaliyo wazi, na maswali ya kudodosa. Pitia aina hizi tatu na mifano yake kama yalivyoorodheshwa hapa chini na uwaambie washiriki wakupatie mifano. AINA YA SWALI Mswali yaliyofungwa: Kupata taarifa maalum : Maswali yaliyo wazi: Kufahamu kumhusu mteja hisia zake, imani, na uelewa. Kudodosa : kufuatilia kwa kutumia sentensi aliyotumia mteja MFANO "Je unao watoto wangapi " "huwa uanjisikiaje kuhusu kondom "Je unafahamu nini kuhusu saratani ya shingo ya kizazi ?" "Unaweza kunieleza zaidi kuhusu kwa nini unafikiri sio muhimu kutumia kondom na rafiki yako?"

Baada ya kupitia aina za maswali: Uliza; je ni aina gani ya taarifa unayojaribu kupata kutoka kwenye kila aina ya maswali? Tumia taarifa hii hapa chini kuhakikisha maswali yanajibiwa kwa usahihi kwa aina ya maswali ya aina tatu. Maswali yaliyo wazi: Yanamruhusu mteja kuelezea na kutoa taarifa. Mteja anaweza akawa na uhuru wa kucha gua wapi na namna gani anweza kuelekeza swali lake. Ina msaidia mhudumu kupata taarifa zaidi kuhusiana na mteja.. Maswali yaliyofungwa: Maswali yaliyofungwa hayaruhusu ufafanuzi bali majibu mahususi. Yanakuwa na majibu ndio au hapana au majibu 1-2. Yanafaa sana katika kukusanya taariafa za ukweli bali sio kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ambapo maamuzi yanaweza kufanyika. Kwa kutumia mlolongo wa maswali yaliyofungwa mhudumua anakuwa AMETAWALA mazungumzo. . Mteja ataweza kuweka wazi taarifa kuhusiana na mawali maalum yaliyoulizwa, bali itakuwa ni mwanzo tu na yatapaswa kufuatiliwa na maswali yaliyo wazi na

86

maswali ya kudodosa. Kudodosa: Maswali ya kudodosa huchukua jambo maalumu, hisia au jambo maalum na kuchambua kwa kina. Hii ni muhimu pale ambapo wateja wanapodhihirisha dondoo iliyokuwa imerukwa. Kudodosa ni muhimu wakati wa kuongea kuhusu mada nyeti ambazo zinaweza kuwa ni vigumu kwa wateja kuelezea kwa uwazi wao wenyewe

Eleza kwamba ladha ya sauti ni muhimu wakati wa kuuliza maswali. Sauti inapaswa isiwe yenye kuhukumu, wahudumu wanapaswa ladha ya sauti ambayo inaonyesha kutamani kufahamu zaidi na kujali. Uliza swali hilohilo kwa sauti ya ladha tofauti: Unao marafiki wa kingono zaidi ya mmoja sasa? Ili uweze kuona tofauti?" .

7.5 Taarifa Rahisi na Sahihi

Hatua ya Kwanza Alika watu wawili wajitolee kusoma majibizano haya : Mteja: Habari ya asubuhi Mhudumu wa saluni : Nzuri habari za kwako nikusaidie nini ? Mteja: Nahitaji kusuka nywele zangu sasa .... Pia nitafanya usafi wa kucha ...........I Mhudumu wa saluni: Ndio, unataka kusuka nywele na kusafisha miguu leo, je ulisha fanya makubaliano ya kukutana ? Mteja: Hapana ..........sikupiga simu .....ila nilikuja hapa mwezi uliopita Jenny alihudumia nywele zangu r...... Mhudumu wa saluni : Leo Jenny yupo ila ana mteja mwingine kwa sasa, unaweza kusubiri hadi amalize? Tunaweza kuhudumia kucha zako kwanza wakati ukiwa unaendelea kumsubiria..... .... Mteja : Ndio nataka kumsubiria Jenny , ndio sawa nihudumie kucha zangu kwanza. , Mhudumu wa saluni: Ndio naweza kuhudumia kucha zako na Jenny atahudumia nywele zako mara tu akimaliza na mteja wake...njoo upande huu tafadhali...

87

Hatua ya Pili Waulize washiriki ni nini walichojifunza kwenye majibizano haya? Majibu: Salamu ilikuwa sawa aliuliza maswali yaliyo wazi na yaliyofungwa. Waambie washiriki: Kwamba wanatakiwa waone pia kwamba mhudumu wa saluni alikuwa anarudia baadhi ya maneno yale yale alyosema mteja, kwa kurudia maneno aliyosema mteja, anajisikia vyema kwamba mhudumu wa saluni hakika anamsikiliza na kujibu kulingana na mahitaji yake. Hii ni aina nyingine ya stadi ambayo inaongeza uelewa wakati wa majadiliano. Alika mtu mwingine ajitolee kusoma Kitini cha Mawasiliano ya ana kwa ana,. Kuongea kwa lugha nyepesi ni stadi nyingine ambayo itasaidia kuongeza uelewa wakati wa mazungumzo ya ana kwa ana. Kutumia lugha inayoeleweka kwa uarahisi kwa kila mtu na kurudia taarifa sahihi kuhakikisha kwamba wewe na mteja wako wewe na mteja wako nyote mmeeleweka. Wakati mwingine ni muhimu kurekebisha lugha ili iweze kukidhi kiwango cha elimu ya wateja wako. Hatua ya Tatu Waambie washiriki wako: Kuna habari za uongo na zilizopotoshwa kuhussiana na baadhi ya mada amabzo tumesha jadiliana kwenye warsha zilizotangulia huussani suala la kondom. Soma kwa sauti mfano unaofuata: Kondom zina matundu na hivyo sio salama katika kuzuia VVU; vijidudu vinapita kwenye matundu , kwa hiyo sio njai nzuri ya kuzuia VVU. Washiriki wawili wawili wajadiliane na kutambua njia za kuweza kutoa taarifa sahihi ili kuondokana maneno potofu kuhusiana na kondom. Tumia maneo yale yaliyosemwa na mteja. Waalike washiriki watoe majibu. Majibu unayoweza kuyatarajia: Kondom ni njia nzuri sana ya kujilinda na VVU. Hazina matundu na virusi haviwezi kupita kwenye kondom.

88

7.6 Zana Saidizi

Hatua ya Kwanza Waambie washiriki kwamba stadi nyingine ambayo inatumika wakati wa mawasiliano ya ana kwa ana ni kutumia vijarida, vijitabu, mabango, na machapisho mengine au vielelzo vingine vya picha ambavyo vilishaandaliwa ili kusaidia kuongeza uelewa kuhusiana na mada fulani. Hatua ya Pili Wagawe washiriki kwenye makundi mawili makubwa na waambie wana kikundi kimoja kitaje faida za kutumia zana saidizi na kundi la pili lijadili kuhusu mapungufu ya kutumia zana saidizi. Kila kikundi kiwasilishe majibu yake. Hakikisha kwamba faida na mapungufu yaliyoainishwa hapa chini yamejadiliwa. FAIDA Inavutia usikivu Ina taarifa sahihi Inaekezea kila hatua kwa utaratibu Inawezesha kufanya mawazo magumu kuweza kuwa rahisi Inaibua Majadiliano Inasaidia kufanya majadiliano ya masuala nyeti Kuwa nataarifa za kwenda nazo nyumbani kujikumbusha Kushirikisha taarifa kwa wanafamilia wengine Kila moja ankuwa na taarifa hiyohiyo. MAPUNGUFU Haifanikishi endapo mtu hajui kusoma labla yawe yamendaliwa maalum kwa ajili ya watu wa amabo hawajasoma. Haifanikishi ikitumiwa kwenye kundi kubwa la watu Hutoa taarifa kwa ajili ya jambo muhimu tu liloko kwenye zana Inaweza ikahitaji tarifa za nyongeza Inakuwa na mapungufu ya fedha za kwenye kuchapisha zaidia na kusambaza. Ni rahisi kupotea au kutupwa

89

Hatua ya Tatu Waambie washiriki waorodheshe zana saidizi walizo nazo kwa ajili ya Lady Pepeta Dume na Flexi P. Wapatie washiriki baadhi ya zana hizi. Mwambie kila mshiriki aelezee ni wakati gani wa kutumia zana saidizi. Mtu mmojawapo ajitolee kuonyesha jinsi ya kutumia zana saidizi wakati wa somo la mazoezi ya Lady Pepeta. Vijarida vijitabu, mabango, vitini au michoro vinaweza kutumika wakati wa maonyesho ya saluni za urembo, kuwa na kukkundi kidogo cha majadilianao ama mazungumzo ya mtu mmoja mmoja. Waambie washiriki kwamba zana zilizotengenezwa kuboresha ufahamu kuhusiana na mada zinaweza kuboresha uelewa kuhusiana na mada maalumu na kumsaidia kufanya mabadiliko ya tabia. Onyesha na upitie zana mbalimbali za kuwezeshea zilizopo.

7.7 Kufanyia mazoezi ya stadi za mawasiliano ya ana kwa ana

Hatua ya Kwanza Wapatie Kitini cha stadi za mawasiliano ya ana kwa ana na upitie kwa pamoja na washiriki: Salamu inayofaa - Humwezesha mteja kujisikia amekaribishwa. - Hakikisha kuwa kuna utamaduni wa kusalimiana na inakubalika. Kusikiliza kwa makini: - Uwe makini na ujumbe wa wateja wa maneno na usio wa maneno. - Tumia mawasiliano ya maneno na yasiyo ya maneno ili kuonyesha unafautila na kufurahia wanachosema. Uliza maswali Tumia maswali yaliyo wazi yaliyofungwa na kudodosa ili kuhamasisha majadiliano na kupata taarifa zaidi. Ongea kwa lugha nyepesi: - Tumia maneno ambayo yanaeleweka kwa urahisi

90

- Rudia taarifa ili kuhakiksha kuwa umemwelewa mtja wako ka usahihi - Sahihisha kila upotoshwaji kwa kutumia lugha rahisi inayoeleweka. Tumia zana saidizi - Saidia kuhakikisha kwamba taarifa ianyopatikana ni sahihi naya uhakika - Uwe mkumbushaji wa yale waliyojifunza

Hatua ya Pili Kama inawezekana fanya igizo la moja ya visa mkasa kutokana na kitini cha stadi za mawasiliano ya ana kwa ana mbele ya wshiriki kama njia ya kuonyesha jinsi ya kufanya kwa vitendo Stadi za mawasiliano ya ana kwa ana. Chagua kisa mkasa kimoja na kuigiza kile lichojiri kwa kumsirikisha mwezeshaji msaidizi. Waambie washiriki wao wawe watazamaji na waandike ni stadi gani za mawasiliano ya ana kwa ana zilizotumika wakati wa uigizaji. Waambie washiriki wapendekeze nini kifanyike ili kuboresha igizo. Waambie washiriki wawe tayari kufanya MAZOEZI. Hakikisha unakila zanya kusaidia majadilanno ili waweze kutumia wakati wa kuigiza. Hatua ya Tatu Wagawe washiriki kwenye makundi ya watu watatu watatu na uwapatie kitini cha Maigizo ya visa mkasa vya kuigiza. Washiriki wachague kisa mkasa wanachotaka kukitumia, mmoja ataigiza kama mhudumu wa saluni na mwingine ataigiza kama mteja na mwingine kama mtazamaji. Mtazamaji ataangalia kwenye orodha ya stadi zilizotumiwa na mhudumu wa saluni: Salamu iliyo sahihi, kusikiliza kwa makini, kuuliza maswali, matumizi ya lugha nyepesi kurudia maneno, kutoa taarifa sahihi na matumizi ya zana wakati wa mazungumzo ya ana kwa ana. , Mara baada ya igizo la kwanza kuisha kikundi kibadilishane majukumu na kuanza kisa mkasa kingine. Mwishowe kila mshiriki atapaswa awe ameshiriki majukumu yote matatu kwenye visa mkasa tofauti..

91

Baada ya kila igizo, kila kikundi kipitie na kujadliana maoni ya mwamnaglizi kuhusian nan satdi mabalimbali zilizotumiwa n mhudumu wa saluni wakati wa mkutano wake na mteja. Hatua ya Nne Baada ya zoezi hili kukamilika waulize washiriki kama wana swali lolote na hitimisha ujumbe muhimu kutoka kwenye mada. Wapatie washiriki ujumbe muhimu: Kitini cha Mawasiliano yaenye tija ya ana kwa ana.

Ujumbe maalumu stadi za mawasiliano ya ana kwa na yenye tija Mawasilino ni utaratibu wa kutoa ujumbe na kupokea taarifa (kwa maneno na pasipo maneno) kuhusiana na mada maahususi baina ya watu wawili ama zaidi kwa lengo la kufikia mauafaka. Mawasiliano ya ana kwa ana ndio njia yenye nguvu zaidi kwa ajili ya kueleta mabadiliko ya tabia. Salamu ni hatua ya kwanza ya kukutana kwenye mawasiliano ya anakwa ana na yanawezesha kufanya mazingira yawe mazuri kwa ajili ya mazungumzo yote yatakayo fanyika. Ni muhimu kuonyesha heshima wakati wa kusalimiana.. Kusikiliza kuna husisha zaidi ya kusikia maneno, ni pamoja na kuangalia kwa makini ujumbe wa maneno na usio wa maneno ili kufikia muafaka Kuuliza maswali ni njia mojawapo ya kuhamasisha kila mmoja kushiriksha wengine taarifa kuhusiana na hali ama kuelezea hisia. Tumia mchanyiko wa maswali yaliyo wazi yaliyofungwa na kwa kudodosa., . Tumia maneno kama anayotumia mteja wako ili waone kwamba unawasikiliza na uwapatie taarifa sahihi na uweze kusahihi upotosahji wowote. Aina nyingine ya stadi inayofanikisha wakati wa mawasiliano ya ana kwa ana ni matumizi ya zana kama vile vijitabu vijarida mabango, na zanazingine zilizochapishwa mahususi kwa ajili ya mada husika: - Toa salamu kwa heshima - Sikiliza ujumbe wa maneno na usio wa maneno - Uliza maswali kuanzisha majadiliano - Tumia maneno rahisi katika kutoa taariafa sahihi - Tumia zana saidizi kutoa taarifa zilizo sahihi na za uhakika

92

Hatua ya Tano Waambie washiki kwamba sasa tumemaliza mafunzo yetu sehemu ya tatu kwa ajili ya Mpango wa Jipende kwa ajili ya saluni za urembo. Asante sana kwa kuja na kushiriki leo na tutakutana tena wiki ijayo kumalizia mada nyingine nzuri sana. Kabla hamjaondoka tafadhali jazeni fomu ya tathmini kwa ajili masomo haya. Wapatie washiriki fomu yenye maswali na uzikusanye kabla hawajaondoka.

93

KITINI CHA MADA YA 7

MAWASILIANO YA ANA KWA ANA

Mawasiliano yana maana nyingi na yanaweza kumaanisha kitu tofauti kwa watu tofauti. . Mawasiliano ni kubadilishana mawazo taarifa, hisia maoni au taswira baina ya watu wawili ama zaidi au kikundi cha watu. Mawasiliano ni utaratibu wa kupashana habari na kupokea habari ( kwa njia ya maneno au bila maneno) Kuhusiana na jambo au mada maalumu baina ya watu wawili au zaidi kwa lengo la kufikia muafaka wa jambo. Jambo muhimu kwenye mawasiliano ni uwezo wa kupeleka ujumbe wenye maana ilei le baina ya watu wawili au zaidi walioshirikishwa kwenye kubadilishana habari. `

KUSALIMIA

Kutengeneza mazingira mazingira mazuri kuanzia mwanzo ni muhimu sana ili kuanzisha mahusiano mazuri.. Msalimie mhusika kwa heshima tumia salamu inayokubalika kulingana na utamaduni wa mahali husika, mawasiliano ya lugha ya mwili na maneno yanawza kutumika kuonyesha heshima na kuwa unajali,kuwepo kwa hali hii itasaidia kuwa na mkutano wenye muonekano chanya.

KUSIKILIZA KWA MAKINI

Kusikiliza kwa makini miitikio yote iwe ya maneno ama bila maneno na kutoa mrejesho wa maneno na usio wa maneno. Yaliyo ya Maneno: Rudia maneno yaleyele, uliza maswali, tumia lugha ileile na tumia sauti ambayo inahimiza majadiliano zaidi .......tumia sauti iliyo ya kirafiki. Yasiyo ya maneno: angalia lugha ya mwili, mtazame mtu unayewasiliana naye, mwangalie machoni onyesha kuwa unafuatilia mazungumzo kwa kutingisha kichwa, na usikilize ladha ya sauti.

94

KUULIZA MASWALI

AINA YA SWALI Maswali yaliyofungwa: Taarifa maalumu : taarifa maalum Maswali yaliyo wazi: kujifunza kuhusu hisia, imani na ufahamu wa mteja MFANO "Je unao watoto wangapi "

"Huwa unajisikiaje kuhusu kondomu "Unafahamu nini kuhusu saratani ya shingo ya uzazi?" Kudodosa : Kufuatilia ya kauli ya mteja "Unaweza kunieleza zaidi kwanini unafikiri kwamba kutumia kondomu na rafiki wa kiume haina maana yoyote?

TAARIFA RAHISI NA YA UHAKIKA

Kuongea kwa lugha nyepesi ni stadi nyingine ambayo itasaidia kuongeza uelewa wakati wa mazungumzo ya ana kwa ana. Kutumia lugha rahisi kwa kila mtu aweze kuelewa na kurudia taarifa hiyo kwa usahihi kuhakiksha kwamba nyote yaani wewe na mteja wako mmeelewana kwa usahihi.

ZANA ZA KUWEZESHEA

FAIDA Inavutia usikivu Inatoa taarifa sahihi Inaelezea hatua kwa utaratibu Inawezesha mawazo magumu kuwa marahisi kwa kutumia michoro. Inachochea majadiliano Kusaidia kujadili mambo nyeti Unachukua taarifa nyumbani kama kumbukumbu Kushirikisha wanafamilia wengine taarifa Kila mmoja nakuwa na taarifa hiyo hiyo. MAPUNGUFU Haifanikishi endapo watu hawawezi kusoma la sivyo zana hizo ziwe zimeanadaliwa mahususi kwa ajili ya watu wasiojua kusoma . Hazifanikishi kwa makundi makubwa ya watu Inatoa maelezo maalumu ya taarifa zilizopo kwenye zana. Pengine inaweza kuhitaji maelezo ya ziada Usambazaji na uzalisha wa nakala unakwazwa na ukosefu wa fedha za kutosha. Kupotea kwa uarhisis au kutupwa

95

96

KITINI CHA MADA YA 7

ORODHA YA STADI ZA MAWASILIANO YA ANA KWA ANA o o o o Salamu Muafaka Hakikisha mteja wako anajisikia amekaribishwa vema Hakikisha kuwa kuna utamaduni wa kusalimiana Kusikiliza kwa makini: Weka maanani kuhusu mawasiliano ya maneno na yasiyo ya maneno Tumia mawasiliano ya maneno na yasiyo ya maneno ili kuonyesha unapendezwa na mazungumzo na unamsikiliza mteja wako Uliza Maswali Tumia maswali yaliyo wazi na yaliyofungwa na kudodosa ili kuanzisha mazungumzo na kupata taarifa zaidi. Ongea kwa lugha nyepesi: Tumia maneno yanayoweza kueleweka kwa wepesi Rudia taarifa uliyoambiwa kuhakikisha kama umemwelewa vema mteja wako Sahihisha upotoshwaji wa tarifa kwa kutumia lugha nyepesi. Tumia zana za kusaidia kuwezeshea Saidia kuhakikisha taarifa ni sahihi na za uhakika Uwe unawakumbusha kile walichojifunza

o

o o o o o

97

KITINI CHA MADA YA 7

MAWASILIANO YA ANA KWA ANA: VISA MKASA VYA IGIZO DHIMA

Kisa cha 1: Lisa Anaulizia kuhusu kondom, kwa vile amekuwa akisikia kwamba kondom zina matundu hasa kamautaiweka mfukoni kwa muda mrefu Kisa cha 2: Catherine anatamani kufahamu kuhusu kondomu za kike za Lady Pepeta na anakuuliza zinafanya kazi namna gani na je zinaweza kutumika zaidi ya mara moja? Kisa cha 3: Miriam amesikia kwamba wakati mwingine kondom huwa zikivaliwa hazienei vya kutosha na hivyo hazifanikishi sana kwenye kuzuia mimba. Kisa cha 4: Upendo anataka kununua kondom ya Lady Pepeta, ila hataki umwelekeze namna ya kuitumia, je utamwambia nini? Kisa cha 5 Kim amesikia kwamba kondom moja haitoshelezi na hivyo mtu atahitaji kuvaa mbili kwa ajili kinga zaidi Kisa cha 6 Rita anataka kufahamu JIPENDE ni nini na kwanini fulana yako imeandikwa JIPENDE Kisa cha 7: Mary ni mwanafunzi na angependa kufahamu ni kwa jinsi gani kondom inaweza kuzuia maambukizi ya magonjwa ya ngono Kisa cha 8 Rose anataka kufahamu namna atakvyoongea na rafiki yake wa kiume kuhusu kondom kaw sababu hataki kupata mimba Kisa cha 9 Sara anafanya kazi ya bar na rafiki yake mpya wa kiume ambaye ni mtu mzima zaidi yake ameshampatia vitu vingi vizuri ambavyo amekuwa akimuomba na sasa huyu rafiki yake anamuomba afanye naye mapenzi. Anaogopa kuongea nae kuhusu VVU. Je unawez kumsaidia kwa namna gani? Kisa cha 10 Imma amekuwa kwenye ndoa kwa miaka kadhaa sasa na mtoto mmoja, mume wake hufanya kazi nje ya mji kwa miezi kadhaa kwa mwaka, atakuwa anarudi nyumbani na amekuwa akiwaza naman ya kuongea nae kuhusu VVU na jinsi ya watakavyoweza kulindana. Unaweza kumsaidia kwa namna gani na je utamwambia nini?

98

Kisa cha 11 Tunu amekuwa mteja wako kwenye saluni kwa miezi kadhaa sasa na anakuja saluni kwako asubuhi akionyesha ana hofu. Anakwambia anawasiwasi amepata maambukizi ya VVU .....Amekuwa akitokwa majimaji sehemu zake za siri ...... Kisa cha 12. Pili anakuuliza utajuaje kama mtu amepata maambukizi ya VVU Kisa cha 13: Florida anafikiri ni mjamzito na amesikia kwamba mtu ukiwa na ujazito ni lazima utapima VVU, na pia angependa kufahamu iwapo mwenzi wake atapimwa, ana hofu, je utamwambia nini? Kisa cha 14: Unataka kuweleza kuhusu jinsi ambavyo wanawake wanaweza kujilinda kutokana na magonjwa ya ngono, je utawaambia nini wateja wako, mf. mwanamke kijana ambaye amekuwa akija kwenye saluni kwa miezi kadhaa sasa?

99

KITINI - MADA YA 7

UJUMBE MUHIMU: STADI ZA MAWASILIANO YA ANA KWA

ANA

Mawasiliano ni utaratibu wa kupeleka na kupokea taarifa (kwa maneno na bila maneno) kuhusiana na jambo mada fulani baina ya watu wawili ama zaidi kwa lengo la kufikia maelewano ya pamoja. Mawasiliano ya ana kwa ana ni njia yenye nguvu sana katika kuleta mabadiliko ya tabia. Salamu ni jambo la kwanza kabisa ambapo kunakuwa na mawasiliano ya ana kwa ana na salamu zinatengeneza mazingira kwa ajili ya mazungumzo mengine yote yatakayofanyika. Ni muhimu kuonyesha heshima wakati wa kusalimiana. Kusikiliza ni zaidi ya kusikia maneno, ni pamoja na kuwa mwangalifu kwa ajili ya ujumbe wa maneno na usio wa maneno ili kufikia maelewno ya pamoja. Kuuliza maswali ni njia ya kumhamasisha mtu kushiriki katika kutoa taarifa zaidi kuhusiana na hali zao. AU kueleza hisia zao. Wakati wa kudodosa tumia mchanganyiko wa maswali yaliyo wazi na yaliyofungwa. Tumia maneno aliyosema mteja wako ili wafahamu kwamba umekuwa unawasikiza na utoe taarifa sahihi na kusahihisha kila aina ya mitazamo potofu. Jambo jingine linalofanikisha kwenye mawasilano ya ana kwa ana ni matumizi ya zana kama vile majarida vijitabu mabango, na machapisho mengine ambayo yaliandaliwa ili kukuza uelewa kuhusiana na mada husika. Stadi zinazofanikisha za mawasilaino ya ana kwa ana zinazotumika ili kuendeleza mahusiano mazuri na mabadiilko ya tabia: o Salimia kwa heshima o Sikiliza ujumbe wa maneno na usio wa maneno o Uliza maswali ili kuanzisha majadiliano o Tumia maneno rahisi ili kutoa taarifa sahihi o Tumia zana za kusaidia kutoa taariafa za kuaminika na sahihi

100

MAFUNZO YA 3: FOMU YA TATHMINI

Fomu hii ni ya siri. Usiandike jina lako kwenye fomu hii. Asante. 1. Je matarajio yako kwa ajili ya mafunzo haya yamefikiwa? (weka mduara kwenye jibu) NDIO HAPANA Kama hapana, kwanini?

2.

Je ni mada gani umeipenda zaidi? Kwanini?

3. Mada gani hujaipenda? Kwanini?

4. Ni mada ipi tulihitaji kuipa muda zaidi?

5. unaweza kupima namna gani mtindo wa uwezeshaji? (zungushia duara jibu moja) i. nzuri sana j. Wastani k. Nzuri l. Dhaifu Maoni: 6. 6.Je tunaweza kufanya nini tofauti ili kuboresha yaliyomo kwenye mafunzo haya?

7. Tunaweza kufanya nini tofauti ili kuboresha utaratibu mzima wa mafunzo haya (muda, mapumziko ya chai/ kahawa, n.k)

101

8.

Kwa ujumla, unaweza kuyapa mafunzo haya kiwango gani cha ufanisi (Weka duara kwenye jibu moj a) Nzuri sana b. Nzuri c. Wastani d. Dhaifu Tumia nyuma ya ukurasa huu kama unayo maoni zaidi.

9.

102

MAFUNZO YA 4

Karibuni wote tena kwenye sehemu ya mwisho ya mafunzo ya Kituo cha afya za wanawake cha JIPENDE. Wakati wa warsha iliyopita, tuliongelea kuhusu umuhimu wa mawasiliano ya ana kwa ana na jinsi ya kutoa taarifa ujumbe wa afya wenye ufanisi kwa wateja wa saluni za urembo. Kuboresha stadi za mawasiliano katika kupeleka ujumbe unaohusiana na Magonjwa ya ngono na kuzuia VVU, uelewa kuhusu saratani na tabia nyingine za afya ya uzazi kunaweza kuleta mabadiliko kwa afya za wateja wako. Mada ya leo ni kuhusu umuhimu wa uzazi wa mpango kwa wanawake. Takwimu zinaonyesha kwamba hapa Tanzania vifo vya wanawake wakati wa kujifungua viko juu sana. Matatizo wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua ni sababu ya kwanza kabisa inayosababisha vifo vya wanawake wenye umri kati ya miaka 14-49 hapa Tanzania. Tutajadiliana kuhusu faida za uzazi wa mpango na namna ambavyo zinaweza kusaidia kuokoa maisha ya wanawake. Mada hii ni ya mwisho ya mafunzo haya.

103

MADA YA NANE:

UZAZI WA MPANGO NA AFYA YA MAMA

Mada ndogo 8.1 Dhana ya uzazi wa mpango 8.2 Sababu za kutumia njia za uzazi wa mpango 8.3 Faida za uzazi wa mpango 8.4 Njia za Uzazi mbadala zilizopo Tanzania 8.5 Njia za uzazi wa mpango zinazotolewa kwenye vituo vya afya Madhumuni: Mwisho wa somo tutakuwa tumeweza ... Kujadiliana kuhusu dhana ya uzazi wa mpango Kutambua sababu za kutumia njia za uzazi wa mpango Kuzifahamu faida za uzazi wa mpango Kujadiliana kuhusu njia mbadala za uzazi wa mpango zilizoko Tanzania. Kutambua njia za uzazi wa mpango zilizoko kwenye vituo vya afya Zana: Mabango na kalamu (markers) Mifano wa njia za uzazi wa mpango Kijarida cha njia za uzazi wa mpango Kitini cha Vidonge (njia ya uzazi ya kumeza) Kitini cha kondomu Kitini cha njia za Uzazi wa Mpango kwenye vituo vya afya Kitini cha Njia Asilia za Uzazi wa Mpango Kitini cha Ujumbe Muhimu: Njia za Uzazi wa Mpango Muda : Saa 1 na dk 30 Wageni: Mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi au Muuguzi

104

7.1 Dhana ya Uzazi wa Mpango

Hatua ya kwanza Kama inawezekana alika mtaalamu wa uzazi wa mpango au muuguzi ili aweze kuongoza kwenye sehemu hii ya somo. Kikundi kwa pamoja, bunga bongo kuhusu maana ya uzazi wa mpango. Pata majibu kutoka kwenye kikundi na uandike kwenye bango. Elezea kwa ufupi maelezo yao kwa kutumia maana iliyoko hapa chini: Njia za uzazi wa mpango ni pale ambapo mtu binafsi au wenzi wanapofanya maamuzi sahihi kuhusu lini wanataka kupata watoto idadi ya watoto wanaowataka na mtoto mmoja apishane umri na wengine kwa miaka mingi. Washiriki wafahamu kwamba watu wote bila kujali hali ya yao ya usawa au ndoa wanayo haki ya kupata taarifa kuhusiana na uzazi wa mpango, elimu na kupatiwa huduma.

7.2 Sababu za kutumia Njia za Uzazi wa Mpango

Hatua ya kwanza Waambie washiriki kwamba sasa tutafanya kazi kwenye makundi madogo. Wagawe kwenye makundi sita madogo. Waambie wanakikundi kwamba tutajadiliana kuhusu sababu za kwanini ni muhimu njia za uzazi wa mpango ziwepo hapa Tanzania. Tutapanga sababu hizi kama ifuatavyo: sababu za kiafya, sababu za kiuchumi na sababu za haki za binadamu. Wagawie wanakikundi kila kimoja mojawapo ya makundi haya.kila aina ya kundi linaweza kufanyiwa kazi na kikundi zaidi ya kimoja. Wapatie wana kikundi dakika 10 kutengeneza orodha zao. Waambie wanakikundi wenye aina za sababu zinazofanana kuwasilisha waliyoyagundua kwa pamoja, waambie washiriki walio amabao sio wana kikundi hiki kama watakuwa na nyongeza kwenye orodha hizo. Toa ufafanuzi wa swali lolote ama hali yoyote ya kutokuelewana. Baada ya kila aina ya sababu kuwasilishwa hakikisha kwamba sababu zilizoorodheshwa hapa chini zimejadiliwa pia. i) Sababu za Kiafya;

105

Kuwa na watoto wengi mno kunaathiri afya ya mama na mtoto. Hatari zinazoambatana na kuzaa watoto hapa Tanzania: o Mapema mno (wanawake wanakuwa wajawazito kabla ya umri wa mika 18) o Karibukaribu mno (chini ya miaka 2 ya umri kati ya ujauzito mmoja na mwingine ) o Nyingi mno (zaidi ya mimba nne ) o Kuchelewa sana (zaidi ya mika 35 ) Kuzuia idadi ya mimba zisizotakiwa Kupunguza vifo vya watoto/magonjwa ya utotoni Kupunguza utoaji wa mimba Kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya VVU kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa kutumia kondom. ii) Sababu za kiuchumi na demografia. Endapo ongezeko la idadi ya watu halitadhibitiwa miundo mbinu iliyopo haiitaweza kukidhi mahitaji ya watu kama vile: Makazi Huduma za afya Shule Ardhi Utunzaji wa Mazingira Chakula Ajira iii) Haki za binadamu Uzazi wa mpango ni haki ya msingi ya binadamu. Kila mmoja anayohaki ya kupata taarifa sahihi na huduma kuhusu afya ya uzazi kila mwanamke anahitaji kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na masuala ya afya

106

ya uzazi.

7.3 Faida za Uzazi wa Mpango

Hatua ya Kwanza Waambie washiriki kwamba sasa tutajadiliana kuhusiana na faida binafsi atakazopata mtu endapo atatumia njia za uzazi wa mpango kwa ajili ya mama baba, mtoto mchanga, watoto na jamii kwa ujumla? Wagawe washiriki katika makundi madogo ya majadiliano, uwe na walao makundi manne (yasiwe na washiriki zaidi ya watano kwa kila kikundi) kipatie kila kikundi kazi: Kundi la Kwanza ­ orodhesha faida atakazopata mama Kundi la Pili ­ orodhesha faida atakazopata baba Kundi la Tatu ­ orodhesha faida atakazopata mtoto mchanga Kundi la Nne ­ orodhesha faida jamii itakazozipata Wapatie kila kikundi dakika 10 za kujadili na kuandika majibu. Wazungukie kwenye makundi ili kama kuna hoja uweze kuielezea Waambie wana kikundi wachague mwakilishi wao mmoja atakayewasilisha majibu yao. Wajadiliane majibu ya kazi zilizowasilishwa pamoja na darasa zima. Hakikisha kuwa faida zilizoorodheshwa hapa chini zinakuwemo kwenye majadiliano. Faida atakazopata mama Mwanamke anayetumia njia za uzazi wa mpango: Ataweza kupata afya na kuondokana na msongo wa uzazi uliotangulia Anakuwa na muda zaidi wa kuangalia familia na watoto wake Anakuwa na nguvu ya kushiriki kwenye shughuli za kujiingizia kipato na kuweza kuwa na uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha Anaweza kuwa na muda wa kutosha na mume wake/ mwenzi wake na kufurahia tendo la ngono akiwa na utulivu wa akili. Anakuwa na muda wa kushiriki kwenye shughuli za maendeleo. Faida atakazopata baba Mwanaume anaetumia njia za uzazi wa mpango anaweza: Kuwa na utulivu zaidi katika kupanga pato la familia.

107

Kuwa na muda wa kuangalia watoto wake kwa kuweza kukidhi mahitaji yao ya msingi kama vile elimu/ shule , malazi, nguo na huduma ya tiba Anakuwa na muda wa kutosha kushiriki kwenye shughuli za maendeleo Faida kwa mtoto Endapo wazazi wanatumia njia za uzai wa mpango mtoto atakuwa: Amenyonyeshwa kwa kipindi kirefu zaidi (hadi kufikia miaka 2 ama zaidi) na hivyo kupunguza utapiamlo, maambukizi ya kujirudia rudia na kusaidia kuongeza kasi ya kukua na kuendelea zaidi. Kupata uangalizi mkubwa zaidi na mapenzi zaidi kutoka kwa wazazi wake na wanafamilia kwa ujumla. Faida wanazozipata jamii /uchumi wa taifa Jamii yenye wanawake wanaopanga uzazi watakuwa na : Watu wachache na kuweza kuwapatia shule bora zaidi na hudu nyingine za kijamii kama vile huduma za tiba, huduma za maji, na hali nzuri ya usafi wa mazingira. Kuwa na uwiano ulio bora zaidi kati ya rasilimali zilizopo na watu wanaozitumia. Wanakuwa na yatima wachache wa kuwahudumia

7.4 Njia za Uzazi wa Mpango zinazopatikana hapa Tanzania

Hatua ya kwanza Waambie washiriki wataje njia mbalimbali za uzazi wa mpango zilizopo/ au zinazotumika hapa Tanzania . Orodhesha majibu yao kwenye bango. Jadili majibu yaliyopendekezwa na uulize kama kuna yeyote aliye na uzoefu wowote binafsi amabo angpenda kuwashirikisha kuhusiana na njia mojawapo. hakikisha unasashihisha upotoshaji wa dhana wowote au imani mbaya zitakazoweza kujitokeza . Hatua ya Pili Onyesha mfano wa njia mbalimbali za Uzazi wa Mpango kwa ajili ya washiriki. Wazungushie ili kila mmoja aweze kuziona. Waambie washiriki kwamba njia uzazi wa mpango zinazopatika hapa Tanzania zinaweza kuwekwa kwenye makundi matano: Njia za maumbile, Njia za vizuizi

108

zinazodhoofisha mbegu, Njia za kutumia vichocheo, Njia za asili, na Kufunga kizazi kwa hiari. Wapitishe washiriki kwenye kila kikundi. Uwaulize kama wanafahamu ni njia ipi iko kwenye kundi lipi. Baada ya hapo wapatie kitini cha njia za mpango hapa Tanzania. Mpitie kwa pamoja na kikundi na kuonyesha njia za uzazi wa mpango kila unapoiongelea njia hiyo. 1. Vichocheo (Hormonal) Kinywa (ORAL) - Vidonge vyenye vichocheo zaidi ya kimoja ( Combined oral Contraceptive (COC) Pills (Flexi-P) - Vidonge vye kichocheo kimoja (Progestin Only Pills) SINDANO - Depro ProveraMegestron Vipandikizi (IMPLANTS) - Kipandikizi aina ya Norplant (yenye vipandikizi 6 ) - Kipandikizi aina ya Implanon (yenye kipandikzi kimoja ) Njia ya Vizuizi (Barrier Methods) - Kondom (kiume - Dume, kike -Lady Pepeta) Kitanzi (Intra Uterine Contraceptive Device- IUCD) - Shaba (Copper T 380A) Njia asilia (Natural Methods) - Kupima ute (Billings Ovulation Method/Cervical Mucus Method BOM/CMM) - Njia maziwa ya mama wakati wa kunyonyesha (Lactation Amenorrhea Method- LAM) - Kalenda - Joto la mwili (Basal Body Temperature) Upasuaji wa hiari wa kufunga kizazi (Voluntary Surgical ContraceptionVSC) - kufunga kizazi kwa hiari kwa wanawake (Tubal ligation) - kufunga kizazi kwa hiari kwa wanaume (Vasectomy male)

2. 3. 4.

5.

Hatua ya Tatu Wanakikundi wanatakiwa akufahamu kuwa vidonge, njia ya homini njia ya vizuizi zinapatika mahali pengi hata maeneo ya biashara na kwenye vituo vya

109

afya. Njia nyingine zilizobakia zinapatikana kwenye vituo vya afya tu na zinatakiwa zitolewe na mtaalamu wa afya. Sasa tutajadiliana kuhusu kuhusu vidonge na kondom kwa kina zaidi. Kama kuna muuguzi au mtaalamu wa masuala ya uzazi wa mpango waalike ili waje kujadili kuhusu taarifa zifuatazo. Endapo hakuna mtaalamu rejea taarifa ifuatayo na wanakikundi. Wapatie vidonge (njia ya kupanga uzazi kwa kumeza). Vidonge (Oral Contraceptives) Kuna aina mbili za vidonge zinazotumika hapa Tanzania Muunganiko wa estrojeni na projestini mf Makroginon, Lo femenal na Duofem Zenye projestini peke yake -microluti na Microval.

Vidonge vyenye muunganiko wa vichocheo kama vile Flexi P. VIdonge vilivyo na homoni zaidi ya moja ni nini? - Hivi ni vidonge vya kuzuia mimba ambavyo vina homoni mbili esterojen na projesteron (two hormones estrogen and progestin). Vidonge hivi vyenye homoini zaidi ya moja vinafanya kazi kwa namna gani? - Vinazuia kupevuka kwa yai (ovulation) - Zinasababisha eneo la ndani ya mji wa mimba lisifae kwa ajili ya kurutubisha yai - Zinafanya ute wa kizazi kuwa mzito na kusababisha iwe ni vigumu kwa mbegu za kiume kupenya na kuingia kwenye mji wa mimba - Kufanikisha : vidonge hivi vinafanikisha sana kama vikitumiwa vema . Faida zake - Kuzuia mimba zisizotakiwa - Kurekebisha hedhi - Hupunguza kiasi cha damu ya hedhi na maumivu wakati wa hedhi - Huongeza ashki ya kufanya mapenzi kwa baadhi ya wanawake kwa vile hofu ya kupataujauzito inakuwa imeondoka - Zinapatikana kwenye maeneo ya kibishara na hat kupitia wasambazji wa ngazi ya jamii. - Haziingiliani na tendo la ngono - Ukiacha kutumia inakuwa rahisi mwili kurudi katiak hali yake na kubeba mimba tena (easily reversible) Nani hawezi kutumia aina hii ya njia ya uzazi wa mpango

110

Mwanamke mjamzito au ambae huenda ana mimba Mwanamke mwenye tatizo la ugonjwa wa ini - Mwanamke mwenye kutokwa na damu ukeni bila sababu zilizo wazi - Mwanamke mwenye kuumwa kichwa cha kipanda uso - Mwanamke mwenye kutokwa na mishipa ya verikosi (varicose veins) Madhara yanayoweza kuwepo - Kichefuchefu, dalili ya kutokwa na damu katikati ya siku za hedhi kuongezeka uzito kidogo, kizunguzungu, kichwa kuuma kidogo Dalili za tahadhari ambazo zitahitaji uangalizi wa haraka wa kidaktari; - Maumivu ya kichwa na kutoona vizuri - Maumivu makali chini ya tumbo - Maumivu ya kifua - Maumivu kwenye misuli ya calf - Moyo kwenda kasi Kuzuia magonjwa ya ngono pamoja na VVU - Vidonge vya mchanganyiko wa homoni haviwezi kukulinda na magonjwa y ngono ukiwemo UKIMWI Vidonge vya kichocheo kimoja cha projestini peke yake (Progestin Only Pill) Vidonge vya projestini peke yake ni nini? - Ni kidonge kilicho na homoni moja aina ya projestini tu. Zinafanya kazi kwa namna gani - Zinafanya ute wa shingo ya kizazi kuwa mzito na kusababisha iwe vigumu mbegu za kiume kupenya na kuingia kwenye mji wa mimba . - Huzuia yai kupevuka - Zinasababisha sehemu ya ndani ya mji wa mimba kutokuwa mahali panapofaa kutunga mimba Inavyofanikisha Inafanikisha sana kama zikitumika kila siku kwa wakati ule ule Faida zake - Zinazuia mimba - Hazipunguzi wingi ama ubora wa maziwa ya mama kwa hiyo wanawake wanaonyonyesha wanaweza kutumia njia hii. - Ukiacha kutumia inakuwa rahisi mwili kurudi katiak hali yake na kubeba mimba tena (easily reversible) Nani wanaweza kutumia njia hiii? - Wanawake wote walio kwenye umri wa kuzaa wanaweza kutumia( miaka 18- 49)

111

- Wanawake wanaonyonyesha (walio na watoto chini ya miezi 6) Nani hawawezi kutumia njia hii? - Mwanamke mjamzito au ambae huenda ana mimba - Mwanamke anayetokwa damu ukeni bila kuwepo na sababu inayoeleweka Madhara yanayoweza kuwepo Kuwa na dalili ya damu au hedhi kusimama - Kuwa na hedhi isiyokuwa na mpangilio kati ya mzunguko mmoja wa hedhi na mwingine Dalili za hatari ambazo zitahitaji uangalizi wa haraka wa daktari: - Kuwa na maumivu makali chini ya tumbo pamoja na kukosa kuona hedhi - Endapo mtumiaji ataendelea kusahau kutumia vidonge au kunywa akiwa amechelewa muda aliojiwekea. ( taking them late) - Kutokwa damu nyingi (Excessive bleeding) Kuzuia magonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI - Vidonge vya uazi wa mpango vyenye homoni zaidi ya moja haviwezi kukulinda na magonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI Tahadhari : Wanawake hawapaswi kuanza kutumia vidonge vya uzazi bila kupata ushauri wa mtaalamu wa afya ili kuepuka mataizo ya kiafya na kuweza kupata taarifa sahihi na maelekezo sahihi ya jinsi ya matumizi. Maelekezo kwa kiongozi wa Rika Tumeshaongea kuhusu kondom ya kiume na ya kike kwenye kipindi kilichopita, ila tunaweza kuwakumbusha washiriki kuhusu majina ya kondom za kike na kiume tulizozijadili. Kama muda unatosha pitia taarifa na kama la wapatie washiriki kitini cha Kondom na muendelee kwenye hatua ya 4: Kazi ya igizo dhima. Wapatie kitini cha Kondom na upitie na wanakikundi. Wakumbushe wanakikundi kwamba tayari tumesha ongelea kuhusu kwenye somo lilopita na kwamba tutapitia taarifa kuhusu kondom kwa kutumia kitini. Kondomu kama vile Dume na Lady Pepeta. Kondom ni nini? - Kondom za kiume ­ Ni kifaa cha plastiki kinachovaliwa kwenye uume uliosimama kabla ya tendo la ngono - Kondom ya kike - ni kifaa cha plastik kinachovaliwa ndani ya uke

112

kabla ya kuanza tendo la ngono Huwa inafanya kazi kwa namna gani? - Kondom huzuia mbegu za kiume zikitoka zisiingie kwenye njia ya uke ya mwanamke Inavyofanikisha - Kondom zinafanikisha sana kama zikitumika kila wakati na kwa usahihi Faida zake s - Haihitaji kupimwa na mganga kabla ya kutumia unanunua na kuamua kutumia - Ni rahisi kutumia, kupatikana (zipo kwenye maduka na vibanda vingi) - Ni salama inafanisha na inabebeka kwa urahisi - Inatosheleza hasa wakati ambapo kuna haja ya kuwa na njia ya uzazi ya muda mfupi Nani anaweza kutumia kondom? - Wanawake na wanaume wote - Wenzi ambabo kwa sababu zozote hawawezi kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango - Wenzi ambao wako katika matibabu ya magonjwa ya ngono - Wenzi wanaohitaji njia ya akiba (backup method) - Wenzi wanaohitaji njia ambayo inafanikisha mara tu baada ya kufanyiwa upasuaji wa kufunga njia ya mbegu za baba ­ kwa ajili ya kumwaga manii baada ya kufanyiwa operesheni au miezi mitatu baada ya kufanyiwa operesheni. - Wateja wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa wa kufunga njia ya mbegu za kiume Nani ambao hawaruhusiwi kutumia kondom? - Wale ambao uwezo wa uume kusimama hautabiriki - Wale wanaopata mzio kutokana wa mpira Hasara zinazoweza kuwepo - Muwasho ama mzio I - Uhitaji wa kutakiwa kuvaa kondom nyingine kila baada ya manii kutoka Dalili za hatari zinazohitaji kumuona daktari kwa haraka - Hakuna labda kwa wale ambao wanapata mzio Inazuia magonjwa ya ngono na UKIMWI: - Pia huzuia kuenea kwa magonjwa ya ngono na UKIMWI

113

Hatua ya Nne Waambie washiriki kwamba watakaa kwenye makundi ya watu watatu na kufanya igizo. Mtu mmoja kutoka kwenye kila kikundi atakuwa ni mhudumu wa saluni na mmoja atakuwa mteja na mwingine atakuwa mtazamaji. Baada kila igizo mtazamaji ataongea na timu yake kuhusu kile alichokiona, ikiwa ni pamoja na kama taarifa sahihi kuhusiana na njia za uzazi wa mpango ilitolewa na je ni stadi gani za mawasiliano ya ana kwa ana zilizotumika (kusalimia, kusikilza kwa makini, kuuliza maswali, kutumia lugha nyepesi na kutumia zana za kuwezeshea) kila mmoja kwenye makundi madogo atapaswa kuwa na fursa ya kuwa mhudumu wa saluni, mteja, na mtazamaji. Baaada ya vikundi vikiwa vimeshapat fursa ya kufanya mazoezi ya maigizo, waambie wanvikundi kwamba waigize moja ya maigizo na kujadiliana jinsi ambvyo kila kundi lilivyofanya kwenye kundi kubwa. Visa mkasa vya kuigiza Njia za Uzazi wa Mpango Kisa mkasa cha kwanza Andiko (script) kwa ajili ya mhudumu wa saluni Nuru alianza siku zake za hedhi siku tatu zilizopita. Mwane ana miezi 8 na anataka kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Amwahi kusikia kuhusu vidonge na anataka kuwa mtumiaji wa vidonge. Je ni maswali gani ushauri upi na mapendekezo gani utampatia? Andiko (script) ya mteja Wewe ni Nuru mama wa watoto wawili, unataka watoto wako waachane kwa kipindi cha miaka miwili. Umewahi kusikia kuhusu vidonge vya kumeza na kwamba ni rahizsi kupatikana kwenye maduka ya dawa na vituo vya afya. Uantaka kuvitumia lakini haufahamu sana kuhusu vidonge hivyo. Kisa mkasa cha Pili Andiko (script) ya Mhudumu wa Saluni Mama Mwajabu alijifungua siku 40 zilizopita. Ananyonyesha na aataka kutumia vidonge, amekuwa akisikia kuhusu vidonge maalum vilivyopo amabvyo vianweza kumsaidia kuzaa watoto kwa muachano mzuri. Je utamshauri na kupendekeza afanye nini?

114

Andiko (script) ya mteja Wewe ni Mama Mwajabu na umeju=ifungua siku za karibuni. Huyu ni mtoto wako wa kwanza na unataka kuwe na mwachano kati ya mtoto wa kwanza na wa pili miaka miwili. Umesikia kuhusu kwamba kuna vidonge unavyoweza kutumia kama mamaanyenyonyesha, ila hufahamu nini vya aina gani, vinafanya kazi namna gani na wapi unapoweza kuvipata. Kisa mkasa cha Tatu Andiko (script) ya mhudumu wa saluni Yusufu anataka kutumia njia za uzazi wa mpango na mwenzi wake ambayo itakuwa ni sahihi kwa ajili ya malengo yake ya kupanga uzazi. Je utampa ushauri gani na mapendekezo gani? Andiko (script) la mteja Wewe na Yusufu, baba wa mtoto mmoja, mnataka kutumia njia za uzazi wa mpango amabo utawalinda wewe na mwenzi wako ili msipate mimba ama maambukizi. Muulize mhudumu wa saluni akushauri na kukupendekezea ni njia ipi unaweza kuifikiria kuitumia.

7.5 Njia za Uzazi wa Mpango zinazotolewa kwenye Vituo vya Afya

Angalizo kwa kiongozi wa Rika: Taarifa ifuatayo inaweza kutolewa na Muuguzi ama mtaalamu wa uzazi wa mpango endapo kuna muda wa kutosha, vinginevyo elezea dhana muhimu kabisa kuhusiana na njia za uzazi wa mpango zinazopatikan kwenye vituo vya afya. Kila njia ya uzazi wa mpango inazo faida na madhara yake. Wahudumu wa Saluni za urembo wanaweza kuwaelekeza wateja wao kwenye vituo vya afya ya familia ili waweze kupata maelekezo ya kina zaidi kuhusu njia za uzazi wa mpango zinazopatikana hapa Tanzania. Taarifa zaidi kuhusiana na njia hizi ipo kwenye kitini kwa ajili ya kurejea zaidi. Hatua ya Kwanza Waambie washiriki kwamba mbali na njia zilizotajwa (vidonge na kondom) amavzo hupatikana kwenye maeneo ya kibishara, zipo njia nyingine zinazopatikana kwenye vituo vya huduma za afya na zinahitaji kutolewa na

115

mtaalamu wa afya. . Washriki wanapaswa kufahamu kwamba utaeleza kwa ufupi sana njia hizi na utawapatia kitini chenye maelekezo ya kina zaidi ambapo kinaweza kutumika baadae kama mwongozo rejea. Waambie washiriki kwamba ni muhimu kuwaelekeza wateja wao kwenye vituo vya kutolea huduma endapo wateja watakuwa na maswali ambayo hawawezi kuyajibu. Hapa chini kuna taarifa ambayo unaweza kuitumia kwenye hitimisho lako kuhusu Njia za uzazi wa mpango ambazo watazipata kwenye kituo cha afya: KITANZI ni kipande kidogo cha plastiki laini na shaba kandokando chenye umbo la T. kina nyuzi nyembamba mbili zimewekwa kwenye sehemu ya mwisho. Inaingizwa kwenye mji wa mimba kupitia ukeni na shingo ya mji wa mimba na mtaalamu aliyesomea. Baada ya kifaa hicho kuwekea kweny mji wa mimba vikamba viiwili tulivosema hapo awali huachwa vikiningia kupitia kwenye shingo ya uzazi hadi kwenye uke ili kwamba mteja wa kifaa hicho aweze kujichunguza ili kuhakikisha kama kiko mahali pake. Kitanzi (IUD) ni njia inayofanikisha sana. Haikulindi na mgonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI. Sindano (Depo- Provera & Megestron) hizi ni njia za uzazi wa mpango zinazofanikisha zenye kichocheo kimoja ambacho hutolewa kwa njia ya sindano. Njia hii ina kichocheo kinachoitwa projestini. Sindano moja tu inakukinga dhidi ya mimba kwa miezi mingi. Sindanio haikulindi dhidi ya magojwa ya ngono ukiwemo UKIMWI. Vipandikizi (vijiti): (Implants: Norplant and Implanon) hivi ni viplastiki mithili ya vijiti vidogo vyenye dawa vinawekwa chini ya ngozi kwenye mkono. Ina vichocheo sawa na sindano ya depo provera na vidonge vya Minni. Kipandikizi kinaweza kukupatia kinga dhidi ya mimba kwa miezi kadhaa. Ila haikulindi na magonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI Upasauji wa hiari wa kufunga kizazi : Ni njia ya kufunga kizazi ya upasuaji ambapo huweza kufanyiwa mwanaume au mwanamke. Zote ni njia za kudumu. Kwa mwanamke inajulika kama kufunga mirija ya kupitisha yai la kike (Tubal-ligation). Kwa wanaume hujulikana kama kufunga mirija miwili inayopitisha mbegu za kiume (vasectomy) a) Kufunga mirija inayopitisha mayai kwa mwanamke (Tubal-ligation)

116

ni njia ya uzazi wa mpango ya kudumu kwa wanawake . ni salama mkato wake ni rahisi. Sehemu ndogo ya mirija ya fallopian hufungwa pamoja na kukatwa. b) Kufunga mirija miwili inayopitisha mbegu za kiume (vasectomy) ni njia ya kupanga uzazi ya kudumu kwa wanaume ambao hawataki kuzaa watoto zaidi. Ni salama na ni upasuaji rahisi ambao huwa hauchukui zaidi ya dakika 30. Wakati wa operesheni mirija miwili amabyo husafirisha mbegu za kiume kutoka kwenye kifuko cha mmbegu testis kwenda kwenye uume vinafungwa na kukatwa. Mwnaume ataendelea kutoa manii lakini manii hayatkuwa tena na mbegu za kiume. Njia Asilia za Uzazi wa Mpango , Hizi ni njia nyingizo ambazo wenzi wanaweza kuzitumia kujikinga na mimba bila kutumia njia za kisasa. Hizi zinahitaji uelewa kuhusiana na mwili wa mwanamke na mawasiliano mazuri baina ya wenzi ili iweze kufanikisha. Baadhi ya njia hizi ni : a. Njia ya kutumia kipindi cha kunyonyesha (Lactational Amenorrhoea Method LAM) ni njia ya asili ya kuzuia mimba kwamba mama anayenyonyesha anaweza kuitumia miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaa kujilinda asipate mimba. Njia hii itafanya kazi kama mama atakuwa hajapata hedhi tangu alipojifungua. Endapo anatumia maziwa yake peke yake kumlisha mtoto walao mara 6-10 kwa siku moja ikiwa ni pamoja na masaa ya kumnyonyesha usiku) na endapo mtoto ana yuko chini ya miezi 6. b. Ute (CMM) ni njia ambayo mwanamke anaweza kuelewa siku zake za kupevuka kwa yai kwa kuchunguza mabadilko ya ute . kuacha kufany ngono katika siku ambazo ute unakuwa mzito, mweupe usiokatika kirahisi) unakuwa ni ute ulo tayari kupokea mimba.. Hatua ya Pili Wambie washiriki waeleze kwa ufupi kile walichojifunza wakti wa warsha hii. Wapatie kitini cha Ujumbe Muhimu wa Uzazi wa mpango. Wasome ukurasa huo. Ujumbe Muhimu : Uzazi wa Mpango Mimba na matatizo wakati wa kujifungua ni sababu kuu za vifo vya wanawake kati ya miaka 14- 49.

117

Uzazi wa Mpango unaokoa maisha na haki ya msingi ya binadamu. Kutumia Uzazi wa Mpango kunamnufaisha mama, baba, mtoto na jamii Njia za Uzazi wa Mpango zilizopo hapa Tanzania zinaweza kuwekwa kwenye makundi matano:n Homoni, vizuizi , kitanzi operesheni ya hiari na njia asilia. Njia zote sin faida na madahara yake.. Mwanamke au wenzi watatakiwa kwenda kupata huduma ya uhsauri nasaha, kupima afya zao na kushauriwa ili waweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu njia za uzazi wa mpango. Hatua ya Tatu Wanakikundi wafahamu kwamba wameshamaliza mada ya Uzazi wa Mpango. Wapatie kitini cha Njia za Uzazi wa Mpango kwenye ngazi ya kituo cha kutolea huduma zaAafya na kitini cha Njia Asilia

118

KITINI CHA MADA YA NANE

VIDONGE (ORAL CONTRACEPTIVES)

Kuna aina mbili za njia za uzazi za vidonge hapa Tanzania Muunganiko wa estrojeni na projestini mf Makroginon, Lo femenal na Duofem Zenye projestini peke yake -microluti na Microval.

Vidonge vyenye muunganiko wa vichocheo kama vile Flexi P. VIdonge vilivyo na homoni zaidi ya moja ni nini? - Hivi ni vidonge vya kuzuia mimba ambavyo vina homoni mbili esterojen na projesteron (two hormones estrogen and progestin). Vidonge hivi vyenye homoini zaidi ya moja vinafanya kazi kwa namna gani? - Vinazuia kupevuka kwa yai (ovulation) - Zinasababisha eneo la ndani ya mji wa mimba lisifae kwa ajili ya kurutubisha yai - Zinafanya ute wa kizazi kuwa mzito na kusababisha iwe ni vigumu kwa mbegu za kiume kupenya na kuingia kwenye mji wa mimba - Kufanikisha : vidonge hivi vinafanikisha sana kama vikitumiwa vema . Faida zake - Kuzuia mimba zisizotakiwa - Kurekebisha hedhi - Hupunguza kiasi cha damu ya hedhi na maumivu wakati wa hedhi - Huongeza ashki ya kufanya mapenzi kwa baadhi ya wanawake kwa vile hofu ya kupataujauzito inakuwa imeondoka - Zinapatikana kwenye maeneo ya kibishara na hat kupitia wasambazji wa ngazi ya jamii. - Haziingiliani na tendo la ngono - Ukiacha kutumia inakuwa rahisi mwili kurudi katiak hali yake na kubeba mimba tena (easily reversible) Nani hawezi kutumia aina hii ya njia ya uzazi wa mpango Mwanammke mjamzito au ambae huenda ana mimba Mwanamke mwenye tatizo la ugonjwa wa ini - Mwanamke mwenye kutokwa na damu ukeni bila sababu zilizo wazi - Mwanamke mwenye kuumwa kichwa cha kipanda uso - Mwanamke mwenye kutokwa na mishipa ya verikose (varicose veins) Madhara yanayoweza kuwepo - Kichefuchefu, dalili ya kutokwa na damu katikati ya siku za hedhi

119

kuongezeka uzito kidogo, kizunguzungu, kichwa kuuma kidogo Dalili za tahadhari ambazo zitahitaji uangalizi wa haraka wa kidaktari; - Maumivu ya kichwa na kutoona vizuri - Maumivu makali chini ya tumbo - Maumivu ya kifua - Maumivu kwenye misuli ya calf - Moyo kwenda kasi Kuzuia magonjwa ya ngono pamoja na VVU - Vidonge vya mchanganyiko wa homoni haviwezi kukulinda na magonjwa y ngono ukiwemo UKIMWI Vidonge vya kichocheo kimoja cha projestini peke yake (Progestin Only Pill) Vidonge vya projestini peke yake ni nini? - Ni kidonge kilicho na homoni moja aina ya projestini tu. Zinafanya kazi kwa namna gani - Zinafanya ute wa shingo ya kizazi kuwa mzito na kusabaisha iwe vigumu mbegu za kiume kupenya na kuingia kwenye mji wa mimba. - Huzuia yai kupevuka - Zinasababisha sehemu ya ndani ya mji wa mimba kutokuwa mahali panapofaa kutunga mimba Inavyofanikisha Inafanikisha sana kama zikitumika kila siku kwa wakati ule ule Faida zake - Zinazuia mimba - Hazipunguzi wingi ama ubora wa maziwa ya mama kwa hiyo wanawake wanaonyonyesha wanaweza kutumia njia hii. - Ukiacha kutumia inakuwa rahisi mwili kurudi katiak hali yake na kubeba mimba tena (easily reversible) Nani wanaweza kutumia njia hiii? - Wanawake wote walio kwenye umri wa kuzaa wanaweza kutumia( miaka 18- 49) - Wanawake wanaonyonyesha (walio na watoto chini ya miezi 6) Nani hawawezi kutumia njia hii? - Mwanamke mjamzito au ambae huenda ana mimba - Mwanamke anayetokwa damu ukeni bila kuwepo na sababu inayoeleweka Madhara yanayoweza kuwepo Kuwa na dalili ya damu au hedhi kusimama

120

Kuwa na hedhi isiyokuwa na mpangilio kati ya mzunguko mmoja wa hedhi na mwingine Dalili za hatari ambazo zitahitaji uangalizi wa haraka wa daktari: - Kuwa na maumivu makali chini ya tumbo pamoja na kukosa kuona hedhi - Endapo mtumiaji ataendelea kusahau kutumia vidonge au kunywa akiwa amechelewa muda aliojiwekea. ( taking them late) - Kutokwa damu nyingi (Excessive bleeding) Kuzuia magonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI - Vidonge vya uazi wa mpango vyenye homoni zaidi ya moja haviwezi kukulinda na magonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI Tahadhari : Wanawake hawapaswi kuanza kutumia vidonge vya uzazi bila kupata ushauri wa mtaalamu wa afya ili kuepuka mataizo ya kiafya na kuweza kupata taarifa sahihi na maelekezo sahihi ya jinsi ya matumizi

121

KITINI CHA MADA YA 8

KONDOM

Kondom ni nini? - Kondom za kiume ­ Ni kifaa cha plastiki kinachovaliwa kwenye uume uliosimama kabla ya tendo la ngono - Kondom ya kike - ni kifaa cha plastik kinachovaliwa ndani ya uke kabla ya kuanza tendo la ngono Huwa inafanya kazi kwa namna gani? - Kondom huzuia mbegu za kiume zikitoka zisiingie kwenye njia ya uke ya mwanamke Inavyofanikisha - Kondom zinafanikisha sana kama zikitumika kila wakati na kwa usahihi Faida zake s - Haihitaji kupimwa na mganga kabla ya kutumia unanunua na kuamua kutumia - Ni rahisi kutumia, kupatikana (zipo kwenye maduka na vibanda vingi) - Ni salama inafanisha na inabebeka kwa urahisi - Inatosheleza hasa wakati ambapo kuna haja ya kuwa na njia ya uzazi ya muda mfupi Nani anaweza kutumia kondom? - Wanawake na wanaume wote - Wenzi ambabo kwa sababu zozote hawawezi kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango - Wenzi ambao wako katika matibabu ya magonjwa ya ngono - Wenzi wanaohitaji njia ya akiba (backup method) - Wenzi wanaohitaji njia ambayo inafanikisha mara tu baada ya kufanyiwa upasuaji wa kufunga njia ya mbegu za baba ­ kwa ajili ya kumwaga manii baada ya kufanyiwa operesheni au miezi mitatu baada ya kufanyiwa operesheni. - Wateja wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa wa kufunga njia ya mbegu za kiume Nani ambao hawaruhusiwi kutumia kondom? - Wale ambao uwezo wa uume kusimama hautabiriki - Wale wanaopata mzio kutokana wa mpira

122

Hasara zinazoweza kuwepo - Muwasho ama mzio I - Uhitaji wa kutakiwa kuvaa kondom nyingine kila baada ya manii kutoka Dalili za hatari zinazohitaji kumuona daktari kwa haraka - Hakuna labda kwa wale ambao wanapata mzio Inazuia magonjwa ya ngono na UKIMWI: - Pia huzuia kuenea kwa magonjwa ya ngono na UKIMWI

123

KITINI CHA MADA YA 8

NJIA ZA UZAZI WA MPANGO ZINAPATIKANA KWENYE VITUO

VYA AFYA

Kitanzi (IUD) Kitanzi ni nini? - KITANZI ni kipande kidogo cha plastiki laini na shaba kandokando chenye umbo la T. kina nyuzi nyembamba mbili zimewekwa kwenye sehemu ya mwisho. Inaingizwa kwenye mji wa mimba kupitia ukeni na shingo ya mji wa mimba na mtaalamu aliyesomea. Baada ya kifaa hicho kuwekea kweny mji wa mimba vikamba viiwili tulivosema hapo awali huachwa vikiningia kupitia kwenye shingo ya uzazi hadi kwenye uke ili kwamba mteja wa kifaa hicho aweze kujichunguza ili kuhakikisha kama kiko mahali pake. Kitanzi (IUD) ni njia inayofanikisha sana. Haikulindi na mgonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI. Inafanya kazi namna gani - Inazuia mimba kwa kuzuia kupandiza yai kwenye mji wa mimba. - Shaba inayotoka kwenye kitanzi (IUD) inaua nguvu ya mbegu za kiume (spermicidal) na hivyo kupunguza kasi ya mbegu za kiume Inavyofanikisha: - Inafanikisha ni ya kuaminika Faida s - Haina madhara ya kihomoni yanayohusianishwa nayo - Ina ulinzi wa muda mrefu (hadi miaka 10) - Haiingiliani na tendo la ngono - Inaweza kuondolewa wakati wowote - Haiingiliani na tiba - Inaweza kuwekwa mapema tu mara baada ya kujifungua - Huzuia mimba punde tu inapowekwa - Uzazi hurudi mara tu baada ya kuindoa. Nani wanaweza kutumia kitanzi (IUD) - Wanawake /wenzi ambao wanataka kuzuia mimba kwa kindi kirefu - Wanawake walio kwenye mahusiano dhabiti ya mume mmoja - Wanawake wanaonyonyesha baada ya kujifungua - Wale ambao hawezi kutumia uzazi wa mpango wenye vichocheo vya homoni

124

Wanawake ambao wamekamilisha kuza watoto lakini bado hawako tayari kwa ajili ya njia za kudumu za kufunga kizazi Nani amabo hawezai kutumia kitanzi (IUD) - Wajawazito - Wanawake amabo wamepata maambukizi (PID) katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita - Wanawake walio na historia ya kutokwa na damu nyingi ya hedhi - Wanawake wenye matatizo ya moyo - Wanwake walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa ya ngono Kukulinda na magonjwa ya ngono na VVU - Haikupi ulinzi dhidi ya magonjwa ya ngono na VVU. Uwezekano wa madhara - Kupata maumivu sehemu ya chini ya tumbo na maumivu wakati wa hedhi - Kupata matone ya dmau katikati siku kabal ya hedhi. - Inaweza ikachomoka - Kutoka majimji ukeni ingawaje hayana harufu mbaya Dalili za hatari amabzo zitahitaji uanggalizi wa daktari; - Kuchelewa au kukosa hedhi kabisa - Maumivu makali chini ya tumbo au kutokwa na damu wakati wa kujamiiana - Kutokwa na uchafu kwenye uke wenye harufu mbaya - Kutokwa na damu ukeni kwa muda mrefu - Kikamba kutoonekanaau kuwa fupi sana au kurefuka sana Sindano (Depo- Provera & Megestron) Hii ni nini: Hii ni njia ya uzazi wa mpango yenye kichocheo kimoja ambacho hutolewa kwa njia ya sindano. Njia hii ina kichocheo kinachoitwa projestini. Sindano moja tu inakukinga dhidi ya mimba kwa miezi mingi. Sindano haikulindi dhidi ya magojwa ya ngono ukiwemo UKIMWI Inafanya kazi namna gani; - Huzuia mwili wa mwanamke kutokuachia yai la kila mwezi - Hufanya ute kuwa mzito na hivyo kuwa vigumu kwa mbegu za kiume kupenya na kuingia kweny kizazi

125

Inafanya iwe vigumu kwa yai lililo rutubishwa kuweza kukaa kwenye mji wa mimba (embed) Inavyofanikishas - Inafanikisha sana Faida zake - Haipunguzi kiasi cha maziwa ya mama - Inaweza kutumiwa na wanawake ambao hawawezi kutumia vidonge vye vichocheo vya aina mbili - Ukiacha unapata mimba (Reversible) - Inaweza kutolewa majuma sita baada ya kujifungua - Ni njia ya muda mrefu; sindano moja inaweza kukulinda kwa miezi mitatu - Ni makini Nani anaweza kutumia - Wanawake wengi wakiwemo wale ambao hawawezi kutumia vidonge Nani hawawezi kutumia - Wanwake ambao wanahisiwa au wamepima na kugundulika wana mimba - Wanawake wanaotaka kupata mimba mara moja baada ya kuacha kutumia njia za uzazi wa mpango. - Wanawake wanotokwa damu bila kuwa na sababu maalumu Uwezekano wa Madhara - Kukosa hedhi au kupata matone damu. - Kuchelewa kupata ujauzito kati ya miezi 4-9 baada ya kuacha kutumia sindano. Kuzuia magonjwa ya Ngono na VVU - Hakuna ulinzi wa magonjwa ya ngono na UKIMWI Dalili za hatari amabzo zitahitaji uangali wa daktri; - Kutokwa kwa damu kwa muda mrefu - Msongo - Maumivu ya kichwa - Kuongezeka uzito sana Vipandikizi (Norplant and Implanon) Vipandiki ni nini? - Hivi ni vijiti vidogo sita au kimoja vyenye dawa vinawekwa chini ya ngozi kwenye mkono. Ina vichocheo sawa na sindano ya depo provera na vidonge na vya Minni.

126

Vinafanya kazi namna gani ; - Huzuia mwili wa mwanamke kuachilai yai kila mwezi - Hufanya ute wa kizazi kuwa mzito na kuwa vigumu kwa mbegu ya kiume kupenya kwenda kwenye kizazi - Inakuwa vigumu kwa yai kukaa kwenye mji wa mimba (embed) Inavyofanikisha: Zinafanikisha sana mara baada ya kuwekewa uhakika wa matumizi mazuri ni hakika. Faida - Inafaniksha masaa 24 baada ya kuiweka - Haiathiri unyonyeshaji - Inatoa ulinzi kw akipndi kirefu hadi miaka 3-5 - Haiingiliani na tendo la ngono Nani wanweza kutumia - Wanawake wanaotaka kuzuia mimba kwa muda mrefu - Wanawake ambao wameshapata watoto wa kutosha na hawako tayari kwa ajili ya kutumia njia ya kudumu ya kufunga kizazi - Wanwake wenye ugonjwa wa upungufu wa damu kutokana na seli mundu ( sickle cell) - Wanawake ambao hawawezi kutumia vidonge Nani hawawezi kutumia njia hii - Wajawazito - Wanawake wenye kupata mabadiliko ya hedhi kila mwezi - Wanawake wenye ugonjwa wa ini - Wanawake wenye kutokwa damu ukeni bila kuwa na maelezo yanayoeleweka Athari za vipandikizi (Norplant/Implanon) - Kubadilika kwa mzunguko wa hedhi ­ kupata matone, au kuja bila kuwa na mpangilio maalumu au kukosa hedhi kabisa - Kuongeza au kupungua uzito sana Kuzuia magonjwa ya ngono na UKIMWI Haiwezi kukulinda na Magonjwa ya ngono na UKIMWI Dalili za tahadhari ambazo zitahitaji uangalizi wa haraka wa kidaktari ; - Maumivu makali chini ya tumbo - Kutokwa kwa damu nyingi ukeni - Kutokwa na usaha au kutokwa na damu au kufa ganzi - Kuumwa kichwa sanakuwa na tatizo la kutokuona vizuri

127

-

Kuongezeka sana uzito Kipandikizi kuchomoka Mteja kukosa hedhi kwa miezi miwili tangu awekewe kipandikizi

Njia ya Uzazi wa mpango ya Upasuaji wa hiari kwa wanawake na wanume a) Kufunga mirija ya mayai Tubal-ligation kufunga mirija ya mayai ni kitu gani? Kufunga mirija ya maya I ni njia ya kdumu ya uzazi wa mpango kwa wanawake. Ni njia ya usuaji ulio rahisi na salama.sehemu ndogo ya mirija ya uzazi (fallopian tubes) hufungwa kwa pamoja na kukatwa. Baada ya upasuaji huo yai haliwezi kukutana na mbegu ya kiume na mwanamke hawezi kubeba mimba na kuzaa watoto tena. Inavyofanikisha Kufunga mirija ya uzazi inafanikisha sana. Endapo itweza kushindwa kuzuia mimba huenda ikawa ni kwa sababu: o `pengine mteja alikuwa mjamzito wakati upasuaji huo ndogo ulipofanyika o Upasuaji haukufanyika kwa usahihi Faida zake - Ni njia ya kudumu, upasuaji mmoja tu unakupatia kinga ya uzazi kwa maisha yako yote na huwa haiwezi kurudia hali yake ya awali ya kuweza kuzaa. - Haiingiliani na kiasi cha maziwa yam am yatakayotoka - Hakuna haja ya kwenda kuachunguzwa na daktari mara kwa mara - Haiingiliani na mabadiliko ya kawaida ya kimwili yanayompata mwanmke - Maumivu kidogo tu baada ya upasuaji Nani anaweza kuitumia njia hii - Wanawake/ wenzi amabo hawataki kuwa na watoto zaidi Nani hawezi kutumia njia hii - Mwanamke yeyote au wenzi amabo bado wanahitaji kupat watoto zaidi - Wanawake ambao huenda ni wajawazito - Wanawake wenye maambukizi kama vile magionjwa ya ngono ambayo hayjatibiwa. Uwezekano wa madhara - Kunaweza kuwa na matatizo kutokana na upasuaji kama vile kutokwa na damu au kupata maambukizi - Kunaweza kuwa na maumivu kiasi kwa siku kadhaa baada ya upasuaji

128

Kuzuia Magonjwa ya Ngono ukiwemo UKIMWI - Haiwezi kukulinda usipate magonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI Dalili za hatari zitakazohitaji uangalizi wa daktari: - Kutokwa na damu au usaha kweny mshono - Maumivu makali ya tumbo ambayo hayakomi - Homa katika kipindi cha siku saba baada ya upasuaji - Dalili za ujauzito - Kidonda kuchelewa kupona b) Kufunga mirika ya mbegu za kiume kufunga mirika ya mbegu za kiume ni nini? Ni njia ya kudumu ya kupanga uzazi kwa wanume amabo hawatki kuendelea kupata watoto zaidi. Ni njia ya upasuaji iliyo rahisi na salama ambayo haichukui zaidi ya dakika 30. Inafanya kazi namna gani Wakati wa upasuaji mirija miwili amabyo husafirisha mbegu za kiume kutoka kwenye korodani kwenda kwenye uume zinafungwa pamoja pamoja na kukatwa. Kwa kufanya hivyo mbegu za kiume haziwezi kuingiakwenye majmaji ya kiume ambayo hutolewa wakati wa tendo la ngono. Mwanaume ataendelea kufikia kilele bila kutoa mbegu za kiume wakati wa tendo la ngono. Mbegu za kiume zinaingia kwenye mfumo w amwili kama kawaida. Inavyofanikisha - Ni njia inayofanikisha sana baada ya uasuaji. Wenzi watatkiwa kuendelea kutumia kondom kwa kipindi cha miezi mitatua au baada ya kufikia kilele baada ya tendo la ngono mara 20 baada ya upasuaji. Faida zake - Ni njia ya kudumu ianyokupanga uzazi kwa maisha yako yote. Haiingiliani na uwezo wa uume kusimama, au kutoa majmaji ya uume ama kufurahia tendo la ngono. Nani anaeweza kutumia - Mwanaume yeyote/ wenzi amabo hawataki kupata watoto zaidi. Nani hawezi kutumia - Mwanaume yeyote/ wenzi amabo bado wanhitaji kupat watoto zaidi Uwezekano wa madhara - Kunaweza kukawa na matatizo kidogo wakati wa upasuaji kama vile kutokwa na damu au kupat maambukizi - Maumivu kidogo baada ya upasuaji

129

Kuzuia magonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI - Haiwezi kuklinda na magonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI Dalili za hatari zitakazohitaji kumuoan daktari - Maumivu makali kwenye kinena au homa - Kutokwa na damu au usaha kutoka kwenye mshono - Eneo lililopasuliwa kuvimba - Kidonda kuchelewa kupona

130

KITINI CHA MADA YA 8 TOPIC 8 HANDOUT

NJIA ZA UZAZI WA MPANGO ZA ASILI

Njia za uzazi wa mpango za asili ni njia ambazo wenzi wanaweza kuzuia mimba bila kutumia njia za kisasa. Baadhi ya njia hizi ni: - Njia ya unyonyeshaji ( Lactational Amenorrhea Method LAM) - Njia ya kuangalia ute (Cervical Mucus Method) Njia ya unyonyeshaji ni nini? Ni njia ya asili ya kuzuia mimba ambapo mama anayenyonyesha anaweza kuitumia kwa kuzuia mimba kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kujifungua Inafanya kazi namna gani Njia ya unyonyeshaji (Lactational Amenorrhea Method (LAM) hii ni njia ambayo unyonyeshaji huathiri mwili wa mwanamke. Mtoto anaponyonya huzuia vichocheo vya mwili ambvyo hutumika kwenye kuachiliwa kwa yai. Inavyofanikisha Inafanikisha sana endapo mama nampa mtoto maziwa yake peke yake bila kumlisha vyakula vingine na kwamba unyonyeshaji huu uendelee sio chini ya miezi 6 baada ya kujifungua na kabla ya kurejea mzunguko wake wa hedhi. Faida zake - Inahimiza tabia ya unyonyeshaji bora - Hakuna cha kununua - Haiingiliani na tendo la ngono - Kinga ya kimya kwa mtoto - Hakuna vifaa vinavyohitajika - Hakuna maandalizi yanayohitajika Nani anaweza kutumia njia hii: - Wanawake wote wenye kunyonyesha na wale wanoweza kumpa mtot maziwa yam am tu kwa miezi 6 mfululizo baada ya kujifungua. - Wanawake au wenzi ambao imani zao za kidini haziwaruhusu kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Nani hawawezi kutumia njia hii: - Wanawake ambao hurudi kwenye mzunguko wa hedhi mwezi mmoja tu baada ya kujifungua - Wanawake ambo hawawezi kunyonyesha mtoto maziwa yam am tu bila kumpa chakula kingine chochote

131

Uwezekano wa madhara Hakuna Dalili za hatari zitakazohitaji kumuona daktari: - Kuwa na mashaka penfine ana mimba - Anapata shida wakati wa kunyonyesha - Uvimbe, vidonda au chuchu kuwa nyekundu B) Njia ya Ute wa shingo ya kizazi (CMM) Ute wa shingo ya kizazi? Ni njia ambayo mwanamke anaweza kufahamu siku zake amabzo yai limepevuka kwa kuangalia mabadiliko ya ute wa shingo ya uzazi Inafanya kazi namna gani Kutofanya tendo la ngono wakati wa siku amabzo ute wa uzazi unakuwa kama ute wa yai la kuku bichi (mweupe kama maji na unavutika ). Inavyofanikisha - Inafanikisha (sana endapo itatumika mara kwa mara na kwa usahihi Faida zake - Haihitaji maelekezo ya daktri - Haina athari za kiafya au madhara yatokanayo na matumizi - Inaongeza uelewa wa kuzuia mimba - Inawajengea wanwake uwezo wa kuwez akudhibiti matamanio yao ya kingono na kufanya maamuzi kuhusiana na uzazi wa mpango Nani wanweza kutumia njia hii ya ute (CMM) - Wanwake wenye matatizo wakitumia njia za kisasa za kupanga uzazi - Wenzi amabo huwa wanpanga ni lini wafanye ngono Nani amabo hawawezi kuitumia njia hii ya ute - Wenzi amabo hawawezi kuacha kufanya tendo la ngono wakati wa siku za hatari kwenye mzunguko wa siku za hedhi - Wanawake ambao siku zao za hedhi huwa zinabadilikabadilika - Wanawake amabo hawawezi kudhibiti matamanio yao ya kufanya ngono Uwezekano wa madhara - Hakuna Kuzuia magonjwa ya ngono ukiwemo ukimwi Hakuna Dalili za hatari zitakazoweza kuhitaji uangali wa daktari: - Dalili za ujauzito

KITINI CHA MADA YA 8

132

UJUMBE MUHIMU: UZAZI WA MPANGO: UZAZI WA MPANGO

Mimba na matatizo wakati wa kujifungua ni chanzo kikuu kinachosababisha vifo vya wanawake kati ya miaka 14-49 . Uzazi wa mpango unaokoa maisha na ni haki ya msingi ya binadamu Kutumia uzazi wa mpango kunamnufaisha mama, baba na mtoto na jamii kwa ujumla. Njia za Uzazi wa mpango zilizoko Tanzania zinaweza kuwekwa kwenye makundi matano: vichocheo, njia za vizuizi, kitanzi (IUD), njia ya uzazi ya upasuaji wa hiari, na njia asilia. Kila njia ina faida zake na madhara yake. Mwanamke au wenzi wanapaswa kupatiwa ushauri nasaha, kupimwa afya na kushauriwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi kuhusu njia za uzazi wa mpango.

133

MADA YA TISA: KUMALIZIKA KWA MASOMO YA MUHIMU

Mada ndogo 9.1 Madhumuni ya warsha na mada zilizofanyika 9.2 Zoezi la mwisho la mafunzo 9.3 Tathmini ya mafunzo 9.4 Kugawa vyeti Madhumuni: Mwisho wa somo tutakuwa a tume fanya yafutayo... kutathmini kile tulichojifunza kuhusu afya ya wanawake Kutathmini ni jinsi gani stadi nzuri za mawasiliano ya ana kwa ana zinaweza kutumika kuleta mabdiliko ya tabia Kujiandaa kutenda kama watu wa mgfano mzuri katika kuongea na kuchangiana mawazo na wanwake watu wazima hapa Tanzania kuhusu kile tulichojifunza kuhusu afya ya uzazi na jinsi ya kujilinda na magonjwa ya ngono, VVU na jinsi ya kuboresha afya zetu. Kupata vyeti vinavyoonyesha kwamba tumeshiriki na kumaliza mafunzo ya masomo haya muhimu. Zana: Leta jaribio la awali wakati mafunzo yalipoanza Bango na kalamu (markers) Dodoso la jaribio la mwisho Tathmini ya mafunzo Muda: Saa 1 na dk 30

8.1 Mada za Warsha

Hatua ya kwanza Waambie washiriki waelezee baadhi ya mada zilizomo kwenye mafunzo haya na ni kwa njia gani zinazohusiana na kuboresha afya za wanawake. Waambie washiriki kwamba somo hili ni fursa ya mwisho kwao kuuliza maswali kuhusuiana na yaliyomo kwenye mafunzo kuhusiana na taarifa za kiafya na jinsi ya kuzuia, afya ya uzazi, stadi za mawasiliano ya ana kwa ana, na athari zake kwenye mabadiliko ya tabia. Pitai mada zote zinazotokana na

134

warsha. Hatua ya Pili Waambie washiriki kuaigiza mada ambazo wataongelea na wateja wao . Wapatie dakika kadhaa na baada ya hapo waalike watakaopenda kujitolea kushirikisha wenzao mawazo yao. Andika majibu yao kwenye bango. Hatua ya Tatu Soma madhumuni ya warsha yaliyoko hapa chini kwa sauti na uwaambie wanakikundi wajadiliane ni kwa namna gani madhumuni yamefikiwa ama hayakufikiwa. Madhumuni ya Jumla ya warsha: Mwisho wa warsha wahudumu wa saluni za urembo na wamiliki wao watapata taarifa za uhakika kuhusiana na afay ya uzazi, uelewa kuhusiana na saratani ya matiti na shungo ya kizazi, magonjwa ya ngono na VVU na jiansi ya kuzuia katika jitihada za kuboresha afya za wanawake wa Tanzania. Watakuwa pia wameongeza kiwango cha stadi za kufanya majadiliano na mawasiliano ya ana kwa ana wao na wateja wa saluni ili kuongeza mauzo.

8.2 Taarifa za warsha -Jaribio la mwisho la Warsha

Hatua ya kwanza Waambie washiriki kwamba utawapatia dodoso. Waelekeze washiriki kwamba wanazo dakika 20 tu za kujibu maswali. Waambie hapaswi kupata taarifa zozote kutoka nje ya mada. Na wanapaswa kujibu maswali kwa kuzingatia wanachokifahamu tu. Baada ya dakika 20 kusanya makaratasi ya jaribio. Hatua ya Pili Linganisha matokeo ya jaribio la awali na jaribio la mwisho la mafunzo. Weka angalizo kwa maswali ambayo yamepata kiwango kidogo cha majibu sahihi .

135

9.3 Tathmini ya Mafunzo

Wapatie washiriki fomu maalum zilizoandaliwa za kutathmini mafunzo na zijazwe kila mtu kwa usiri wake. Kusanya fomu hizo na uzipitie baadae.

9.4 Kufunga Warsha

Fanya sherehe fupi ya kufunga na kuwapatia vyeti. Washukuru wote kwa kuhudhuria warsha na kwa kushirikishana taarifa kwa siku nzima na baada ya hapo funga mafunzo rasmi. Wapatie namba za simu za wafanyakazi wa T-MARC na uwahakikishie kwamba wanakaribishwa wakati wowote kuwasiliana nasi kwa ajili ya taaria zaidi. Tutafawatembelea kwenye maeneo yao baada ya wiki 2 ili kufuatilia utekelezaji na kujibu maswali.

136

KITUO CHA WANAWAKE CHA AFYA JIPENDE!

JARIBIO LA MWISHO LA MAFUNZO

1. Nini ni sababu kuu ya vifo miongoni mwa wanawake kati ya miaka 18 hadi 49 hapa Tanzania? UKIMWI, Mimba/ Matatizo wakati wa kujifungua, Magonjwa ya ngono, Malaria , 2. Je VVU ni tatizo kubwa kwa wanaume au wanawake ? Wanaume wanawake 3. je inawezekana kuwa na ugonjwa utokanao na ngono na usijifahamu kama unao? NDIO HAPANA 4. Kuwa na magonjwa ya ngono kunaongeza uwezekano wa: kupata saratani kupata VVU Kupata mimba kupata Malaria 5. Taja njia tatu za kuzuia VVU : a. ____________________ b. ____________________

c.______________________

6. Ipi ni njia pekekee ya kuweza kutambua kama una VVU? _____________________ 7. Taja njia mbili ambazo unyanyapaa unaathiri jitihada za kuzuia VVU na kutibu hapa Tanzania : a. ____________________________________________________ b. ____________________________________________________ 8. Ni kwa kiasi gani wanwake wanapaswa kuchunguza sartani ya matiti ? Kila siku mara moja kwa wiki mara moja kila mwezi mara moja kwa mwaka 9. ipi ni njia ya mawasiliano yenye ngivu zaidi katika kubadili tabia za watu? Redio mawasiliano ya ana kwa ana luninga vipeperushi

137

10. taja njia sita za uzai wa mpango zinazopatikana hapa Tanzania : a. ___________________ d.____________________ b. ___________________ e._____________________ c. ___________________ f.______________________

138

FOMU YA KUTATHMINI MAFUNZO

Fomu hii ni ya siri. Usiandike jina lako kwenye fomu. Asante 1. Je matarajio yako kwa ajili ya mafunzo haya yamefikiwa? (weka mduara kwenye jibu) ? (Weka mduara) NDIO HAPANA Kama hapana, kwanini?

6. Je ni mada gani umeipenda zaidi? Kwanini? 7. Mada gani huajipenda? Kwanini? 8. Ni mada ipi tulihitaji kutumia muda mwingi zaidi?

9. Kwa ujumla mtindo wa uwezeshaji ulikuwaje? ( zungushia duara jibu moja) m. Nzuri sana n. Wastani o. Nzuri p. Dhaifu Maoni: 10. je tunaweza kufanya nini tofauti ili kuboresha yaliyomo kwenye mafunzo haya? 11. Tunaweza kufanya nini touti ili kuboresha utaratibu mzima wa mafunzo haya ? (Muda, mapumziko ya chai/ kahawa, n.k) 12. Kwa ujumla, unaweza kuyapa mafunzo haya kiwango gani cha ufanisi? (Weka duara kwenye jibu moja) . Nzuri sana b. Nzuri c. Wastani d. Dhaifu

13. Tumia nyuma ya ukurasa huu kama unayo maoni zaidi.

139

Information

JIPENDE

139 pages

Report File (DMCA)

Our content is added by our users. We aim to remove reported files within 1 working day. Please use this link to notify us:

Report this file as copyright or inappropriate

303425


Notice: fwrite(): send of 197 bytes failed with errno=104 Connection reset by peer in /home/readbag.com/web/sphinxapi.php on line 531